Dr. Slaa kawasaidie wana Igunga!

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
Namshauri Dr Slaa akagombee Ubunge Jimbo lililoachwa wazi na Fisadi Na. 1 Tanzania, Rostam Aziz, arudi tena Bungeni kuongeza nguvu!
Nawasilisha! Tujadili!
 
Bungeni si kwa DR yeye anafaa kuwa raisi wangu tuu ubunge anajishusha sana!
Unataka aaambiwe anauroho wa madaraka dr usigombee huko!
 
Bungeni si kwa DR yeye anafaa kuwa raisi wangu tuu ubunge anajishusha sana!Unataka aaambiwe anauroho wa madaraka dr usigombee huko!
Watasema watakacho, hata akirudia kugombea urais ataambiwa "ana uroho wa madaraka!"
 
waliopo wamewaelemea magamba kila kona, ni bora akangalia majukumu ya kitaifa zaidi. Morover, Igunga sio 'kwake', isije kuwa kama Hussein Mwinyi: kutoka Mkuranga mpaka ZNZ!
 
Jamani hata 'Dr' Lyatonga Temeke si 'kwake' lakini aligombea! Huyo Mwinyi hata kama asili yake ni Mkuranga lakini ni Mzanzibari! Ukitaka kumtafuta Mzanzibari Original unaweza kumkosa maana utakuta kuna wenye asili ya wanyamwezi, waarabu, wahindi, wangoni, nk!
 
Namshauri Dr Slaa akagombee Ubunge Jimbo lililoachwa wazi na Fisadi Na. 1 Tanzania, Rostam Aziz, arudi tena Bungeni kuongeza nguvu!
Nawasilisha! Tujadili!

Tupo kibao vijana wake na tupo tayari kabisa kupambana kulingoa jimbo la Ingunga kutoka katika utawala wa ki magamba magamba na kupeperusha bendera ya haki na demokrasia ya kweli kwa watu wote.
 
Kijana unatakiwa ujifue kweli dhidi ya magamba maana wanapenda sana ushindi wa mezani kupitia Tume isiyo Huru ya Uchaguzi!
 
Dr. ni Mtanzania na ana haki ya kugombea mahali popote maana anatetea watanzania... naunga mkono hoje 100 kwa 100
 
Kuna habari isiyo rasmi kwamba Dr slaa atagombania jimbo la Igunga. JE ANASIFA ZA KUSHINDA
 
sio easy kama unavyofikiria
dr slaa alisimama nafasi ya urais na alipata kura nyingi
hawezi kukubali kusimama jimboni,yeye ana uwezo mkubwa zaidi
kwanza haiwezekani
 
Kuna habari isiyo rasmi kwamba Dr slaa atagombania jimbo la Igunga. JE ANASIFA ZA KUSHINDA
Sifa na uwezo wa kushinda anao bt maamuzi ya kugombea huko igunga hana, hafikiri jimbo, mawazo yake yapo ktk kushika dolla ya nchi.
 
ubunge ndio size yake ama urais alikuwa amepotea. Kwani mpaka aende yeye Tabora hakuna mwanachama wa cdm anayekubalika? au ndio kusema maslahi kwanza? Mistake zilizokwisha tokea kama taifa ebu tusizirudie,namaanisha kuwa mgombea wa sehemu yoyote atokane na watu wanaoishi pale na siyo mtu atoke kilimajnaro eti akagombee Rukwa,dhana nzima ya uwakilishi inakuwa haipo. Napendekeza mgombea atokane na wana Igunga wenyewe, unajua kama wewe ni mgombea wa kuja kuna matatizo ya sehemu husika hutoyajua mpaka usimuliwe kitu ambacho utakuwa huyafili. Mshaurini aache kwani ataumbuka
 
Hakuna topic hapa, hawezi kugombania pale ila atamweka kamanda mzuri
na atampigia debe mpaka ashinde. Jimbo letu wanakabidhi lini?
 
Sifa na uwezo wa kushinda anao bt maamuzi ya kugombea huko igunga hana, hafikiri jimbo, mawazo yake yapo ktk kushika dolla ya nchi.

nchi gani hiyo? Kwanza jamaa kukaa benchi inamuuma maana anaona wenzie wanachukua sifa mjengoni anahisi kwenye medani za siasa anaanza fifia that why kila tamko na habari ya chama anataka aitowe yeye as if chama hakina hafisa habari/katibu mwenezi
 
Kweli hakuna NCHI tanganyika. Magamba wameiuza tayari.
 
nchi gani hiyo? Kwanza jamaa kukaa benchi inamuuma maana anaona wenzie wanachukua sifa mjengoni anahisi kwenye medani za siasa anaanza fifia that why kila tamko na habari ya chama anataka aitowe yeye as if chama hakina hafisa habari/katibu mwenezi
Usisiem wako utakuponza, endelea kupiga domo lapda mukama atakufanyia mpango!
 
Back
Top Bottom