Dr. Slaa kawasaidie wana Igunga!

Naanza kwa kusema siungi mkono hoja hiyo. Ndg zangu dk tumwache afanye kazi za chama na aendelee kupanga mikakati ya kuchukua nchi 2015, wape watu wa CDM wana uwezo mzuri wanaweza kulichukua jimbo lile ni la kwao. Lipumba akienda kule mm nawashauri CDM wamuunge mkono kwa masharti ya kutogombea urais 2015 ili asitupunguzie kura badala yake agombee ubunge huohuo, awe kama Mrema ajue kabisa urais siyo size yake tena amexpire machoni kwa wananchi akapiganie ubunge.
 
Kamati kuu ya pitisha jina la dr slaa kuwa mgombea wa kiti cha ubunge katika jimbo la Igunga. lilo achwa wazi baada ya rostam kujiuzulu
 
haya yatakuwa mawazo yako mwenyewe,hakuna cha tetesi,ni vema kuacha uzushi
 
kama sio dr slaa nani mwingine anayeweza kuuzwa na cdm akauzika kwa wananchi. Ccm wanamweka kubenea au bashe

Hivi kubenea ni CCM?au siyo kubenea huyu anayeiponda serikali ya ccm kila kukicha!

Na huyu Bashe si walisema Si Mtanzania?

Mimi nimesikia Selelii ndo anasimama pale! Na chadema wanamtuma Mzee wa CCJ
 
Kuna habari isiyo rasmi kwamba Dr slaa atagombania jimbo la Igunga. JE ANASIFA ZA KUSHINDA

Kwani yeye ni mkazi wa Igunga au ana asli ya hapo. Nafikiri watu wa Igunga watakosa fadhila kama watamchagua mtu kuwawakilisha Bungeni wakt sio mkazi wala ana asli ya hapo kama ilivyo kwa takriban 98% ya wabunge wote wa kuchaguliwa na wananchi huko Tanzania.
 
Dr Slaa sio MREMA..........Alipokosa urais 1995 akakimbilia jimbo la Temeke....na akajimaliza kabisaa
 
Hata kama Dr Slaa angekuwa ni mzaliwa au mkazi wa Igunga, tayari ana majukumu muhimu zaidi kuliko kuliongoza jimbo la Igunga au kuwa mbunge wa jimbo lolote lile. Dr Slaa hana uchu wa madaraka kiasi hicho, ni kiongozi shupavu mwenye uwezo na nia ya kweli ya kuleta maendeleo Tanzania. Makamanda wa CDM waliopo bungeni cheche zao zinatosha kuwasha moto nadhani wote mnashuhudia, Dr Slaa aendelee tu na kuuchochea moto wa mabadiliko kupitia elimu ya uraia tena yenye hamasa kwa wananchi nchi nzima.

Miaka minne iliyosalia ni muda tosha kwa CDM kuhakikisha wananchi wamehamasika vya kutosha kuing'oa CCM kwenye utawala wa nchi hii. Kwa mwendo huu, wabunge 2015 majority watakuwa wapinzani!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom