Dr. Slaa atakuwa adui namba 4 kati ya maadui wa 3 wa Mwl Nyerere

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,840
Dr Slaa hakuzaliwa wala kukulia Chadema.Naye alikaribishwa kama mwenzie lowassa Na hakuna aliyepinga kupokelewa kwake hata kidogo.Chadema walienda mbali zaidi na kumpa dhamana ya kuwa Katibu mkuu wa chama.

Nikiwa kama mwanachama hai wa Chadema niliyezaliwa na kukulia ndani ya chama hiki,Nasema"Endapo Dr slaa atakigeuka chama wakati huu mzuri tukiwa tunahitaji mabadiliko na fikra mpya.Atakuwa ndio adui wangu namba moja wa siasa za mabadiliko tanzania tunazozililia kwa miaka 20 sasa.

Dr Slaa ni nani hata apingane na wengi,Tena kamati kuu ya chama?

Dr Slaa ni nani apingane na nguvu kubwa ya mabadiliko na ukombozi wa kiuchumi?

Bila shaka nipo tayari kuamini ipo nguvu kubwa toka chama tawala inayomshawishi Dr kufanya haya kwa masilahi yake na yao binafsi.Na si wengine ni Ccm,Baada ya muungano wa Ukawa walikosa usingizi na sasa rasilimali zao zote zikiwemo rasilimali fedha na watu wameziamishia kwa Dr ilimradi tu ndoto hizi njema zisitime.

Sipo tayari na naomba wana Chadema wote tuungane kwa hili.

Na kama Dr atatusaliti tumwainishe katika maadui wakubwa kati ya wale maadui aliowataja mwalimu Nyerere.

Maradhi,Ujinga na Umasikini adui wa nne tutamwongeza Dr Slaa asiposikia vilio vya wapenda mabadiliko.


Napenda nichukuwe furusa hii kumuliza maswali mawili tu katibu wangu mkuu Dr slaa.
Je,Dr Slaa kama Lowassa angejiunga na Chadema na wewe ukabaki ndiye mgombea wetu wa Urais October ungesusa ujio wake?
Au umesusa baada ya Lowassa kupendekezwa kupeperusha bendera na wewe kuachwa?
Jibu maswali hayo mawili,Mengine yote tutakuvumilia
 
chadema ni kubwa kuliko yeye....hivyo chama hiki hakiyumbishwi........mtu mkubwa katibu wa chama una susa wakati chama kina elekea katika vikao vikuu vya maamuzi!....maajabu haya...Lowassa ni mtaji mkubwa.......pia anakubalika na ukawa sasa nini tena...shindeni uchaguzi,,mengine yatafuata
 
Yaani nashindwa kuelewa wafuasi wa Chadema sijui wenzetu ubongo wao una mafuta ya taa au ni wa ndege maana hawakawii kusahau.Leo mnamtukana slaa kisa lowasa.nawafananisha na mwanke anaesaliti ndoa yake kisa kapewa sh 10000/=ya Mara moja na kusahau Huduma za mumewe za kila siku.
 
Tunamheshimu tunampenda na mtendaji mzuri kwa hili la kuja lowasa chdm aondoke cc tutampigia lowasa
 
Lakini whaterver a ushabiki juu
1, ananyang'anywa tonge la kugombea
2. Lowasa aliktawa kakimbia , sasa yeye kukatwa wacha akimbie ruksa!
3, EL hajajisafisha kabisa!! jamani alinuka! anahitaji kwa makusudi afungtuke, wengi bado wanadhani yule EL fisadi!! je katioka huko? au bado!, au hakuwahi kuweko? aje na data sio porojo
 
Nilikua na mheshimu na kumwamimi dor katika mabadiliko ya kweli. Kama yeye amnaweza kujitoa ukawa basi hatafaa kuwa kiongozi hata wa nyumba kumi. Tunahitaji mabadiliko na siyo mambo ya mke ukawa tutasongabele daima.
 
Dr. Slaa siyo mtu wa unafiki, alichokisema jana ndicho hicho hicho atakachokisema kesho na kuendelea, kwa sasa mtamtukana sana lakini historia imeshaandikwa tayari kuwa Dr Slaa huwa anasimamia alichokisema

ni kweli, na hapo ndipo mimi naona tofauti kubwa kati ya mwanasiasa na Mwanaharakati. Mwana harakati anenda by principles na kuhold on to what he/she believes is right. Mwanasiasa goes by oportunity as long as what they belives becomes. Mbowe ni Mwanasiasa mkubwa sana Tanzania na tunatakiwa tufurahi kuwa nae...viva Chadema
 
Back
Top Bottom