Dr. Slaa anasa nyaraka za siri za CCM za kuingiza silaha nchini

Mambo yapi yasiyomwendea vizuri Slaa.Mimi mbona naona mambo ya CDM ni super.CCM mambo yao ndio hogojogo.Maloloso matupu.
Mikael P Aweda,
Dar Slaa, ni msanii amekuwa mara nyingi akitoa tuhuma za uongo, hasa pale anapoona matokeo hayamuendei vizuri.
 
Last edited by a moderator:
Hivi wewe unajua kuwa hata tume ya Taifa ya Uchaguzi walishindwa kuyaweka matokeo ya Urais kutoka majimbo yote ya nchini?

Jimbo la ubungo tu hapa mjini ambalo nilikuwa mwenyekiti wake nalo mlichakachua, je, itakuwa kule vijijini ambako kabla ya M4C Chama hakikuwa strong?

Sasa, kati ya watz wengi wanaomwamini Dr Slaa na wewe unayesema ni mwongo hebu niambie tumwamini nani? wewe au watz?


Ebu niambie Chadema mlitumia vigezo gani kuyakataa matokea ya urais halafu mkayakubali matokeo ya ubunge na udiwani.
 
Wakubwa mbona mambo ya kimsingi mnaropoka? Kwani mangapi kashasema mkaropoka kuwa uongo na baadae mkaumbuka? Hata Ulimboka angesema mnge mropokea! Hivi ndivyo majambazi ya CCM yanavyojipanga kung'angania madaraka, na wananchi tumeshafahamu sasa TUNASEMA IMETOSHA tunataka haki kwa kila mtanzania. CCM wameibia nchi kupitia viongozi wao kama inavyo onekana wazi, wanazima haki na Demokrasia kama walivyofanya kwa madaktari na waalimu je, hayo hamuyaoni? Tuchunguze kwanza ukweli wa Slaa kabla ya kuropoka maana itapobainika ukweli mtaumbuka kama EPA & RICHMOND.
 
Ni mbinu za kujitafutia umaarufu ,ila mimi sishangai kwani ni mbinu za vita ya kisiasa na zinakubalika katika medani ya vyama vya siasa.

Sitoshangaa kesho akiamka akisema kuna watu walitaka kumuua silaha zikawaanguka !
 
Hivi kwa nini chadema wasianzishe jeshi lao kama lile la umkhonto we sizwe....
 
Mwiba unachekesha sana...hivi slaa anataka umaarufu gani pale alipo..maana ni maarufu kuliko aliyeko magogoni...
 
Siasa hizi ni za kizamani sana. Tujifunze siasa za kisasa. kama ushahidi upo, umwage tupate ukweli, sio kusingizia uongo.
 
Mwiba unachekesha sana...hivi slaa anataka umaarufu gani pale alipo..maana ni maarufu kuliko aliyeko magogoni...
Aloo wewe ni mgeni wa mambo ya kisiasa ,hizo ni aina za propaganda za kisiasa ,hivi CCM wanashida ya kuagiza silaha kutoka nje ? Fikiria jambo hilo tu ,huenda ukafunguka.
 
Nahongezea ,huyu mzee asipo angalia anaweza akapandishwa mkenge ,kwani anaweza akapewa nyaraka au siri za kubuni ili aingizwe mjini ,akizitangaza tu kwa kuamini kuwa makaburasha aliyopewa ni ya kweli basi amekwisha ,bora ,nawapa ushauri wa bure ,habari hizo watangaze walio chini yake na asipewe yeye. Take my advice.
 
uongo wa kwanza ni pale alipodanganya kanisa kuwa atatii sheria za mungu matokeo yake akaasi.
pili alipoaminiwa na ROSE kamili matokeo yake akamtelekeza yeye pamoja na watoto akaanza uzinifu na Josephine

uongo mwingine ni huu kwamba CUF wameingiza kontena la visu na lile la kura kule mpakani na msumbiji
Unajua ukiwa mwongo uwe pia na kumbukumbu. Hivi aliyesema CUF wameingiza visu alikuwa Dr. Slaa? Siyo mtumwa wenu aliyekuwa mkuu wa polisi zamani Omar Mahita tena.
Masanduku ya kura kutoonekana haina maana kwamba hayakuingizwa. Hii ni nchi ambayo taasisi za serikali ikiwepo polisi, TRA na taasisi zingine zinazolinda mpaka zinaongozwa na viongozi wanaoteuliwa na huyo aliyekuwa mgombea wa ccm bwana Mrisho. Kupotezea ushahidi kabla watu hawajashtuka na kuja na ushahidi wa kimaghumashi unaaonyesha kinyume si jambo la kushangaza. Kuhusu maisha binafsi ya Dr. Slaa natumaini kichwa chako kitakuwa japo na ubongo kidogo kujua ukweli wake zaidi ya huu uongo unaopakaza humu ndani.
 
Ving'ang'anizi wa ccm naona hapa mmeshikwa pabaya. Kitu kimoja tu nashindwa kuelewa. Hivi kama ni kweli hampendi hii picha mbaya kwa chama chenu kwanini mswaipige marufuku hawa wapuuzi wanaofanya hivi visa kwenye chama chenu? Zamani za ujinga mliweza kuwashawishi watanzania kwa kila lililobaya dhidi ya wapinzani na wakawaanini kwa kuwa walikuwa hawajawajua kuwa ndio mashetani kuliko shetani mwenyewe. Sasa mambo yamebadilika watanzania hawashiwishiki kirahisi kwa kuwa wameshawajua. Cha ajabu badala ya kuona hizi mbinu hazifanyi kazi mnazizidisha. Yaani kama ni kuzama kwenye matope ccm mnaizamisha taratibu na sasa imebakiza mikono tu na kwa mbinu mnazofanya kuinasua hata mikono inakaribia kupotea kwenye tope asiloweza kutoka mtu. R.I.P ccm.
 
uongo wa kwanza ni pale alipodanganya kanisa kuwa atatii sheria za mungu matokeo yake akaasi.
pili alipoaminiwa na ROSE kamili matokeo yake akamtelekeza yeye pamoja na watoto akaanza uzinifu na Josephine

uongo mwingine ni huu kwamba CUF wameingiza kontena la visu na lile la kura kule mpakani na msumbiji

Kwa hivyo wewe ndo ingizo jipya la Nape humu jamvini..ila mbona kama amechukua mtu mropokaji sana..manake mate yanavyokuruka hata akili haifanyi kazi tena..sasa embu niambie,wewe umewataja cuf hapo juu,ni wapi dr. Slaa amezungumzia kuhusu cuf kuingiza silaha??..embu kuwa kama wenzio akina zomba na ritz ili walau udumu kwenye payroll kidogo..
 
Majibu ya Nape ni swadakta Dr Slaa ni muongo mkubwa, mwizi, mnafiki, msaliti, na ugonjwa wa kisukari umeathiri ubongo wake kwa sehemu kubwa.

Sawa, pamoja na hayo yote, he is the next president... of course your president, whether you like or not, because we the majority will vote him in.....!!!! you know what I mean anyway
 
naona wana Jf tunapotea njia,hivi kwa mtiririko wa wachangiaji, napata shaka kama kuna "great thinkers" humu,
inawezekana tunaweka mbele ushabiki wa kisiasa.ni jambo la hatari sana. si kwa CDM au CCM wala CUF bali watanzania wote nitawaeleza,

kwanza niwape kisa kimoja kilichotokea ujerumani, mchungaji mmoja aliyenusurika kuuwawa na majeshi ya manazi anaeleza
. waliwauwa wayahudi sikujali sikukemea wala kuchukua hatua kwa kuwa sikuwa myahudi
waliwauwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi sikujali sikukemea wala kuchukua hatua kwa kuwa sikuwa kiongozi
. waliwauwa viongozi wa vyama vya siasa sikukemea wala kuchukua hatua kwa kuwa sikuwa mwanasiasa
. walipowamaliza wote sasa wakanijia mimi sikuwa na jinsi...........
kwa kisa hiki tujifunze kwamba yanayotokea sasa si ya DR.Slaa CDM yakiachwa hivi hivi yanaweza kuwarudia hata nyinyi mnaobeza bila kutumia bongo zenu.

tunapoituhumu CCM ni pamoja na serikali yake

1. mtakumbuka lile sakata la filamu ya mapanki, kulikuwa na biashara ya silaha ilikuwa inafanyika katika maziwa makuu na tanzania ilihusika

2. miaka kama miwili imepita zilikamatwa silaha kule mwanza mpaka leo hazijulikani zilikuwa ni za nani na zilikuja kwa nani

3.Harison Mwakyembe alitahadharisha jinsi baadhi ya wanaCCm wenzake wnavyopanga mikakati ya kumuua yeye dr.slaa mwandosya na wengine.kilichotokea tumeshuhudie kwa macho yetu. hata wana CCm wenyewe hawaaminiani kammuulize sita atakueleza jinsi wana CCm wenzake waliyompa H. mwakyembe sumu. hata JK alisha sema wana CCM hawaachiani glass. sasa mnabeza tuhuma za dk slaa????

3.tumeshuhudia kitendo cha kutekwa na kuteswa kwa dk Ulimboka. mwanahalisi wakawataja waloiohusika wakafungiwa

4. Kubenea na Tegambwage walimwagiwa tindikali na nani na kwa nini jiulize

5. mauaji ya wana CDM Igunga na Arusha

6. mbona waziri Malima alikutwa na silaha za kivita kinyume na sheria na bado ni waziri

6. mbona tuhuma za mtoto wa kigogo anayemiliki mtambo wa spoofing SMS hazijakanushwa alafu na hajakamatwa
kwa mtiririko wa matukio haya mtu mwenye akili hawezi puuzia madai ya dk slaa.na kama hamuamini maneno ya dk mkamuulize kada mwenzenu Mwakyembe
 
Back
Top Bottom