TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
Katika tukio lisilo la kawaida ambapo kituo cha Matangazo cha ITV kiliandaa mjadala wa kujadili hali ya kisiasa nchini na masuala mbalimbali ya kitaifa ambapo kwa busara za watendaji wa ITV waliwaalika wasemaji wakuu wa mjadala huo kuwa Viongozi waandamizi wa Vyama vya Siasa wakianza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahaman Kinana na Katibu Mkuu wa CHADEMA Ndugu Slaa.
Kutokana na hudhuri wa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana ambapo amesafiri kuelekea Dodoma kwenda kuhudhuria kikao cha kamati kuu jana na kubanwa na majukumu mengine muhimu ya kichama na kitaifa, alimuagiza Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, ndugu Nape Nnauye kumuwakilisha katika mjadala huo wa viongozi wa vyama vya siasa katika kujadili hali ya kisiasa na mustakabali wan chi yetu.
Baada ya kufika katika Ofisi za ITV zilizopo mikocheni asubuhi ya Leo, Nape pamoja na Slaa walikutana na Nape kueleza kuwa atamuwakilisha Katibu Mkuu wake katika mazungumzo hayo ambapo baada ya kusikia kauli hiyo, Dr Slaa alianza kuhamaki na kudai kuwa hawezi kuongea na Nape kwa sababu anamtaja vibaya kwenye mikutano yake, hata busara zilipotumika za kumsihi apungumze munkari na kumtaka kuangalia umuhimu wa mazungumzo hayo na kipindi hicho kwa watanzania, bado Slaa aligoma na kuondoka katika ofisi za ITV.
Baada ya tahamaki hiyo, mijadala ya pembeni ya mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa kimsingi Slaa anamuogopa Nape katika mijadala ya kisiasa, nah ii ni kutokana na uwezo wa Nape katika kujenga hoja na kuzilinda na kuzitetea hoja hizo, ambapo kwa Slaa ni aghalabu kuweza kufanya hivyo hasa kutokana na kuchoka katika utafakari kunakotokana na Umri mkubwa alionao.
Lakini tukio hilo linadhihirisha kukosa uvumilivu wa kisiasa (lack of political tolerance) ambako viongozi wa CHADEMA hasa Slaa wanao. Hii ni kwa sababu Nape alimtaka aeleze ni kusemwa vibaya kupi ambako yeye Slaa anakumaanisha na akashindwa kubainisha. Lakini hali hiyo pia imeonesha taswira ya political immaturity kuwa viongozi wa aina hii hawajakomaa na hawatoshi kukabidhiwa dhamana ya aina yeyote si tu kwa level ya kitaifa bali hata kwa level ya chini yake.
Pia, tukio hilo linaweka wazi kuwa CHADEMA hawako tayari kuyazungumzia ana kwa ana matatizo yaliyotokana na Siasa mbovu mbovu wanazozifanya na hasa kauli za viongozi wao wakuu. Tabia hii ya kukwepa kuyashughulikia makosa ya kisiasa kutalileta Taifa letu madhara makubwa sana. Kama Chama tawala, CCM inaona ni kasoro kulifumbia macho jambo hili, kukataa kulikubali tatizo tulilonao la siasa mbofu zenye kuhamasisha chuki, utengano, udini, ukabila na hata kuendesha matukio ya kudhuru watu na mauaji ni makosa. Hatuwezi kuogopa au kupuuza kuyazungumza haya hivi sasa.
Ni muhimu kuhimizana katika uzalendo wan chi na Utaifa, ni lazima tuhimizane katika kutunza maadili yetu kama watu wa Taifa lenye utu na ustaarabu ili kutunza heshima na amani tuliyonayo. Wakati serikali ikipambana kushughulikia utulivu na kuboresha hali ya amani lazima viongozi, watendaji, wanachama na mashabiki wa Siasa hapa nchini kulitambua jukumu lao katika kuimarisha amani na utulivu hapa nchini. Si busara kukimbia na kukwepa mazungumzo yenye kulenga kujadili kwa kina hali yetu ya siasa kwa sasa hapa nchini.
----- Ufafanuzi Kutoka kwa Dr.W.Slaa ------
----- ------

TandaleOne,
Ni kwanini mtunawe na ujasiri kusema uwongo ambao dakika ya pili, utaonekana dhahiri ni uwongo. Ni kielelezo cha jinsi Taifa letu lilivyozama kwenye Tope nene.
1) kwanza niseme kuwa ninkweli tukio lilikuwepo. Majira ya saa 3.00 asubuhi, muda uliopangwa nilikuwa kwenye Gate la ITV, na kupokelewa na Mwandishi na mratibu wa Program hiyo. Nyuma yangu likawa linaingia Gari. Aliteremka Nape, nikadhani amemsindikiza Katibu Mkuu wake, Mhe. kinana. Tukasalimiana kwa kishikana mikono, na kutaniana kidogo.
2. Ndipo nikamwuliza Boss wake yuko wapi, ndipo akanijibu kuwa amemtuma yeye. Nikauliza, mbona sikujulishwa, kwa kuwa ningelijua, ningemtuma afisa wangu, size ya Nape. Nape alikubaliana nami. Nikamwambia basi, kipindi hakitawezekana, na Nape na Mwandishi wote wakakubaliana nami. Kipindi kikaahirishwa.
3. Waandalizi wa kipindi tukakubaliana kuwa kwa kuwa ni vigumu kupata ratiba itakayokubaliana, basi Mimi nitaendelea na kipindi Kesho ( kurekodiwa) saa 5 asubuhi na CCM itakuwa na siku yake. Sijui sasa Propaganda ya nini hata katika jambo Kama hili. Nami ningelipenda ningelienda mbali zaidi, kwani kipindi tangu kinapangwa zaidi ya siku 10 iliyopita nilihusika mmoja kwa mmoja. Kimsingi ni viongozi wa ajar wasioheshimu appointments, na Kama kweli kulikuwa na dharura si tungelipeana taarifa basi? Nadhani nisiendelee zaidi, wenyenkuelewa watakuwa wameelewa, na walioleta propaganda ya Dr Slaa kukimbia.... Wajue kuwa propaganda itajibiwa vilivyo, na ukweli utashinda daima.