Dr Slaa akataa mjadala na Nape ITV badala na Kinana

Status
Not open for further replies.

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Katika tukio lisilo la kawaida ambapo kituo cha Matangazo cha ITV kiliandaa mjadala wa kujadili hali ya kisiasa nchini na masuala mbalimbali ya kitaifa ambapo kwa busara za watendaji wa ITV waliwaalika wasemaji wakuu wa mjadala huo kuwa Viongozi waandamizi wa Vyama vya Siasa wakianza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahaman Kinana na Katibu Mkuu wa CHADEMA Ndugu Slaa.

Kutokana na hudhuri wa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana ambapo amesafiri kuelekea Dodoma kwenda kuhudhuria kikao cha kamati kuu jana na kubanwa na majukumu mengine muhimu ya kichama na kitaifa, alimuagiza Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, ndugu Nape Nnauye kumuwakilisha katika mjadala huo wa viongozi wa vyama vya siasa katika kujadili hali ya kisiasa na mustakabali wan chi yetu.

Baada ya kufika katika Ofisi za ITV zilizopo mikocheni asubuhi ya Leo, Nape pamoja na Slaa walikutana na Nape kueleza kuwa atamuwakilisha Katibu Mkuu wake katika mazungumzo hayo ambapo baada ya kusikia kauli hiyo, Dr Slaa alianza kuhamaki na kudai kuwa hawezi kuongea na Nape kwa sababu anamtaja vibaya kwenye mikutano yake, hata busara zilipotumika za kumsihi apungumze munkari na kumtaka kuangalia umuhimu wa mazungumzo hayo na kipindi hicho kwa watanzania, bado Slaa aligoma na kuondoka katika ofisi za ITV.

Baada ya tahamaki hiyo, mijadala ya pembeni ya mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa kimsingi Slaa anamuogopa Nape katika mijadala ya kisiasa, nah ii ni kutokana na uwezo wa Nape katika kujenga hoja na kuzilinda na kuzitetea hoja hizo, ambapo kwa Slaa ni aghalabu kuweza kufanya hivyo hasa kutokana na kuchoka katika utafakari kunakotokana na Umri mkubwa alionao.

Lakini tukio hilo linadhihirisha kukosa uvumilivu wa kisiasa (lack of political tolerance) ambako viongozi wa CHADEMA hasa Slaa wanao. Hii ni kwa sababu Nape alimtaka aeleze ni kusemwa vibaya kupi ambako yeye Slaa anakumaanisha na akashindwa kubainisha. Lakini hali hiyo pia imeonesha taswira ya political immaturity kuwa viongozi wa aina hii hawajakomaa na hawatoshi kukabidhiwa dhamana ya aina yeyote si tu kwa level ya kitaifa bali hata kwa level ya chini yake.

Pia, tukio hilo linaweka wazi kuwa CHADEMA hawako tayari kuyazungumzia ana kwa ana matatizo yaliyotokana na Siasa mbovu mbovu wanazozifanya na hasa kauli za viongozi wao wakuu. Tabia hii ya kukwepa kuyashughulikia makosa ya kisiasa kutalileta Taifa letu madhara makubwa sana. Kama Chama tawala, CCM inaona ni kasoro kulifumbia macho jambo hili, kukataa kulikubali tatizo tulilonao la siasa mbofu zenye kuhamasisha chuki, utengano, udini, ukabila na hata kuendesha matukio ya kudhuru watu na mauaji ni makosa. Hatuwezi kuogopa au kupuuza kuyazungumza haya hivi sasa.

Ni muhimu kuhimizana katika uzalendo wan chi na Utaifa, ni lazima tuhimizane katika kutunza maadili yetu kama watu wa Taifa lenye utu na ustaarabu ili kutunza heshima na amani tuliyonayo. Wakati serikali ikipambana kushughulikia utulivu na kuboresha hali ya amani lazima viongozi, watendaji, wanachama na mashabiki wa Siasa hapa nchini kulitambua jukumu lao katika kuimarisha amani na utulivu hapa nchini. Si busara kukimbia na kukwepa mazungumzo yenye kulenga kujadili kwa kina hali yetu ya siasa kwa sasa hapa nchini.


----- Ufafanuzi Kutoka kwa Dr.W.Slaa ------
----- ------

TandaleOne,

Ni kwanini mtunawe na ujasiri kusema uwongo ambao dakika ya pili, utaonekana dhahiri ni uwongo. Ni kielelezo cha jinsi Taifa letu lilivyozama kwenye Tope nene.

1) kwanza niseme kuwa ninkweli tukio lilikuwepo. Majira ya saa 3.00 asubuhi, muda uliopangwa nilikuwa kwenye Gate la ITV, na kupokelewa na Mwandishi na mratibu wa Program hiyo. Nyuma yangu likawa linaingia Gari. Aliteremka Nape, nikadhani amemsindikiza Katibu Mkuu wake, Mhe. kinana. Tukasalimiana kwa kishikana mikono, na kutaniana kidogo.

2. Ndipo nikamwuliza Boss wake yuko wapi, ndipo akanijibu kuwa amemtuma yeye. Nikauliza, mbona sikujulishwa, kwa kuwa ningelijua, ningemtuma afisa wangu, size ya Nape. Nape alikubaliana nami. Nikamwambia basi, kipindi hakitawezekana, na Nape na Mwandishi wote wakakubaliana nami. Kipindi kikaahirishwa.

3. Waandalizi wa kipindi tukakubaliana kuwa kwa kuwa ni vigumu kupata ratiba itakayokubaliana, basi Mimi nitaendelea na kipindi Kesho ( kurekodiwa) saa 5 asubuhi na CCM itakuwa na siku yake. Sijui sasa Propaganda ya nini hata katika jambo Kama hili. Nami ningelipenda ningelienda mbali zaidi, kwani kipindi tangu kinapangwa zaidi ya siku 10 iliyopita nilihusika mmoja kwa mmoja. Kimsingi ni viongozi wa ajar wasioheshimu appointments, na Kama kweli kulikuwa na dharura si tungelipeana taarifa basi? Nadhani nisiendelee zaidi, wenyenkuelewa watakuwa wameelewa, na walioleta propaganda ya Dr Slaa kukimbia.... Wajue kuwa propaganda itajibiwa vilivyo, na ukweli utashinda daima.
 

Attachments

  • IMG-20130515-01250.jpg
    IMG-20130515-01250.jpg
    715.2 KB · Views: 1,387
Nape kumpambanisha na Dr Slaa ni kumdhalilisha tu Dr Slaa;Nape apambane na msemaji wa CHADEMA MB Mnyika ambaye pia nina uhakika Mnyika atamgaraza vibaya Nape!

Mwenyekiti wenu mwenyewe JK alikimbia kukutana na Dr Slaa ndiyo itakuwa huyu Nape kweli ahahahahahah!
 
Dr Slaa ni Katibu Mkuu wa CHADEMA. Kinana ni Katibu Mkuu wa CCM. Lengo la ITV ni kwamba mjadala uwe wa makatibu wakuu. Sasa kama Kinana ameshindwa kufika, ulitaka Dr Slaa aongee na Nape? Nape kitengo chake ni uenezi na angeweza kukutanishwa siku nyingine na Mnyika ambaye yupo uenezi CHADEMA. Dr Slaa alikuwa sahihi kutoongea na Nape. Kwa ufupi Nape is too low kwa Slaa
 
Mwaliko ulikuwa ni Dr Slaa na Kinana lkn CCM wakamtuma Nape;Katibu wa chama makini hawezi kuongea na sisimizi mliyemtuma!Then unabandika maneno hapa yasiyo na msingi!!

Nape apambanishwe na msemaji wa CHADEMA MB Mnyika na sio Dr Slaa!NAPE HANA HADHI YA KUKAA MEZA MOJA NA Dr Slaa kujadili hoja,huyu wenzake ni akina Mnyika na watamgaraza kwenye hoja!
 
Hahaahaha,

Dr ametoka nduki.

Chadema hawana ubavu wa kusimama na CCM.

Nape peke yake mnamuogopa je ingekuwa safu nzima ya CCM ingekuwaje?
Ni kweli kabisa. Kama 2010 chadema walipowakataza wagombea wao kushiriki midahalo ya TBC. Kubwa kuliko zote ni pale mgombea urais wa chadema alipogoma kushiriki mdahalo pale Kempinsky na badala yake akajitungia maswali akawapa waandishi makanjanja wamuulize pale Karimjee.
 
Dr. Slaa hawezi kufanya mjadala na mtu mdogo kama nape

Kinana kwa cheo chake na uwezo wake ndiye wa level moja kukaa na kujadiliana na Dr. Slaa.
Mtoto mdogo kama wewe nape ambaye bado unanuka maziwa una uwezo gani wa kufanya mjadala na Dr. Slaa ambaye hata mwenyekiti wako anamuogopa.
Mkuu hiyo inaitwa nitoke vipi. Kama huyo jamaa post no. 2 anavyolazimisha umaarufu kupitia Kamanda Lema, Dr. Slaa na CHADEMA kwa ujumla.
 
Mkuu TandaleOne kwanza rekebisha hiyo title yako isomeke" Kinana amkimbia Dr.Slaa" YES! kamkimbia kwani kwenye hicho kikao napi hatakiwi kuhudhulia?

Ok, Ni sahihi kwa Dr, Kukataa

kuna tuofauti kubwa sana kati ya DR na Nape, huyu ni mwenezi huyu ni katibu mkuu...
Nape huropoka bila data... angalia thread zake hapa jamvini..

Mara ngapi nape hata hapa JF anakimbia? viongozi wa JF walishamuita apambane na kamanda Yeriko Nyerere akakimbia, tena tukapendekeza achuane na Ben Saanane mpaka leo kimia, kila siku anatoa udhuru, mkuu AishaDii kajitahidi lakini wapi.
 
Ningemshangaa kama Dr.Slaa angekubali kukaa eti kujadiliana nawe Nape ... For which merits do you think you qualify to be in the same platform with the Dr.!!?? You got what you deserved Mwenezi...
 
Huyo nape apambanishwe na Dr Slaa?? Nape si alidharauliwa bungeni kwa kauli ile ya " wabunge na mawaziri wasifanye kazi za nape" leo hii ndo apambanishwe na Dr!! dharau gani hii?
Wanaccm wenyewe wanajua nape anafanya propaganda na hatoagi kauli serious.
 
Acha kuzunguka mbuyu, kwani hata hili unalijua wazi kwamba HOJA NI MOJA TU HAPO, KWAMBA DR. SLAA siyo level yako. Dr. Slaa hawezi kuwa kwenye mjadala na wewe ili ujiongezee CV kwamba kuna siku uliwahi kuwa kwenye mjadala na Dr. Slaa. Dr. Slaa alihudhuria kwasababu alijua wanakutana na Katibu mkuu wa CCM na siyo wewe Nape. Kinana baada ya kuona kwamba ana kashfa nyingi sana zinazokinzana na interest za nchi, akaamua kutafuta sababu.

Na wewe Naüe, kwasababu huna kazi na huna hoja as a product ya thesis yako ya Mzumbe ya Masters, ukaona hii ni nafasi pekee ya kujiongezea umaarufu kwa kuropoka kwa kutafuta Public Sympathy kwamba Dr. Slaa amekosa political tolerance!

Ni politoical tolerance ipi unaouongelea kwa Dr. Slaa na hata viongozi wengine wa CHADEMA ambao kila siku, wewe Nape, ukiwa pamoja na kikundi chako maaarufu kama CHAMA CHA MATUSI dhidi ya CHADEMA ukiwa na members wengine kama Mtela, Shonza, Mwigulu , na wengineo, mmekuwa mkiwatukana na kuongea maneno machafu dhidi ya Dr. Slaa na mara zote hujawahi kumsikia akikujibu kwa upuuzi wenu? hii ni kwasababu anajua wewe una UPEO MDOGO SANA katika mambo mbalimbali.


kwa ufupi ni kwamba wewe HAUKO KWENYE LEVEL SAWA NA DR.SLAA KTK POLITICAL ARENA.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom