Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,884
Nashukuru wana JF. Nchi ni yetu tushirikiane kuijenga.
Karibu Katibu Mkuu
Nashukuru wana JF. Nchi ni yetu tushirikiane kuijenga.
Sijui niseme jina langu?Shida hamta niamini.Ila naunga mkono siku moja tuseme majina yetu mtashtuka.Wengine mtapata heart attack.
anaitwa Mhshimiwa Dr Abeid Amani Karume.
Mheshimiwa Dr Wilbroad Slaa welcome onboard.
wrong.. even the british law is based from Canon Law. Canon Law is the foundation and basis of modern civil law. Unafikiri hicho kilatini cha kwenye sheria kinatoka wapi?
zitto,I know what you mean........... Nilishtuka siku moja nilipoambiwa na mkuu mmoja kuhusu post yangu dakika chache baada ya kupost..... JF inakua na itakua kama jukwaa la watanzania la kutoa maoni yao kwa uhuru kabisa
Ushauri wa kwanza kabisa kwa DK SLAA kama mkichukua nchi.
Mujaribu kuujenga mfumo wa UCHUMI kwa kuangalia mfano KAMA WA TAIFA LA JAPAN.
Ni mfumo wa UCHUMI wenye kuzingatia maslahi ya MJAPAN na si vinginevyo.
Ahsante.
Naomba niingili hapa mara moja.
a. Hakuna mwanachama ambaye atavushwa hapa kwa kuangalia jina lake au mchango wake mahali kwingine. Akija Kikwete, Salim, hata mmojawapo wa wa mitume watapanda daraja taratibu kama wengine walivyofanya. Hivyo hilo wazo la kurusha watu madaraja sidhani kama lina nafasi katika JF. Njia za kupata daraja ni pamoja na michango ya mtu, kuanzia ya mabandiko yake na ya kuiwezesha JF.
Dr. Slaa na wengine watapanda chati taratibu kwa kufuata njie ile ile waliyoifuata wengine. Hilo hata hivyo halina maana ya kumshusha hadhi au kumfanya duni bali ni kuonesha kuwa katika JF wanachama wote ni sawa.
Dr. Slaa amekuwa mwanachama hapa kwa muda mrefu na amekuwa akifuatilia kwa kina yanayosemwa hapa na sasa umefika wakati wa kujiunga tena rasmi. Note the word "tena". Alishajiunga hapa lakini alipoteza password yake na leo aliamua tu kujisajili upya.
b. Swali kwamba ni yeye hilo lisiwatie shaka na kuna watu wanaangalie nenno kama "nondo" jamani lugha hii wazee nayo wanayo. Nimewahi kumpigia simu Waziri Mmoja tuliposalimiana akaniambia mambo vipi nikasema "pouwa za huko" akaniambia "Pouwa tu". Sasa enzi zile ningeona anatumia neno la ajabu! Then akaja Bush.. guess aliwasiliamiaje watu "mambo!". Kwa hiyo, ameamua kuingia kwa jina lake ili kusiwe na utata wowote ule. Mojawapo ya vitu ambavyo tumekuwa tukivifanya ni kuona kuwa anapoingia mtu mwenye cheo fulani serikalini kwa jina lake tunacheki moja kwa moja na mtu huyo au wasaidizi wake wa karibu.
Miezi ka miwili iliyopita kuna mtu aliingia hapa na kujiandikisha kwa jina la Kikwete na kutoa speech moja ndefu sana. Mara moja tukazungumza na Ikulu (within minutes) na kukuta Rais alikuwa anauchapa usingizi na msaidizi wake akatuhakikishia kabisa aliyeandika siyo Rais na hakuna mtu aliyeidhinishwa kufanya hivyo. Well tukafuta na jamaa aliyeingia akafungiwa. So, kina invisible wanachukulia haya ya kutumia majina halisi very serious.
c. Kujiunga kwa Dr. Slaa rasmi ni mfano mwingine wa kuthubutu kwa viongozi wetu. JF siyo adui yao lakini ni mahali ambapo yote yanazungumzika. Dr. Slaa anajua kwa kutumia jina lake amejiweka kama swala kwenye mbuga iliyozungukwa na simba! Atapata personal attacks na vurugu mechi za kila aina. Hilo bila ya shaka litakuwa ni wimbi la kwanza na akisurvive basi sidhani kama kuna magumu mengine. Uamuzi wake uwe mfano kwa wabunge wengine kuungana nasi, wakijua wazi kuwa ni bora zaidi kuingia kwa majina ya kupachika kuliko majina halisi (ni distraction kubwa sana) kwani akimfokea mtu barabarani na mwana JF akikuona watakuandika humu! Ukionekana umeshikana mkono na mtu basi jina lako litatangaa. Ndio maana kutumia majina halisi kunapoteza sana hoja muhimu. Hata hivyo mtu akishapima pro and cons kwa upande wake binafsi basi afanye kila anachotaka. Hivyo tunawakaribisha wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu waidara n.k kuungana nasi kwani hapa ndiyo Jamii Forums.. where we dare talk openly!!! Hapendwi mtu, haogopwi mtu, na hapendelewi mtu.
Field Marshal ES,
Thanks a lot. Kimsingi, kinachotusukuma ni uzalendo kwa nchi yetu. Kwangu mimi siasa ya vyama inachukua namba ya mwisho. Kwanza sisi ni Watanzania, na watanzania wawe walalahoi kama wanavyoitwa, au wa ngazi ya juu sana (japo naamini binadamu wote sawa) wote wana mchango katika kuijenga, kuilinda na kuitetea nchi yao. Hakuna mwenye ukiritimba wala hati miliki ya nchi. Hivyo nadhani mchango wa kila mmoja nitauheshimu sana na utaheshimiwa na kila mmoja wetu. Ni kweli JF mimi si mgeni, hivyo kipya ni kujisajili upya. Thanks for the warm welcome.
Kuna mtu yeyote ana BIO ya DR Slaa,nataka kumjua huyu mpiganaji maana namsikia tuu!
...Slaa hii mbona unaipita bila jibu? tunataka kujua viongozi wetu!
Jamani Kumkaribisha Mtu Aliekuwepo Hapa Kwa Dahari Sio Fair .
Halafu Waje Watueleze Sababu Za Kumtimua Wangwe, Au Na Wao Ndio Vibaraka Wa Mbowe Fisadi
Nawashukuru kwa sasa najiandaa kwenda Bungeni. Nondo ziwe na ukweli tena ukweli mtupu ili tuweze kuwanusuru vijana hadi vitukuu vyetu.