Dr. Slaa aitolea nje serikali ya Tanzania

Wale woote wanaotumiwa na serikali yetu kama secret service wahakikishe wanafanya kazi yao kwa uangalifu na tahadhari ya hali ya juu sana kwani watakapofanya kosa la kiufundi wajue nao ndo mwisho wao. Hawa watu hawako makini kabisa kwanza hawafanikiwi mipango yao, lakini pia mipango yao ingundulika kabla ya utekelezaji na mambo yao yanaharibika katikati ya utekelezaji ama baaba ya utekelezaji usiokuwa na mafanikio.
 
mbona ninyi huwa mkitukana humu nanyi ni punguani? Mimi sioni mantiki ya Slaa kukataa kuhojiwa na kutaka polisi waende mahakani huko ndio akaseme, sasa hao polisi wataendaje mahakamani bila maelezo ya kufungulia mashtaka! Dr Slaa hana cha kuiogopa serikali ya JK na ni kweli serikali hii haina uwezo wa kumlazimisha, basi aende ili kuwasadikisha wafuasi wake kuwa alichosema ni kweli!

Tunamwamini 1000000009000%
Thats y tukamchagua.. Jamaa jembe na sio Dhaifu..
Kama c yeye leo KUCNGEKUAPO NA KUVUANA GAMBA.. Anajua n anafanya na mnaumia sana jamaa kuwa nje ya Mjengo... Pamoko Dr wa ukweli.....
 
THE GOVERNMENT CANNOT STAND ACCUSED FOR 'A CONTINUED PLANNED POLITICAL KILLINGS' AND AGAIN PRESENT ITSELF AS AN INVESTIGATOR AND THE JUDGE IN A CASE AGAINST HER OWN SELF!!

Ewe Ndugu CHAMA,

Kama ni kweli wewe ni Great Thinker mojawapo humu, na kwamba unajua kusoma na kuandika vema, basi sina neno zaidi kwako zaidi ya kukuelekeza kusoma upya na pengine kuendelea kupingana na NGUVU YA HOJA nilioikwishaitundika hapa ubaoni kama ifuatavyo ...

It beats logic and common sense for anybody to expect Dr Slaa to present himself for an interogation by the NOW POLITICALLY SCANDALOUS ARMED FORCES that are widely believed to be on the loose in KILLING THE CITIZENS of dissenting voices throughout the country.

Many heinious killings by police in the country to-date are still fresh in everyone's mind yet nothing is being done to bring people to justice apart from shear concerted efforts by the authorities to undertake state cover-up on everything.

Kimsingi, serikali kamwe haiwezi ikasimama kuwa Mpelelezi katika shutuma nzito kama hii dhidi yake. Ikitokea hali kama hiyo basi itakua ni jambo la ki-historia ajabu AND ONLY IN TANZANIA.

The next best thing that the scandal-ridden Kikwete government can at least do at this point is to let the same authority of the COMMANDER-IN-CHIEF OF THE ARMED FORCES, if any in our country, to revoke his illegal orders on a cross-section of the forces to kill, by guaranteeing a 24-hour safety and security of all CHADEMA leaders already in threat.

Anything lest of a 24-hour guaranteed safety and security of the CHADEMA threatened leaders, in my humble opinion,
is nothing but a TICKING BOMB yet to explode in the face of the much oppressing minority and desolate and most desparate Kikwete government the moment the youths chose to step in to defend and protect their CHADEMA leaders.

Ewe ndugu Uwezo Tunao
For not supporting Chadema does not means that I can`t use my common sense to express my views; If your leaders does not trust the Government the best option they have is to seek temporary asylum; the police and other machinery works for the interest of the country; the police have proved you wrong in many occasions; just give me the data showing how many people have been killed by police; let the police do their job all you need is support their efforts to maintain peace and harmony in our country.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
mmmmmmmmmmmm
Acha kuweweseka wewe, tangu ahojiwe walipokuta vinasa sauti kwenye kitanda chake akiwa mbunge kuna taarifa gani hilo jeshi la polisi limetoa? Atahojiwa vipi na majambazi hao hao wanaotaka kumtoa roho! Hata huhitaji elimu kubwa kujua polisi wetu wanatumiwa na ccm
 
mkuu, hapa inaonesha dr atakataaa kataaaa! ila lazma ataenda kuojiwa kwa njia yoyote ile! au unaonaje?
Yaah, na mimi naamini hivyo, lakini katika hilo polisi hawatashindwa kumkamata kwa nguvu na kumpeleka kituoni akatoe maelezo. Maana hawawezi kupeleka kesi mahakamani bila kuwa na maelezo yake. Ndiyo maana nasema namna nzuri ya kulimaliza hili ilikuwa ni serikali kunyamaza kimya, lakini kitendo cha kuanza kutunishiana misuli litaiweka serikali pabaya sana. Maana wakimkamata, wanaweza kusababisha machafuko, na wakimwacha wataonekana ni kweli walitaka kuwaua viongozi wa CHADEMA. Mmh, patamu hapo!
 
mchumba wake alipovamiwa na majambazi na risasi kurindima ni polisi hao hao waliofanya juhudi za kuwasaka na hatimaye kunaswa na mchumbawe akaitwa kuwatambua na aliwatambua...... leo hii hana imani nao...!!!! SIASA MCHEZO MCHAFU!!!
 
Yaah, na mimi naamini hivyo, lakini katika hilo polisi hawatashindwa kumkamata kwa nguvu na kumpeleka kituoni akatoe maelezo. Maana hawawezi kupeleka kesi mahakamani bila kuwa na maelezo yake. Ndiyo maana nasema namna nzuri ya kulimaliza hili ilikuwa ni serikali kunyamaza kimya, lakini kitendo cha kuanza kutunishiana misuli litaiweka serikali pabaya sana. Maana wakimkamata, wanaweza kusababisha machafuko, na wakimwacha wataonekana ni kweli walitaka kuwaua viongozi wa CHADEMA. Mmh, patamu hapo!

mkuu, ntakupa mchele fulani kwenye private msg!
 
Dr Slaa yupo sahihi kabisa kwenye hili. Kitendo cha nchimbi akiwa kama waziri mwenye dhamana ya jeshi la polisi kwenda kwenye TV na kuanza kuanzisha political spin, kuwa hata CDM walizushiwa kumuua Chacha Wangwe ila wao hawakukurupuka kama serikali kuchukulia umaarufu uvumi huo inaonesha wazi kuwa ajenda na kutaka mahojiano ni ya kisiasa zaidi ya kiusalama wa walitishiwa.

Jeshi la polisi limeendelea kutumia kutumika kama rungu la kisiasa badala ya kuwa chombo cha usalama wa raia. Mahojiano hayo ya kuyalazimisha waziri kupitia TBC ni void. Kama kweli jeshi la polisi lipo kama chombo cha usalama wa raia halihitaji mwanasiasa mwenye tope zito la tuhuma mbaya dhidi ya wapinzani wake kisiasa kulisemea. Ilikuwa ni wajibu wa jeshi kuwatafuta na kuwahoji bila ya amri ya Nchimbi.
 
Slaa akiwa rais fukuza askari wote wa jeshi la polisi (Makofi ..)

Slaa akiwa rais fukuza askari wote jeshi la wananchi hawafawi wanampendela rais JK (makofi...)

Slaa akiwa rais fukuza usalama wa taifa wote (TISS) hawafai wanaipendelea ccm na JK (makofi..)

Slaa wewe kiboko aisee unawaamini wale askari wa magwanda tu wenye miwani kama wauza unga..
 
mchumba wake alipovamiwa na majambazi na risasi kurindima ni polisi hao hao waliofanya juhudi za kuwasaka na hatimaye kunaswa na mchumbawe akaitwa kuwatambua na aliwatambua...... leo hii hana imani nao...!!!! SIASA MCHEZO MCHAFU!!!
Mkuu mbona una akili za mende? Waliompora mama Slaa walikuwa vibaka au majambazi na sasa wanaotaka kumuua sasa hivi ni Polisi wenyewe + TISS. Vipi uwe na imani ya ishu yako kuchunguzwa na mtu unayemtuhumu?
 

dk-slaa-safitop.jpg
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa​
Fredy Azzah na Fidelis Butahe
KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema hawezi kujipeleka polisi kuhojiwa kutokana na kauli yake kwamba yeye na viongozi wengine wawili wa chama hicho wanatishiwa kuuawa na kigogo mmoja wa Idara ya Usalama wa Taifa, huku akieleza sababu mbili za kugomea wito huo wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi.Juzi, Dk Nchimbi aliliagiza Jeshi la Polisi kuwahoji viongozi wote wa Chadema waliotoa tuhuma za kutaka kuuawa hata kama wao hawana imani na jeshi hilo.

Akizungumzia na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Dk Slaa alisema yeye na wenzake, Mbunge wa Ubunge, John Mnyika na Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema hawatakwenda polisi kuhojiwa na jeshi hilo likitaka liwakamate.

Alilishauri jeshi hilo kutumia njia zake za kiitelijensia kujua ukweli wa mambo badala ya kufikiri kwamba wanaweza kupata maelezo kuhusu suala hilo kutoka kwake au viongozi wengine wa chama hicho.
“Leo (jana) asubuhi Ofisa wa Makao Makuu ya Polisi amenipigia simu kuomba appointment (miadi) lakini nasema sina muda. Sisi hatuendi (polisi) kwa sababu walishatudanganya mara nyingi tu.

Kama wanataka watukamate. Wao wana wapelelezi na usalama wachunguze,” alisema Dk Slaa na kuongeza:
“Kwani wao wanavyotukataza kufanya mikutano wakisema wana taarifa za kiitelijensia, huwa tunawauliza ni nani kawaambia? Na wao wachunguze kwa vyombo vyao kwa sababu ni jukumu lao kulinda usalama wa wananchi .”

Sababu za kutoamini polisi

Dk Slaa alisema sababu ya kutokuwa na imani na polisi ni pamoja na kutomweleza mpaka leo, vilipo vinasa sauti walivyovichukua katika hoteli aliyokuwa akiishi mjini Dodoma... “Walivichukua vile vinasa sauti na hawakutuambia ni nini kilichokuwa ndani, wangetupa tupeleke kwa wataalamu tukavichunguze.”

Alisema sababu nyingine ni tukio la kupigwa kwa wabunge wa chama chake mkoani Mwanza, akidai kwamba licha ya polisi kupewa taarifa mapema, hawakuchukua hatua yoyote.

Kutokana na hayo, alisema haoni sababu ya kuhojiwa na polisi kwani viongozi wa chama hicho kwa muda mrefu wamekuwa wakieleza mambo mbalimbali yanayotishia usalama wa wananchi na nchi, lakini jeshi hilo limeshindwa kuyafanyia kazi.

“Sasa kama wameshindwa hayo sasa wanataka kutuhoji kwa lipi? Hatuendi sisi tumeshawaeleza kinachoendelea kazi ni kwao,” alisema Dk Slaa.
Alisema taarifa walizozipata juzi ni kwamba maofisa wa jeshi hilo walikaa kikao muda mfupi baada ya kusikia tuhuma zilizotolewa na chama hicho na kuongeza kwamba wanachokisubiri hivi sasa ni kukamatwa.

Alidai kuwa jeshi hilo linaendelea kufanya makosa huku likitambua wazi kuwa maisha ya Watanzania yapo hatarini.

“Ndiyo maana, madaktari wameomba Umoja wa Mataifa (UN), kumwekea ulinzi Dk Steven Ulimboka katika hospitali aliyolazwa, hii yote ni ishara kwamba hali si shwari,” alisema Dk Slaa.
Alisema kazi ya polisi ni kutekeleza wajibu wao mara baada ya wananchi kutoa taarifa zinazohitaji kufanyiwa uchunguzi.

“Chadema ni chama makini, tunajua kuwa polisi walifanya kikao, wanatakiwa kujua kuwa nyumba yao inavuja… sasa kama nyumba yao inavuja sisi hatuoni haja ya kwenda kuhojiwa. Tunamuomba Mungu na tunajua atatulinda na wao acha waendelee kufanya vikao vyao.”

Operesheni Sangara kuendelea

Katika hatua nyingine, Chama hicho kimeanza sehemu ya pili ya Operesheni Sangara baada ya kufanya hivyo katika Mikoa ya Morogoro, Iringa, Singida, Dodoma na Manyara.

Dk Slaa alisema jana kwamba katika operesheni hiyo inayotarajiwa kuanza wiki ijayo, watapita katika majimbo 44, kata 406 na vijiji 4,000.
Alisema katika operesheni hiyo, watawatumia wabunge wao, viongozi wa halmashauri kuu na makada wake wengine.
Dk Slaa amvimbia Waziri Nchimbi
 
Back
Top Bottom