MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 705
Naunga mkono hoja. Kieleweke kwamba, si Kikwete anayepingwa na kususiwa, ila ni mfumo mbovu wa utawala dhalili, usiojali misingi ya usawa, haki na demokrasia, bali unaotetea na kuendeleza maslahi ya watu wachache! Katika hili, tukikumbuka kwamba TANZANIA NI YA WATANZANIA WOTE, hatuwezi kuwa vipofu au kujifanya kama mbuni, akifukia kichwa chake ardhini na kuacha mwili wake nje, akidhani yuko salama. Kuendelea kufanya hivi ni kukaribisha vita na upotevu wa amani hapa nchini. Bado HATUJAJIFUNZA kutoka kwa majirani zetu wa karibu na wa mbali?
Sasa tuelekeze nguvu zetu katika mabadiliko yatakayoleta uwiano sawia, kwa Watanzania wote, bila kujali itikadi, dini, rangi wala kabila, kwani hii ndiyo misingi aliyoijenga Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, alipotuasia kwamba Umoja ni Nguvu!
Tunapoteza umoja, tunapoteza uzalendo. Ni wangapi kati yenu wanaofikiria, hata kwa siku moja tu, suala lolote la kutatua matatizo ya nchi? Kwa mfano, Jijini Dar es Salaam, asilimia 70 ya wakazi wanaishi kwenye asilimia 70 hadi 80 ya maeneo ambayo YAMETHIBITIKA kuwa HAYAFAI KWA MAKAZI NA MATUMIZI ya binadam! Lakini bado tunasema CCM imetuletea maendeleo, na inapaswa kuungwa mkono! Ndani ya Jiji la Dar bado kuna maeneo - HATA KARIAKOO - ambapo kuna zile nyumba za tembe, yaani, "nyumba za mbavu za mbwa", ambazo watu wamejenga kwa miti na kukandika kwa udongo! Katika Karne Hii, hiki ni sawa kweli? Kwa nini tuwe na umaskini wa kutisha namna hii, ilhali Tanzania inahesabika kuwa NCHI YA TANO DUNIANI kwa uzalishaji wa DHAHABU?
Panapofuka moshi, pana moto. Lisemwalo lipo, kama halipo, LAJA! Anayekutahadharisha anakusaidia kutambua lililopo mbele yako, au linalokunyemelea. Na ukiona mwenzio ananyolewa, tia maji kichwani.
KANU ilitamka kwa kibri kikubwa, kwamba ingeitawala Kenya milele! Leo hii, KANU ni chama cha UPINZANI! Wananchi wakielimishwa, wanao uwezo wa KUIONDOA CCM MADARAKANI! Sisi wa CHADEMA tutawaelimisha ili kuwaamsha usingizini. Kama imeshindikana leo, 2015 tutaweza!
Mpaka Kieleweke!
A Luta Continua!
-> Mwana wa Haki
P.S. Nieleweke kwamba namtambua Rais Kikwete kama rafiki yangu, ndugu yangu na KAKA yangu. Ninamfahamu, ninamheshimu, yeye kama yeye, lakini sikubali misingi ya utawala anayoitetea na kuilinda. Sina chuki naye, ni ndugu yangu. Tukubali kutofautiana. Siwezi kumchukia binadam yeyote hapa duniani, lakini nina haki ya KUPINGA na kutofautiana na yale anayoyasimamia na kuyatetea. Haki ya Kupinga bila Kufanya Vurugu (Non-Violent Protest) ni haki ya msingi kabisa ya kila binadam. Wabunge wa CHADEMA wasilaumiwe kwa yale waliyoyafanya! Wanawawakilisha WATANZANIA WOTE, walio wanachama na wasio wanachama wa CHADEMA au wa chama chochote kile cha siasa. Ukishakuwa Mbunge, wewe ni mwakilishi wa Watanzania wote, bila kujali kama alikupigia kura au la, na bila kujali chama chake, itikadi yake, dini yake, rangi wala kabila, na bila kujali iwapo ni mkazi wa jimbo lako ama la! HIYO NDIYO MAANA SAHIHI ya kuwa Mbunge!