DR Slaa aeleza sababu ya CHADEMA kususa

Ubovu wa mfumo anauogelea Dr. Slaa huu hapa:
Rais anamteua mwenyekiti wa tume ya uchaguzi; na akishafanya hivyo hakuna chombo chochote huru kinachoweza kuhoji sababu za kumteua au vigezo alivyotumia kumteua! Hapa inaonekana wazi rais anamteua mtu kwa urafiki tu - na haipingiki mahakamani - period.
Uchaguzi ukishafanyika, mwenyekiti huyo wa tume akishatangaza kuwa fulani ndiye kashinda hakuna chombo chochote kinachoweza kuhoji uhalali wa matokeo hayo na hayawezi kupingwa hata mahakamani- period.
Ni wazi basi kuwa watu hawa wawili (au taasisi hizi mbili - serikali na tume ya uchaguzi) sheria imewatengenezea mazingira ya urafiki mbaya. Nakuteua uwe mwenyekiti wa tume na wewe baadaye nitangaze kuwa nimeshinda (na hakuna wa kuhoji hata mahakama).
Ni mazingira haya yaliyoifanya tume ishindwe kusikiliza hoja za Chadema.
Hivi kama kweli JK alikuwa na uhakika kuwa ameshinda, kwanini tume isingesikiliza malalamiko ya Chadema na kuiumbua kuwa inasema uongo.
Mazingira haya ya urafiki wa tume na rais ndiyo yalisababisha kenya ikaingia kwenye machafuko. Kumbuka Kibaki alivyotangazwa na haraha haraka akaapishwa!
Haijalishi wewe ni CCM au Chadema - tunapaswa kudai mfumo huru, siyo tung'ang'anie mfumo mbovu ati kwa sababu tu unatuhakikishia kuwa madarakani.
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE
 
Huu siyo upuuzi tu bali pia ni UJINGA mtupu. Wako baadhi ya watu ndani ya CHADEMA ambao wana mwelekeo wa uhaini. Wabunge wa CHADEMA kususia hotuba ya JK ni kielelezo cha upungufu na ufinyu wa mawazo na fikra na pia kukosa heshima kwa RAIS na jamii nzima. Wanachojaribu kufanya CHADEMA ni kuchochea uasi dhidi ya RAIS na mamlaka. Wanataka ionekane kuwa Tanzania haitawaliki. CHADEMA wamekosea mno. It is a political blunder. It is the beggining of CHADEMA's demise. Definetly watanzania walio wengi hawawezi kukubaliana na upuuzi wa CHADEMA. Come 2015 CHADEMA will never get more than five seats in the parliament. Unasusia hotuba wakati unatembelea gari la serikali ya JK, unapata posho inayotolewa na serikali ya JK; unapiga kura kwa jina la Waziri Mkuu lililoteuliwa na JK. ama huu siyo upuuzi na ujinga ni nini basi?
 
Ebo kwanini Wabunge wanaweza kupingwa mahakamani na raisi asiweze kupingwa mahakamani,hayo ndio mapungufu,kuna hatari tume kuja kutangaza FISADI kuwa raisi na wananchi tukaishia kutawaliwa na FISADI
Mfianchi pole sana,hivi bado hujui kuwa huyu aliyepo ni FISADI pia? Kwa tume hii na kwa katiba hii,bado itaendelea kula kwetu kwa muda mrefu sana.
 
Umefika wakati tutambuwe kuwa haki yawezwa kutafutwa kwa njia nyingi tu,na nadhani wabunge wa chadema wamefikisha ujumbe waliotaka ufike,sasa ni swala la rais kutilia maanani ama not,tuelewe kuwa hizi si zama za ndiyo kwa kila kitu kama @dsm anavyofikilia,kuna ya kusema ndiyo na kuna yakusema sio,tuwaache chadema watumie haki yao kikatiba,na mimi nawaamini chadema kwani %kubwa ni wasomi na wanaupeo wa kuona mbali hivyo kila jambo wanalolifanya linamaana sana bwana@dsm
mapinduziiiiii daimaaaaa
 
Sipati picha ni aje maraisi wastaaafu wanavyo mshangaaa...huyu bwana(Kikwete) ambayo wanamcheka katika uongozi wake...pengine walimshauri kistaarabu zaidi kwa lugha anayo elewa katika miaka ya mwanzoni...kwa kutokuwa na hekima na kuchambua na kuweka kila
jambo pahala pake akawaweke viongozi anao waona wanafaaa..mwisho wa siku tanzania inashuhudia mambo ambayo haikuwahi kuyaota.

Fadhila kwa weliomuweka madarakani...dah..maisha haya..huyu bwana kama hataki CCM Imfie mikononi..lazima katika miaka yake mitano hii afanye juhudi kubwa sna.
 
TRUTH,labda utueleze vizuri kwanini unasema hii ni bad move,kisha pia utuambie ipi ni good move na sio kuja kutushibisha upuuuzi wako.kama ww unafaidika na ccm unatakiwa uwaconvice watu kwa nguvu ya hoja na sio hoja ya nguvu,kama ulivyofanya hapo,au pengine huelewi,harakati za kisiasa.shame on u TRUTH................
 
Bwana Vumbi mbona kichwa cha habari yako"DR Slaa aeleza sababu ya CHADEMA kususa" hakiendani na maelezo uliyoyatoa?????. Acha kuwatimulia VUMBI wa JF

haaa! Usiniambie hujaelewa sababu hapo.
Au ulitaka aandike;
sababu ya kwanza.....
Sababu ya pili.......

Sababu ya mwisho......
Nimemaliza.
 
Huu siyo upuuzi tu bali pia ni UJINGA mtupu. Wako baadhi ya watu ndani ya CHADEMA ambao wana mwelekeo wa uhaini. Wabunge wa CHADEMA kususia hotuba ya JK ni kielelezo cha upungufu na ufinyu wa mawazo na fikra na pia kukosa heshima kwa RAIS na jamii nzima. Wanachojaribu kufanya CHADEMA ni kuchochea uasi dhidi ya RAIS na mamlaka. Wanataka ionekane kuwa Tanzania haitawaliki. CHADEMA wamekosea mno. It is a political blunder. It is the beggining of CHADEMA's demise. Definetly watanzania walio wengi hawawezi kukubaliana na upuuzi wa CHADEMA. Come 2015 CHADEMA will never get more than five seats in the parliament. Unasusia hotuba wakati unatembelea gari la serikali ya JK, unapata posho inayotolewa na serikali ya JK; unapiga kura kwa jina la Waziri Mkuu lililoteuliwa na JK. ama huu siyo upuuzi na ujinga ni nini basi?

Umesoma na kuelewa maelezo ya Dr.Silaa au umekuja na mawazo yako asubuhi hii...ukiwa umeandika kwenye word without ku reffer Dr.silaa na kumwelewa kwa undani uka paste na kuondoka kuelekea kwenye mishughuliko yako?
 
Huu siyo upuuzi tu bali pia ni UJINGA mtupu. Wako baadhi ya watu ndani ya CHADEMA ambao wana mwelekeo wa uhaini. Wabunge wa CHADEMA kususia hotuba ya JK ni kielelezo cha upungufu na ufinyu wa mawazo na fikra na pia kukosa heshima kwa RAIS na jamii nzima. Wanachojaribu kufanya CHADEMA ni kuchochea uasi dhidi ya RAIS na mamlaka. Wanataka ionekane kuwa Tanzania haitawaliki. CHADEMA wamekosea mno. It is a political blunder. It is the beggining of CHADEMA's demise. Definetly watanzania walio wengi hawawezi kukubaliana na upuuzi wa CHADEMA. Come 2015 CHADEMA will never get more than five seats in the parliament. Unasusia hotuba wakati unatembelea gari la serikali ya JK, unapata posho inayotolewa na serikali ya JK; unapiga kura kwa jina la Waziri Mkuu lililoteuliwa na JK. ama huu siyo upuuzi na ujinga ni nini basi?

Hivi watu wengine hua mnasoma ujumbe na kumengenya yaliyomo kweli? manake tukiwa na mitazamo kama ya kwako hatutafika tunapotaka kwenda. nasikitika kama mtu unayeweza kutumia intaneti unaangalia mambo katika mtazamo finyu namna hii sijui kama tutaendelea nchi hii..:A S angry:
 
Watu wengine uelewa wao no mdogo sana au wananufaika sana na mifumo hii mibovu ambayo sisi waTZ wengi tumekuwa tukiyalalamikia.

Usifikiri waTZ ni wajinga 2015 ndo mwaka wa kuwamwaga CCM na nyinyi mafisadi kama ambavyo tumefanya kwa baadhi yao mwaka huu.

Dr. Slaa na Chadema wapo sahihi na tupo nao pamoja sisi wananchi tulio wengi.

Peoples power
 
Dar es Salaam kwa nampongeza kwa upeo wake ndogo na ndiyo maana watanzania tunapata shida kwa akili kama zake. Dr. Slaa alichosema ni ujumbe ambao wabunge wa chadema wamepeleka kwa jumuiya za kimataifa kujua nini kiliendelea wakati wa uchaguzi sasa kama dar es Salaam anaona ni upuuzi yeye ndiye mpuuzi zaidi
 
Kwani kuna tofauti gani na nchi zenye wafalme,huku tukijidanganya kuwa tuna demokrasia.Nawapongeza sana CHADEMA kwa kitendo chao cha kizalendo walichokifanya.Mbona hutaki kufikiri zaidi,kwa ukweli ni kuwa nchi hii inaongozwa kifalme na mfalme huyo ni Tume ya Uchaguzi ambayo haihojiwi wala kuulizwa kwa aliyetangazwa.Huu ni upuuzi,tena mkubwa.Wasomi,viongozi wa dini na wanadplomasia hebu jaribuni kufikiri juu ya uhuni huu unaofanywa na tume ya uchaguzi tanzania.
Hii ni laana na itakuwa kwenye historia juu ya Watanzania wenzetu kututawala bila idhini yetu.Tume ya Uchaguzi ni akina Chief Mangungo na Kimweri walioiuza nchi kwa mikufu ya shaba.Tume hawana tofauti na Yuda Iskariote aliyepokea vipande thelathini vya fedha ili kumuuza Yesu.
Hakika Tume ya Uchaguzi historia itawahukumu.Shame on you!!!!
 
Huu siyo upuuzi tu bali pia ni UJINGA mtupu. Wako baadhi ya watu ndani ya CHADEMA ambao wana mwelekeo wa uhaini. Wabunge wa CHADEMA kususia hotuba ya JK ni kielelezo cha upungufu na ufinyu wa mawazo na fikra na pia kukosa heshima kwa RAIS na jamii nzima. Wanachojaribu kufanya CHADEMA ni kuchochea uasi dhidi ya RAIS na mamlaka. Wanataka ionekane kuwa Tanzania haitawaliki. CHADEMA wamekosea mno. It is a political blunder. It is the beggining of CHADEMA's demise. Definetly watanzania walio wengi hawawezi kukubaliana na upuuzi wa CHADEMA. Come 2015 CHADEMA will never get more than five seats in the parliament. Unasusia hotuba wakati unatembelea gari la serikali ya JK, unapata posho inayotolewa na serikali ya JK; unapiga kura kwa jina la Waziri Mkuu lililoteuliwa na JK. ama huu siyo upuuzi na ujinga ni nini basi?
Wewe acha upuuzi toka lini mwizi akaheshimiwa? Kama ccm mmezoe kuwaheshimu wezi na mafidi hukohuko, usituletee maTZ habari hiyo. Wabunge wamwchaguliwa kutetea maslahi ya waTanzania wote, na walioibiwa kura ni wa TZ hivyo mbunge yoyote makini lazima asimame na kutetea haki hiyo. Huu sio wakati wa kunyenyekea kinafiki, posho na gari ni za jasho la waTZ walioibiwa kura zao na sio jk. Tutaendelea mpaka lini kuwaangalia na kuwapigia makofi watu wanaoidhalilisha demokrasia kama jk, lewis makame na kiravu na cuf. Viva wakombozi!!
 
Those against CHADEMA
remember ur words n write somewhere you to remind urself in 2015 that u r a fake prophets much like sheik yahya. Never undermine Tanzanians,they ar neither,or, sober! Ts high time to practise reality and set aside hypocritic elements. Escape from vandalism,now we gonna get Tanzanian Independence after 1961 given to Tanganyika,remember Tanzania as Tanzania has no independence,only Tanganyika and Zbar are independent and now Dr.Slaa needs independence for Tanzania,with him my hand shall be stretched to pull our Independence from black colonialist. Once in life British Prime Minister in South Africa addressed the then S.A white regime that "Africans are silly,you give them guns they kill each other" this is what happens in bongoland!
 
Hello wana JF

Huu msimamo wa CHADEMA na viongozi wake na WABUNGE wetu unafaa na kustahili KUUNGWA MKONO kwa gharama yeyote ile na watu wote. Ni lazima tuwakubali na kuwatia moyo. Tuwaunge mkono katika mchakato huu wa kupigania haki na demokrasia. Natambua ni mchakato na siyo kitu cha siku moja.

Haki haiji kirahisi.......Ni lazima watu wenye kuthubutu, wenye mwamko na utayari, wenye kujitolea wajitokeze katika harakati za kupigania haki na demokrasia ambayo kwayo maendeleo ya kweli ya kijamii, kiuchumi na hata kisiasa hupatikana. Nathubutu kusema hakuna maendeleo pasipokuwepo na haki na demokrasia. Hakuna kuheshimiana paipkuwepo na haki na demokrasia.

Ni lazima tupiganie haki na demokrasi sahihi ili tuweze kuboresha taasisi zetu za kusimamia haki. Hatuwezi kuwapata viongozi bora na wenye vision thabiti pasipokuwepo na haki na demikrasia na tena hatuwezi kuwawajibisha viongozi wetu hata pale wanapovunja mkataba wa kazi tuliowapa, mfano kwenda kinyume au kuvunja na katiba........Narudia kusema ya kuwa haki na demokrasia haiji kirahisi, watawala hawatakubali kukuwekea mezani uchukue kirahisi. Historia inaonesha kuwa mara zote hupiganiwa. Si lazima sana kutumia ncha ya upanga kwani si jadi yetu tangu enzi za kupigania uhuru wa nchi yetu, lakini ni muhimu tutumie umoja na mshikamano wetu kama watanzani bila kujali vyama na itikadi zetu, dini zetu, ukabila wetu na tofauti yeyote ile ili kuleta haki na demokrasia iliyo ya kweli. Anyimae haki, uhuru na demokrasia kwa watu wake anaowatawala hakika huyo anafanya kazi ya mwovu shetani na ni lazima kama taifa kwa umoja wetu tuungane na kudai hii tunu iliyo bora.

Nikirudia katika hoja ya msingi napenda niwaunge mkono WABUNGE wetu wa CHADEMA kwa uamuzi ambao hakika ni wa kijasiri. Ni lazima tuwatie moyo na tuwaunge mkono. Sisi wananchi tuko nyuma nyao katika mapambano haya. Na mimi nina hakika tukiwa wa kweli na kusimamia haya yote kwa umoja wetu watoto wa wajukuu zetu watatukumbuaka tena watatuombea kheri huko akhera..........

Nawasilisha.......daima idumu JF
 
Hivi watu wengine hua mnasoma ujumbe na kumengenya yaliyomo kweli? manake tukiwa na mitazamo kama ya kwako hatutafika tunapotaka kwenda. nasikitika kama mtu unayeweza kutumia intaneti unaangalia mambo katika mtazamo finyu namna hii sijui kama tutaendelea nchi hii..:A S angry:

Usipoteze muda wako kujadili mambo muhumu na mtu mjinga,kwani kufanya hivyo ni kujizalilisha na wewe mwenyewe!!
 
Back
Top Bottom