mambomengi
JF-Expert Member
- May 16, 2009
- 829
- 242
Chenye matatizo hapa ni Katiba. Kama sheria ya nchi inatafsiriwa kuwa Tume ya Uchaguzi ikiishatangaza mshindi hakuna atakayeweza kuhoji matokeo yake, tunapoteza muda kumtafuta Makame & Kiravu Co. Ltd. Jamani, basi sheria ingetupa mwanya hata kuwaburuza hawa akina Makame kwa Pilato walau watimuliwe kazi zao.
Suala zima la kujumuisha kura lilienda kombo. Sidhani hio "program" wanayosema ilisababisha kompyuta ku-crash ni kweli. Jamani, kura hizo zinaingizwa kwenye spreadsheet, sasa watuambie walikuwa wanatumia programu ipi? Ingekuwa tunapiga kura kwenye kompyuta ningeweza kukubali kidogo kisingizio cha ku-crash. Nafikiri wanatudanganya wanafikiri watanzania hatujui kompyuta inavyofanya kazi.
Dr. Slaa tunakuomba uweke ushahidi wako wote hadharani na kopi zake uwape nchi marafiki na wahisani wajue pesa wanazotupa tunazitumia vipi.
Huu ni wakati wa kuambiana ukweli na wala sio wakubaki nyuma na kulalama. Dr. Slaa inabidi uelewe kuwa hata yale yalioitwa matokeo rasmi waliyoyatangaza haya-kubalance. Yaani namba za kujumlisha na kugawanya kuweka asilimia, ziligoma.
Kama huwezi kuvipeleka Mahakamani, tumwagie hapa vielelezo vyako vyote, na sisi tutakuwa Mahakama .