Dr Shein amtimua kazi Waziri Himid!

naona tumekluwa na rais wa kuhudhuria dhifa za kitaifa ugenini kila wiki as if nyumbani ugali hakuna, simtofautishi na mtoto mdogo anayekataa kurudi kwao ili mradi kaona kwa jirani kuna chakula kitamu anachokipenda kimepikwa, hivyo hulazimika kusubiri hadi wapakue

mkuu, hasa hasa wali maharage.
 
Wanaposema wanataka muungano wa mkataba wanakusudia nini? niliposoma gazeti la nipashe juu ya hoja hii ya muungano wa mkataba nilitamani jussa angekuwa ametoa maelezo ya namna ya huo muungano wa mkataba wanaoutaka.

Kwa kweli binafsi sielewi wanamaanisha nini wanaposema wanataka muungano wa mkataba, kwa akili ya kawaida nadahani kwamba muungano wowote ule lazima unakuwa ni mkataba.
 
Kama wazenj wamechoka na neema toka bara si muwaache wende zao? Nadhani Shein analijua hili. Hataki hawa wanaopiga kelele baadaye wamsumbue wakilia lia baada ya kupata kitu tofauti na walivyodanganywa baada ya muungano kuvunjika. Watu wengine hata hawafikirii vizuri. Hivi zenj bado haioni inavyobebwa kwa kipande cha ardhi kisicholingana na hata wilaya ya kibaha kupewa hadhi ya nchi?
mkuu Wacha kutukana nchi ya watu zenj,zenj ilikuepo zaid yamiaka 500 iliyopita,unaposema kipande cha ardhi wakati nyerere alimhadaa karume akamdanganya atapinduliwa akaunganisha zenj na tanganyika upohapo?
 
Huyu Jussa kabanwa na Warioba jana aseme Muungano wa katiba maana yake nii na atoe angalao mfano mmoja akashindwa.

Jussa namuona kama Bogus ambaye anajifanya anajua sana wakati mweupeeee, huyu ukaribu wake na Maalim seif ni janga kwa CUF, watamkumbuka Hamad Rashid siku moja hawa watu
 
Duu, mkuu hapo umeua.

Mkuu inaniumaga ujue, mtu simply kumbeba tu anapewa uwaziri bila wizara maalum, anapata stahili zote kama waziri na hizo ni kodi zetu tunaoamka saa kumi kukwepa foleni ambazo si za kuisha leo wala kesho!
 
naona tumekluwa na rais wa kuhudhuria dhifa za kitaifa ugenini kila wiki as if nyumbani ugali hakuna, simtofautishi na mtoto mdogo anayekataa kurudi kwao ili mradi kaona kwa jirani kuna chakula kitamu anachokipenda kimepikwa, hivyo hulazimika kusubiri hadi wapakue

Ndugu yangu wazanzibar lao moja huyo sheni atashindwa karibuni hivi,yeye lazima atafanya hivyo tu kujaribu kuzuia na kuwafurahisha watanganyika waliompa urais .

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
I hope it is true kwani mkala yangu ya mwishi ilimtaja Shein kuwa Anawaendekeza. Wakitaka muungano wa mkataba watoker ccm na cuf kwanza halafu waanze harakati za kudai uhuru. Lazima afuatie mwanasheria mkuu wa Zanzibar naye.

Ni kweli.

Shein afanya mabadiliko katika Baraza la Mapinduzi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt Ali Mohammed Shein amefanya mabadiliko katika Baraza la Mapinduzi. Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Abdulhamid Yahya Mzee imesema katika mabadiliko hayo, Rais Dkt Shein amemteua Shawana Bukheti Hassan kuwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi.

Rais Dkt Shein amefuta uteuzi wa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi, Mansoor Yussuf Himid.

Katika uteuzi mwengine Dkt Shein amewateua Mtumwa Kheir Mbarak kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Maliasili na Mohammed Said Mohamed kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi. Katika hatua nyengine, Rais Dkt Shein amefanya mabadiliko ya baadhi ya Makatibu Wakuu katika Wizara za Miundombinu na Mawasiliano, Wizara ya Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati.

Dkt. Juma Malik Akili ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano akichukua nafasi ya Dkt. Vuai Idd Lila atapangiwa kazi nyengine. Ali Khalil Mirza ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati.
Kabla ya uteuzi huo, Mirza alikuwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar,aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Mwalimu Ali Mwalimu atapangiwa kazi nyengine.

Taarifa ya Ikulu imesema pia Rais Dkt Shein amemteua Tahir M. Abdulla kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Msanif Haji Mussa atapangiwa kazi nyengine.
Uteuzi mwengine ni Mustafa Aboud Jumbe ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo alikuwa Tahir M Abdulla ambaye amehamishiwa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano.

Rais Dkt Shein ameteua CDR Julius Nalim Maziku kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kapteni Juma Abdulla Juma ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar hivi karibuni.

Uteuzi mwengine ni Juma Ameir Hafidh ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais(Fedha,Uchumi na Mipango ya Maendeleo) ambaye amechukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Abdi Khamis Faki aliyeteuliwa kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar.

Aidha, aliyepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar, Saleh Ramadhan Ferouz ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar ambaye anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Ali Khalil Mirza aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Makaazi,Maji na Nishati.

Pia Rais Dk Shein amemteua Mussa Haji Ali kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu uchumi Zanzibar. Uteuzi huo wote unaanza Oktoba 15 mwaka 2012.
 
Nadhani watu wataanza kuelewa Jussa alichokiongea kwenye interview ya CNN, inside afrika, nimepost hapa asubuhi, jamaa anasema zanzibar huru wanaodai ni ccm, pamoja na cuf, so najua Jussa alukuwa anaelewa kuna namba kubwa tu ya wana ccm zanzibar wanaunga mkono ili, so siyo huyo mmoja tu wapo wengi.
 
Ni kweli.

Shein afanya mabadiliko katika Baraza la Mapinduzi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt Ali Mohammed Shein amefanya mabadiliko katika Baraza la Mapinduzi. Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Abdulhamid Yahya Mzee imesema katika mabadiliko hayo, Rais Dkt Shein amemteua Shawana Bukheti Hassan kuwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi.

Rais Dkt Shein amefuta uteuzi wa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi, Mansoor Yussuf Himid.

.

Asante mkuu EMT
 
Last edited by a moderator:
Dhambi ya ubinafsi inawatafuna...si wanasema mfumo kristu ndio tatizo?? Kazi wanayo...sasa hivi vita vya wenyewe wa znz vinakuja
 
Kiwalacho ki nguoni mwao...wanachoma makanisa bure!! Au CDM ndo imeleta shida zanzibar??
 
What about Maalim na mawaziri kutoka CUF ambao wanasema hadharani MKATABA! Watatimuliwa pia?
On ma opinion Shein anajitutumua ila amechelewa sana, hawezi shinda hii battle.
 
Back
Top Bottom