Dr. Mwakyembe na Powerpool: Kuna mgongano wa maslahi na Dowans/Richmond?

Status
Not open for further replies.
NAFIKIRI MWAKYEMBE ANA UWEZO WA KUJITETEA ZAIDI KULIKO WEWE na kwa vile hili lipo wazi basi tusubiri majibu yake na hapo tutakuwa na wasaa wa kutafakari uongo na ukweli wa hilo.

Hata hivyo hii ni Bongo chini ya Chukua Chako Mapema tutayasikia mengi.

Mkuu hapa sitaki kumtetea yeyote, na sisemi kuwa Mwakyembe hana hiyo kampuni ya kufua umeme. Ninachosema ni kuwa siamini kama ana personal interest kwenye issue hii. Hata kama ana kampuni ya kufua umeme siamini kama ilishiriki kwenye process ya kuomba tenda na kushindwa, siamini hata kama ilikuwa na uwezo huo. Kwa ufupi ni kuwa huyo Mwakyembe ninaemfahamu alikuwa mhadhiri wa chuo kikuu, na baada ya hapo akawa mbunge wa bunge la Afrika Mashariki, inawezekana kuwa somewhere in between aliingia kwenye biasha za kuzalisha umeme, lakini haiwezekani kuwa amekuwa na kampuni kubwa kiasi cha kuifanya iweze hata kujaribu kusupply umeme Tanzania. Huo ni uongo ambao mtanzania yeyote mwenye akili anaweza kutambua.
By the way hapa tunaangalia vita dhiti ya ufisadi, na sio vita dhidi ya mafisadi. Let us not be distracted and make the whole battle look like it is between Mwakyembe Vs Lowassa/Rostam. It is more than that, hatuwezi kufanywa watoto. Soon tutaanza kusikia Slaa amefanya hivi, Seleli amefanya hivi, Kilango amefanya hivi. Kama Mwakyembe na yeye fisadi fact zitakuja tu na nyani atakomwa giladi as usual. Tanzania daima.
 
Last edited:
Safi sana Mwakyembe...Umeme wa upepo ni hatua....Tunataka na solar pia.
Sasa ina maana hao wengine wanaotaka Dowans na wao ni Dowans? Mwenye topic hii anadai kuwa nia ya Mwakyembe ni ku lobby for the company that he has shares on it,licha ya kwamba hakuna ushahidi wa yeye kufanya hivyo,bado nina amini ana nia nzuri na Taifa na kama ubinafsishaji ndio huo wa kumilikishana njia kuu za uchumi kwa watu binafsi....Then kabla mafisadi hawajaona kibanzi kwenye jicho la Mwakyembe ni bora watoe kwanza Boriti kwenye mijicho yao.
 
katika mfumo kama huu wa uchumi ambao mabepari ndo wabunge, haohao majaji, haohao wakuu wa serikali utegemee nini? lakini braza hebu tuleteeni ushahidi kama ule wa kagoda, na kama hiyo kampuni ipo tupeni Memo na article of association
 
Dowans walitakiwa wasupply 100MW. Hii kampuni ya Mwakyembe minimum potential ni 50MW. Mahitaji ya Tanzania ni makubwa zaidi ya capacity ya hizo kampuni zote.

Hata kama Dowans kweli wana nia nzuri, wajipange basi waje na mitambo ya 500MW na kuendelea, maana Tanzania itahitaji tu umeme.

Yaani argument zingine ni unigambile styupidi kabisa infronti of my waifu.
 
Hiyo ya Mwakyembe ina historia ya ufisadi? hawa mafisadi sasa wanatapatapa kwekli kweli. gazeti lilitoa habari hiyo -- Mtanzania -- linamilikwa na Rostam na hapo ndiyo utajua ni kwa nini. Rostam ni mwenye Dowans ingawa sasa katumia gazeti la T. Daima kumtoa Mmanga wa Oman eti ndiyo mwenye Dowans.

Tangu sakata la Richmond kuuzwa kwa Dowans zaidi ya miaka miwili iliyopita hatujasikia eti ni ya Mwarabu wa Oman ndiyo mmiliki. Au sikumbuki vizuri? Nisaidieni jamani wana JF. Ghafla katokea wapi?

Na msishangae kwa Tanzania Daima kutoa habari hizo kwani Rostam amewanunua wahariri wake, akiwemo mhariri wake mkuu (Kibanda na Mullinda) na mwenye gazeti -- inasadikiwa ni Freeman Mbowe wa Chadema -- analielewa hilo fika, pengine anaogopa tu kuwatimua kwani akifanya tu hivyo wote wataenda kufanya kazi katika magazeti ya Rostam na huko wakaweza kumuumbua zaidi Mbowe.

Wahariri wawili waliokuwa kwa Mbowe, Balile na Manyerere tayari wako kwa Rostam -- na wako mstari wa mbele kumtumikia Bwana wao kwa utiifu mkubwa
hasa kupenyeza hizi stori za kumpigia debe kuhusu Dowans.

Kwa ujumla, magazeti ya Rostam ndiyo pekee yako mstari wa mbele kutetea ununuzi wa Dowans. Linalofuata ni T. Daima, ambalo hufanya hivyo kwa njia ya kiujanjaujanja.
 
Ni baadhi ya wapiganaji wa CHADEMA wamenunuliwa ama ni wafanyakazi wa mwenyekiti (wahariri) peke yake?
Coz sijui kama ni magazeti yalianza kuifagilia Dowans ama....
 
-kubwa kuliko yote ni jinsi atakavyojihusisha na kuuza umeme toka katika kampuni yake(kama kweli anayo).
-Tanzania tunahitaji usafi katika kupewa huduma yeyote, hiki ndicho kilichokosekana kwa DOWANS, IPTL na Richmond.
 
Hiyo ya Mwakyembe ina historia ya ufisadi? hawa mafisadi sasa wanatapatapa kwekli kweli. gazeti lilitoa habari hiyo -- Mtanzania -- linamilikwa na Rostam na hapo ndiyo utajua ni kwa nini. Rostam ni mwenye Dowans ingawa sasa katumia gazeti la T. Daima kumtoa Mmanga wa Oman eti ndiyo mwenye Dowans.

Tangu sakata la Richmond kuuzwa kwa Dowans zaidi ya miaka miwili iliyopita hatujasikia eti ni ya Mwarabu wa Oman ndiyo mmiliki. Au sikumbuki vizuri? Nisaidieni jamani wana JF. Ghafla katokea wapi?

Na msishangae kwa Tanzania Daima kutoa habari hizo kwani Rostam amewanunua wahariri wake, akiwemo mhariri wake mkuu (Kibanda na Mullinda) na mwenye gazeti -- inasadikiwa ni Freeman Mbowe wa Chadema -- analielewa hilo fika, pengine anaogopa tu kuwatimua kwani akifanya tu hivyo wote wataenda kufanya kazi katika magazeti ya Rostam na huko wakaweza kumuumbua zaidi Mbowe.

Wahariri wawili waliokuwa kwa Mbowe, Balile na Manyerere tayari wako kwa Rostam -- na wako mstari wa mbele kumtumikia Bwana wao kwa utiifu mkubwa
hasa kupenyeza hizi stori za kumpigia debe kuhusu Dowans.

Kwa ujumla, magazeti ya Rostam ndiyo pekee yako mstari wa mbele kutetea ununuzi wa Dowans. Linalofuata ni T. Daima, ambalo hufanya hivyo kwa njia ya kiujanjaujanja.

Zak hii nadharia yako tete inaongeza utata. Kuna uhusiano gani kati ya Rostam vs Zitto na Mtanzania/Rai vs Tanzania Daima? Kwa nini tunalinda mashujaa wetu hata kama ukweli unaonesha kuwa samaki mmoja akioza wote wameoza ndio maana kuna kulindana sana kule Bungeni na huko vyamani?

Hivi unaamini Shujaa wetu alisema ukweli wote (the whole truth nothing but the truth) kuhusu Richmond/Dowans wakati ule aliposoma ripoti yake kwa mbwembe nyingi? Je, mbona hakuna ukali wowote bungeni kuhusu kutekeleza maazimio ya Kamati yake na kila baada ya muda Waziri Mkubwa anasema uchunguzi unaendelea? Umeishia wapi mori wao uliomuangusha Nywele Nyeupe?
 
Mleta habari ya Mwakyembe na waandishi wa habari hiyo mjipange upya na mlete habari yenye kichwa na miguu. Hii imekaa kama Mchungaji anayesoma Biblia kwa kuruka hapa na pale ili kuithibitisha point yake. Hii ripoti ni nyepesi sana kiasi kwamba ukisoma kama una akili zake timamu, unashangaa huo uhusiano unatoka wapi.
Jiandaeni LOOSERS, siku zenu zimeshahesabika. Ombeni tu sasa hivi aje rais mwenye huruma ili asiamuru MPIGWE RISASI HADHARANI. Wengine watakimbilia kwao kama President Fujimori.
 
Zak hii nadharia yako tete inaongeza utata. Kuna uhusiano gani kati ya Rostam vs Zitto na Mtanzania/Rai vs Tanzania Daima? Kwa nini tunalinda mashujaa wetu hata kama ukweli unaonesha kuwa samaki mmoja akioza wote wameoza ndio maana kuna kulindana sana kule Bungeni na huko vyamani?

Hivi unaamini Shujaa wetu alisema ukweli wote (the whole truth nothing but the truth) kuhusu Richmond/Dowans wakati ule aliposoma ripoti yake kwa mbwembe nyingi? Je, mbona hakuna ukali wowote bungeni kuhusu kutekeleza maazimio ya Kamati yake na kila baada ya muda Waziri Mkubwa anasema uchunguzi unaendelea? Umeishia wapi mori wao uliomuangusha Nywele Nyeupe?

Mkuu mjadala wa maslahi binafsi ulishakuwa mkali sana hapa JF...Nakumbuka tulimwomba Dk Slaa apeleke hoja kuwa ni lazima wabunge waweke masalhi yao wazi kabla ya upigaji kura huko bungeni. Tulipata taarifa kuwa asilimia kubwa ya wabunge wanafanya maamuzi kutokana na wanavyoguswa kimaslahi.
So hilo tatizo likimalizika then tunaweza kusema kuwa maamuzi wanayofanya ni kwa manufaa ya wananchi...Ni suala la sisi wenyewe watanzania kulipatia hili tatizo ufumbuzi la sivyo tutabakia kwenye siasa huku tunaliwa kwa kuuvamia ubepari bila kutia akili.
 
Huyu Mwakyembe, hivi hawa watu wananfahamu kweli au bora waseme tu. Mwakyembe alianza kupiga vita ufisadi tangu zamani hadi aliandika kitabu cha "PEPO YA MABWEGE" tangu enzi za mwalimu, Mafisadi wanapika habari kwa kutumia taasisi yetu ya usalama wa taifa ili kutuondoa kwenye vita hii na mafisadi tuanze kujadili miradi midogo ya kimaendeleo (kama upo kweli) ambayo wazalendo halisi wanataka kuanzisha kwa manufaa ya wapiga kura wao watanzania, hawa mafisadi hata wakitumia magazeti yao kuwachafua hawa wazalendo wachache waliojitokeza kupigana vita hii, wataweza kuzima moto huu kwani watanzania wa leo si MABWEGE tena!
 
Wind of change blows in Tanzania

By Daniel Dickinson
BBC News, Singida, central Tanzania
A group of villagers gather at the local bicycle repair shop at Njiapanda, a dusty roadside hamlet on the rift valley in Singida region in central Tanzania, to marvel at magazine pictures of massive electricity-generating wind turbines.

They have never seen anything like this before and are clearly impressed.

They will soon find out exactly what the turbines are like. In a matter of months, 24 of these 100m-plus-high power generators will be erected next to their homes, as part of the first commercial wind farm in sub-Saharan Africa.

This is one of the poorest parts of Tanzania. There is little agriculture, no industry, but one thing there is plenty of is wind.

It is an untapped resource, but one which could hold the key to providing much-needed electricity to central and northern Tanzania and kick-starting the development of the region.

“ The people of Singida are expecting a lot of this project ”
Regional Commissioner Parseko Kone

The 24 turbines, which should be in operation within 18 months, will generate 50 megawatts (MW) of power, almost 10% of Tanzania's current power needs.

The company behind the $113m project is Wind East Africa. "It's important that Tanzania diversifies its power sources," says project manager Mike Case.

"The country is very reliant on hydro-electric power, which means in times of drought, there is a power deficit. Oil-generated power is very expensive, so wind power offers a cheaper and more reliable alternative."

Fewer blackouts

The demand for power in Tanzania is growing by more than 50 MW a year, fuelled partly by an expansion of gold and nickel mining in the north of the country.

At present, electricity is sourced from power plants more than 1000km away. The wind farm at Njiapanda will mean that power-hungry industries will soon be provided with electricity generated locally.

The wind farm will benefit the local economy, providing jobs during the construction phase and a handful of jobs when it is up and running.

Regional Commissioner Parseko Kone is also hoping the rest of his impoverished region will profit.

"The people of Singida are expecting a lot of this project," he says.

"They're hoping it will help to develop our economy and because wind is free, they're also expecting cheaper electricity tariffs."

It is unlikely that tariffs will come down, as electricity is already heavily subsidised, but it does mean that Tanzanians can expect fewer power blackouts.

Power play

Wind power on a commercial scale is unknown in sub-Saharan Africa, despite the existence of constantly blowing and consistently strong winds, especially along the top of the rift valley, the mountain plateau which runs through East Africa from Ethiopia to Malawi and Mozambique.

In Europe, the industry is well developed. Germany, the European leader in terms of generation, produces more than three gigawatts of power (3000 MW) from wind turbines. The target in many European countries is to have 50% of all power generated by wind.

Africa is now set to benefit from the progress made in Europe. The equipment is becoming cheaper, as well as more robust.

According to wind expert Dr Ladislaus Lwambuka, from the University of Dar es Salaam, Africa is now ready for wind power on a commercial scale.

"If the Wind East Africa project is a success, then it could lead to more wind farms, not just in Tanzania but in the rest of Africa, particularly along the rift valley, where we know the winds are strong."

There are already plans, if the first phase of the project goes well, to double the number of wind turbines and increase Wind East Africa's output to up to 100 MW.

The people of Njiapanda and the surrounding dusty plateau may not know it now, but this small part of the rift valley will, by then, be the epicentre of wind power in sub-Saharan Africa.

Story from BBC NEWS:
BBC NEWS | Business | Wind of change blows in Tanzania
 
" The people of Singida are expecting a lot of this project "

Mimi nadhani sasa ni wakati wa kuifagilia hiyo kampuni yenye kutumia teknolojia ya upepo period...Hizo mashine za Dowans wameliwa kwasababu wamesha wala wananchi vya kutosha....Lets change the cause people.
 
Haiwezekani muwe na bidhaa moja halafu kusitokee mgongano ,mgongano ambao ni kuhodhi sehemu kubwa,mgongano ambao unaweza kuhatarisha bidhaa ya mwingine isipate soko ,mgongano ambao mmoja ya wenye bidhaa akawa anajipendelea yeye tu ,kila mmoja alikuwa na mbinu zake za kuanzisha mradi. Sasa hivi huyu Mwakyembe aliorodhesha mali hizi kule ambako Mzee wa vijisenti alibania ?

Uozo uozo uozo wa wafuasi wa Sultani CCM ,yaani kila ukimuona ana makelele na anakuwa mkali basi ujue huwa kuna kitu anaficha na hivyo anatumia makelele na ukali ili watu waogope wamwogope kumuhoji ,Mengi anaenda mahakamani ili kuwatisha waandishi japo waliyoandika hayana ukweli lakini kitendo cha kwenda mahakamani na kufanya ni suprise ni kujificha tu hakuna kingine. Lakini kila uovu utafunguka na kuwaweka wafuasi wa Sultani CCM uchi.

Kwa kweli hizi kambi au mitandao ya Wafuasi CCM ni katika kugawana mali na hazina za Taifa hili la Tanzania kama ilivyogawiwa bara la Afrika na hawa wanagawana mapato ya nchi hii kila mmoja anaweka mrija akiwapa ajira ndugu na jamaa zake,ndio maana yake ukiwaona wamekaa kama kupe kwa vitambi au wamenyanyuka mabega kama umbu wa maleria.

Watu hawa ni hatari sana kwa jamii ya WaTanzania ,hasa kwa vile ni viongozi ni lazima haki itavurugwa tu ,mnyonge hataweza kujiendeleza , mnyonge inabidi aanze kutoa chauchau tokea kwa balozi wa nyumba kumikumi au siku hizi sijui anaitwa diwani sasa fikiria akianza kutoa chochote kuanzia huko hata akifika ngazi ya Taifa kwa kweli anakuwa yuhoi ,akitizama anakotoka anaona ni hasara tupu.

Viongozi hawa wamekwama kumshitaki Mkapa si kwa sababu hawezi kushitakika ,maana wanaojua sheria kibao wamesema Mkapa anaweza kabisa kupelekwa mahakamani .Kukwama kwao kwa sababu na wao wana biashara zao ambazo ni kubwa na mirija yake si ya kawaida pengine na usajili wake ni wa mizengwemizengwe na ni viongozi wa serikali tena wa ngazi za juu .Nani atamshitaki nani ? Kwa jambo gani ?

Viongozi hawa au wafuasi hawa waSultani CCM ndio ukawaona wakali sana pale inapodaiwa Katiba ,pale unapoouliziwa Muungano ,pale inapouliziwa Tume ya Uchaguzi pale inapouliziwa Mahakama kwa sababu maficho yao ni vyombo hivyo.

Hawa walafi walioota mizizi na kufikia uroho wa hali ya juu kiasi ya kupokonyana tonge ni hatari kwa hatua za maendeleo ya mmoja mmoja katika Nchi hii ,kila sehemeu wameweka sheria ambazo wao wanaziruka na wala haziwaoni ,sheria ambazo zinakuwa kigingi cha maendeleo ya Mwananchi wa kawaida ,viongozi ambao naamini kwa sheria zilizopo hawaruhusiwi kuwa na biashara, zaidi wawe wameziainisha na kupitiwa au kukaguliwa kabla hawajakabidhiwa uongozi kwa muda mchache inakuwa hawagusiki na wakali wala hawaonekani kuchanganyika tena na raia wa kawaida pindi tu wanapokabidhiwa uongozi ,nasema ni wezi wa mali ya umma.

Kuna kodi kibao ambazo haziwagusi ,kuna malipo kibao ambayo hawayalipii yote hayo huangushiwa mlala hoi kuanzia shamba lake la muhogo ,nyumba yake ya makuti na duka lake la kuuza nguru na samaki wakavu mlala hoi itabidi alipie tena kwa nguvu na kugongewa mlango juu alipie kimoja kimoja. Huku Vigogo wakizisubiri hela hizo kama zao.

Huu ni ukiritimba wa Wafuasi wa Sultani CCM ,hakuna alie safi ni wazuri wa maneno tu lakini nyuma ya maneno yao ni wafanya biashara ndani ya serikali.
 
Jamani mimi bado nafikiri ushauri wa mzee Ndesamburo wa kuwanyonga hawa watu hadharani ufanyie kazi otherwise Rostam na Lowasa wanataka kuharibu nchi watapaka watu matope na mambo mengi sasa hili la Dr kuwa na Kampuni ubaya uko wapi,Richomond na hiyo Dowans ni wizi aliko singizia mtu ni wapi? kama kweli alisingizia mbona hakuna anyejitokeza na kutwambia kuwa ni mmiliki wa Richmond na hiyo Dowans wote wanona ni kimeo ndo maana wanazikataa kampuni zao , ya Mwakyembe iko halali ndo maana inajulikana na hana hata aja ya kuikana after all ina aim nzuri ya kutumia a Renewable energy hence clean environment na mpa pongezi sana kama atafanikiwa kuzalisha umeme kwa njia hii Up Dr. Mwakyembe,
 
wewe mwiba ni mpumbavu. watu wanajadili point wewe unatuletea propaganda. Embicile

Upumbavu wake nini lakini? Yeye kaangalia source ya matatizo yote kuwa ni ubinafsi na utawala msonge wa CCM. Sasa kama unaweza kuitofautisha CCM na Mwakyembe unaweza kumsaidia.
 
Hii si breaking news!!!!!

Hao mtanzania wasitake kutuchanganya. Mwakyembe kama mtanzania ana haki ya kuwa na kampuni au hisa katika mradi wowote halali. Ishu hapa ni wizi wa hiyo Richmond, Dowans etc. Well hata hii kampuni ya kina Mwakyembe ikifanya wizi tutasema tu.

Huyu Rostam vp? Mbona anatapatapa sana sasa hivi?????????????

Well said Nyambala!! Hapa issue tuliyonayo ni kuhusu ufisadi wa Richmond/Dowans. Kama kampuni ya Mwakyembe nayo imehusika na ufisadi wowote basi tutaianika hadharani bila woga wala aibu. Ikumbukwe kama sikosei mwaka juzi kulikuwa na uwezekano wa Serikali kuruhusu watu binafsi kuingia katika biashara ya kufua umeme ambayo ilipigiwa kelele na Watanzania wengi na baadhi ya Wabunge kwamba ni biashara ambayo itakuwa ni biashara itakayomilikwa na wakubwa na nia yao kubwa ni kuimaliza kabisa TANESCO. Karamagi alilipigia debe sana hili la watu binafsi kuruhusiwa kufua umeme lakini hakufanikiwa.

Tusubiri ufafanuzi wa Mwakyembe katika hili, lakini sioni yeye kupinga ufisadi wa kununua mitambo chakavu ya Dowans kwa bei mbaya kama inaonyesha chochote kuhusiana na yeye kuifagilia kampuni yake, bali kwa maoni yake alifanya hivyo huku akiweka maslahi ya Watanzania mbele badala ya mafisadi wa Dowans. Tumsubiri Mwakyembe atoe ufafanuzi, lakini kama Mtanzania mwengine yeyote ana haki ya kuwa na hisa katika kampuni yoyote ile lakini kama kuna ufisadi basi uwekwe hapa na wanaJF hatutasita kumuweka kwenye kiti moto na kumjadili kwa mapana na marefu.
 
Well said Nyambala!! Hapa issue tuliyonayo ni kuhusu ufisadi wa Richmond/Dowans. Kama kampuni ya Mwakyembe nayo imehusika na ufisadi wowote basi tutaianika hadharani bila woga wala aibu. Ikumbukwe kama sikosei mwaka juzi kulikuwa na uwezekano wa Serikali kuruhusu watu binafsi kuingia katika biashara ya kufua umeme ambayo ilipigiwa kelele na Watanzania wengi na baadhi ya Wabunge kwamba ni biashara ambayo itakuwa ni biashara itakayomilikwa na wakubwa na nia yao kubwa ni kuiamliza kabisa TANESCO. Karamagi alilipigia debe sana hili la watu binafsi kuruhusiwa kufua umeme lakini hakufanikiwa.

Tusubiri ufafanuzi wa Mwakyembe katika hili, lakini sioni yeye kupinga ufisadi wa kununua mitambo chakavu ya Dowans kwa bei mbaya kama inaonyesha chochote kuhusiana na yeye kuifagilia kampuni yake, bali kwa maoni yake alifanya hivyo huku akiweka maslahi ya Watanzania mbele badala ya mafisadi wa Dowans. Tumsubiri Mwakyembe atoe ufafanuzi.

Ufisadi wa kampuni ya Mwakyembe ni upi huo? Upepo?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom