Dr. Mwakyembe na Powerpool: Kuna mgongano wa maslahi na Dowans/Richmond?

Status
Not open for further replies.
Huyu alieandika hana akili. Windi energy na DOWANS inaconflict gani...? Unless kama wana ambitions zaku wauwa TANESCO which i doubt. The man is smart, watu mnataka afe njaa! lol..

Nyie mnataka mtu akiwa anapinga ufisadi basi awe maskini-mbwa.. akili za nyerere hizo alikua anawadanganya while he lives comfortable kwenye mansion lake na satalite TV...lol

This is garbage.
 
Hivi ni conflict of interest gani iliyopo kwa wazalishaji umeme unaotumia upepo na usio na madudu ya capacity charge na hawa wa magenerator wenye kutunyonya kupitia hilo tundu la capacity charge? Huu ni utumbo mwingine wa mafisadi. Kwanza hata yakinunuliwa hayo magenerator ya Dowansa hayawezi zalisha umeme wa kuziba pengo lililopo, kwa hiyo kila anayeingia kwenye uwekezaji wa nishati hiyo analihakikishia taifa uhakika wa nishati ya umeme ambayo tangu uhuru imekuwa tatizo kwa Watanzani.

Cha msingi hapa ni kwa serikali kuwa wazi kwenye uwekezaji kwenye nishati hiyo ili Wazawa wengi zaidi wajitokeze kuwekeza badala ya kuwaachia hawa jamaa wapita njia kumiliki kila kitu na ndio maana leo hii hawaoni uhalali wa wazawa kuwekeza kwenye nishati ya umeme.
 
Hii inaumiza. Hiro wetu wa mbwembwe nyingi naye ana utata. Hakika inabidi tukubali matokeo. Haiwezekani uwe na kampuni ya umeme inayojaribu kupata dili huku unaichunguza kampuni nyingine ya umeme yenye dili kwa rungu la Bunge. Huu nao ni mwanzo wa kufa kisiasa kwa shujaa wetu wa Kamati Teule. Hivi kumbe ni kweli, kizungukacho huzungukwa. Harakati dhidi ya ufisadi, do, ndio kwanza zinaanza!
 
Watu wasirukie mijadala bila kuwa makini.Kama mlimsikiliza vizuri Dr slaa alipohojiwa na ITV kuhusu suala la ununuzi wa mitambo ya Dowans alilalamika kuwa Tanesko ingeweza kutosheleza umeme kwa kupata umeme wa upepo katika mradi wa singida hapo conflict of intrest inapoanza.sasatusianze kumtetea mwakyembe kwa sababu ya mahaba ajieleze.Ndivyo great thinker wangependa kujua undani wa madai hayo.vinginevyo tukianza kumlinda mwakyembe bila yeye kujitetea then unapoteza sifa za kuwa grat thinker
 
wazee habari za ma week endi,kweli mimi ningekuwa na scud nigemaliza mafisadi wote.sasa ngoja niulize maswali moja mbili.1. kwani dr mwakeyembe kuchaguliwa kuwa chairperson ya hiyo kamati ya kufichua ufisadi na yeye kumiliki hiyo kampuni ilikuwa ni coincidence?wanasema alikuwa na hiyo kampuni kabla ya dowans,sasa kama asingechaguliwa kuwa chairperson,angewezaje kuwa na mgongano wa kimaslahi?sijui kama mnanipata?2.hata kama asingekuwa chairperson bado angemiliki hiyo kampuni yake,sasa mgongano huu unatoka wapi?jamani sometimes media zetu ni wajinga tu,yaani hawana commonsense.duh miye ngoja niondoke tu,huyoooo.
 
Watu wasirukie mijadala bila kuwa makini.Kama mlimsikiliza vizuri Dr slaa alipohojiwa na ITV kuhusu suala la ununuzi wa mitambo ya Dowans alilalamika kuwa Tanesko ingeweza kutosheleza umeme kwa kupata umeme wa upepo katika mradi wa singida hapo conflict of intrest inapoanza.sasatusianze kumtetea mwakyembe kwa sababu ya mahaba ajieleze.Ndivyo great thinker wangependa kujua undani wa madai hayo.vinginevyo tukianza kumlinda mwakyembe bila yeye kujitetea then unapoteza sifa za kuwa grat thinker

Sidhani kama kunahaja ya kumtetea mwakyembe hapa, ila kuna haja ya kuona aliyosema na kuyatetea kuhusu richmond na dowans yalikuwa ya maana. Kama yalikuwa ya maana dowans must go na walihusika na ufisadi wa dowans wafikishwe mbele ya sheria.

sasa kama huko kwenye umeme wa upepo kuna walakini mwenye data amwage.

Mwakyembe kasema wazi ununuzi wa mali chakavu ni kuvunja sheria za manunuzi za mashirika ya umma kama ni uongo toeni data.
Pia kasema sheria za nchi za tender zinasema kampuni/mtu aliyeshiriki na kupewa tender na kufanya ufisadi na kutoa uongo na rushwa hata ruhusiwa tena kutender au kuiuzia kampuniya umma na serikali kwa muda wa miaka kumi. kama haya ameyatunga tujadili.
alisema richmond mjukuu wa dowans ni fafa. je huu ni uongo.

Vita hii ni kubwa na ninajua mafisadi wananguvu sana na dowans itaingizwa ndani ya tanesco kwa kuruka au kinyumenyume ila siku inakuja watakimbia kwa kilio kikuu.
 
Huu ujinga tu wa Rostam. Huyo Mwakyembe hata kama anamiliki, lakini HAJAIBA ni juhudi zake na ubunifu wake, sasa kosa liko wapi. Huyo Rostam na Mtanzania yake ni wezi tu, basi. acha watapetape. aachane na Mwakyembe kabisa.
 
Ilianza attack kwa Zitto Kabwe sasa imekuja kwa Mwakyembe, na kuna uwezekano kuwa itaendelea na kuendelea. Hii ni vita dhidi ya ufisadi kila upande unatumia mbinu zake. Bado sitaki kuamini kama Mwakyembe ana kampuni binafsi ya kufua umeme ambayo ingeweza kuwa competitor wa kampuni yoyote ya kuzalisha umeme Tanzania, sounds bollocks to me.


NAFIKIRI MWAKYEMBE ANA UWEZO WA KUJITETEA ZAIDI KULIKO WEWE na kwa vile hili lipo wazi basi tusubiri majibu yake na hapo tutakuwa na wasaa wa kutafakari uongo na ukweli wa hilo.

Hata hivyo hii ni Bongo chini ya Chukua Chako Mapema tutayasikia mengi.
 
Hivi serikali kweli kodi zetu inakusanya inashindwa kuwekeza kwenye miradi kama hii???
Enzi za mwalimu mambo hayakuwa hivi wizi mtupu.
Yaani Kila mtu akiona oportunity kidogo tu anataka ku outsource. atafutwe mandarasi kweli tutafika????

Haya yngeanza enzi za mwalimu hata kidatu, Mtera zingekuwa za mafisadi wachache.
Mi natoa wito serikali iangalie na itengeneze sera za mambo ya outsourcing la sivyo kutakua na matatizo makubwa.
Makampuni binafsi yakuuza umeme ruksa ila yatengeneze miundombinu yake na itafute wateja wake. Sio mambo ya kutafuta miteremko na kutaka kula kiulani.

Haya makampuni yataipeleka taneco pabaya. Watu hatulipi bili hizi kampuni zitataka chake na wakati huo labda hata umeme wake haujasambazwa.

Kama kuwekeza na kufanya biashara na serikali n kuzuri hawa mafisadi wa dowans na wengine si watengeneze barabara za kukodisha tukipita tuwalipe.
 
wazee habari za ma week endi,kweli mimi ningekuwa na scud nigemaliza mafisadi wote.sasa ngoja niulize maswali moja mbili.1. kwani dr mwakeyembe kuchaguliwa kuwa chairperson ya hiyo kamati ya kufichua ufisadi na yeye kumiliki hiyo kampuni ilikuwa ni coincidence?wanasema alikuwa na hiyo kampuni kabla ya dowans,sasa kama asingechaguliwa kuwa chairperson,angewezaje kuwa na mgongano wa kimaslahi?sijui kama mnanipata?2.hata kama asingekuwa chairperson bado angemiliki hiyo kampuni yake,sasa mgongano huu unatoka wapi?jamani sometimes media zetu ni wajinga tu,yaani hawana commonsense.duh miye ngoja niondoke tu,huyoooo.

Du mkuu wewe ni muulizaji mzuri, hujapata jibu tayari umeshairukia hiyo Media unayoiuliza.
Ingekuwa busara Kwa shujaa wako (kama kweli anamiliki hiyo kampuni) kujiondosha mapema katika mjadala ambaounaonyesha conflict of interest.
 
Mafisadi ni noma.
Wameenda kupandikiza kampuni kwa jina la DR.ili watuzuge kwamba maslahi binafsi yanasababisha kudorora kwao.
Wamekwisha.
Aliyesoma barua ya ZITTO KWA watanzania naomba anipe dondoo zake

Hapa JF tuwe objective. Mtu wa kusema hayo ni Dk. Mwakyembe mwenyewe na si mwingine kama kweli kazushiwa.

La msingi hapa ni kuwa kwa kanuni za kawaida, ingebidi Dk. afanye declaration alipochaguliwa ku head Kamati Teule ya Bunge kuwa nayeye pia anayo kampuni ya kufua umeme ambayo nia yake ni kuiuzia Tanesco umeme utakao fuliwa kwa misingi ya kulipwa capacity charges au vinginevyo. Hapo Kamati ya Bunge ya Madini na Nishati ndio ingetoa maamuzi ya kuwa awe Mwenyekiti wa Kamati Teule au apewe mtu mwingine nafasi hiyo. Na hata ujumbe wake pia katika Kamati Teule ingebidi ujadiliwe.

Uhalali wake wa ku serve kwenye kamati hiyo ungetokana na yeye ku declare ineterest zake kwenye hiyo kampuni ambayo ina nia ya kufanya shughuli hizo hizo zinazichunguzwa.

Kwa misingi hiyo bado nasisitiza kuwa hii ni breaking news kwani hata wote waliochangia inaonyesha walikuwa hawajui kuwa Dk. alikuwa na mahusiano kama hayo.

Mimi niko neutral kabisa na wala nisieleweke vibaya.
 
Kimsingi sijaona conflict of interest kwenye hiyo habari na mwandishi wa habari kashindwa kujenga hoja kuonyesha hiyo conflict of interest.

Kungekuwa na mgongano wa kimaslahi iwapo hiyo kampuni ya Dr. Mwakyembe ingekuwa ina mitambo sawa na ya dowans na pia wana nia ya kuiuzia serikali, hapo ndipo ningesema kuna mgongano wa kimaslahi kwa kuwa unampiga nyundo mwenzako ukitegemea wewe upate biashara.

Mgongano mwingine wa kimaslahi ungetokea iwapo Dowans wangetaka kuweka mitambo hiyo somewhere na waamue kuzalisha umeme kwa ajili ya kuiuzia serikali halafu Dr. Mwakyembe kupitia Kamati ya Nishati na Madini aikataze TANESCO kununua umeme kutoka kwa Dowans. Hapo ningeona kuna mgongano wa kimaslahi.

TANESCO wametoa takwimu zao ambazo wao wanadai kwamba hata kama wakinunua mitambo ya Dowans bado kutakuwa na nakisi (dificit) ya mahitaji ya umeme kwa kuwa mahitaji ya umeme yanaongezeka kila kukicha. TANESCO hawajaweza kukidhi mahitaji ya umeme kwa watanzania na hivyo investment kwenye sekta ya nishati bado inahitajika sana.
 
At the end of the day Richmond na Dowans zitabaki kampuni za kifisadi zilizotaka kutuingiza mkenge. Hakuna conflict of interest yoyote kwa Dr Mwakyembe kuwa share holder katika kampuni halali ya nishati.
 
There is no sabotage by Mwakyembe on Richmond/Dowans to get the deal. According to Ngeleja, Singida Wind Power is already part of the wider plan to be introduced in the near future:
Forty megawatts would also be injected into the national grid through "standardized small power purchase agreements" from the private sector, while all Tanesco plants would be serviced.

He said by October, the Tegeta gas plant (45MW) would be completed, a 60MW project would be implemented in Mwanza.

According to Mr Ngeleja, the Singida wind power plant estimated to produce 50MW would be ready by 2010, Kiwira plant project (400MW) by between 2011 and 2014, Kinyerezi plant (240MW) by 2011 alongside Ruhudji hydroelectric plant (358MW).
TheCitizen Newspaper
 
Huu ni upuuzi mtupu! watanzania wa sasa siyo mabwege tena, hatuko tayari kuandaliwa taarifa na mafisadi na kutuletea ili kutusahaulisha vita dhidi ya mafisadi ! M wakyembe na wenzako msife moyo vita iendelee hadi wezi wote wachomwe moto.
 
Kwa nini tunaandikia mate ilhali wino upo. Taarifa za makampuni zinahifadhiwa wapi? Maadam wote tunajua zilipo si twende tukaangalie hizo data kuhusu shujaa wetu. Au tunasubiri wajaribu kuliunguza jengo tena? Kama alikuwa na kampuni hiyo kabla ya kuwa Mwenyekiti wa Tume Teule na kama hakuliambia Bunge kuwa ana kampuni kabla ya kupitishwa kuwa Mwenyekiti na Bunge Tukufu basi hapo kuna mgongano wa kimaslahi.

Kuna hitaji la kuweka mapenzi pembeni. Mimi nampenda sana shujaa. Namnukuu mara kwa mara. Ni hiro wangu. Ila kama na yeye alikuwa na mgongano wa kimaslahi kuhusu umeme basi inabidi awajibike. Sheria msumeno. Alafu kwa nini shujaa alikiri kuwa kuna mambo hawakutuambia kwenye ripoti yake? Au ndio hayo ya mgongano wa kimaslahi?

"Put it on the table, who is Richmond?" - Waziri Mkubwa Mjiuzulu
 
hivi ni kosa kwa mtanzania kuwa na hisa katika kampuni yeyote? mi nashangaa kakampuni kama hako ambako hata hakafahamiki leo hii kawe na mvutano wa kimaslahi na Dowans, mi nafikiri hapa kuna watu wanatafuta jinsi ya kufukia aibu zao. cha msingi hapa hatuhitaji mitambo mibovu thats all. Hii inanikumbusha hadithi za zamani kwamba mwanamke ukimtongoza akikukataa ndipo unaanza kuangalia mapungufu yake na kuyatumia hayo kumwangamiza je hayo hukuyaona mwanzo mpaka akukatalie?. Hapana hatutaki hayo mambo yanayofanana na mfano huo watanzania wa sasa sio wa miaka minne iliyopita tumeamka acheni hizo bwanaaaa..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom