Dr. Mwakyembe na Powerpool: Kuna mgongano wa maslahi na Dowans/Richmond?

Status
Not open for further replies.
huyu jamaa, kama ambayo yanaongelewa ni ya uongo, naunga mkono aitishe press conference, asipende kuwatumia vibaraka wake ambao ni wahariri wa magazeti ya RA.
 
Labda katika press conference hiyo awaite vibaraka wake tu -- Muhingo, Balile, Manyerere na sarah Mossi -- na si wale upright reporters/editors wanaofahamika na wanaotoka magazeti yanayoheshimika.

Hivi kwanini jamani tusibebe hata mapanga siku moja tuamua kumtimua RA nchini kwetu? Maana hali mbaya ya uchumi wa taifa letu naweza kusema yeye anachangia kwa kiasi kikubwa mno hasa kwenye hii awamu ya nne. Kagoda, Richmond, Dowans, etc. Anahisa 19 % Vodacom, mitambo kwenye makampuni ya kuchimba madini etc. Na kaweka watu wake huko. Ngeleja alikuwa mwanasheria wa Vodacom kabla ya kupelekwa na RA kugombea ubunge, Rashid alishawahi pia kuwa MD wa Vodacom kwahiyo wanafahamiana vizuri. Jamaa inaionyonya hii nchi si kawaida. Na sijui kama analipa kweli hata kodi kwenye hizo biashara zake. Masha naye ni kijana wa Lowasa ambaye ni mbia wa RA pia, du!!!!!!
 
Huu mjadala umefungwa kwahiyo nimeweka link ili musome kilichoandikwa mwaka 2009
kuhusiana na hii kampuni ya Mwakyembe ambayo leo anairuka. Hii kampuni ya Power Pool inaelekea ilijadiliwa sana mwaka 2009. Hii link hapa chini imefungwa na huwezi kuchangia bali kusoma tu. Labda admins waifungue.

Dr. Mwakyembe na Powerpool: Kuna mgongano wa maslahi na Dowans/Richmond?

Soma na hapa chini akijivunia kuanzisha hii kampuni

MICHUZI BLOG: ya dk.mwakyembe, dowans, iptl na rostam

Wamilika wa hisa ni pamoja na;

Dk. Mwakyembe anayemiliki hisa 1,485 katika kampuni hiyo, wengine wenye hisa katika kampuni hiyo ni Emmanuel Kasyanju (99), Victor Mwambalaswa (99), Mwacha Kagoswe (4,455), Josephine Pina (99), Athumani Ngwilizi (99), Prosper Tesha (99), TBC (199 Limited inayomilikwa na Isaac Mwamango (297) na MECCO Limited, inayomilikwa na Maungo Kwabibi hisa moja.

Wengine ni Beston Mwakalinga (99) Niels Dahlmann (891) na Leonard Tenende (99).
 
Hoja yako ipo wapi sasa? Kama uzi umefungwa, iweje sasa uanzishe tena? Unajua kwa nini umefungwa?
 
Chabruma,
Baada ya kusoma mabishano ya sasa kati ya gazeti la Dira na Mwakyembe kuhusu utapeli kwa Mkorea kupitia kampuni hii. Ndio nimeiona hii post ambayo ni ya mwaka 2009 Ila ni relevant kwenye mjadala huu mpya. Ila imefungwa ndio maana sikuchangia huko moja kwa moja.
 
Hoja yako ipo wapi sasa? Kama uzi umefungwa, iweje sasa uanzishe tena? Unajua kwa nini umefungwa?
Binafsi sijui kwanini umefungwa, kwa swali lako la unajua kwanini umefungwa definately una majibu ya kwanini umefungwa. Unaweza sasa kutueleza kwanini umefungwa?
Ahsante!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom