Kyela: Dr. Mwakyembe amtolea Uvivu Rostam

"...don't take a knife to a gunfight!"

...tatizo la wana siasa wetu wa bongo kelele miiiiiiiiiiiiiiiiingi, ...yule mtikila naye alimshikia bango Rostam Aziz, kumbe naye alikuwa kakunja Milioni 3 za huyo huyo Rostam kwa ajili ya repair ya nyumba yake, ...since then kimyaaaaaaaaaaaaaaa!

...Mh Mwakyembe naye tunampa heshima zote katika sakata la Richmond, lakini kidogo kidogo imani inaanza kunitoka kumbe naye ana 'kamradi' kake ka vijisenti kibao ka kuzalisha umeme huko Singida kwenye ngome ya Rostam Aziz? what is happening? conflict of interest?

"...dont start a gunfight which you know you can't win!"

Msituyumbishe hapa watanzania...maslahi ya taifa mbele, siyo matumbo yenu!
 
Kwa nini Mwakyembe anaendelea kumpa Rostam Umaarufu wa bure?

Au tumesahau siasa za Tanzania? Mnakumbuka Mrema alivyovuma na kujitutumua kwa kutukana CCM lakini siku ya siku watu wakaipigia kura CCM?

Kama wizi wa Rostam unathibitika pamoja na ushahidi, kwa nini mpaka leo anaendela kudunda bila wasiwasi mpaka anakuja Makanisani mwetu kutufadhili?

Iweje Rostam atushike K en de Taifa zima? alitufahili na kitu gani leo tunalipa fadhila kwa kumwachia ajifanyie anachotaka?

Kazi ya kumtukana Rostam, mwambieni Mwakyembe atuachiye sisi. Akiifanya yeye na kujivuruga ndani ya miiko ya Chama chake na kiapo chake cha Bunge, yatamtokea puani na kuanguka kwake kutakuwa kwa kishindo mithili ya Oldonyo Lengai kulipuka!
 
keep pressure on mafisadi that what we can do now.
Anachofanya Mwakyembe ni poa inabidi kila kukicha mafisadi wajue tunaamka nao, funua kila jiwe na kila kona mpaka wabaki uchi mwisho wataanza kudata na tutawaweka kwenye kona tu.
 
Kwa nini Mwakyembe anaendelea kumpa Rostam Umaarufu wa bure?...

Kazi ya kumtukana Rostam, mwambieni Mwakyembe atuachiye sisi. Akiifanya yeye na kujivuruga ndani ya miiko ya Chama chake na kiapo chake cha Bunge, yatamtokea puani na kuanguka kwake kutakuwa kwa kishindo mithili ya Oldonyo Lengai kulipuka!

maneno mazito tena yalojaa hekima hayo mkuu,... atayesikia na asikie.

Kinyume na hapo nahisi kuna wana CCM fulani walioshika mpini wanamuachia ajikaange tu mwenyewe, siku ya siku waje wamporomoshe kama walivyokuwa wabunge wengine machachari toka mkoani Mbeya, kina mar.Tuntemeke Sanga, Njelu Kasaka nk...
 
Katika mkutano wake alikuwa ameongozana na waandishi habari kutoka Mbeya baada ya wale wa Kyela kupigwa marufuku kuhudhuria mkutano huo kwa madai kwamba huwa wanamwandika vibaya.

Pia inaelekea kuna mpambano mkali unaandaliwa Kyela 2010 kati ya Dr. Mwakyembe na jamaa mmoja nasikia yuko nje ya nchi.

Hapa Dr. anachemka kama mkutano wake alioufanya Dar, alikuwa akiulizwa maswali na waandishi wa Magazeti ya Habari, anajibu wametumwa na Rostram. Sasa hebu fikiri Dr. anabagua waandishi, anataka wale wanaomuandika yale ayatakayo, walio kinyume naye hawataki. Na ikumbukwe huyu (Mwakyembe) naye alikuwa mwandishi, anajua kuwa mwandishi unatakiwa kuwa huru. Sasa iweje waandishi wote wakubaliane naye?, hapa anachekesha na kuonesha alivyo mtupu.

Kuhusu suala la kuandaliwa mtu kugombea Kyela, kwani Mwakyembe aliandaliwa na nani?. Hakuna mtu mwenye jimbo, uwe mtetezi wa wananchi ama usiwe, ukimaliza miaka mitano ni haki kwa raia yoyote wa Tanzania mwenye kutimiza masharti kugombea. Hapa ndio nawashangaa hawa wanaopigania wananchi, wakiona mtu anataka kugombea haraka haraka kupata huruma ya wananchi wanasema anatumiwa ama katumwa na mafisadi. Kila mtu ana haki ya kugombea.
 
maneno mazito tena yalojaa hekima hayo mkuu,... atayesikia na asikie.

Kinyume na hapo nahisi kuna wana CCM fulani walioshika mpini wanamuachia ajikaange tu mwenyewe, siku ya siku waje wamporomoshe kama walivyokuwa wabunge wengine machachari toka mkoani Mbeya, kina mar.Tuntemeke Sanga, Njelu Kasaka nk...

Kwa kuweka kumbukumbu sasa Tuntemeke Sanga hakutokea Mbeya, bali wilaya ya Makete mkoani Iringa
 
Kwa kuweka kumbukumbu sasa Tuntemeke Sanga hakutokea Mbeya, bali wilaya ya Makete mkoani Iringa

...shukran mkuu, upo sahihi ndugu yangu, hizi cheap politics zinakera mpaka makosa ya kumbukumbu yanaanza kujitokeza.
 
Kwa nini Mwakyembe anaendelea kumpa Rostam Umaarufu wa bure?

Au ttumesahau siasa za Tanzania? Mnakumbuka Mrema alivyovuma na kujitutumua kwa kutukana CCM lakini siku ya siku watu wakaipifgia kura CCM?

Kama wizi wa Rostam unathibitika pamoja na ushahidi, kwa nini mpaka leo anaendela kudunda bila wasiwasi mpaka anakuja Makanisani mwetu kutufadhili?

Iweje Rostam atushike K en de Taifa zima? alitufahili na kitu gani leo tunalipa fadhila kwa kumwachia ajifanyie anachotaka?

Kazi ya kumtukana Rostam, mwambieni Mwakyembe atuachiye sisi. Akiifanya yeye na kujivuruga ndani ya miiko ya Chama chake na kiapo chake cha Bunge, yatamtokea puani na kuanguka kwake kutakuwa kwa kishindo mithili ya Oldonyo Lengai kulipuka!

Mkuu kishoka,

- Heshima mbele sana, unaonekana unaijua vizuri sana siasa ya bongo, yako ndio elimu inayotakiwa hapa JF.

- Kwa wale wapambe wa Mwakyembe mnaojaribu kumtukana Mzee Malecela, kwa sababu ya haya maneno ya Mwakyembe hamumsaidi ila mnamharibia sana tena sana, Mwakyembe na Mwandosya, wasingekua kwenye siasa kama sio Malecela ndiye aliyewafikisha national, unless wanataka kutoka CCM hasa Mwakyembe, lakini kama hawatoki hamuwasaidii na maneno yenu ambayo tunaamini mnatumwa naye,

- Siasa anazozicheza sasa sidhani kama anazijua vizuri, yeye mwenyewe anajua kwua ni mtandao ndio waliomsaidia kutoka EAC na kuja ubunge wa Kyela, na tunajua ugomvi wake unatokea kule alipokatwa jina lake na el kwenye baraza jipya la mawaziri, sina tatizo na Mwakyembe as a person, lakini unless ana mpango wa kuingia upinzani, sioni a smart political strategy ya future yake hapa ndani ya CCM,

- Mengi hawezi kumsadia ndani ya CCM ingawa anamsaidia sana huko nje, tayari ameshaambiwa asubiri kwenda mbele ya CCM na kusema matatizo yake against Rostam, Chadema majuzi wamesema wazi kwamba Rostam na Mwakyembe wanagombea uwanja wa umeme Singida, ninamuaminia sana Mwakyembe, lakini sasa ninaanza kuwa na wasi wasi naye kwa sababu kama ameshaambiwa na chama chake kutulia na akazidi tu kurusha mashambulizi, maana yake ni moja kwamba sasa anaamini kwamba yuko juu ya chama, na chama chenyewe ni CCM, ninahisi kwamba ana mpango wa kuingia upinzani,

- Lakini kama that was the ishu hii njia anayotumia sio sawa, kwa sababu asichoelewa ni kitu kimoja tu, kwamba sasa maadui wote wa ndani ya CCM wataungana na kumgeuzia kibao kama Mrema, man! hahitaji hiyo tena huko Mbeya kwa Mzee wangu Mwakipesile the real mtandao ataishia kuumia tu wakati wananchi tunamuhitaji sana ndani ya bunge na serikali kwa ujumla.

- Nyinyi wapambe wake hamumasaidii hata kidogo, kwa sababu hata ile press yake ya mwisho kulikuwa na malalamiko mengi ya chini chini ya viongozi wengi wanaomuunga mkono kwamba ameharibu na anyamaze, sasa this tena kwa kweli tutakao-pay the price ni sisi wananchi wa kawaida, kwa sababu Rostam hawezi fikishwa kwenye sheria na haya tu maneno ya Mwakyembe, ambayo hayana legal facts zaidi tu ya hearsay! Mwakyembe afike mahali aelewe kwamba hayuko juu ya CCM, kama haamini amuulize Komandoo Salmin.

Mungu Aibariki Tanzania.

FMES!
 
- Haya maneno ya kuandaliwa ni upuuzi mtupu, kwani Mwakyembe alilikuta jimbo halina mbunge?

- Halafu huyu anayeandaa wengine lakini yeye hataki uongozi huo huo anaoandalia wengine ni nani hasa hapa bongo?

- Hizi za kuandaliwa mtu ni cheap strategies za kuweka milango wazi ya kutokea iwapo kutakuwa na kushindwa, hakuna anayemiliki jimbo wala anayeandaliwa,

Sio siri kwamba Mwakyembe ana kazi kubwa sana ya kulirudisha jimbo, yeye ni kiongozi makini hana sababu ya malumbano yasiyo na msingi, atulie afanye kazi jimboni, na aelewe kwamba ni haki ya wengine pia kugombea kwa sababu hana umiliki wa jimbo ambalo alimtoa mbunge wmingine kama yeye.

- The bottomline haandaliwi mtu yoyote, isipokuwa ni maneno na matendo yake hasa kwa sasa mpaka uchaguzi ndio yatamuandaa mtu kuchukua jimbo lake, atulie afanye kampeni tutamsaidia, lakini akishaanza malumbano yasiyo na msingi na walioko CC, hajisaidii kabisa ndani ya CCM.

Respect

FMES!
 
Kuna tetesi ambazo nimezisikia hapa, nasema tetesi kwasababu siwaamini wanaozisema. Wanasema Dr. Mwakyembe anatafuta njia ya kuhamia CHADEMA.

Wanasema kwenye mkutano wa leo yule kijana wa CHADEMA aliyewahi kuwekwa ndani wakati ule wa ziara ya JK ndiye alikuwa mbele katika waandaaji. Pia wanataja uhusiano wa Dr. Mwakyembe na Mbowe pamoja na Mengi kama sababu za kuamini hivyo.

Pia inaelekea kuna mpambano mkali unaandaliwa Kyela 2010 kati ya Dr. Mwakyembe na jamaa mmoja nasikia yuko nje ya nchi.

Mimi nilikuwa hapa kwa muda na niliyoyaona leo sina hamu, hii wilaya imegawanyika kweli kweli. Sikuona viongozi wowote wa CCM pale mbele badala yake kulikuwa na wapambe wa mheshimiwa waliokuwa wanamwaga sifa kibao.

Angalieni hili jimbo 2010 inaelekea kutakuwa na vituko.

Ninahofu hiyo tetesi ni ya kweli na hili la Mwakyembe linafanana kidogo na la Muhunzi wa CUF kule Pemba alieamuwa kutafuta sapoti ya CCM kwa kuenda kinyume na msimamo wa chama chake. Naye Mwakyembe anapuuza wito wa chama chake juu ya kukashifiana. Huyu Mwakyembe amekuwemo ndani ya CCM na kuibeba na sera zake za Ufisadi kwa kipindi chote huku akielewa kuwa chama chake kina mafisadi na hata huko kuingia kwao madarakani kulikuwa kwa ufisadi.
Zengwe la Richmond lilikuwa kafara yake na alikubali kutumiliwa na kundi moja la CCM huku akitegemea kuwa atakuwa salama. Matokeo yake ni uhasama na kila mmoja ameruka kivyake na kumuacha yeye mgeni na kwa kuelewa hili ameshajitambuwa kuwa yeye kwa CCM hana chake 2010 na hivyo hasira zake ni kuenda mrama na wengine na bado tutasikia mengi ya kuichafua CCM kutoka kwa Dr kabla hajafukuzwa au kuacha CCM na kujiunga na CHADEMA. Wasiwasi wangu kuwa kutokana na makundi tayari kwao sijui kama hata akigombea kwa kupitia upinzani kama atafanikiwa.
 
Mwakyembe kujiunga na CHADEMA sioni kama ni tatizo, lakini huu si wakati muafaka wa kufanya hivyo kama kweli ana nia ya kujiengua CCM. Kwa maoni yangu Mwakyembe ana nafasi nzuri zaidi ya kubaki CCM na kupambana na mafisadi akiwemo ndani ya chama hicho. Akiamua kuingia CHADEMA wakati huu basi CCM itammaliza kabisa kisiasa maana mashambulizi dhidi yake yatakuwa si ya kawaida lakini hawatakuwa tayari kumshambulia akiwemo ndani ya CCM.

Mwakyembe hawezi hata kidogo kuibadilisha CCM kwani waliomo ni ndumilakuwili wanaoangalia maslahi yao. Mtandao bado una nguvu na makelele ya watu wa CCM ni nje lakini wakifika vikaoni wanafyata. Ni nani ataweza kumgatuwa JK sasa hivi? Hivyo tuna historia ya kumgatuwa Mwenyekiti? Mwakyembe atakaloweza kufanya ni kuomba samahani kwa matamshi yake kama bado anataka ulaji. Akifanya hivyo CCM wanajilabu kuwa wao wanasuluhisha matatizo yao kwa vikao sio majukwaani. Lakini hata akiomba radhi Mtandao hausahau haraka sijui kama hawatamwangusha 2010.
 
Nionavyo mimi humu JF kuna mapandikizi ya mafisadi, kazi yao kubwa ni kuchomekea posts za kutetea au kuvuruga mada iluiyopo dhidi ya mafisadi. Bila shaka wanafanya hivyo kwa malipo maana bila ya fedha hawa hawawezi kutetea chchote, achilia mbali mafisadi -- ni mamluki. Lakini napata faraja kubwa kuona kwamba hawa ni wachache mno, tena mno, idadi kubwa sana ya wanaochangia mada ni wapiganaji wa dhati wa ufisadi, HONGERA SANA!!!!

Hapa hatuongei vitabu vya dini wala hatupo kwenye Bongo Star Search. Tuko kwenye majadiliano na majadiliano yana pande nyingi. Haiwezekani watu wenye akili wote wakawa na mitizamo sawa. Ufisadi hakuna anaeushabikia lakini hatuko tayari kuendeshewa nchi kwa kutegemea vita vya ufisadi. Vita hiyo ni sehemu tu ya maendeleo na tukianza kuachia kila mmoja ajikweze kwa kisingizio ya ufisadi hatufiki pahala. Hivyo Mbunge hana mchango wowote zaidi ya kusema kuwa napigana na ufisadi tumfanye kila kitu katika kuleta maendeleo?
 
Insurgent,
...
Jamani hakuna sehemu hata moja Mwakyembe ameanza kudai credits kutokana na Richmond, kazi kaifanya na aliiwakilisha Bungeni hata kama kuna mtu aliyemsaidia hili sio swala kabisa..Hilo file limeisha fungwa kwake..
Mwakyembe amekuja chafuliwa na kamati ya kutundika kwa posho na lunch hotelini iliyokubali kununua mitambo ya Dowans, hapo ndipo utata ulipoanza na mara zote yeye amekuwa ktk kujitetea..Kaitwa majina yote lakini leo hii kasimama yeye na kuanza kukibadilisha kibao mnaanza kumlaumu tena.. Na ajabu ni kwamba sijaona wala kusikia mtu toka kundi lenu akizungumzia Rostam na jinsi anavyotafuta umaarufu...
Inanipa hofu kwamba yawezekana kweli Rostam kapandikiza watu humu ndani, iweje watu kila siku mnamsakama Mwakyembe lakini hamzungumzi lolote baya kuhusu Rostam hata ile acknowledgement tu ya machafu yake . Picha nzima ni Mwakyembe na Rostam sasa jaribuni kutuambia makosa ya kila mmoja wao inapotokea na sio kudandia Mwakyembe tu inapofikia Rostam kuwa kichwa cha hoja mnaingia mitini..

Mkandara,

Katika suala la kununuliwa mitambo ya Dowans Mwakyembe ametajwa na nani?
Mwakyembe ameingia kwenye mgogoro kwa kutajwa kuwa alikuwa na conflict of intererst juu ya umeme. Alijitetea na kuanzia hapo alikuwa na sapoti nzuri tu. Hata waliomakini wamejaribu kumtahadharisha lakini sikio la kufa.
Hebu angalia watakapofika kikaoni Mwakyembe atakuwa na ushahidi gani kuwa Rostam amemchafua? Makala ya gazeti iliyoandikwa na mtu wa tatu ndiyo inakufanya umtukane mtu majukwaani? RA atakuwa na kesi nzito na NINA HOFU KUWA HILI LILIPANGWA MAKUSUDI KUMPROVOKE na wakubwa wanaoona mbali walipomshauri basi angefuata ushauri lakini hivi anavyofanya sijui kama JF itamsaidia kitu kwa hili.
 
"Habari za kutoka hapa Kyela ni kwamba dr. Mwakyembe leo kamvaa Rostam kweli kweli. Kamwita fisadi namba moja, kaiba mali ya Tanzania na ni mbumbumbu, hajui kitu, hata bungeni haongei. Anasema Rostam katumia ufisadi kuiba viwanda viwili alivyoanzisha Nyerere na sasa kafanya godowns zake."

Umeshamsikia Rostam akifungua kinywa chake Bungeni? Je, wananchi wa jimbo lake walmchagua ili akawe bubu katika vikao vya bunge? Hapo juu Mwakyembe kasema ufisadi mwingine wa Rostam ambao wengi tulikuwa hatuujui wa kuiba viwanda viwili vilivyoanzishwa na Mwalimu (RIP) na inaonyesha alivipata kwa njia za kifisadi. Sasa kama kuyasema hayo si kutetea maslahi ya Taifa sijui wewe unaziweka katika category ipi.

Inaelekea unafaidika kwa namna moja au nyingine na ufisadi wa fisadi Rostam mpaka kufikia kumpa ushauri. Kila la heri katika utetezi wako wa mafisadi.

BUBU, angalia jinsi cheap politics inavyotumiwa na Mwakyembe. Nini lengo la kumtaja Nyerere? kupata sapoti ya wananchi wasioelewa mambo. Nafikiri kwa wewe mwelew unajuwa kuwa viwanda karibu vyote vilivyoanzishwa wakati wa nyerere tuliviua na baadae majengo tukauza. Huoni desperation ya Mwakyembe na badala yake eti unaita kuwa anasema kwa maslaha ya Taifa. Kama ni mfuasi wa Nyerere basi asingekuwa na hisa huku akiwa Mbunge. Najua kuwa hakuna tatizo kuwa na hisa baada ya sisi wenyewe kuamuwa hivyo nakwa njia hiyo hiyo najuwa kuwa hakuna tatizo la kuweka godowns kwenye majengo ya kiwanda tulichokiuwa.

Mkuu shujaa wetu kaamuwa kututelekeza na kutetea maslahi yake kwa kutumia migongo yetu.
 
Ninahofu hiyo tetesi ni ya kweli na hili la Mwakyembe linafanana kidogo na la Muhunzi wa CUF kule Pemba alieamuwa kutafuta sapoti ya CCM kwa kuenda kinyume na msimamo wa chama chake. Naye Mwakyembe anapuuza wito wa chama chake juu ya kukashifiana. Huyu Mwakyembe amekuwemo ndani ya CCM na kuibeba na sera zake za Ufisadi kwa kipindi chote huku akielewa kuwa chama chake kina mafisadi na hata huko kuingia kwao madarakani kulikuwa kwa ufisadi.
Zengwe la Richmond lilikuwa kafara yake na alikubali kutumiliwa na kundi moja la CCM huku akitegemea kuwa atakuwa salama. Matokeo yake ni uhasama na kila mmoja ameruka kivyake na kumuacha yeye mgeni na kwa kuelewa hili ameshajitambuwa kuwa yeye kwa CCM hana chake 2010 na hivyo hasira zake ni kuenda mrama na wengine na bado tutasikia mengi ya kuichafua CCM kutoka kwa Dr kabla hajafukuzwa au kuacha CCM na kujiunga na CHADEMA. Wasiwasi wangu kuwa kutokana na makundi tayari kwao sijui kama hata akigombea kwa kupitia upinzani kama atafanikiwa.

- Good analysis, unless Mwakyembe ana ni aya kujiunga na upinzani, then anayoyafanya sasa makes sense, lakini kama ni kubali CCM na kwenda kinyume cha maagizo ya chama chake sijui ni strategy gani anayoifikiria,

- Kama lengo lilikuwa kupingana na ufisadi, then unasema exactly how Rostam stole our money, lakini anamiliki baada ya kuiba viwanda viwili vilivyoanzishwa na Mwalimu, that is all?

- I mean kama sio njia za kifisadi kutumika Mwakyembe angekua bado yuko kule chuoni anachora chaki ubaoni, angekua bado bubu kule EAC, hapendi ufisadi aseme yote, sasa akishaanza kuwakaidi hata waliomfikisha alipo inakuwa vigumu sana wengine kumuelewa analenga nini? Na wapi?

- Ndio maana ninasema ninamuona akihamia upinzani, kwa sababu akienda mbele ya CCM, ni nani atakayemuunga mkono kiongozi aliyekaidi maagizo ya CCM? Hata Chadema walipomuambia Wangwe asubiri vikao, alipogoma walimsimamisha uongozi, sasa why is Mwakyembe doing this tunashindwa kupata jawabu,

- Labda anatafuta sympathy na wananchi, lakini bila kusema legally what is his or our case against Rostam, hatusaidii wananchi na taifa ingawa sio siri anapata cheap popularity kama ya Mrema mwanzoni alipotoka CCM, unless anatayarisha political gorund work ya kuingilia upinzani then it makes sense anyoyafnya sasa hivi.

- Ukweli ni kwamba after this Mwakyembe amewaweka pabaya sana wale wote viongozi muhimu wanaom-support kwa chini chini, na hata publicly kwa sababu sioni anacholenga zaidi tu ya kuingia upinzani, watamsaidiaje kwa kumshambulia kiongozi mwenziwe ambaye hajawahi kumshambulia hadharani zaidi tu ya kujibu tu mashambulizi yake last time tena kwa one sentence?

- Hapa ninaacha wazi scenario moja tu ambayo imewahi kutumika in the past, kwamba is Muungwana behind him? Kwamba do it ili niwatose kina Rostam kwenye uchaguzi ujao? Hii scenario ni very attempting, lakini can Muungwana pull urais bila Rostam and the gang? Ili atafute urais na nani? Majuzi kwenye matatizo ya UV-CCM Muungwana took Nchimbi's side against his son over Isaack aliyekuwa katibu wa muda wa umoja huo,

- Na ni jana amemteua Isaack Nchimbi's man kuwa DC, kwenye uchaguzi wa uwt wote yaani Muungwana na Rostam's gang walikuwa one side ya Auntie Sophia, eti sasa Muungwana anataka kuwageuka wenzake kwa kumtumia Mwakyembe? Wengine mnisaidie kufikiri, lakini until nitakapopata the inside bado ninaziamini hizi scenario mbili, na ni mawazo yangu tu!

1. Mwakyembe anataka kujiunga na upinzani, hii ninaipa 90%.

2. Muungwana anamtumia ku pull a monkey over Rostam and the gang 10%.

Wazee wa sauti ya umeme FMES!
 
Sina mengi ya kusema bali 'MGEMA AKISIFIWA POMBE HUITIA MAJI'.
Haya ngoja tumsikie Six atambeba kwa mbeleko gani, maana anayoyafanya Dr. ni wazi kuwa hali yake ni mbaya sana juu ya tuhuma za mgongano wa kimaslahi zilizotolewa hivi karibuni.
"Ukiuwa kwa upanga basi na we mauti yako yatakuwa ni kwa upanga tu"
 
- Good analysis, unless Mwakyembe ana ni aya kujiunga na upinzani, then anayoyafanya sasa makes sense, lakini kama ni kubali CCM na kwenda kinyume cha maagizo ya chama chake sijui ni strategy gani anayoifikiria,

- Kama lengo lilikuwa kupingana na ufisadi, then unasema exactly how Rostam stole our money, lakini anamiliki baada ya kuiba viwanda viwili vilivyoanzishwa na Mwalimu, that is all?

- I mean kama sio njia za kifisadi kutumika Mwakyembe angekua bado yuko kule chuoni anachora chaki ubaoni, angekua bado bubu kule EAC, hapendi ufisadi aseme yote, sasa akishaanza kuwakaidi hata waliomfikisha alipo inakuwa vigumu sana wengine kumuelewa analenga nini? Na wapi?

- Ndio maana ninasema ninamuona akihamia upinzani, kwa sababu akienda mbele ya CCM, ni nani atakayemuunga mkono kiongozi aliyekaidi maagizo ya CCM? Hata Chadema walipomuambia Wangwe asubiri vikao, alipogoma walimsimamisha uongozi, sasa why is Mwakyembe doing this tunashindwa kupata jawabu,

- Labda anatafuta sympathy na wananchi, lakini bila kusema legally what is his or our case against Rostam, hatusaidii wananchi na taifa ingawa sio siri anapata cheap popularity kama ya Mrema mwanzoni alipotoka CCM, unless anatayarisha political gorund work ya kuingilia upinzani then it makes sense anyoyafnya sasa hivi.

- Ukweli ni kwamba after this Mwakyembe amewaweka pabaya sana wale wote viongozi muhimu wanaom-support kwa chini chini, na hata publicly kwa sababu sioni anacholenga zaidi tu ya kuingia upinzani, watamsaidiaje kwa kumshambulia kiongozi mwenziwe ambaye hajawahi kumshambulia hadharani zaidi tu ya kujibu tu mashambulizi yake last time tena kwa one sentence?

- Hapa ninaacha wazi scenario moja tu ambayo imewahi kutumika in the past, kwamba is Muungwana behind him? Kwamba do it ili niwatose kina Rostam kwenye uchaguzi ujao? Hii scenario ni very attempting, lakini can Muungwana pull urais bila Rostam and the gang? Ili atafute urais na nani? Majuzi kwenye matatizo ya UV-CCM Muungwana took Nchimbi's side against his son over Isaack aliyekuwa katibu wa muda wa umoja huo,

- Na ni jana amemteua Isaack Nchimbi's man kuwa DC, kwenye uchaguzi wa uwt wote yaani Muungwana na Rostam's gang walikuwa one side ya Auntie Sophia, eti sasa Muungwana anataka kuwageuka wenzake kwa kumtumia Mwakyembe? Wengine mnisaidie kufikiri, lakini until nitakapopata the inside bado ninaziamini hizi scenario mbili, na ni mawazo yangu tu!

1. Mwakyembe anataka kujiunga na upinzani, hii ninaipa 90%.

2. Muungwana anamtumia ku pull a monkey over Rostam and the gang 10%.

Wazee wa sauti ya umeme FMES!

Hii assumption ya pili sio kabisa kwani kinachoonekana hapa ni deseparation ya Mwakyembe against cool calculation ya RA.
Mimi bado naamini kuwa Mwakyembe amatanabahi kuwa alifanywa mbuzi wa kafara na sasa amebaini kuwa ngoma aliyocheza ni nzito. Naamini pia kuwa anaelewa hata akienda upinzani hatofanikiwa na hivyo ameamuwa to hell to whatever may come. Si unakumbuka aliposema kuwa hana mkataba na Bunge anayo profession yake? Kauli ile ilikuwa na maana kubwa.wabunge machachari wanalikiuka hili na kibaya MZEE MALECELA keshajikosha kuwa yeye anamuunga mkono JK. Patamu hapo.
Hebu angalia hata
 
Mwakyembe inaelekea kuwa yuko so bitter...yaani vagi lake na Rostam juzi jumamosi alilihamishia kwenye fainali ya kombe la NSSF kwenye mechi ya timu ya UHURU v/s HABARI CORP.

So sad huyu jamaa nilikuwa namheshimu miaka ileee alipokuwa na kile kiofisi chao cha LEGAL AID na Dr MVUNGI pale kwenye jengo la SUKITA enzi hizo Mwakyembe alikuwa ni mtu kweli kweli sasa tangu aingie kwenye siasa amekuwa kama mwehu vile

Mpka leo sielewi what was the point ya kupandishana pesa jumamosi...lakini ndio hao wanasiasa wetu

AMA KWELI PESA MWANA HARAMU

Lakini hata kama akitambika uchi huyu mwakyembe, ukweli utabaki pale pale kuwa yeye ni miongoni mwa wale wabunge waliokula milioni 5 za Rostam wakati wa Kampeni sasa leo hii asitake kujidai yeye ni msafi kuliko wote.

In short Rostam ni kama Nyerere tena naweza kusema zaidi kwenye hii game ya Politics za TZ, Maana mwalimu yeye alikuwa ni mcheza Game kwenye politics tuu lakini Rostam ni mpaka Biashara in other words HE OWNS THE CURRENT RULING ELITES na hawana cha kumfanya baada ya kula pesa zake

So Mwakyembe should spare himself further embarrassment kuendelea kutukanana na mtu ambaye hamjibu except ana rewind ule mkanda wa makabidhiano now and then

Mwisho zaidi nasema I CANT KNOCK ROSTAM'S HUSTLE....jamaa ni mtafutaji na anaitumia opportunity anavyoona itamnufaisha

Ugonjwa wetu mnajua tatizo lake lilianzia wapi na dawa yake wote mnaijua
 
FMES,
Jinsi ninavyoona ni kuwa Dr. amenogewa na ubunge na sasa anaona ameshafanya blunders ambazo zinaweza kumgharimu kisiasa kwa hiyo anatafuta kuhakikisha aendelee kuwepo ndani ya duru za bunge baada ya 2010.
Dalili za kuanza kuishiwa na hoja ndiyo hizi, unatafuta cheap popularity. Kama unakumbuka katika press conference aliyoifanya Dar, alijaribu kukwepa kujibu maswali ya msingi na kutafuta mambo ambayo wananchi watamwonea huruma, kama vile sisi waafrika hatupewi mikopo, suala la malipo ya umeme kwa wazalishaji wa nishati hizo nk, mambo ambayo yako bungeni na yanajadiliwa huko kufikai mwafaka. kitendo chake cha kuyaongele pale ilikuwa ni kukwepa hoja ya msingi na kutaka kupata sympath ya wananchi. Na kitendo cha kumvaa RA ndiyo kimeonesha kuwa huyu Dr si makini kabisa na hili linadhihirika kwa jinsi alivyoshindwa kuelwa hoja ya msingi iliyopo juu yake.
Lakini wacha aendelee kufanya hivyo kwani ni sawasawa na kucheza tombola hana uhakika what will be next. Mzee Malecela alionya kuwa mchezo wanaocheza hauna manufaa kwa chama na kwa umma lakini anaendelea kukaidi, maana yake ni nini, ni kwamba ana nguvu nyingi ambayo anaweza kitumia nje ya chama chake.
Historia inatuonesha kuwa wale wanaotoka CCM kwa staili kama yake huwa nimizigo au wavurugaji katika vyama wanavyohamia. Si dhani hata kama Dr leo atahamia CHADEMA kama atakuwa ni msaada kwa chama hicho kwa ni hulka ya yake ya kudharau viongozi kwa kujiita kuwa yeye ni msomi hataiwacha, guess what akiwa CHADEMA?
 
Back
Top Bottom