Tujikumbushe: Dr. Mwakyembe apelekwa India kwa matibabu ya ugonjwa wa ngozi usiojulikana

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Dr. Harrison Mwakyembe1.jpg
Mwakyembe2.jpg

Monday, October 10, 2011
KUTOKANA NA HALI KUENDELEA KUBADILIKA DR,HARRISON MWAKYEMBE APELEKWA INDIA KWA MATATIBABU ZAIDI

10_11_zatmhv.jpg

Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe wakati alipomtembelea nyumbani kwake Kunduchi Mtongani Dar es Salaam. (Picha na Freddy Maro)

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe amepelekwa katika Hospitali ya Apollo nchini India kwa matibabu baada ya hali ya afya yake kuwa tete kwa kuugua ugonjwa unaomsababishia kuvimba mwili wake. Akizungumza na gazeti hili, Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa (CCM), alikiri kuwa Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, anasumbuliwa na maradhi hayo na amesafirishwa jana kwenda India kwa matibabu zaidi.

“Ni kweli Mheshimiwa Waziri ameondoka leo (jana) mchana na ndege ya Qatar Airline kwenda India kwa matibabu zaidi,” alisema Mwambalaswa ambaye kama Dk. Mwakyembe anatoka mkoani Mbeya. Kwa mujibu wa Mwambalaswa, hali ya Dk. Mwakyembe si mbaya sana kwa kuwa anaweza kula na kutembea vizuri ingawa bado amevimba baadhi ya sehemu mwilini.

Dk. Mwakyembe anadaiwa kusumbuliwa na ugonjwa wa ngozi unaojulikana kitaalamu kama Exfoliative Dermatitis na alianza kusumbuliwa na ugonjwa huo zaidi ya miezi mitatu iliyopita, lakini kwa sasa hali ya ugonjwa huo imezidi kuwa mbaya. Kwa upande wake, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda alisema hana taarifa za kuugua kwa Dk. Mwakyembe kwa kuwa alikuwa safarini, lakini aliahidi kuzungumzia suala hilo baada ya kupata ripoti zaidi.

Mwakyembe alizungumza juzi na gazeti moja la kila siku na kukiri kuwa anaumwa na kwamba hata sura yake imebadilika huku akikanusha madai ya kulishwa sumu. Ugonjwa unaomsumbua Dk. Mwakyembe unadaiwa huathiri wanaume na wanawake wenye umri kuanzia miaka 55 na dalili zake ni kuwashwa, mwili kuishiwa nguvu na sehemu ya juu ya ngozi kupukutika.

Chanzo cha ugonjwa huo hakijajulikana, lakini kinahusishwa na magonjwa ya ngozi na madhara ya matumizi ya dawa mbalimbali. Hospitali ya Apollo aliyopelekwa Dk. Mwakyembe, ndiko alikolazwa Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya kwa muda mrefu sasa, baada ya kufanyiwa upasuaji wa mgongo, ambaye kwa sasa hali yake imeelezwa kuendelea vizuri. Juzi, Rais Jakaya Kikwete alikwenda kumjulia hali Dk. Mwakyembe nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam.
 
Liende tu, tena likawekeee midripu itakayochukua miaka 6 ili akute uchaguz wa TLS ushafanyika. Bora lisepe tu
 
Mahakama za mafisadi zimekosa wahalifu. Escrow,lugumi,richmond ni baadhi ya ufisadi. Kweli bado hakajapona. Na wasiwasi naye kuwa huenda alifanyiwa mitihani. Au ukiwa mwanasheria lazima uwe mwongo mwongo
 
Nilikutana naye Mlimani City nikamshika mkono alikuwa anatoka Mbeya siku hiyo na JK alikuwa huko. Nasema hivi ili kama yumo humu anikumbuke. Yeye mwenyewe anajua alichoniambia ila mikono yake ilikuwa kama gamba la nyoka. Ukimshika ni kama umeshika ngozi ya kenge. Atueleze msaidizi wake alifariki vipi na kuzikwa mbeya kiharaka haraka. Anajua na aje hapa akanushe.
 
Back
Top Bottom