Dr. Helen Kijo Bisimba kamjia juu mkuu wa mkoa wa Dar kwa matamshi yake

Kwa wale waliosikiliza hotuba ya Tundu Lissu na mfano wa moto huko Ujeruman wanajua maana yake.....If you missed that masterpiece, very sorry..
 
Kwanini mnashangaa kauli ya makonda?,,hivi mtaani kwako ukimkamata mwizi wa spika unampeleka polisi? si unampiga na kumuua na polisi wanakuja kuchukua mzoga!,usishangae kauli ya makonda kabisa
 
Huyo mama mbona walivyouliwa police hajasema neno lolote...
Ndio hayo maajabu ya huyu mama alikuwa mzuri sana kwa sasa amwshikiwa akili zake na wapinzani. Yaani Tamko tu analivalia njuga. Lakine kitendo cha polisi kuuawa kawa kimya sina imani nae tena!
 
Hata useme kwa herufi kubwa, ongeza na font kabisa ulichoandika hapo ni ujinga mtupu.
Kufiwa na yeyote yule sio sababu ya kuchukua harsh decisioms kama zile ambazo zitaishia kuua watu wasio na hatia, mahakama ipo kushughulikia watu kama hao, we ndugu yako auliwe na jambazi, alafu polisi wamkamate mtu yeyote ambaye hawana uhakika kama alihusika, wakampiga bila uchunguzi kwanza na kumuua ikaja gundulika hakuhusika, moyo wako utaridhika?

Hakuna chochote kinachojustify upumbavu, hata uje na mifano milioni. Siku hizi kila kiongozi mbabe, na tatizo wengi vila,za, mtakaoumia ni nyie wenyewe, yeye kila,za atakua anasuuza macho tu na kuuza headlines kwenye media.
ACHA UJINGA NA WEWE NA HATA UPUUZI aliousema huyo mama kijo Bi Simba
fuatilia Clip sio kumparamia mtu yeye ni nani amsema Makonda?mbona sijasikia waliosemwa ni kuna matamshi ya kuwatishia viongozi wa Vyama, Serikali Polisi na wananchi
Wanaosema
  • UKUTA
  • Dikteta UCHWARA
  • TUTAWASHUGHULIKIA
  • viberiti vya gesi
  • SIJARIBIWI
chuki zako ni binafsi na ninjama moja na mleta Mada (Uzi)
 
Huyo mama mbona walivyouliwa police hajasema neno lolote...
Wangetoa maneno gani zaidi ya Pole kwa Askari. Hivi ukimlaani Jambazi kwa mauaji si sawa na kumpigia mbuzi gitaa. Jambazi kazi yake ni kuua na anakuwa mtu ambaye ameshatokwa na ubinadamu. Lakini askari polisi kazi yake ni kulinda raioa pamoja na mali zake. Pia kumbuka sio kazi ya polisi kuua bali ni kushitaki mahakamani na mahakama ndio itatoa hukumu kulingana na uthibitisho wa makosa. Hebu imagine majambazi yaliyoua yakawa yanafukuzwa na kuingia nyumbani kwako halafu polisi waseme hii nyumba wote ni majambazo tupige risasi tuue wote. Je na wewe utakuwa jambazi?
 
Yaani haki za binadamu kwa majambazi. Ndugu waliouawa nani anawapa haki zao?
Unaelewa vizuri kazi ya mashirika ya kutetea haki za binaadamu?.alafu unalinganishaje hayo matukio ilhali hayafanani?.mauwaji ya binaadamu (yoyote yule)ni tafauti na kutoa amri/kuitekeleza amri ya kupigwa/kugongwa mtuhumiwa wa uhalifu kwasababu si kila mtuhumiwa huwa na hatia.na ndio maana serikali na dunia nzima ikaamua kuweka kitu kinaitwa "due process",kwamba mtuhumiwa wa kosa lolote hatakiwi kuadhibiwa kabla ya kupelekwa mahakamani tuhuma kuthibitika na kuhukumiwa kwa kufuata katiba

Due process - Wikipedia, the free encyclopedia

Kutia uhai wa polisi wasio na hatia ni unyama,ukatili na kitendo kisicho kubalika lakini kuruhusu watuhumiwa wapigwe kabla ya kufikishwa mahakamani kwa sababu tu wamehisiwa kuhusika ni uvunjaji wa sheria na katiba na abuse yahaki za binaadamu tulizokubali kujicomit nazo kwenye mikataba ya kimataifa na ni na ni kazi ya mashirika yanayoshuhulika na haki za binaadamu na wapenda utawala wa sheria wote kukemea uvunjwaji huo.
Nadhani umenielewa

Presumption of innocence - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Tunza haki za wenzio upewe haki yako,
Mtu muuaji asiethamini maisha ya mwingine na wengine wanaomtegemea utasimamaje na kumpigania haki yake??

Acheni unafki, ungekuwa ni wew ndugu yako, mlezi wako ndio kauwawa usingekuja mbele za watu na kutoa mimate eti utawala wa sheria ufatwe.
 
Namuunga mkono mama HELEN KIJO. Kauli kama hizi zinaweza kusababisha hata wananchi kujichukulia hatua mkononi na kuua watuhumiwa wa uhalifu.
 
Huyo mama mbona walivyouliwa police hajasema neno lolote...
Watetezi wa haki za binadamu wnatetea raia wanaonyimwa haki...wasioweza kujitetea kwa silaha au kwa maneno....Raia wakiunda kundi na kubeba silaha kuanza mapigano hawatetewi na hawa wanaharakati...polisi ni kundi lenye nguvu..
 
Huyo mama mbona walivyouliwa police hajasema neno lolote...

huyu mama si unaona hadi lafudhi y huku kwetu , shirimatunda, ni KADA MAARUFU wa CDM wameuwa police wetu yeye yuko kimya , kwa analolitaka kutokea limetokea
 
Usiombe ndo ndugu yako au kaka yako au baba yako ndo ameuwawa na majambazi sizani kama utalipinga hili la Makonda

Baada ya baba yako, kaka yako etc ambao ni polisi kuuawa na majambazi, alafu siku chache kadhaa mjomba wako, mdogo wako etc. wanauawa na polisi kufuatia agizo la makonda. Njia ya kutatua matatizo haipaswi kuzalisha matatizo mapya.
 
Huyo mama mbona walivyouliwa police hajasema neno lolote...
mama Helen anahusika na haki za binadamu. sasa polisi kumpiga raia na kumfanyia vitendo vyovyote vinavyokiuka katiba na haki za binadamu lazima vikemewe kwa nguvu zote. lakini tukio la ujambazi halihusiani na tumevya haki za binadamu.
 
Huyu mama ni mnafiki mkubwa angekuwa mwanachadema kauwawa saa kumi nambili asubuhi tungemsikia akilalama aache unafiki
 
Kweli kbsa
Makonda alionyesha jazba kwenye msiba wa askari waliouawa na anaweza kusamehewa kwa jazba zile kutokana na uzito wa msiba ule lakini mbona wao hawakuenyesha hisia zozote zile za kulani kitendo kile cha kinyama?????? Au ndiyo hivyo tena 'Mkuki kwa binadam mchungu?'
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom