Ni kweliKweli kbsa
Ni kweliKweli kbsa
Kufuatia tamko alilolitoa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Ndg Paul Makonda juu ya wahalifu wakamatwe wapigwe na wakimuuliza wampeleke kwake mwanamama shupavu na mpigania haki za binadamu amenukuliwa akisema hivi;
"Kongozi wa ngazi ya mkoa hapaswi kuongea kwa jazba. Ni kweli inaudhi na kuhuzunisha majambazi au mtu yeyote kufanya yaliofanyika Mbande . Lakini jawabu si kauli kama hizi. Tuna sheria nzuri zichue mkondo wake".
Kama ya Ukuta.. na kubadili gia AnganiUtawala wa sheria subirini baada ya 2020 hivi sasa tuna utawala wa matamko tu
Kwani Makonda aliwaongelea majambazi?Usiombe ndo ndugu yako au kaka yako au baba yako ndo ameuwawa na majambazi sizani kama utalipinga hili la Makonda
Nakubaliana nawe moja kwa moja kuwa inapotokea jambazi au mtu yeyote amesababisha kifo cha raia asiye na hatia inauma sana.Usiombe ndo ndugu yako au kaka yako au baba yako ndo ameuwawa na majambazi sizani kama utalipinga hili la Makonda
Hata useme kwa herufi kubwa, ongeza na font kabisa ulichoandika hapo ni ujinga mtupu.
Kufiwa na yeyote yule sio sababu ya kuchukua harsh decisioms kama zile ambazo zitaishia kuua watu wasio na hatia, mahakama ipo kushughulikia watu kama hao, we ndugu yako auliwe na jambazi, alafu polisi wamkamate mtu yeyote ambaye hawana uhakika kama alihusika, wakampiga bila uchunguzi kwanza na kumuua ikaja gundulika hakuhusika, moyo wako utaridhika?
Hakuna chochote kinachojustify upumbavu, hata uje na mifano milioni. Siku hizi kila kiongozi mbabe, na tatizo wengi vila,za, mtakaoumia ni nyie wenyewe, yeye kila,za atakua anasuuza macho tu na kuuza headlines kwenye media.
Sasa kwa kauli hiyo ndo ataondoa ujambazi?Pinda aliwahi kusema wapigwe tu lakin cha kushangaza ni askari ndo walizidi kupigwa na kuuawa na majambazi.Kiongozi ni busara sio jazba.
Kwa makusudi mnapenda kujitoa ufahamu. Kuna mahali umeambiwa polisi watamkamata mtu yoyote na kuchukua hatua ya kumpiga bila uchunguzi? Umeambiwa wahalifu wakamatwe, sasa ukishakuwa muhalifu kuna kuuliza tena? Ukishakuwa muhalifu utakamatwa, utapigwa na pengine hata kuuwawa yote yanawezekana!
Maoni YanguYaani haki za binadamu kwa majambazi. Ndugu waliouawa nani anawapa haki zao?