Dr. Hamis Kigwangalla, Kugoma ni sawa?

Salaam,nimeskia katika Radio moja ikisoma Magazeti kuwa Tahariri inamlaani Dr(mb)Hamis Kigwangala kugomesha madaktari wenzake,
Napenda mnisaidie kujua ni sawa kwake kama Mbunge kfanya hivyo?au kama Daktari ni sawa kuacha wagonjwa wafe kwa ajili ya posho?naomba sana kujua kutoka kwenu....

Hapo hajagoma kama Mbunge. Amegoma kwasababu na yeye ni daktari. Kama tunawa-support madaktari wengine kugoma ili walipwe stahili zao kwanini tuna question kugoma kwa Dr Kigwangala? Anajua kwamba ipo siku anaweza kuacha ubunge akarudi kwenye fani yake.
 
Kinachofanywa na Kigwangala ni uhuni na unafiki tu, si kweli kwamba anakubali kuwa serikali ya Kikwete si sikivu; na sio kwamba haijali wafanyakazi tu bali na hata wananchi kwa ujumla wao. Rais mwenyewe alishaonyesha kwa mifano jinsi ambavyo wafanyakazi wa nchi hii wasivyo na kipaumbele chochote kwake cha maana, alishaahidi kuwatwanga risasi endapo watamkosesha usingizi, sasa wafanyakazi wategemee nini kutoka kwa watendaji wengine?

Hawa wote ni sawa na nyani, tumbili, ngedele, kima na nguruwe kwenye shamba linaloitwa Tanzania, na wataendelea kuliharibu mpaka pale wenye shamba (waTanzania) watakapoamua kulilinda shamba lao!
Teh teh teh teh vipi siku hizi watumishi wa umma hamummiss Kikwete?

Maana enzi zile Kikwete aliposema, "Kama watumishi mnataka niwaongezee mishahara niko tayari kukosa kura zenu." watu walimtafsiri vibaya kwamba "Kikwete hataki kura za watumishi wa umma."
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom