Dr. Chitage: Mashine moja ya CT scan ni sawa na bei ya Toyata shangingi moja!

Ok Zomba, lets say upo right. sasa tupe faida ya shangingi over CT scan kwa waTz.

Mheshimiwa mbowe anakwenda nayo sita pale mkutanoni, mbona hatuulizi faida na hasara yake? kadanganya umma kuwa amelirudisha la Serikali, tukabainishiwa kuwa njia ya mnafiki ni fupi kalichukuwa tena.

Na huyu daktari na taaluma yake yote bado anasema uongo. Hapo hujaweka gharama za "consumables", hapo hujaweka gharama za wataalaam wa CT scan, kuwafundisha kuitumia na kuwafundisha mdaktari kujuwa kusoma report za CT Scan.

Msiwe mnadanganywa kijinga na kuwa eti ni daktari tu anaetetea maslahi yake kwa kuuwa wananchi.

Mbona hamsemi kuwa wamepelkwa vijana nje kusomea kufanya opereshen za moyo? mbona hamsemi kuwa kimefunguliwa kituo cha kufundisha madaktari wa moyo? mbona hamsemi kuwa wamepelekwa vijana kusomea magonjwa ya mishipa midogo? mbina hamsemi kuwa kwa sasa tunaweza kufanya opereshen za moyo hapa Tanzania. Na pia mseme kuwa hayo ypte ni wakati wa Kikwete, na pia mseme kuwa mashine za CT scan ziliopo kwa sasa ni wakati wa Kikwete ndio zipo. Mbona hayo yote mnakaa kimya? yalikuwepo kabla ya Kikwete? wacheni unafik, kuweni wakweli.
 
Katibu wa jumuiya ya madaktari nchini ameweka wazi kuwa bei ya mashine moja ya CT scan ni sawa na bei ya kununulia shangingi moja.Alisema kama serikali ingekuwa na nia ya kununua mashine hiyo isingeshindwa. kwa habari zaidi soma gazeti la mwananchi la leo. Binafsi habari hii imichefua na kunisikitisha kuona ni jinsi gani serikali yete inavyoendekeza anasa wakati inashindwa kutoa huduma za msingi kwa watu wake.Mashine ya CT scan pale muhimbili kwa mujibu wa vyombo vya habari imekuwa mbovu kwa muda wa miezi saba ila serikali inapiga dana dana kuitengeneza na matengenezo yake ni kama milioni mbili hivi kama sikosei.Kama nimekosei hiyo gharama ya matengenezo mwenye uhakika atujuze. Mbali na mashine hiyo kuna hospitali zingine hapa nchini hazina hata x-ray machine.Kama uliangalia taarifa ya habari ya ITV juzi usiku tatizo la kukosekana kwa mashine ya x-ray liliripotiwa ktk hospitali ya serikali mkoani Tanga ambapo mtu aliepata ajali alishindwa kuhudumiwa kutukona na kukosekana kwa mashine hiyo. Nasema hii ni aibu kwa serikali na inabidi kwenye katiba mpya tupitishe uamuzi wa kutaka viongozi wa serikali nao watibiwe hapa nchini na ipige marufuku viongozi kutibiwa nje ya nchi.Labda hii itasaidia kuondoa dhuluma hii. Sasa madaktari wanapogoma nani wa kulaumiwa kama sio serikali?Hivi haya ndio maisha bora kwa kila mtanzania!

Haya maneno nimeyapenda sana.Hawa viongozi wenye tabia za Kuhuuni wanatufanya watanzania ni wajinga sana.Wanakusanya kodi zetu sisi walalahoi wao wanakwenda kutibiwa ulaya/india,hii ni dhihaki .
 
Niliwahi pitia taarifa moja toka Wiizara ya Afya kwa mwaka 2010 iliyoonyesha kuwa, kati ya X-ray machines 350 zilizokuwepo nchini mwaka huo, 75 zilikuwa mbovu (21.4 %), na kati ya utra Sound machine 251 zilizokuwepo nchini mwaka huo, 8 zilikuwa mbovu (3.2 %). Vilevile kati ya viti 477 vya kutumia kutumia kutibia meno, 77 vililikuwa vibovu (16.1 %), na kati ya X ray machine 58 za kuchunguzia meno, 17 zilikuwa mbovu (29.3 %). Takwimu hizi hazioonyesh dalili njema kuhusu upatikanaji wa huduma za vipimo vya huduma za afya kwa watanzania. Kwa mwaka jana, na huu sijui kama ndiyo hoi zaidi au nafuu maradufu. Nendeni Wizara ya Afya mukawaulize, au tembelea website yao (Ministry of Health & Social Welfare) labda waweza ambulia kitu, (mimi nimejaribu nimeshindwa kupitia simu yangu ya kizamani).

Nani alioziharibu?

Kuna mashine za kupima virusi vya vvu zilipelekwa Tumbi hospital, na zikamiminiwa maji ili ziharibike eti kwa sababu kwanini kachaguliwa fulani ndio akafundishwe hizo mashine. Uliza hili Tumbi, linajulikana.

Sasa kama vifaa vinaletwa na haohao wanafanyiana roho mbaya mpaka kuviharibu eti kwa sababu mtu hakuchaguliwa yeye kusomeshwa hizo mashine, halafu mulaumu Kikwete. Wacheni hizo.

Kikwete kwenye sekta ya Afya kafanya kuliko yeyote wa kabla yake na takwimu za kungezeka kwa life span yetu kwa miaka 5 kwa kipindi chake tu kinathibitisha hilo. Wacheni kuwa wanafik.

Huyu daktari kaja hapa anadanganya na nyinyi mnakubali tu, hamchukui hata dakika moja kuuthamini ukweli.

Nimewaletea data hapo za mashine za CT scan, zinaonesha kwa uchahe kama hauna $ 1,000,000/= (million moja) huwezi kupata CT scan ikafanya kazi ipasavyo, labda uinunuwe uje kuiweka urembo.
 
Bei ya gari aina ya Landcruiser V8 model ya kawaida ya mwaka 2012 kabla ya usafirishaji na kodi zote ni £62,285 au US 97,196 au Tshs 151,740,000/= kwa exchange rate ya BOT leo. Kumbuka hii ni model ya kawaida na hizi bei ni kabla ya usafirishaji na kodi zote. Ukiagiza special utashangaa bei yake!!!

toyota-landcruiser v8.jpg
 
Nani alioziharibu? Kuna mashine za kupima virusi vya vvu zilipelekwa Tumbi hospital, na zikamiminiwa maji ili ziharibike eti kwa sababu kwa nini kachaguliwa fulani ndio akafundishwe hizo mashine. Uliza hili Tumbi, linajulikana.

Labda zimepita usable time span yake, au kukosa maintanance, au watumishi waliopelekwa mafunzo kuzitumia siyo wale wanaozitumia!! Hapa zaweza kuwepo sababu multiple, mojawapo ni ile uliyobaininsha wewe kwa mfano wa hapo Tumbi Kibaha. Makubwa!!!
 
Nani alioziharibu?

Kuna mashine za kupima virusi vya vvu zilipelekwa Tumbi hospital, na zikamiminiwa maji ili ziharibike eti kwa sababu kwanini kachaguliwa fulani ndio akafundishwe hizo mashine. Uliza hili Tumbi, linajulikana.

Sasa kama vifaa vinaletwa na haohao wanafanyiana roho mbaya mpaka kuviharibu eti kwa sababu mtu hakuchaguliwa yeye kusomeshwa hizo mashine, halafu mulaumu Kikwete. Wacheni hizo.

Kikwete kwenye sekta ya Afya kafanya kuliko yeyote wa kabla yake na takwimu za kungezeka kwa life span yetu kwa miaka 5 kwa kipindi chake tu kinathibitisha hilo. Wacheni kuwa wanafik.

Huyu daktari kaja hapa anadanganya na nyinyi mnakubali tu, hamchukui hata dakika moja kuuthamini ukweli.

Nimewaletea data hapo za mashine za CT scan, zinaonesha kwa uchahe kama hauna $ 1,000,000/= (million moja) huwezi kupata CT scan ikafanya kazi ipasavyo, labda uinunuwe uje kuiweka urembo.

Ok Zomba tufanye upo sahihi kwa hizn data zako.Sasa inashindikana nini kuwa hata na CT Scan hata 5 tu kwenye kanda zote nchini?Kwa iyo bei ulioweka hapa inaonekana ni bilioni 8 tu zingetosha kwa kuanzia kuwa na hizo mashine tano.Kwenye hizo trilioni 5 taifa linazotumia kwa magari ya uheshimiwa ingewezekana tu kupata magari ya idadi hiyohiyo lakini sio ya kifahari kihivyo pamoja na kuwa na vifaa muhimu mahospitalini.
 
Bei ya gari aina ya Landcruiser V8 model ya kawaida ya mwaka 2012 kabla ya usafirishaji na kodi zote ni £62,285 au US 97,196 au Tshs 151,740,000/= kwa exchange rate ya BOT leo. Kumbuka hii ni model ya kawaida na hizi bei ni kabla ya usafirishaji na kodi zote. Ukiagiza special utashangaa bei yake!!!

Hapo bado hujapata CT scan, wachilia mbali chumba, utaalaam (mafunzo), "consumables".

Huyo dokta alikuwa anaota.
 
Nani alioziharibu? Kuna mashine za kupima virusi vya vvu zilipelekwa Tumbi hospital, na zikamiminiwa maji ili ziharibike eti kwa sababu kwanini kachaguliwa fulani ndio akafundishwe hizo mashine. Uliza hili Tumbi, linajulikana. Sasa kama vifaa vinaletwa na haohao wanafanyiana roho mbaya mpaka kuviharibu eti kwa sababu mtu hakuchaguliwa yeye kusomeshwa hizo mashine, halafu mulaumu Kikwete. Wacheni hizo. Kikwete kwenye sekta ya Afya kafanya kuliko yeyote wa kabla yake na takwimu za kungezeka kwa life span yetu kwa miaka 5 kwa kipindi chake tu kinathibitisha hilo. Wacheni kuwa wanafik. Huyu daktari kaja hapa anadanganya na nyinyi mnakubali tu, hamchukui hata dakika moja kuuthamini ukweli. Nimewaletea data hapo za mashine za CT scan, zinaonesha kwa uchahe kama hauna $ 1,000,000/= (million moja) huwezi kupata CT scan ikafanya kazi ipasavyo, labda uinunuwe uje kuiweka urembo.
piga na hesabu la gharama ya safari zote za J.k tujue tungekua na mashine ngapi
 
kweli shangingi lina raha yake mpaka wamesahau kununua mashine,,,ngoja nionge na mboe tuuze shangingi tununue mashine

naunga mkono hoja
 
Hapo bado hujapata CT scan, wachilia mbali chumba, utaalaam (mafunzo), "consumables".

Huyo dokta alikuwa anaota.

Kupanga ni kuchagua, kama kuna nia thabiti CT scan zitanunuliwa tu na kuacha kununua hizo V8. Huwezi jua, labda pay back / change kwenye V8 ni kubwa kuliko kwenye medical equipment (CT Scan, Xray) ndiyo maana hazipewi kipau mbele!!!
 
V8 prince ya minister mmoja ni TSh 280 million, a Phillips ct scan machine Kama iliyopo muhimbili is 140,000$=TSh 224milioni. Daktari. Hajakosea msipotosje wanajamvi na umma.
Yakiuzwa mashanhingi ya mawaziri kila mkoa tz bara ma b
Visiwani wanapata ct scan moja.
Na kwa sass deni la ct scan ya muhimbili imefikia billion 4 Tshs. Na hili limesababishwa wizara ya afya Iloilo Gia tender na wakala wa Phillips hapa nchini anayesupply all radiology equipments za hospital za serikali Kama vile xray na ultrasound. Hospitality zone za serikali ziko kwenye hii crisis.
Tuwe wakweli, nchi haiendeshwi kwa propaganda
 
hii serikali siku zote inasemaga haina hela ya kuwatumikia wananchi lakini pesa za kulipa tume ya katiba misafara isiyokua ya maana ya viongozi wetu hizo pesa zipo
 
Hapo bado hujapata CT scan, wachilia mbali chumba, utaalaam (mafunzo), "consumables".

Huyo dokta alikuwa anaota.

zomba, kama nimekupata vizuri ni kwamba unasema baba aendelee kula hotelini kwa sababu jiko ni bovu!

Kama taifa ni lini tutaacha kuhemea kwa wanaume wengine waliowekeza kwenye CT-Scan machine na makorombwezo mengine? Omba omba kuanzia vyandarua mpaka vipimo/matibabu! Lakini ni kweli Tanzania haina uwezo huo? Ulishaona magari wanayotumia viongozi wa India?
 
Hapo bado hujapata CT scan, wachilia mbali chumba, utaalaam (mafunzo), "consumables".

Huyo dokta alikuwa anaota.

Ww ndo unaota kubishia watu walioko ndani ya ngoma!dr hawezi kutoa takwim km hizi za uongo,ili imsaidie nn?
 
zomba, kama nimekupata vizuri ni kwamba unasema baba aendelee kula hotelini kwa sababu jiko ni bovu!

Kama taifa ni lini tutaacha kuhemea kwa wanaume wengine waliowekeza kwenye CT-Scan machine na makorombwezo mengine? Omba omba kuanzia vyandarua mpaka vipimo/matibabu! Lakini ni kweli Tanzania haina uwezo huo? Ulishaona magari wanayotumia viongozi wa India?

Umemjibu vema!nimeupenda huu mfano mkuu
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Katibu wa jumuiya ya madaktari nchini ameweka wazi kuwa bei ya mashine moja ya CT scan ni sawa na bei ya kununulia shangingi moja.Alisema kama serikali ingekuwa na nia ya kununua mashine hiyo isingeshindwa. kwa habari zaidi soma gazeti la mwananchi la leo. Binafsi habari hii imichefua na kunisikitisha kuona ni jinsi gani serikali yete inavyoendekeza anasa wakati inashindwa kutoa huduma za msingi kwa watu wake.Mashine ya CT scan pale muhimbili kwa mujibu wa vyombo vya habari imekuwa mbovu kwa muda wa miezi saba ila serikali inapiga dana dana kuitengeneza na matengenezo yake ni kama milioni mbili hivi kama sikosei.Kama nimekosei hiyo gharama ya matengenezo mwenye uhakika atujuze. Mbali na mashine hiyo kuna hospitali zingine hapa nchini hazina hata x-ray machine.Kama uliangalia taarifa ya habari ya ITV juzi usiku tatizo la kukosekana kwa mashine ya x-ray liliripotiwa ktk hospitali ya serikali mkoani Tanga ambapo mtu aliepata ajali alishindwa kuhudumiwa kutukona na kukosekana kwa mashine hiyo. Nasema hii ni aibu kwa serikali na inabidi kwenye katiba mpya tupitishe uamuzi wa kutaka viongozi wa serikali nao watibiwe hapa nchini na ipige marufuku viongozi kutibiwa nje ya nchi.Labda hii itasaidia kuondoa dhuluma hii. Sasa madaktari wanapogoma nani wa kulaumiwa kama sio serikali?Hivi haya ndio maisha bora kwa kila mtanzania!

Mkuu,nani kakwambia serikali hii ipo kwa ajili ya wananchi?? hao viongozi wapo kwa ajili ya chama chao,wao wenyewe na watoto wao!
 
piga na hesabu la gharama ya safari zote za J.k tujue tungekua na mashine ngapi

Na hizo safari anakwenda kucheza huko? leo hii una mashine ya CT scan, kabla ya Kikwete ulikuwa hata huijui ni nini? leo hii una mtambo wa MRI ambao kabla ya Kikwete ilikuwa ni lazima uende Nairobi, au hilo hulijui? Leo unachuo cha kufundisha namna ya kutibu na kufanya upasuaji wa moyo, au hilo hulijui? leo Muhimbili una jengo la "outpatient" bora katika Afrika Mashariki, au hilo hulijui? leo Muhimbili una chumba cha matibabu ya meno bora katika afrika mashariki, kwa vifaa, urahisi na utaalaam, au hilo hulijui? unajuwa kuwa watu wanatoka Afrika mashariki nzima kuja hapa kutibiwa meno? au hilo hulijui? Unajuwa kuwa watu wanatoka Afrika mshariki na ya kati na mpaka Middle East kuja hapa kutibiwa baadhi ya kansa> au hilo hulijui? na hayo yote ni wakati wa Kikwete. Au hilo hulijui?

Tazama hii:https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/136909-ct-scan-mri-muhimbili-buree.html

Ukimaliza, fananisha na hii: How much does an MRI scan cost?

Huyo ndio Kikwete na hizo ndio safari anazozifanya, kwa faida yako na yangu na ya Watanzania wote.

Leo MRI hata US inagharimu si chini ya $ 500 kwa kipimo Tanzania ya Kikwete unafanyiwa kwa ngapi? fata link hiyo ya kwanza, halafu uje kuniambia wale waliokuwa kabla ya Kikwete walikuwa wapi? wamekaa tu ofisini wana saini makaratasi?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom