Dr. Asha-Rose Migiro does better interview than JK?

I agree with you. Asha is a capable indivudual, inteligent woman and hard working person. Kwenye ambayo ina patrichal system kama yetu, kwenda juu kwa wanawake kwenye siasa kunategemea kwa kiasi kikubwa ridhaa ya wanaume. Vilevile ikumbukwe uwezo wa urais hautokani na kufanya interviews nzuri, it is much much more than that.

Hata hivyo pamoja na kuwa Asha haziwezi siasa za ufisadi, majungu, fitan na vitu kama hivyo, lazima tukubali kuwa ana uwezo mkubwa mara nyingi kuliko muungwana. Sasa hivi rais anayetafutwa ni wa 2010 hatuhitaji wa 2015 kwa sababu tatizo sasa liko 2010. I wonder why some people are trying to talk about 2015 while 2010 is a bigger headache that 2015. Are you out of your mind?
Vyeo vya KISIASA havipatikani kwa SIFA na VIPAJI ulivyonavyo PEKEE! Ni lazima apatikane wa kukubeba. Mnamkumbuka Tuntemeke Sanga?
Rais wa 2010 ni JK. Tusipoteze muda.
 
Vyeo vya KISIASA havipatikani kwa SIFA na VIPAJI ulivyonavyo PEKEE! Ni lazima apatikane wa kukubeba. Mnamkumbuka Tuntemeke Sanga?
Rais wa 2010 ni JK. Tusipoteze muda.

Mkuu kama ukisoma vizuri mistari nimesema kukwea kisiasa kwa wanawake kwenye nchi ambayo jamii yake ni patriachal na ambayo mafanikio ya kisiasa hayategemei uwezo na kipaji cha mtu, bali siasa za majungu, ufisadi and alike, it all depends on the will on those in power for women to excel. Kwa maana nyingine ni kuwa pamoja na uwezo alionano Asha, ni kweli alibebwa na JK, is it because of who is she? or what she can do or just because she is a woman?? that is open for debate.

Kusema kuwa JK ni rais 2010 sipingi, lakini you have to justify that with evidence. HWat has JK done to deserve another 5 years. Au ndio bado tuna siasa zilezile za bora liende, kwa sababu Ali alitawala 2 terms, Ben 2 terms na JK 2 terms regardless wanaperform vipi.

Dada yangu ambaye hajui aa wala be anaweza ku-arguei namna hiyo, lakini kwa mwenye critical mind yenye kuweza kuprocess information kuhusu uongozi na utawala wa nchi yetu hawezi kuwa na argument ya kusema eti ni JK tu 2010 bila kuwa na intelligent justification. This is my opinion, lakini naheshimu opinion yako, kwa kuwa kuna uwezekano unachosema wewe ndio kitakachotokea.
 
Bongolander,
Nashukuru unavyojua ku-argue kwa matusi ya kiaina kwa kuziweka hoja zangu sawa na za dada yako ambaye hajui a wala be. JK anafanya kazi vizuri tu za URAIS, kwa mujibu wa KATIBA yetu. Mapungufu anayo kama sisi wengine tulivyo. Niambie wewe kashindwa lipi kama Rais?
 
Mkuu kwanza nasikitika kwa kunielewa vibaya. Naomba usichukulie hiki kitu kuwa ni personal hapa tunaeeweshana tu, hatushambuliani. Kama nimekukwanza na-apologize.

Tatizo la kwanza ambalo naona serious linatokea under the watch of muungwana ni hatari ya nchi kujiingiza kwenye mambo ya udini. Kuna rhetoric ya ajabu ambayo binafsi naona ni hatari sana. Juzijuzi tulisikia watu wa mahakama ya kadhi, ukaja waraka wa wakatoliki. Pamoja na kuwa vimewahi kutokea nyuma this time around rhetoric yake si nzuri, naona hii ni weakness ya uongozi wa juu.

Serikali imesema wazi kuwa inaogopa kuwashughulikia mafisadi, nakumbuka katibu mkuu na waziri mkuu walitoa kauli zinazofanana na hizo. Hii naona ni weakness ya wazi kabisa. Tumempa rais nguvu za dola ili ashughulike mambo kama hayo. Wanaposema hawawezi maana yake nini? kwangu ni udhaifu, wahalifu wapo wanajulikana lakini wako huru na tena wanatukejeli kuwa hatuwafanyi kitu, kama vile hatuna mtu wa kutulinda.

Ukisikia jinsi mikutano ya chama inayoendeshwa unaona wazi kabisa kuwa uongozi wa chama una udhaifu. Hakuna discpline ndani ya chama, sasa hivi kila mtu ni msemaji wa chama, wakati mwingine hata viongozi wa chama wanabishana hadharani na kwenye media hii ni weakness kubwa.

Hakuna hata plan yoyote ya maana innovative ya kuwaendeleza wananchi aliyokuja nayo JK akilinganishwa na jamaa aliyepita. Amefanya kazi kubwa kulinda serikali yake. Mimi natumia vigezo kama hivi kutilia shaka kama kweli 2010 ipite hivihivi, na mkuu apitishwe hivi hivi bila kumuuliza maswali haya.
Again, apologies kama nimekukwaza Wildcard.
 
Kuna vitu Mama Migiro amesema ambavyo ningeshukuru kupata ufafanuzi.

Akiongelea madhara ya global financial crisis kwa wanawake wa Tanzania na Africa, amesema, wanawake ndio wanafanya kazi kubwa shambani, na ndio wanaofanya "petty trade," na hivyo, kutokana na hii credit crunch, na mfumuko wa bei za vyakula, basi vyovyote ambavyo wanawake wamekuwa wakifanya vitadhurika.

Ningependa kuelewa, jee, credit crunch inamwathiri vipi msuka ukili na mchoma chapati na mponda kokoto (petty traders). Mpanda mihogo na mtama ataumia au atafaidika na mfumuko wa bei ya vyakula?

Kwa nchi zenye uchumi wa kuazimana, credit crunch inaathiri vitu kama mikopo ya mortgage, mikopo ya wanafunzi, mabenki, investments za makampuni, na mikopo ya ununuzi wa magari.

Kama sio tabia ya kugeza ya kwingineko, Global credit crunch inamuathiri vipi Mama Ntilie wa Gezaulole?

Mkuu Dilunga, Credit crunch ina madhara kwa kila mtu, hata wale wasiohusika na shughuli zozote za kiuchumi. Mtikisiko huu wa uchumi una madhara zaidi kwa masikini kuliko kwa matajiri. Sababu kubwa ni udogo wa kipato cha masikini na utegemezi wao kwa matajiri.

Nikikusudia kukufafanulia kuhusu uliyotaka kupata ufafanuzi wake hapo juu;msuka ukili na mchoma chapati na mponda kokoto (petty traders). Mpanda mihogo na mtama ataumia au atafaidika na mfumuko wa bei ya vyakula?
Jibu ni ndio, wote hao watapata msukosuko kutokana na kudorora kwa uchumi. Msukosuko huo unatokana na upungufu wa nguvu za wanunuzi kufanya manunuzi kwa utaratibu wa zamani/wa kawaida (kabla ya tatizo hili kujitokeza). Ni dhahiri kuwa watu wengi watabadili utaratibu wa manunuzi na kufanya manunuzi kwa kuzingatia mahitaji muhimu zaidi ya yale yasiyo na umuhimu mkubwa, kwakuwa kipato cha wengi kitakuwa kimeathirika (wengine kiasi kidogo na wengine wataathirika sana).

Mkuu, kumbuka kuwa wengi watapoteza ajira (soko litapungua), wengi watapoteza mitaji (hivyo uwekezaji na purchasing power itashuka) na wengi wanaotegemea uwezeshwaji wa wenye nacho wataathirika kwa kukosa uwezeshwaji huo, ama uwezeshwaji wenyewe utapungua sana.

Chakula ambacho ndicho kitakachokuwa na umuhimu mkubwa zaidi katika soko kwa kipindi chote hicho, kitakuwa cha gharama kubwa kulinganisha na uwezo wa wanunuzi wengi. Hivyo wakulima wanaweza kupata shida kujikimu kwa kushindwa kuendana na mahitaji ya soko na uwezo wa wanunuzi. Vilevile, watu wengi wataanzisha ukulima mdogomdogo (busani za nyumbani) ili kujaribu kukidhi mahitaji ya familia zao kwa chakula. Hii itapunguza pato la mkulima wa mazao kwa makusudio ya biashara. Wakulima wanaoweza kufaidika ni wale wanaoweza kulifikia soko kubwa zaidi ya soko la ndani pekee. Dunia nzima inahitaji chakula na kilimo kinaweza kuleta ukombozi.

Mama Ntilie wa Gezaulole ataathirika kwa kuwakosa wale wateja wake ambao wengi wao watakuwa wamepunguzwa ajira, au miradi waliokuwa wakifanya imesimama kutokana na ukosefu wa uwezo kifedha kwa wale waliokuwa wakiifadhili. Mama Ntilie wengi hufanya kazi kwenye miradi kama barabara, ujenzi wa majengo na kadhalika. Endapo wahusika watashindwa kuendeleza miradi yao, au wakipunguza uwekezaji kwenye miradi hiyo, ni dhahiri Mama Ntilie huyo nae ataathirika sana.

Kwa nchi kama zetu na miradi tunayofanya, athari za mtikisiko wa uchumi si za moja kwa moja na pia hazihusu umoja wa watu wengi. Ni athari zinazokumba mtu mmoja mmoja au na taasisi moja moja. Hii ni kwa kuwa hakuna mfumo unaounganisha nguvu za watu wengi. Ungekuwepo mfumo huo, wengi wangeathirika kwa pamoja, kama ambavyo wangeweza kufaidika kwa pamoja kama hali ingekuwa kinyume.
 
swala la Migiro litabaki kuwa ni yeye na swala la JK litabaki kuwa ni JK ila hapa kuna tofauti kati ya hawa walio lingaishwa na tofauti hiyo utaina tu pale utakapo angalia interview zao.
 
Bongolander,
UDINI na hata UKABILA vilikuwepo siku zote sema tu vilikuwa vimefunikwa na nguvu nyingi alizokuwa nazo Mwalimu ambazo waliomfuata hawana. Kwa kiasi fulani JK ameliacha hili liwe wazi ili tulione kwamba lipo, tulijadili na kulitafutia ufumbuzi kama Watanzania. Vinginevyo lingekuja kulipuka vibaya kuliko tunavyoliona sasa. Tuwe na mjadala MPANA na wa WAZI kwa ajili ya hatma ya NCHI yetu.
Mafisadi wanashughulikiwa ingawa sio kwa kasi na viwango tunavyovitaka. Ndio KATIBA na sheria tulizonazo! JK azifanyeje mahakama zetu ambazo hata kesi za wazi kama samaki wa Magufuli hazijaamuliwa?
Acha CCM waongee ili angalau tuone kama inaweza KUPASUKA! Wengi tunaliombea hili litokee sasa ili mambo mengine yaweze kutengenezwa upya.
 
Kuwa na interview nzuri haina maana kwamba unajua au unaamini kile unachokisema. Nyerere alikuwa mzungumzaji mzuri, interview nzuri, lakini alikuwa haamini kile alichokuwa anakisema. Pamoja na speech zake nzuri, alishindwa kuwasaidia WTZ kimaendeleo, elimu nk. Kwa hiyo, kuwa na interview nzuri, Si kigezo cha kuwa na knowledge ya kuongoza, bali ni kipaji tu cha kuzungumza.

Nakubaliana na wewe kabisa
Yaani ukisikilisha speech za mchonga
Mbona nipoints tupu ila......?
 
Kuwa na interview nzuri haina maana kwamba unajua au unaamini kile unachokisema. Nyerere alikuwa mzungumzaji mzuri, interview nzuri, lakini alikuwa haamini kile alichokuwa anakisema. Pamoja na speech zake nzuri, alishindwa kuwasaidia WTZ kimaendeleo, elimu nk. Kwa hiyo, kuwa na interview nzuri, Si kigezo cha kuwa na knowledge ya kuongoza, bali ni kipaji tu cha kuzungumza.

Mkiamka muwe mnajinyoosha kwanza kabla ya kuanza kutembea. usingizi utawaangusha!
 
Bongolander,
UDINI na hata UKABILA vilikuwepo siku zote sema tu vilikuwa vimefunikwa na nguvu nyingi alizokuwa nazo Mwalimu ambazo waliomfuata hawana. Kwa kiasi fulani JK ameliacha hili liwe wazi ili tulione kwamba lipo, tulijadili na kulitafutia ufumbuzi kama Watanzania. Vinginevyo lingekuja kulipuka vibaya kuliko tunavyoliona sasa. Tuwe na mjadala MPANA na wa WAZI kwa ajili ya hatma ya NCHI yetu.
Mafisadi wanashughulikiwa ingawa sio kwa kasi na viwango tunavyovitaka. Ndio KATIBA na sheria tulizonazo! JK azifanyeje mahakama zetu ambazo hata kesi za wazi kama samaki wa Magufuli hazijaamuliwa?
Acha CCM waongee ili angalau tuone kama inaweza KUPASUKA! Wengi tunaliombea hili litokee sasa ili mambo mengine yaweze kutengenezwa upya.
viongozi wa Afrika tofauti yao ni ndogo sana. unakumbuka yaliyotokea Kenya kwenye matumaini ya watu wa nchi hiyo waliyoyaweka kwenye chama cha NARC? ODM na Odinga wa 2007 ni yuleyule??
 
viongozi wa Afrika tofauti yao ni ndogo sana. unakumbuka yaliyotokea Kenya kwenye matumaini ya watu wa nchi hiyo waliyoyaweka kwenye chama cha NARC? ODM na Odinga wa 2007 ni yuleyule??
Nakubaliana nawe Kigarama kuhusu viongozi wa Afrika. Hata hivyo mabadiliko yanayotokea Kenya mara nyingi yanaegemea kabila ya Kiongozi anayeyaongoza. Wajaluo hauwambii kitu kwa Raila. Hapa kwetu CCM ina nguvu kama TAASISI sio INDIVIDUALS na kabila zao.
 
Mkuu hapa umenena. lakini one of the worries i have na serikali ya sasa ni kuwa hii status inaonekana kutetereka sana. Inaanza kuwa kinyume, indivuduals wanaanza kuwa na nguvu kuliko taasisi, taasisi na vikao vyake vinaendelea kuwa weak, hili ndiio naona moja ya weakness ya utawala wetu wa sasa. Linatisha sana, kama hali haitabadilika soon tunaanza kusikia yale ambayo hayakuwepo Tanzania.
Mara mwislamu, mara mkristo, mara mzanzibari na mafuta yake, mara mpemba na vibanda vyake vya biashara, mara kafiri mara mgalatia,......ujinga mtupu ambao mwalimu alikuwa anauita kuwa unatokana na ulevi wa madaraka. Lakini sasa hivi ni kama unatumika kujipatia nafasi za kisiasa.
 
Bongolander,
UDINI na hata UKABILA vilikuwepo siku zote sema tu vilikuwa vimefunikwa na nguvu nyingi alizokuwa nazo Mwalimu ambazo waliomfuata hawana. Kwa kiasi fulani JK ameliacha hili liwe wazi ili tulione kwamba lipo, tulijadili na kulitafutia ufumbuzi kama Watanzania. Vinginevyo lingekuja kulipuka vibaya kuliko tunavyoliona sasa. Tuwe na mjadala MPANA na wa WAZI kwa ajili ya hatma ya NCHI yetu.

Mafisadi wanashughulikiwa ingawa sio kwa kasi na viwango tunavyovitaka. Ndio KATIBA na sheria tulizonazo! JK azifanyeje mahakama zetu ambazo hata kesi za wazi kama samaki wa Magufuli hazijaamuliwa?
Acha CCM waongee ili angalau tuone kama inaweza KUPASUKA! Wengi tunaliombea hili litokee sasa ili mambo mengine yaweze kutengenezwa upya.

Nguvu ilizonazo taasisi ya Rais ni kubwa mno,kama JK angekuwa na dhamira ya dhati ya kushughulikia ufisadi kwa kutumia madaraka aliyonayo tusengekuwa tunaongelea ufisadi sasa hivi.

Rais anaweza kumtia mtu/watu ndani for more than 48 hrs na bila mtu yoyote kumuuliza kwa kuwa sheria inamruhusu kufanya hivyo(Detention orders).Rais anaweza kuwawajibisha viongozi wa umma bila ya mtu yoyote kumuuliza unachofanya ni nini kama maslahi ya umma yanazingatiwa.

JK kama mwenyekiti wa CCM anaweza kuweka discipline ndani ya chama na kukawa na sauti moja inayosema nini maamuzi ya chama juu ya mambo fulani fulani.Hii ni kwa kifupi tu ni mamlaka gani taasisi ya Rais inayo na uwezo wa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama.

Sasa JK hajatumia hata asilimia 10 ya uwezo wa taasisi ya Rais je hapa mtu atasemaje?hajui mamlaka aliyopewa na umma ama ni dhaifu kiuongozi?
 
Back
Top Bottom