DOWANS wawasha Mitambo yao

al adawi amesema amekuja kuongea na tanesco, wala hana shida na ngeleja. Na amesema yuko tayari kupunguza gharama badala ya bilioni 94 tulizotakiwa kumipa basi atatuunguzia kidogo waau tupate kiasi cha kuwalipa waathirika wa makombora gongo la mboto.
Sasa kama jana tu ametangaza kuongea na tanesco na leo mtambo umewashwa, hiyo ni kusema aliitisha waandishi wa habari huku akiwa amemaliza mazungumzo na tanesco, vinginevyo watakuwa wamezungumza fasta kama kawaida yao inapokuja suala la dharura ni wepesi wa kufanya negotiation na kufikia maamuzi.

mkurugenzi wa tanesco kakanusha kuwa huyo s mgeni wa tanesco
 
Nimeongea na technician wa Dowans amethitisha hilo walifanya kazi hiyo usiku kuamkia leo kutokama na kukamilika kwa mazungumzo kati ya Tanesco na Mliliki wa Dowans na Kamati ya Nishati.
Huwenda MW nyingine zikaongezwa kutokana na uhitaji
 
IPTL inatutafuna zaidi. Acheni wawashe DOWANS. Siasa zikae kando kwanza.
Mramba alisema hata watanzania tule majani ilikuwa lazima ndege ya raisi inunuliwe, mimi nimefikiwa uamuzi wa kukaa gizani kusubiri mvua ya Mungu ijaze mabwawa ya Mtera na Kidatu kuliko umeme wa RA, JK na serikali yake wametusaliti na kututupa kamwe si Mungu, na njia pekee ya kutuokoa watanzania kwa sasa nikupitia matatizo.
 
Wamesahau tu kufanya sherehe ndogo ya kuizindua upya. Mgeni rasmi akawa huyo Brigedia. Wakaalikwa akina Zitto (Mwenyekiti, Kamati ya Bunge, Mashirika ya Umma), Makamba mdogo ( Mwenyekiti, Kamati ya Bunge, Nishati na Madini), Mwakyembe( NW, Ujenzi), Sitta ( Waziri EA), Chenge (AG Mstaafu), RA ( Mjumbe wa CC ya CCM), Mzee Shelukindo, EL (WM Mstaafu, pia muathirika wa Richmond) na Ngeleja akatoa kauli rasmi ya serikali!
 
Jamani waacheni wawashe tupate umeme; mimi nina zaidi ya mwezi sijaweza kuwauliza wanangu wanionyeshe homework zao kutokana na shida ya umeme. Kuna viwanda vinafanya kazi siku tatu kwa wiki kutokana na hii shida.

Ila kama ni kuwalipa DOWANS, walipie kuinunua hiyo mitambo kwa bei yake ya sasa ondoa uchakavu wa miaka mitatu.
 
Mmmmmmm! wapi bed pan nesi, tumbo linanikata!!!!!!!

Leo mtaani kwangu nimelala bila umeme pamoja na nyumba kadhaa kasoro mbili tu, moja guest h'se na nyingine mkurya mmoja ana mashine, sielewi wamepataje wakajikuta wako kisiwani na umeme wakati wengine wote hatuna. Hawakuwa na generator yoyote na wala hawana solar na achilia mbali betri za magari. Ni TANESCO tu. Kabla ya kuja hao jamaa umeme ulikuwa na nguvu ya kutosha, kwa siku hizi hata kiuwasha redio lazima utegeshee ama sivyo haiwaki labda taa ya watt 5.

DSM hapa.
 
Ule msemo wa kwamba Simba akizidiwa ula majani umetimia. Kwa wale wasomaji wa Biblia mtakumbuka mfalme Daudi alishikwa na njaa wakati akipigana vita akaingia Hekaluni akachukua mikate akala ingawa ni makuhani tu walirusimwa kula mikate hiyo!
 
Jamani waacheni wawashe tupate umeme; mimi nina zaidi ya mwezi sijaweza kuwauliza wanangu wanionyeshe homework zao kutokana na shida ya umeme. Kuna viwanda vinafanya kazi siku tatu kwa wiki kutokana na hii shida.

Ila kama ni kuwalipa DOWANS, walipie kuinunua hiyo mitambo kwa bei yake ya sasa ondoa uchakavu wa miaka mitatu.
Mkuu kwa style hii kweli tutashinda hivi vita?
Mambo mazuri yanagharama zake mkuu.
 
Ninavyojuwa kesi iko mahakamani. Dowans waliishitaki TANESCO kwa kuvunja mkataba, sasa "what are they painting there? Kumesainiwa mkataba mwengine? Wamewasha kwa ruhusa ya nani? Tanzania jamani, jamani Tanzania.

Kila uchao usanii mpya, madudu mapya. Ama kweli Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu (sio mpirani tu), na jamvi la wageni. Tanzania Njema, atakaye aje.
 
Hii mitambo ya SONGAS kinachoiua ni nini haswa mpaka tunakula matapishi yetu, ama kweli maskini hawezi kumwadabisha bosi wake ataishia kupiga makelele na makali ya umaskini yanapoongezeka humgeukia bosi wake. Nini kinatufanya TZ tuwe kama gunia la kupangusia miguu wakati wa kuingia na kutoka chooni jamani?
 
lenyewe lililalamika kuwa haliwajui wamiliki....wamiliki wamelete kanyaboya lenyewe limeondoka sijui kwenda mauritania......

hapo hapo mitambo imeanza kuwashwa likirudi litauliza, watalidanganya na wala halitahoji zaidi...jitu hili pumbavu sana
 
kama imewashwa then hapa kuna maswali mapya yanaibuka....
1.deni juu ya deni?
2.msaada wa dharura?
3.mkataba mpya?
4.itanunuliwa?
5.suluhisho la muda mfupi au mrefu?
 
Back
Top Bottom