DOWANS wawasha Mitambo yao

Mkeshaji

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,262
1,416
Wakuu hivi ninavyoandika ni kuwa mtambo mmoja wa Dowans aina ya LM6000 PD 40MW uliopo site A nyuma ya ghorofa la Tanesco umewashwa na hadi sasa unazalisha 37MW.

Nitawaletea habari zaidi lakini nina uhakika kuwa hawataweza kutembeza mitambo yao yote kutokana na sababu ambazo nitazieleza hapo baadae. Kiufundi mtambo huo kwa sasa ume-substitute mtambo wa Songas ambao kwa sasa upo down kutokana na kupata ajali ya moto hapo jana.

Habari kamili baadae.
 
Ndiyo maana leo huku Vijibweni kuna umeme!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mkataba upoje kwa sasa? au ndo watautayarisha baadae? Nchi hii jamani!
 
wamesubiri mvua zimeanza kunyesha ndio waka washa...sasa sijui wanataka wadai kwamba wao ndio wamemaliza matatizo ya umeme?
 
Wakuu hivi ninavyoandika ni kuwa mtambo mmoja wa Dowans aina ya LM6000 PD 40MW uliopo site A nyuma ya ghorofa la Tanesco umewashwa na hadi sasa unazalisha 37MW. Nitawaletea habari zaidi lakini nina uhakika kuwa hawataweza kutembeza mitambo yao yote kutokana na sababu ambazo nitazieleza hapo baadae. Kiufundi mtambo huo kwa sasa ume-substitute mtambo wa Songas ambao kwa sasa upo down kutokana na kupata ajali ya moto hapo jana.
Habari kamili baadae.

Al Adawi amesema amekuja kuongea na tanesco, wala hana shida na ngeleja. Na amesema yuko tayari kupunguza gharama badala ya bilioni 94 tulizotakiwa kumipa basi atatuunguzia kidogo waau tupate kiasi cha kuwalipa waathirika wa makombora gongo la mboto.
sasa kama jana tu ametangaza kuongea na tanesco na leo mtambo umewashwa, hiyo ni kusema aliitisha waandishi wa habari huku akiwa amemaliza mazungumzo na tanesco, vinginevyo watakuwa wamezungumza fasta kama kawaida yao inapokuja suala la dharura ni wepesi wa kufanya negotiation na kufikia maamuzi.
 
Ushindi mwingine kwa akina RA baada kuliteka Bunge.

WildCard,

Huu si ushindi, bali ni kuishiwa nguvu kwa kambi ya RA.. Nimepita pale an hour ago na ni kweli 40MW is up and running! Tanesco Ubungo wamekataa kujibu dukuduku zangu lakini wale "mafundi" wameniambia wana-feed 35MW kwenye grid ya Taifa as of 12:00noon today!

Habari ndiyo hiyo!
 
Kilichokuwa kinatafutwa siku zote ndio hicho unachokiita "Dowans imewasha mtambo wao", na sasa watalipwa.
Game over!
 
hahahaha...... nchi hii kwa usanii tu hawajambo...........kuna siku mtadaiwa trilion 2
 
WildCard,

Huu si ushindi, bali ni kuishiwa nguvu kwa kambi ya RA.. Nimepita pale an hour ago na ni kweli 40MW is up and running! Tanesco Ubungo wamekataa kujibu dukuduku zangu lakini wale "mafundi" wameniambia wana-feed 35MW kwenye grid ya Taifa as of 12:00noon today!

Habari ndiyo hiyo!
Mkuu nafikiri huu ni ushindi kwa RA na wenzake, kama wamewasha mitambo yake unategemea nini tena?
 
Dah! Hii snema nyingine imeanza, DOWANS PART 2, nahamu kweli nione mwisho wake, afu zis time starling ni Sulaiman Mohamed BR.....kazi ipo! MI YANGU MACHO!
 
Mkuu nafikiri huu ni ushindi kwa RA na wenzake, kama wamewasha mitambo yake unategemea nini tena?

Kwa hii tutaambiwa mitambo yao iliwashwa na umeme ukaingizwa kwenye gridi ya taifa na kwahiyo hakuna jinsi lazima tuwalipe.
Usije kushangaa utakapo ambiwa wanaingia kwenye meza ya mazungumzo baada ya kuwasha mtambo, kwahiyo RA ndiye atapanga bei ya kukodisha hiyo plant na tanesco watakuwa hawana njia ya kubisha zaidi ya kulipia huduma toka dowans. Na kwa staili hiyo naziona biioni 94 zimelipwa kwa dowans kupitia mlango wa uani ilihali watanzania wako sebuleni(mahakama kuu) wakisubiri.
 
Bila kuchimbika hapa tutazidi kuonekana wajinga. Natamani siku moja nikutane na ROSTAM nimpe za :frusty: mpaka akome kututania watz.
 
Back
Top Bottom