DOWANS vs. Wastaafu wa EAC....

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Zipo tofauti za kimsingi ambazo zinabainisha kwa nini serikali hii ya kifisadi inakimbilia kuwalipa DOWANS na kukwepa kuwalipa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki yaani EAC. Mazingira hayo ni kama ifuatavyo:-

1) Wote madai yao yana riba na faini lakini kwa vile yale ya DOWANS yana posho za wakubwa kwa maana ya ufisadi ndiyo maana yanatangulizwa kulipwa tena kwa kutumia hizo hizo riba na faini kuhalalisha uharaka huo......................

Yale ya wastaafu wa EAC pamoja na kuwa na riba yanapuuzwa kwa vile wastaafu hao hawawezi kuwalipa hongo watendaji serikalini ili wayaharikishe......................kulipwa.....................................


2) Malipo ya DOWANS ni matunda ya ufisadi uliokithiri serikalini lakini ya wale wastaafu wa EAC ni jasho lao halali...................

3) Muda wa madai ya DOWANS ni chini ya miaka mitano tangia kashfa yao kuanza huku madai ya wastaafu wa EAC yana muda wa zaidi ya miaka 34. Tungelitegemea serikali sikivu hata kuweka bajeti ya kuwalipa wastaafu wa EAC lakini hivi sasa wapo kwenye pilika pilika ya kutafuta fedha kwenye bajeti kuwalipa DOWANS ili kuharakisha kupata kivuno chao cha kifisadi...........................

4) Madai ya DOWANS yalipelekwa kwa msuluhishi na wahusika wote wakakubaliana kimya kimya bila ya kulishirikisha Bunge kuwa Mahakama Kuu iondolewe mamlaka ya kuchunguza uamuzi wa msuluhishi. Madai ya wastaafu wa EAC yalithibitishwa na Msuluhishi na kutungiwa sheria na Bunge kwa ajili ya utekelezaji lakini hadi leo serikali hii ya kifisadi inatafuta mwanya wa kuwadhulumu wastaafu hao haki yao ya kimsingi pamoja na sheria kuwepo zinazowalinda..............................

5) Madai ya DOWANS yanakiuka sheria ya manunuzi ya mwaka 2004 kwa sababu Bodi ya zabuni haikushirikishwa lakini madai ya wastaafu wa EAC msingi wake ni sheria iliyopitishwa na Bunge.......................sasa ni yupi astahili kulipwa?

6) Madai ya kifisadi ya DOWANS yatalipwa hivi karibuni lakini yale ya halali kabisa ya wastaafu wa EAC kamwe hayatalipwa kwa sababu serikali hii ya kifisadi haina mpango wowote wa kuwalipa................................


MUNGU IBARIKI TANZANIA ...............MUNGU UWALAANI MAFISADI.............
 
Blame it on Nyerere. Yeye ndiye aliyefungua utepe wa kukacha kuwalipa hao wazee. Wengi wao wameshatangulia mbele za haki na nadhani wanamgawana Nyerere right this minute.
 
Dr Hosea, hapo ndipo ulipotakiwa kuonyesha umahiri wako. Hii Dowans ingekutoa kaka yangu, ndani na hata nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom