DOUBLE STANDARDS ZA CHADEMA, Lwakatare angekuwa kiongozi wa CCM wangeandamana kushinikiza ajiuzuru

Lukosi, Tokea uhamie CCM umepungukiwa akili manake umekua ukihoji vitu vya kitoto sana ambavyo majibu yake unayo... Usifikiri una akili kuliko vijana wa CDM, hayo unayowaza wewe leo wenzio tulishawaza wiki zilizopita!!
 
Dr. Slaa ameruhusu barua ya Zitto uvuje kwa makusudi.

Kama kuna mtu anayetakiwa kuwajibika kwa kujiuzuru ni Dr. Slaa kwa kushindwa kutunza siri za ofisi yake.

Wewe kweli bongolala, kama barua imevujishwa na ofisi ya katibu Mkuu, nafikiri ingekuwa tayari imeshasainiwa na mwenye barua. Naomba nisiendelee kukujuza manake wewe nafikiri ni miongoni mwa ile Mijuha ambayo hata uiwekee majibu mezani kusoma itakuwa tatizo. Nafikiri na wewe unahitaji kupata tiba kama ya mwenzako lukosi. Magonjwa yenu yanashabihiana sana.
 
Lukosi, Tokea uhamie CCM umepungukiwa akili manake umekua ukihoji vitu vya kitoto sana ambavyo majibu yake unayo... Usifikiri una akili kuliko vijana wa CDM, hayo unayowaza wewe leo wenzio tulishawaza wiki zilizopita!!

Mkuu sio kwamba amepungukiwa akili, kule CHADEMA watu walikuwa wanamsaidia ndo maana matatizo yake hayakugundulika, sasa hivi hana msaada au wanaomsaidia ni bongolala kama yeye ndo maana kila akiibuka na issue hapa jamvini inakuwa ni PUMBA tupu.
 
Mimi nadhani kama kweli mna wataalam wenu na nyinyi mngefanya uchunguzi kuliko kumtetea wakati nyie wenyewe hamjui ukweli ukoje

Lakini brother si umeambiwa kesi ipo mahakamani? Si ungesubiri wataalamu wa sheria wa Chadema na wa serikali wakiongozwa na wale wa chama tawala (maana chama Tawala kina maslahi katika jambo hili) waweke mezani utetezi wao hapo ndio kila kitu kitakuwa wazi.. Kwa Chadema kuamua kumsimamia na kumtetea kiongozi wao ni dhahiri wana sababu za kufanya hivyo na hoja za msingi wanazoziamini kuwa watashinda.

Kwa hiyo tusubiri mpaka kesi itakapoanza kuunguruma ndio tutapata la kusema...
 
Ndugu Zanguni

Nimesoma barua ile iliyowekwa hapa ikidaiwa kuwa imeandikwa na Mh Zitto na pia nimesoma maelezo yake hapa leo na kushangazwa sana na hizi double standards za CHADEMA , chama ambacho ndio kikubwa cha upinzani nchini na ambacho tunategemea ndio kiwe cha kwanza kutuonyesha mfano kuwa wakipewa dola watafanya nini pale viongozi wao wakiharibu au kukumbwa na kashfa yoyote inayohitaji uchunguzi wa polisi.

Wote tunajua kuwa ikitokea kashfa sehemu fulani ndani ya serikali CHADEMA huwa ni wa kwanza kushinikiza mhusika ajiuzuru au asimamishwe kupisha uchunguzi jambo ambalo na mimi nakubaliana nalo kwani huwezi kumchunguza mtuhumiwa wakati bado ni kiongozi. Ili uchunguzi uwe wa huru na haki inabidi muhusika asimamishwe kupisha uchunguzi huo ili asiwe na nafasi yoyote ya kuweza kuharibu ushahidi au kuwanyima nafasi wapelelezi kufanya uchunguzi wa kina kwa kumuonea aibu au huruma. Uchunguzi/upelelezi ukiisha basi hatima yake ndio itajulikana.

Sasa leo chadema wanashindwa kumsimamisha kwa muda Kiongozi wao na wanapinga kwa nguvu zote kuwa ameonewa, Hivi ikija kuonekana kuwa huyo kiongozi ana hatia tutawaelewaje? Kesho mtawezaje kuwanyooshea kidole CCM pale watakapoonekana wana kashfa?

Sidhani kama CHADEMA wanaweza kuchukua maamuzi mazito kama aliyochukua Mh Lowassa pale alipojiuzuru uwaziri mkuu.

Kama lengo lenu ni kuisambaratisha CHADEMA kwa kuwabambika baadhi ya viongozi tuhuma zisizo na mbele wala nyuma basi mjue mnashindana kupiga upepo rangi. Mimi sijui unafanya nini nje ya nchi kama huna hata uwezo wa kufahamu hila za chama unachokiasujudia kiasi hicho. Unanitia shaka sana kwani kama ndio ulipoishia uwezo wako wa kufikiri, unatudhalilisha mbele ya hao unaoishi nao huko nje.
 
Correction: wangeandamana kudai sheria ichukuwe mkondo wake. And that's exactly what's happening - kesi iko mahakmani.

Na wewe ukiwa kama ex-cop you should know better, "everyone is innocent until proven otherwise". So, put that in pipe and smoke it!
Mbona mlitaka kuandamana baada ya form iv kufeli mkitaka Kawambwa na Mulugo wajiuzuru, nani aliprove kuwa wana kosa?
 
Mkuu hawa jamaa ni kama wafuasi wa ngoma ya mdundiko, wao wanafuata midundo tu bila kujua wanaenda wapi
Wengine wameacha hata shughuli zao za kujipatia mkate wa kila siku wameamua kusubiri chadema ichukue nchi ili wawe wakuu wa mikoa
 
Ndugu Zanguni

Nimesoma barua ile iliyowekwa hapa ikidaiwa kuwa imeandikwa na Mh Zitto na pia nimesoma maelezo yake hapa leo na kushangazwa sana na hizi double standards za CHADEMA , chama ambacho ndio kikubwa cha upinzani nchini na ambacho tunategemea ndio kiwe cha kwanza kutuonyesha mfano kuwa wakipewa dola watafanya nini pale viongozi wao wakiharibu au kukumbwa na kashfa yoyote inayohitaji uchunguzi wa polisi.

Wote tunajua kuwa ikitokea kashfa sehemu fulani ndani ya serikali CHADEMA huwa ni wa kwanza kushinikiza mhusika ajiuzuru au asimamishwe kupisha uchunguzi jambo ambalo na mimi nakubaliana nalo kwani huwezi kumchunguza mtuhumiwa wakati bado ni kiongozi. Ili uchunguzi uwe wa huru na haki inabidi muhusika asimamishwe kupisha uchunguzi huo ili asiwe na nafasi yoyote ya kuweza kuharibu ushahidi au kuwanyima nafasi wapelelezi kufanya uchunguzi wa kina kwa kumuonea aibu au huruma. Uchunguzi/upelelezi ukiisha basi hatima yake ndio itajulikana.

Sasa leo chadema wanashindwa kumsimamisha kwa muda Kiongozi wao na wanapinga kwa nguvu zote kuwa ameonewa, Hivi ikija kuonekana kuwa huyo kiongozi ana hatia tutawaelewaje? Kesho mtawezaje kuwanyooshea kidole CCM pale watakapoonekana wana kashfa?

Sidhani kama CHADEMA wanaweza kuchukua maamuzi mazito kama aliyochukua Mh Lowassa pale alipojiuzuru uwaziri mkuu.

Ukiwa mtaani hasa maeneo ya mijini ni dadra sana kusikia mtu anaisifia CCM, wapo watu wanapenda CCM iendelee kuwa madarakani ingawa watu hao huwa hawasemi wazi. Unaweza ukawaona kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia Nick names.

Zifuatazo ni sababu zinazofanya baadhi ya Watanzania kulilia CCM ibaki madarakani pamoja na umasikini, ufisadi uliokithiri kufikia hatua ya kushika nafasi ya pili kwa ufisadi Afrika mashariki, point moja tu baada ya uganda.

1. Watu hao kwa sasa wananufaika na mfumo wa sasa, kwani ni mfumo ambao uko loose,kundi hili ni waajiriwa serikalini. Wafanyakazi wa Serikali wamefanikiwa kuvuna pesa za wizi serikalini wanaomba hali iendelee kuwa kama ilivyo, CCM iendelee kutawala .

Wengi wetu tunawafahamu rafiki zetu walioko serikalini bila kujali kuwa wana nafasi za juu au za chini wamefanikiwa kutajirika ghafla, tunawafahamu lakini hakuna mahali pa kuripot kwakuwa system nzima ni Corrupt.

2. Wako wafanyabiashara wanaokwepa kodi, serikali imegubikwa na rushwa kwa hiyo hawawezi kukusanya kodi, kila kitu kinakwenda kwa dili au ten %. Hawa nao wanasema kidumu chama cha mapinduzi

3. Wako ambao wamezaliwa kwenye familia tajiri, wakiamka asubuhi wanajiuliza ama wale soseji au mayai. Friji zao Zimejaa kuku, samaki nk. Pia wanachagua watoke na aina gani ya gari. Kundi hili halifahamu vizuri umasikini uliowagubika watanzania, shida wanazisikia kwenye vyombo vya habari, maisha yao hawajichanganyi na masikini kabisa, wanasoma shule na vyuo vya kitajiri kwa hiyo umasikini hawaujui. Kwa hiyo hawaoni kosa la CCM

4. Masikini lakini wanaipenda CCM mpaka kesho. Kundi hili liko vijijini. Linaipenda CCM kwa sababu ya kukosa elimu ya uraia, au hawapati habari kabisa. Shughuli yao kubwa ni kulinda nyani wasivamie mashamba yao. Kundi hili halijui maana ya maendeleo, wanatamani hata shule zisiwepo ili watoto wachunge ng’ombe na kulima, wakivuna mazao ya kutosha wakala wakashiba hata kama hawana shilingi ya kununua ndala wao usema CCM oyeeeee

5. Kuna kundi ambalo lenyewe limedanganywa kwa uvumi au kwa mazoea tu. Kwamba bila CCM kutakuwa na vita, linasema CCM imenilea hadi hapa nilipo. Kundi ili liko tayari kuchagua hata fisadi au jiwe ilimradi tu atokee CCM. Kundi hili linafahamu kabisa kuwa serikali haifanyi vizuri lakini kwa mazoea lenyewe limeendelea kuomba CCM ibaki madarakani ili amani iendelee kuwepo.

6. Imani. Kundi hili ni mchanganyiko wa wasomi na wasiosoma. Hawa kwa sababu ya imani kali kwa dini limehamua kuweka dini mbele lakini maendeleo baadae. Kundi hili linafahamu kabisa madudu ya CCM lakini limeendelea kuwa na msimamo kwa CCM. Kundi hili udanganywa kirahisi kwa propaganda za CCM kwamba Chama fulani ni cha dini fulani. Bila kujali msitakhabali wa nchi uamua kushabikia CCM lakini baada ya miaka mitano huwa halioni mabadiliko ya kimaendeleo. Kundi hili ndilo linalochelewesha mapinduzi ya nchi, kundi hili ukesha likiomba CCM iweke mtu wa dini yake bila kujali uwezo wa kiongozi husika, wako tayari hata kupigia kura mgombea mwenye mtindio wa ubongo ilimradi awe wa dini yake.

7. Mafisadi papa. Hili ni kundi ambalo ni chafu kabisa, halina hata dini. Limeiba pesa nyingi za Watanzania bila kujali kuwa kila siku kuna masikini wanakufa kwa kukosa dawa mahosipitalini. Kundi hili kwa kutumia nguvu ya pesa za wizi linatamani ligawie kila mtanzani laki moja ili wapigie kura CCM. Kundi hili linahitaji CCM idumu ili lipate security ya mali zake, liko tayari hata kuua au kung'oa mtu kucha anaehatarisha CCM kuanguka. Linahofu kuwa chama kingine kikiingia madarakani litafilisiwa na kupelekwa mahakamani. Ni kundi lenye nguvu kubwa hata sasa ndani ya CCM
 
Ndugu Zanguni

Nimesoma barua ile iliyowekwa hapa ikidaiwa kuwa imeandikwa na Mh Zitto na pia nimesoma maelezo yake hapa leo na kushangazwa sana na hizi double standards za CHADEMA , chama ambacho ndio kikubwa cha upinzani nchini na ambacho tunategemea ndio kiwe cha kwanza kutuonyesha mfano kuwa wakipewa dola watafanya nini pale viongozi wao wakiharibu au kukumbwa na kashfa yoyote inayohitaji uchunguzi wa polisi.

Wote tunajua kuwa ikitokea kashfa sehemu fulani ndani ya serikali CHADEMA huwa ni wa kwanza kushinikiza mhusika ajiuzuru au asimamishwe kupisha uchunguzi jambo ambalo na mimi nakubaliana nalo kwani huwezi kumchunguza mtuhumiwa wakati bado ni kiongozi. Ili uchunguzi uwe wa huru na haki inabidi muhusika asimamishwe kupisha uchunguzi huo ili asiwe na nafasi yoyote ya kuweza kuharibu ushahidi au kuwanyima nafasi wapelelezi kufanya uchunguzi wa kina kwa kumuonea aibu au huruma. Uchunguzi/upelelezi ukiisha basi hatima yake ndio itajulikana.

Sasa leo chadema wanashindwa kumsimamisha kwa muda Kiongozi wao na wanapinga kwa nguvu zote kuwa ameonewa, Hivi ikija kuonekana kuwa huyo kiongozi ana hatia tutawaelewaje? Kesho mtawezaje kuwanyooshea kidole CCM pale watakapoonekana wana kashfa?

Sidhani kama CHADEMA wanaweza kuchukua maamuzi mazito kama aliyochukua Mh Lowassa pale alipojiuzuru uwaziri mkuu.

Kuna UTOFAUTI GANI???

Maalim Seif:amtakaka Waziri Emmanuel Nchimbi ajiuzulu

Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Mh, Maalim Seif Sharif Hamad amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt, Emmanuel Nchimbi kujiuzulu katika wadhifa wake kutokana na kushindwa kuisimamia Wizara yake katika utekelezaji wa majukumu yanayohusika na wizara hio.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Mbagala Zakhiem Maalim Seif ambae pia ni Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema Dkt, Nchimbi analazimika kujiuzulu kutokana na wizara yake kushindwa kusimamia ulinzi wa Wananchi na mali zao.

Mh,Hamad amesema kua suala la ulinzi wa raia na mali zao ni jukumu la serikali hivyo kupitia Wizara ya mambo ya ndani ya Nchi ambayo ndio yenye jukumu la kusimamia ulinzi imeshindwa kutekeleza wajibu huo na hatimae kumekuwa kukibuka kwa vitenddo mbali mbali vya kihalifu vinavyo hatarisha usalama wa Wananchi na mali zao.

Amesema matukio ya kihalifu yanayo endelea kujitokeza Nchini iwemo kushambuliwa pamoja na kuuwawa kwa viongozi na raia wasio na hatia kunatokana na serikali kushindwa kuimarisha ulinzi kwa raia wake.

"Kumekuwa na matukio mbalimbali ya kihalifu yanayotokea hapa nchini ambayo wziri Nchimbi na wizara yake wamwshindwa kuyatafutia ufumbuzi hadi leo hivyo hana budi kujiuuzulu kwani ameshindwa kutekeleza wajibu wake kamawaziri anaehusikannaulinzi" alisema Maalim Seif.

Akizungumzia matukio ya kushambuliwa kwa viongozi wa dini yaliotokea Zanzibar hiivi karibuni hayapaswi kuhusishwa na itikadi za kidini kutokana na utamaduni wa muda mrefu wa kuvumiliana kidini uliojengeka kwa Wananchi wa Zanzibar.

Aidha Maalim seif amechukizwa na kauli ya Dkt. Nchimbi kulihusisha tukio la kuuwawa kwa Padre Evarist Mushi na matukio ya kigaidi na kusema ttukio hilo si la kigaidi kwani Zanzibar hakuna ugaidi.

"Huyu ana lengo gani na Zanzibar hata kutangaza ugaidi kwa Zanzibar kwani Zanzibar hakuna ugaidi na wala hautatokea kamwe" alisema Maalim Seif.

Akizungumzia mwenendo wa Serikal;I ya Umoja wa kitaifa ya Zanzibar amesema Serikali kwa kiasi kikubwa imefanikiwa kuleta maendeleo kwa Wananchi wake ikiwa ni pamoja kuinua juhudi za wakulima katika ukuzaji wa kilimo chenye tija kwa wakulima na taifa kwa ujumla.

Amesema kuwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyo chini ya mfumo wa umoja kitaifa imefanikiwa kuinua zao la karafuu kwa kupandisha bei ya karafuu kutoka shilingi elfu tatu kwa kilo hadi elfu kumi bei ambayo inampa mkulima asilimia thamanini ya bein ya soko la dunia.

Pia imefanikiwa kukuza kilimo cha mpunga kwa kuwapatia wakulima wa kilimo hicho kwa kuwapatia wataalamu wa kutosha pamoja na kushusha gharama za pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea na dawa za kuulia wadudu ili kuwawezesha wakulima kulima kilimo chenye tija na kuondokana na utegemezi wa chakula kutoka nje.

Aidha amesema kuwa serikali imefanikiwa kuongeza kiwango cha mishahara ya wafanyakazi hadi asilimia ishirini na tano kwa wafanyakazi wa kima chachini ili kuweza kujikimu klimaisha.

Nae Naibu katibu mkuu wa CUF Tanzania Bara Mh, Julius Mtatiro amewataka wanachama hicho kujitokeza katika kuwania nafasi za ujumbe wa mabaraza ya katiba ili kuweza kupata katiba bora itakayo endana na mahitaji ya Wananchi.

Amesema kuwa kutokushiriki katika mabaraza ya katiba ya wilaya kutawapa nafasi watu wasiotaka maslahi mazuri kwa wananchi kuingia katika mabaraza hayo jambo litakalo sababisha kukosekana kwa katiba bora.

Mapema Mbunge mstaafu wa nafasi za wanawake wa Chama cha CUF Bi, Hania Chaurembo amewataka akina mama wa Chama hicho kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi za uongozi katika Chama ili kupata viongozi watakao kiongoza Chama hicho katika kupata ushindi katika uchaguzi mkuu uja wa mwaka 2015.

Hebu tuwe serious kidogo,
??????
 
Lukosi wewe ndiye una nia ya kugombea ubunge? Hata ungewakusanya ukoo wako hutapata kura! Nadhani hata baba na mamako watakukataa, maana akili yako haina akili kabsaaa!!
 
Back
Top Bottom