Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,339
- 9,766
Ndugu zangu Watanzania,
Niliwaambieni humu jukwaani siku chache zilizopita kuwa CCM imeitisha kikao cha dharura na kuwa ukiona CCM imeitisha mkutano au kikao cha dharura cha halmashauri kuu ya Taifa basi ni lazima nchi isimame,ni lazima nchi itetemeke,itekwe kimijadala na kuzima habari zote zinazokuwepo. CCM ikitoa habari zake ni lazima hata habari za simba na yanga ziwe chini kwa kuwa CCM ipo juu ya vyote na yote hapa Nchini.
Sasa leo CCM imekuja na taarifa za kishindo zililzoitetemesha nchi na kuteka habari zote katika anga la Tanzania na katika siasa za Taifa letu na nje ya nchi. Hii ni baada ya uteuzi wa Ndugu Paul Makonda Simba wa nyika ,komandoo wa vita,legendari wa siasa,mwamba wa chuma ,Jabali la siasa kuteuliwa kuwa katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa. Hakika ni uteuzi bora kabisa katika miaka ya hivi karibuni kufanywa na CCM Katika nafasi hiyo ya uenezi .Makonda ni mtu na nusu ,ni komandoo na jasusi mwenye uwezo wa kupenya popote pale na katika kizingiti cha aina yoyote ile, ni mwana mikakati imara sana na bora sana,ni mtu mwenye kujiamini kama simba awapo mbugani ,ni mtu mwenye misimamo na asiyeyumba wala kuyumbishwa ,ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana katika kujenga hoja zenye ushawishi na kuvutia na ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kupangua hoja kwa hoja.
Makonda ni mtu mwenye kujuwa nini kifanyike wakati gani na kwa kutumia watu gani,afanye nini na wapi na muda upi. Chama kimepata mtu sahihi katika wakati sahihi,mtu mwenye uzito unaoendana na uzito wa chama chenyewe. Niambieni namna majukwaani kutakavyo noga huko, niambieni ni hoja ipi itakosa majibu kutoka kwa Paul makonda? Niambieni ni nani kutoka upinzani atasimama katika mjadala na Paul makonda na akaweza kushinda mjadala? Paul makonda Anakwenda kukipa sauti chama kila uchwao,anakwenda kukiweka chama midomoni mwa watu muda wote,chama sasa hakitashambuliwa pasipo kujibu mapigo kana kwamba kimefungwa pingu za mdomo.
Sasa CHADEMA matumbo joto,moja haiendi wala mbili haisomi,wamepoteana na wamebaki wanyonge sana, wamekosa jibu wafanye nini kuziba kimbunga na upepo unaoendelea kuvuma na uliosambaratisha na kuzizima kama mshumaa habari za CHADEMA.sasa watu wake wachache kwa kujikongoja wamebaki wanahangaika kwa kutukana matusi mitandaoni kama vichaa.hii ni kwakuwa wanatambua kuwa ndio mwisho wao na anguko lao limewadia,wanajuwa kuwa mwaka kesho na kesho kutwa wanakwenda kuambulia patupu katika uchaguzi.
Hii ndio CCM chama kiongozi barani Afrika,chama ambacho kinaweza kubadilisha upepo ndani ya siku moja mkabaki mnatetemeka kama wagonjwa wa degedege,hii ndio CCM Ambayo inakupa ajenda kama mfupa ili ubaki unaijadili na kuhangaika nao muda wote wakati yenyewe ikichapa kazi na kujisimika katika mioyo ya watanzania,hii ndio CCM yenye mikakati na mbinu zaidi ya mia moja lakini ikiwa haijatumia mbinu hata mbili kati ya mia,.jiulize vipi itakapotumia mbinu hata tano tu?
Karibu sana Ndugu Paul makonda komando wa vita , mpambanaji wa kweli na unayekifahamu chama nje ndani .karibu sana kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa ilani yetu ya CCM ili kuhakikisha kuwa watanzania wanapata huduma kwa ubora na kwa haraka,karibu sana chamani ambacho kimekupa heshima kubwa ili ukisaidie katika utendaji wake. chama na wanachama tuna matarajio makubwa sana na wewe na tuna imani kubwa sana kwako,.usijiulize CCM itakufanyia nini bali jiulize utaifanyia nini CCM.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.