Dokta Kitila Mkumbo usikimbie hoja mzee wangu

Dokta Kitila wananchi wanachama na ulimwengu mzima unajua chama cha CDM ni Chama Cha DEMOKRASIA na Maendeleo je DEMOKRASIA ya chama cha CDM mchakato wake ndio upo kama hapa kwenye jedwali? Na je unaweza kutupa marks za Mama Msori Vs Joyce Mukya natanguliza shukrani zangu za dhati.
Vigezo vya uteuzi wa wabunge wa viti maalumu kupitia CHADEMA 2010-2015
Na
Kigezo
Alama
1.
Elimu
10
1.1 Shahada ya Uzamivu (PhD) 10
1.2 Shahada ya Uzamili (Masters Degree) 8
1.3 Shahada ya Kwanza/Stashahada ya Juu (Bachelors Degree/Advanced Diploma) 6
1.4 Stashahada/Kidato cha Sita (Diploma/Form Six) 4
1.5 Astashahada/Kidato cha Nne (Certificate/Form 4) 2
1.5 Darasa la Saba (Std VII) 1
1.6 Chini ya Darasa la Saba (Below Std VII) 0
2
Uzoefu wa uongozi wa kisiasa
10
2.1 Uzoefu wa kibunge 10
2.2 Uzoefu kitaifa (BAWACHA, n.k) 8
2.3 Uzoefu katika ngazi ya mkoa/aliyewahi kuchaguliwa kuwa diwani/aliyewahi kuchaguliwa katika ngazi ya serikali ya mtaa/kijiji 6
2.4 Uzoefu katika ngazi ya wilaya/aliyewahi kuwa diwani wa viti maalumu 4
2.5 Uzoefu katika ngazi ya kata 2
2.6 Uzoefu katika ngazi ya kijiji/tawi 1
3
Uzoefu wa uongozi nje ya siasa (km: katika asasi za kiraia, vyama vya wafanyakazi, taasisi za serikali, n.k.)
5
4
Mgombea ubunge katika jimbo la uchaguzi
10
4.1 Katika jimbo la rangi nyekundi (Red Constituency) 10
4.2 Katika jimbo la rangi ya bluu (Blue Constituency) 8
4.3 Katika jimbo la rangi nyeupe (White Constituency) 6
4.4 Katika jimbo vumbi (Dust Constituency) 2
5
Mchango wa hali na mali katika operations za chama na kampeni zinazoendelea
10
5.1 Daraja la I 10
5.2 Daraja la II 8
5.3 Daraja la III 6
5.4 Daraja la IV 4
5.5 Daraja la V 2
6
Umri katika chama
5
6.1 Zaidi ya miaka 10 5
6.2 Miaka 5-10 4
6.3 Miaka 2-4 3
6.3 Chini ya miaka 2 2
6.4 Chini ya mwaka 1 1
Jumla ya Alama
50
a
 
[h=2][/h] Dr.Kitila
Vigezo vya uteuzi wa wabunge wa viti maalumu kupitia CHADEMA 2010-2015

Suala linakuja hivo vigezo ulivipata kwa njia gani? What is your base ya vigezo hivyo?

Kwa sababu unaweza kuunda model ikawa favor wale uwatakao iwapo model yako haina misingi isiyoweza kubadilishwa na mtu mwengine.

* Model ambayo misingi yake ni assumption zinazotokana na hisia na matakwa ya mbunifu wake tu haziwezi kuitwa za kisayansi kamwe, na hazina credibility yoyote katika medani za wanasayansi.
 
Mkuu Sokomoko mbona umekaa Kinape Nape sana?kwa ujumla sijaelewa nini hasa unachozungumzia zaidi ya kuona mada zimechanyikana tuuu...Labda mi kwa ufupi nichangie hivi,

1.Unaposema posho zenyewe zinazopigiwa kelele ni ndogo sana ukifananisha na mishahara ya wabunge na kuwa badala ya kupigia kelelel posho wapigie kelele mishahara,nilivyokuelewa ni kuwa unakubali kuwa posho nazo ni tatizo na mishahara yao ni tatizo.Kama vyote hivyo ni tatizo kwa nini basi tusianze na posho na baadae tuje kwenye hiyo mishahara kama data zako zinavyosema?

2.Kuna wakati kwenye comments zako unajifanya uko neutral,lakini maelezo yako yanalalia kwenye magamba,hueleweki mkuu jipambanue kwani ukijulikana ni wa magambani si dhambi.

3.Hoja ya mchakato wa kuwapata wabunge wa viti maalum wa CHADEMA ni sehemu tu ya tatizo.Mchango chanya wa uwepo wa wabunge hawa bungeni bila kujali wanatoka chama kipi nadhani ndiyo mada ya kuijadili kwani kwa mtazamo wangu sioni walifanyalo zaidi ya kupiga meza na kuongeza idadi wa wabunge wasio na tija.

4.Maneno yako ya "Naona Dr. kakimbia" yanaonyesha ulimkamia kweli Dr.Janvini hatukamiani mkuu-humu ni hoja tu.Inaonekana mkuu Sokomoko ulikuwa na muda mwingi sana leo lakini kumbuka si watu wote wana kazi ya kukaa kwenye JF tu,labda kwa wale wanaoiratibu JF au wale waliotumwa kwa malengo maalum kama watu wa Nape.

Naomba kuwasilisha.
 
Tungo nzuri iliyosimama haya sasa mpelekee kakayo Mh.Raisi Jakaya aka Vasco dagama aka Mtambo hakika akifuata uliyoandika nchi itasimama

Mkuu Farida,

Mimi sipo CCM wala chama chochote cha siasa kwa kuogopa kuwa kipofu kama wewe, nimetoa hoja wenye akili wameelewa hata huyo niliemkusudia ameelewa kuwa chama chao kinaongozwa na mfumo dume! na ndio maana yeye aliwachagua wanawake wa viti maalum. Dr Kitila ni msomi hataki kuelezea sana anajua atajikanyaga hii ni mbinu nzuri sana.
 
Mkuu Sokomoko mbona umekaa Kinape Nape sana?kwa ujumla sijaelewa nini hasa unachozungumzia zaidi ya kuona mada zimechanyikana tuuu...Labda mi kwa ufupi nichangie hivi,

1.Unaposema posho zenyewe zinazopigiwa kelele ni ndogo sana ukifananisha na mishahara ya wabunge na kuwa badala ya kupigia kelelel posho wapigie kelele mishahara,nilivyokuelewa ni kuwa unakubali kuwa posho nazo ni tatizo na mishahara yao ni tatizo.Kama vyote hivyo ni tatizo kwa nini basi tusianze na posho na baadae tuje kwenye hiyo mishahara kama data zako zinavyosema?

2.Kuna wakati kwenye comments zako unajifanya uko neutral,lakini maelezo yako yanalalia kwenye magamba,hueleweki mkuu jipambanue kwani ukijulikana ni wa magambani si dhambi.

3.Hoja ya mchakato wa kuwapata wabunge wa viti maalum wa CHADEMA ni sehemu tu ya tatizo.Mchango chanya wa uwepo wa wabunge hawa bungeni bila kujali wanatoka chama kipi nadhani ndiyo mada ya kuijadili kwani kwa mtazamo wangu sioni walifanyalo zaidi ya kupiga meza na kuongeza idadi wa wabunge wasio na tija.

4.Maneno yako ya "Naona Dr. kakimbia" yanaonyesha ulimkamia kweli Dr.Janvini hatukamiani mkuu-humu ni hoja tu.Inaonekana mkuu Sokomoko ulikuwa na muda mwingi sana leo lakini kumbuka si watu wote wana kazi ya kukaa kwenye JF tu,labda kwa wale wanaoiratibu JF au wale waliotumwa kwa malengo maalum kama watu wa Nape.

Naomba kuwasilisha.

Mkuu heshima mbele,

1. Posho si tatizo kihivyooo ila linakuzwa lionekane tatizo nimeweka bayana kuwa posho kwa kipindi cha miaka mitano hazifiki Milioni 500! Lakini kuna mtu ninaemwamini ndani ya CDM alipata kuwa mbunge wa Karatu alianzisha vita ya wabunge kupunguziwa mishahara ile dhamira hakuna wa kuindeleza kwani hakufanikiwa kurudi tena bingeni baada ya kuhadaiwa. Unajua mishahara ikipunguzwa by 30% to 40% Serikali ita save 12 to 15 bilion kwa muda wa miaka mitano.

Hapa mimi nafanisha posho au ujira wa Mwiha kama kichuguu na Mishahara/viinua mgongo kama Evarest.

2.Mimi ni mtu huru sipo chama chochote chama changu ni Tanzania, nina amini katika siasa za mgombea binafsi asiewajibika kwa Mwenyekiti na vikao vya chama bali kwa wananchi wake. Ikiwa CDM watafanya jambo zuri nitakuwa mwehu kuiponda kadhalika kwa CCM wakifanya jambo la maana sitasita kuwapa pongezi.

Ifike wakati chama chenu kikikosea muwaambie hakuna kitu kibaya chenye kuharibu kama sifa za kijinga na zisizo na tija eti kwa sababu tu ya kuwafurahisha viongozi wetu! Viongozi wanatakiwa waambiwe ukweli ili warekebishe mambo yatakayoonekana hayafai.

3. Nakubaliana na wewe kwenye namba tatu kuwa hakuna tija yoyote zaidi ya kuwabebesha mzigo walipa kodi kwa kwenda kujaza viti bungeni. Ila demokrasia haikuchukua mkondo wake wakati wa uteuzi wa wabunge wa viti maalumu na aliefanya hivi alikuwa ni Dr Kitila Mkumbo! Yeye kama msomi na anajua chama alichopo ni cha DEMOKRASIA asingekubali kutumia vigezo vya kutoa maksi zaidi ya kutumia njia ya kidemokrasia.

4. Huo ndio ukweli na wala sijamkamia Dr juu ya Udaktari wake hawezi kujibu hoja iliyopo mezani kwani anajua fika kuwa chama chao ni cha DEMOKRASIA na alichokifanya ilikuwa kuifunika DEMOKRASIA iliyofanyika kwenye vikao halali vya BAWACHA na kufanya yale yafanywayo na madikteta. Tena nasema kwa kinywa kipana kuwa DOKTA sio kama hakujua ila alifanya ili kutekeleza maagizo ya mwenyekiti! nani asiejua kuwa hivi vyama vina wenyewe? Kule CCM tunawajua wenyewe piga ua garagaza lazima waingie mjengoni na wapo mule tangu vijana na sasa wanazeekea humo. Huku tunakotegemea kutakuwa na demkrasia tumeona copy and paste ile ile ya MAGAMBA! eti kwa kuwa Baba yake au mkwe wake kashwagala ni mmoja wa waasisi lazima kwenye ku rank apate alama za juu tena ikibidi lile jimbo alilogombea tuliweke liwe jimbo jekundu lenye maksi nyingi! huu ni uuawaji wa demkrasia!

Kimsingi hivi vyama vina kila aina ya uoza lakini kwa kuwa wamefanikiwa kuwahadaa na kutumia hoja za matatizo yenu na nyie mkaingiwa na mapenzi hamuwezi kuona kama kuna uoza wowote.

Nadhani utakuwa umenielewa ndugu yangu.
 
[h=2][/h] Dr.Kitila

Suala linakuja hivo vigezo ulivipata kwa njia gani? What is your base ya vigezo hivyo?

Kwa sababu unaweza kuunda model ikawa favor wale uwatakao iwapo model yako haina misingi isiyoweza kubadilishwa na mtu mwengine.

* Model ambayo misingi yake ni assumption zinazotokana na hisia na matakwa ya mbunifu wake tu haziwezi kuitwa za kisayansi kamwe, na hazina credibility yoyote katika medani za wanasayansi.

Mwalimu mimi nipo pamoja na wewe labda kwa kuongezea ni kuwa hiki ni chama cha DEMOKRASIA na MAENDELEO je Demokrasia inaelekeza mchakato aliouandaa Dr Kitila?
 
Thanks Kitila

But i think there is a need to be more scientific, and also more realistic kwenye vigezo, mtu anaweza akascore A kwa chart yako lakini hapendwi hata na fenicha za nyumba yake

MTM inabidi chama kiache demokrasia ichukue mkondo wake na sio kuweka vigezo vya kutea mtu kuwa mbunge au cheo chochote na ndio maana kikaitwa Chama Cha DEMOKRASIA na Maendeleo.
 
..nyinyi mnaopingana na hiyo model ya Kitila mngependekeza model zenu ambazo mnaona ni nzuri zaidi.

..nadhani Kitila amejitahidi kuleta model ambayo ni as fair as possible kwa wagombea wote.

..wagombea walipaswa kuikataa hiyo model kabla hawajaingia kwenye uchaguzi siyo baada ya uchaguzi.
 
Hiyo model haiko fair hata kidogo, kwa sababu iko subjective. Kitila akiamua "huyu katoa mchango mwingi wa hali na mali kwa chama" anampa points za juu wakati akija mtumiaji mwengine wa model ile ile, aliyepewa alama za juu na Kitila anaweza kupewa za chini.

Hiyo kisayansi huwezi kuiita ni model iliyokuwa fair kwa sababu haitoi majibu sawa kulinganisha na anaetumia (mark) kwenye model hiyo.

Ni failed model na Kitila analijua hilo na hawezi kuitumia tena uchaguzi mwengine kwa sababu ilivyo sasa, wabunge wa viti maalum wa sasa hawawezi kukosa alama za juu tena kwenye model hiyo baada ya miaka mitano. Asiyekuwa ndani ya system sasa hawezi kupata nafasi ya kuwashinda waliopo kwenye system sasa kwa kutumia model hiyo abadan asilan
 
Labda ungeomba details zaidi kwa sababu hujajua mchango wa hali na mali ni nini. La pili si kweli kwamba kwa vigezo hivi waliopo hawawezi kuondolewa --- hebu changanua tuone. Akijitokeza mwanamke mwenye PHD, akatoa mchango wa hali na mali kwenye operations za chama, akagombea jimboni, akawa kiongozi kimkoa atashindwa pia? Ndio tukiambiwe tu-introduce vetting process kwenye haya mambo watu hamtaki eti demokrasia. Tunaishia kuwa na viongozi wasanii wenye cv za uongo uongo.
 
Gaijin said:
Hiyo model haiko fair hata kidogo, kwa sababu iko subjective. Kitila akiamua "huyu katoa mchango mwingi wa hali na mali kwa chama" anampa points za juu wakati akija mtumiaji mwengine wa model ile ile, aliyepewa alama za juu na Kitila anaweza kupewa za chini.

Hiyo kisayansi huwezi kuiita ni model iliyokuwa fair kwa sababu haitoi majibu sawa kulinganisha na anaetumia (mark) kwenye model hiyo.

Ni failed model na Kitila analijua hilo na hawezi kuitumia tena uchaguzi mwengine kwa sababu ilivyo sasa, wabunge wa viti maalum wa sasa hawawezi kukosa alama za juu tena kwenye model hiyo baada ya miaka mitano. Asiyekuwa ndani ya system sasa hawezi kupata nafasi ya kuwashinda waliopo kwenye system sasa kwa kutumia model hiyo abadan asilan.

Gaijin,

..haiwezekani kupata model ambayo haina kasoro hata moja.

..model hiyo ina matatizo kama itatumiwa na mtu mmoja tu, lakini kama kuna TEAM/PANEL ya watu wanao interview wagombea basi at the end of the day the process will be as fair as possible.

..asiyekuwepo kwenye system anaweza kushinda kama ana vigezo vingine vizuri kushinda walioko ndani. kukuhakikishia hilo ndiyo maana umeona kwa kutumia model hiyo mwenyekiti wa baraza la wanawake wa chadema alishindwa na "watu wa kuja" ktk chama.

..kwasababu una matatizo na model hii, labda ungependekeza an alternative model ambayo ingewafaa chadema zaidi ya hii waliyoitumia.
 
SOKOMOKO wewe ni mpuuzi nenda kamwambie babako na mamako hivyo mlafi wewe malaya mkubwa umesahau criteria walizozingatiya chadema sasa kama unajifanya unajua mbona bado waleta upuuzi wako hapa usio na maana basi tuseme wewe ndio unakili kuliko prof.baregu,Dr.kitilo mkumbo na wataalam wengine wengi ambao ndio walitwa na chadema kufanya kazi hiyo nipe criteria walizozingatiya CCM zaidi ya kuliwa uroda na au kujuana na mtu fulani au unafikiri chadema ni kama ccm kuwa ambayo utapewa tu kama ni mboga ya wakubwa wanaosema hivyo ni wapuuzi na wajinga kama wewe wanaotumia makalio kufikiri badala ya akili
 
Gaijin,

..haiwezekani kupata model ambayo haina kasoro hata moja.

..model hiyo ina matatizo kama itatumiwa na mtu mmoja tu, lakini kama kuna TEAM/PANEL ya watu wanao interview wagombea basi at the end of the day the process will be as fair as possible.

..asiyekuwepo kwenye system anaweza kushinda kama ana vigezo vingine vizuri kushinda walioko ndani. kukuhakikishia hilo ndiyo maana umeona kwa kutumia model hiyo mwenyekiti wa baraza la wanawake wa chadema alishindwa na "watu wa kuja" ktk chama.

..kwasababu una matatizo na model hii, labda ungependekeza an alternative model ambayo ingewafaa chadema zaidi ya hii waliyoitumia.

Wasioweza kutoka kwenye system ni wale hawa wa sasa kwenye uchaguzi wa 2015. Au unless atokee mwenye Phd, atakaegombea ubunge jimboni, atakaesaidia chama kwa hali na Mali na awe amejiunga kuanzia sasa labda ndio aweze kuwashinda wabunge wa sasa hasa wenye Phd ambao watakuwa na alama zote za juu.

Ikimaanisha kuwa mwenye advanced diploma ambae ataingia kwenye chama miaka miwili kabla uchaguzi, akajitolea mengi, hataweza kamwe kuchukua nafasi ya waliopo sasa japo Kama ni kiongozi mzuri.

Hata ikiwa siwezi kutunga model better zaidi ya hiyo ya Kitila haimaanishi kuwa ya Kitila ni nzuri na isikosolewe.

Yeye mwenyewe anajua kuwa model yake iko instinctive tu, na haina base ya kisayansi hata ndogo.
 
..kwa mtizamo wangu model ina vigezo ambavyo viko fairly diverse.

..i am not saying kwamba it is a perfect model lakini nadhani it is something that Chadema could start with.

..huko mbeleni wanaweza kuiboresha ili ku-deal na mapungufu ambayo umeyabainisha.

..kwa upande mwingine, you seem to have ideas in mind but are reluctant to share with us.

NB:

..nadhani model kama hii inawafaa CDM ukizingatia kwamba hawana mtandao mkubwa wa wanachama pamoja na matawi.
 
Hivi,kama mnaamini na kuisimamia DEMOKRASIA,msingekuwa mnabishana kuhusu model ya kuchagua wabunge wa viti maalum/kuteuliwa.
WATANZANIA HATUTAKI VITI MAALUM/KUTEULIWA.....TUNATAKA WABUNGE WA KUCHAGULIWA NA WANANCHI MAJIMBONI!
 
Viti maalum ni tatizo ni model yoyote itakuwa ni tatizo tu. Tuondoleeni maalum hii, ni mzigo tu! Kwani "Gaijin", umaalum wake hapa ni nini?
 
Viti maalum ni tatizo na model yoyote itakuwa ni tatizo tu. Tuondoleeni maalum hii, ni mzigo tu! Kwani "Gaijin", umaalum wake hapa ni nini?
 
Kwani hao kina Kamata wamechaguliwa kwa vigezo gani kama sio kwa nyimbo za kusifia watu fulani. Swala la mtu kaingia lini kwenye chama sio kigezo kuwa mtu huyo ana uwezo.
 
Back
Top Bottom