Dokta Kitila Mkumbo usikimbie hoja mzee wangu

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
Baada ya mdau sulphadoxine kuleta upupu ufuatao.

Muhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) na Mkuu wa idara ya saikolojia na taaluma ya mitaala Dkt. Kitila
Mkumbo,amesema kuwa wakati huu ndio mwafaka kwa nchi kusimamia uwajibikaji kwa ajili ya maendeleo ya taifa.Dkt alitoa kauli hiyo jana wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi vyeti wanafunzi ambao ni wanachama wa chama cha Demkrasia na maendeleo (CHADEMA),tawi la chuo kikuu Dar es salaam(CHASO-UDSM) ambapo yeye ni mlezi wa wanafunzi hao.

Mheshimiwa Dokta Kitilla Mkumbo akamjibu...........

Habari haijakamilika. Tafuta Gazeti la Majira usome upate context ya hoja zangu vizuri. Sikuongelea uwajibikaji katika context ya serikali. Nilikuwa nawaasa vijana juu ya umuhimu wa kuwajibika kikamilifu kitaaluma na kitaalamu, kuchapa kazi kwa bidii na kuachana na kasumba iliyoanza kujengeka nchini mwetu ya kutaka mafanikio kwa njia ya ujanjaujanja na njia za mkato. Nikasisitiza kwamba waweke kipaumbele kufanya kazi kwa bidii, maarifa na kuipenda nchi yao. Hakuna short cut ya mafanikio zaidi ya kuwajibika na kuchapa kazi kwa bidii na upendo wa dhati kwa nchi.

Sasa watu wamezoea wakisikia uwajibikaji wanafikiria serikali-that was not my point mkuu.

Nilipomwona Dokta wa ukweli yupo online na alikuwa akifatilia mada nikamuuliza

Mheshimiwa Dokta Kitila Mkumbo hisima yako,

Nikiwa Mtanzania mwenye uchungu na nchi hii sijafurahiwa na hatua iliyochukuliwa na wabunge wa chama chako mpaka sasa kuhusu kupunguza matumizi ya Serikali. Kama kawaida yetu kwa ajili ya ujuha tulionao mmefanikiwa "kututeka" na hoja ya posho. Lakini ukiangalia hizo posho wanazozizungumzia kina Zitto Bungeni ni pesa ndogo sana.

Je ni lini mtarudia ile dhamira ya Mhe Dr Slaa ya kupunguza mishahara ya wabunge? maana hapo ndio Serikali itafanya savings ya uhakika si tunafahamu kwa mujibu wa kiinua mgongo kwa wabunge kinatolewa kwa mujibu wa sheria ya mafao ya viongozi wa kisiasa namba 3 ya mwaka 1999 ambayo ilianza kutumika 2000 na kisha kufanyiwa marekebisho mwaka 2005 katika kipengere cha sheria namba 12.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, iliyotokana na marekebisho ya sheria ya awali ya mafao ya viongozi maalum wa kitaifa ya mwaka 1986, sio wabunge wote watakaovuna kiasi hicho cha fedha, kwa kuwa muda wao wa kuwa bungeni unatofautiana.

Mfano tukichukulia idadi tuseme Bunge la Jamhuri ya Muuungano lina wabunge 327, kati yao 49 ni mawaziri na manaibu waziri. Ukiondoa mawaziri na manaibu wao ambao kinua mgongo chao hulipwa na serikali, hivyo watakaolipwa na Bunge ni 278. Kwa mantiki hiyo, jumla ya Sh12,724,704,000 zitalipwa kama kiinua mgongo kwa wabunge hao ukiondoa mawaziri.

Fedha hizo ni sawa na asilimia 40 ya mishahara ya miaka yote mitano ya utumishi bungeni ambapo kwa mujibu wa marekebisho ya mishahara ya viongozi wakuu wa nchi na viongozi wa kisiasa yaliyofanywa Julai mwaka 2009.

Ukilinganisha na kazi wanayoifanya wabunge hawastahiki kupokea kiwango kikubwa kama hiki huu ni unyonyaji na wizi wa mchana kweupe kuliko wizi wa posho ambazo mnazipigia kelel ili kuwin popularity. Tujaribu kuwa wazalendo kidogo tufanye ya ukweli.

Asante sana mheshimiwa na ni matumaini yangu kina Zitto wataibua hoja ya mishahara ya wabunge ili kupunguza viinua mgongo vyao.

Songela sana/

Mheshimiwa Mkumbo.

Japo mimi ni mtanzania lakini sina usahaulifu kama wengi miongoni mwetu tulivyo, nakumbuka wewe ni mmoja wa watu walioinajisi demokrasia ndani ya chama cha "demokraisa" kwa kuwachagua wanawake watakaopita kwenye viti maalumu ndani ya chama chako. Vigezo ulizingatia mwenyewe kwani katiba ya chama haijaainisha vigezo vya watakao teuliwa viti maalumu.

Tunajua kulifanyika mchakato wa kidemokrasia kupitia baraza la wanawake la chadema BAWACHA lililokuwa likiongozwa na mwana mama aliejitolea kwa hali na mali kukuza chama MS Letcia Musori. Huyu mama alikuwa miongoni mwa wanawake waliochaguliwa na vikao halali vya BAWACHA lakini mchakato ule wa BAWACHWA ulianchwa ukachaguliwa wewe "mwanaume" uwachagulie "wanawake" wawakilishi wao what a joke! Anyway sio mbaya lakini unaposema
ilikuwa nawaasa vijana juu ya umuhimu wa kuwajibika kikamilifu kitaaluma na kitaalamu, kuchapa kazi kwa bidii na kuachana na kasumba iliyoanza kujengeka nchini mwetu ya kutaka mafanikio kwa njia ya ujanjaujanja na njia za mkato. Nikasisitiza kwamba waweke kipaumbele kufanya kazi kwa bidii, maarifa na kuipenda nchi yao. Hakuna short cut ya mafanikio zaidi ya kuwajibika na kuchapa kazi kwa bidii na upendo wa dhati kwa nchi.
Wakati wewe ulikuwa mmoja wao uliewafanyia short cut baadhi ya waheshimiwa ina maana rahisi sana kuwa wewe hutembei kwenye maneno yako! Hatujui utashi gani kuwa weka juu kina Rose Kamili aliekuwa CCM na Diwani mpaka kabla ya uchaguzi mkuu Mama yangu Mama Naomi Kahihula aliekuwa ananifundisha CBE mpaka kabla ya Uchaguzi hawa wamekuwa wanawake wa juu CDM wamewapita hata wale waliokuwepo tangu mwiaka ya mwanzoni mwa 2000. Siri mnaijua wewe na mwenyekiti wako ila ukweli ni kwamba wewe mwenyewe hukuwajibika kikamilifu kitaaluma na kitaalamu Vipi wanafunzi uliokuwa ukiwahutubia wawajibike na sio kufuata nyayo zako?

Binafsi sifurahiwi sana na utendaji wako unaonyesha wewe ni mtu wa mizaha na usie na hoja nakumbuka ulitoa jibu kuwa
quote_icon.png
Originally Posted by Kitila Mkumbo
Tatizo la huyu mama yetu alikariri kwamba yeye lazima ilikuwa awe mbunge wa viti maalumu kwa sababu tu alikuwa mwenyekiti wa BAWACHA kitaifa. Bahati mbaya kwake ni kwamba hatukuwa na kigezo specific cha kumlenga mwenyekiti wa bawacha au kiongozi yeyote mwingine. Katika vigezo tulivyotumia yeye aliangukia kwenye namba 29 kama inavyoonekana katika orodha hapa chini ya first 40 candidates.

Katika safari hii ya mapambano sio abiria wote watakaofika mwisho wa safari; wapo watakaoshukia njia-huyu ni mojawapo!!

Orodha ya wanaopendekezwa kuwa wabunge wa viti maalumu-CHADEMA

Orodha ya wanawake 40 wa juu

1.Lucy Fidelis Owenya
2. Esther Nicholas Matiko
3. Mhonga Said Ruhwanya
4. Anna MaryStella John Mallac
5. Halima James Mdee
6. Paulina Philipo Gekul
7. Conjesta Leos Rwamlaza
8. Susan Kiwanga
9. Grace Sindato Kiwelu
10. Susan Lyimo
11. Regia Mtema
12. Christowaja Mtinda
13. Anna Valerian Komu
14. Mwanamrisho Abama
15. Joyce Mukya
16. Leticia Mageni Nyerere
17. Naomi Kaihula
18. Chiku Abwao
19. Rose Kamil Sukum
20. Christina Lissu Mughiwa
21. Raya Ibrahim Hamisi
22. Philipa Geofrey Mturano
23. Mariam Salum Msabaha
24. Rachel Mashishanga Robert
25. Sabrina Hamza Sungura
26. Rebecca Michael Mngodo
27. Cecilia Daniel Pareso
28. Subira Shabani Waziri
29.
Leticia Gati Musore
30. Helen John Kayanza
31. Rosana Osemu Chapita
32. Mona Shomary Bitakwate
33. Evarim Adrian Mpangama
34. Asha Sudi Kayumba
35. Hija Rashid Wazee
36. Mary James Martin
37. Sophia Hebron Mwakagenda
38. Bupe Odeni Kyambika
39. Magreth Thadei Mangowi
40. Esther Cyprian Daffi

Hukutupa data ya jinsi ulivyo wa rank hawa wanawake wa juu kwani kwa kuzingatia haki Mama Musori alikuwa Mwenyekiti wa baraza la wanawake Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema na Mweka Hazina wa Umoja wa Madiwani wa Chadema na kukidhi vigezo vilivyowekwa pia Musori alikuwa anajua Kiingezera, Kijerumani na Kiswahili akiwa na Cheti cha Nurse Midwife (Diploma) aliyoipata Ujerumani pia amekuwa akiitumikia CDM kwa muda na kina Rose Kamili wamemkuta!

Sote tunajua mbunge akimaliza muda anapata kiinua mgongo cha asilimia 40 ya mshahara wake kwa mazingira uliyowateua itakuwa ni vigumu kuamini hakukuwa na rushwa na upendeleo hatujui ulipata/utapata nini kama ahsante ya uteuzi wako uliotukuka. Kwa uchache kina Rose Kamili wataondoka na kitu kama 45 mil baada ya kumaliza term yao ya ubunge ni dhahiri umewatafutia short cut ya nguvu na kwa hili nakupa hongera sana.

Kumalizia napenda kukufahamisha umewasaidia short cut kina Rose Kamili, Naomi Kaihula, Chiku Abwao ya maisha ungewaacha waweke vipaumbele kwenye kufanya kazi kwa bidii ya kukuza chama, maarifa na kukipenda chama chao. Hakuna short cut ya mafanikio kwenye chama zaidi ya kuwajibika na kuchapa kazi kwa bidii na upendo wa dhati kwa chama na kwa wananchi.

Dokta napenda uelewe kuwa
"You can fool some of the people all of the time, and all of the people some of the time, but you cannot fool all of the people all the time." – Abraham Lincoln

Unafiki wa waandishi wa habari.

Kuna waandishi wa habari wanasifika kwa vichwa vizuri vizuri vya mada zao kama Maswali Magumu na Ansert Ngurumo, Kuna mmoja anajiita yeye ni mwana wa shambani ilhali anakula bata Marekani amepewa coverage kubwa sana kule TZ Daima hawa hata siku moja huwezi kuwasikia wakiuliza maswali magumu ya kuihusu CDM nasema CDM kikifa tusmtafute mchawi sote tunatunahusika watazamaji na wachezaji kumbukeni CDM nyie ndio tumaini la vijana wengi wanyonge ipo siku watagundua hila na uozo wenu na kuingia mitini.

Uchu wa cheo waiza,macho wengi hupofuka,
Mwenyewe hujilemaza,kuvaa kustahika,
Siachi kujiuliza,vipi atasetirika ?
Hata upake marashi,kilicho'za kimeoza.

Wavivu tunawaoza,kwa vyeo kuwajibika,
Ajizi zinapoanza,jukwaani twalalamika,
Jamaa twapa vyeo kwanza ,ukubwa kuwapachika,
Hata upake marashi,kilicho'za kimeoza.

Vigumu nawaeleza,nchi kuweza jengeka,
Huku tunafuga funza,madaraka kuja shika,
Vidole kuviongoza,twende tunapopataka,
Hata upake marashi,kilicho'za kimeoza

Kuzoza nilikizoza,si mtu wa kusikika,
Hodari waliojifanza,waona wameelimika,
nini utachowafunza,waweze tena kushika,
Hata upake marashi,kilicho'za kimeoza.

Yangu sasa namaliza,cheo sitaki kushika,
Najificha na ajuza,shaibu nimetosheka,
Anijalie Muweza,hatima kurehemeka,
Hata upake marashi,kilicho'za kimeoza

Dk Mkumbo sio size yako tafuta shughuli nyingine ufanye. Mshauri Mama Musori aende CCM wanakochaguana kwa kukaa kwenye chama kwa muda mrefu. Unatupotezea muda bana!
 
Dk Mkumbo sio size yako tafuta shughuli nyingine ufanye. Mshauri Mama Musori aende CCM wanakochaguana kwa kukaa kwenye chama kwa muda mrefu. Unatupotezea muda bana!

Well kuhusu CCM juu ya mambo yao ya ufisadi wanao mfumo wa kidemokrasia wa kuchagua wanawake wa kuwawakilisha wanawake wenzao bungeni juu ya mambo yao ya ufisadi hutasikia ameteuliwa John wala Edward kuwachagua wanawake watakao wawakilisha wanawake kwenye viti maalum bungeni.
 
Dk Mkumbo sio size yako tafuta shughuli nyingine ufanye. Mshauri Mama Musori aende CCM wanakochaguana kwa kukaa kwenye chama kwa muda mrefu. Unatupotezea muda bana!

Sio size yangu kwa sababu yeye anakaa uzunguni mie nakaa uswahilini kwa mtogole? no ni saize yangu mie natoka Nduguti na yeye anatoka moja ya tarafa za wilaya ya Iramba mimi na yeye wote tumekulia matogo na sasati. Ila yeye anaweza akawa matawi kwa kuwa ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani kwahiyo ki status ana cheo lakini tukirudi nyumbani sie sote ni wanyiramba bila kujali huyu anatoka gumanga au kinangiri!
 
Baada ya mdau sulphadoxine kuleta upupu ufuatao.

Mheshimiwa Dokta Kitilla Mkumbo akamjibu...........

Nilipomwona Dokta wa ukweli yupo online na alikuwa akifatilia mada nikamuuliza

Mheshimiwa Mkumbo.

Japo mimi ni mtanzania lakini sina usahaulifu kama wengi miongoni mwetu tulivyo, nakumbuka wewe ni mmoja wa watu walioinajisi demokrasia ndani ya chama cha "demokraisa" kwa kuwachagua wanawake watakaopita kwenye viti maalumu ndani ya chama chako. Vigezo ulizingatia mwenyewe kwani katiba ya chama haijaainisha vigezo vya watakao teuliwa viti maalumu.

Tunajua kulifanyika mchakato wa kidemokrasia kupitia baraza la wanawake la chadema BAWACHA lililokuwa likiongozwa na mwana mama aliejitolea kwa hali na mali kukuza chama MS Letcia Musori. Huyu mama alikuwa miongoni mwa wanawake waliochaguliwa na vikao halali vya BAWACHA lakini mchakato ule wa BAWACHWA ulianchwa ukachaguliwa wewe "mwanaume" uwachagulie "wanawake" wawakilishi wao what a joke! Anyway sio mbaya lakini unaposema Wakati wewe ulikuwa mmoja wao uliewafanyia short cut baadhi ya waheshimiwa ina maana rahisi sana kuwa wewe hutembei kwenye maneno yako! Hatujui utashi gani kuwa weka juu kina Rose Kamili aliekuwa CCM na Diwani mpaka kabla ya uchaguzi mkuu Mama yangu Mama Naomi Kahihula aliekuwa ananifundisha CBE mpaka kabla ya Uchaguzi hawa wamekuwa wanawake wa juu CDM wamewapita hata wale waliokuwepo tangu mwiaka ya mwanzoni mwa 2000. Siri mnaijua wewe na mwenyekiti wako ila ukweli ni kwamba wewe mwenyewe hukuwajibika kikamilifu kitaaluma na kitaalamu Vipi wanafunzi uliokuwa ukiwahutubia wawajibike na sio kufuata nyayo zako?

Binafsi sifurahiwi sana na utendaji wako unaonyesha wewe ni mtu wa mizaha na usie na hoja nakumbuka ulitoa jibu kuwa
quote_icon.png
Originally Posted by Kitila Mkumbo
Tatizo la huyu mama yetu alikariri kwamba yeye lazima ilikuwa awe mbunge wa viti maalumu kwa sababu tu alikuwa mwenyekiti wa BAWACHA kitaifa. Bahati mbaya kwake ni kwamba hatukuwa na kigezo specific cha kumlenga mwenyekiti wa bawacha au kiongozi yeyote mwingine. Katika vigezo tulivyotumia yeye aliangukia kwenye namba 29 kama inavyoonekana katika orodha hapa chini ya first 40 candidates.

Katika safari hii ya mapambano sio abiria wote watakaofika mwisho wa safari; wapo watakaoshukia njia-huyu ni mojawapo!!

Hukutupa data ya jinsi ulivyo wa rank hawa wanawake wa juu kwani kwa kuzingatia haki Mama Musori alikuwa Mwenyekiti wa baraza la wanawake Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema na Mweka Hazina wa Umoja wa Madiwani wa Chadema na kukidhi vigezo vilivyowekwa pia Musori alikuwa anajua Kiingezera, Kijerumani na Kiswahili akiwa na Cheti cha Nurse Midwife (Diploma) aliyoipata Ujerumani pia amekuwa akiitumikia CDM kwa muda na kina Rose Kamili wamemkuta!

Sote tunajua mbunge akimaliza muda anapata kiinua mgongo cha asilimia 40 ya mshahara wake kwa mazingira uliyowateua itakuwa ni vigumu kuamini hakukuwa na rushwa na upendeleo hatujui ulipata/utapata nini kama ahsante ya uteuzi wako uliotukuka. Kwa uchache kina Rose Kamili wataondoka na kitu kama 45 mil baada ya kumaliza term yao ya ubunge ni dhahiri umewatafutia short cut ya nguvu na kwa hili nakupa hongera sana.

Kumalizia napenda kukufahamisha umewasaidia short cut kina Rose Kamili, Naomi Kaihula, Chiku Abwao ya maisha ungewaacha waweke vipaumbele kwenye kufanya kazi kwa bidii ya kukuza chama, maarifa na kukipenda chama chao. Hakuna short cut ya mafanikio kwenye chama zaidi ya kuwajibika na kuchapa kazi kwa bidii na upendo wa dhati kwa chama na kwa wananchi.

Dokta napenda uelewe kuwa
"You can fool some of the people all of the time, and all of the people some of the time, but you cannot fool all of the people all the time." – Abraham Lincoln

Natilia shaka lengo lako. Kama ni mwanachama wa CDM tafadhali rejea taraibu za chama. Kama ni wa CCM haikuhusu na nadhani ingekua vyema ukajadiri taratibu za chama chenu hapa tuzilinganishe zinaweza kuwa bora. Ila sisi "wengine" tunaamini Dr. Mkumbo alifanya kazi kitaalamu.
 
Sokomarazote huwa natofautiana na wewe ila kwenye hili tuko pamoja mkuu
15. Joyce Mukya alijiunga na cdm june 2010 hata kusimama jukwaani kujieleza mpaka sasa ni utata wananchji wa arusha hamjui huyu ni mkazi wa tangibovu mbezi jiji dar arusha alikuwa na hawarayake EAComunity akaishi kama miezi mitatu akarudi dar

Kitila ulichemsha na kama lema anasema kuwa anaamini kwenye haki mbona hili hakuliongelea au kwa kuwa ndiye aliyemkuwadia kwa Mbowe?
 
Mimi nadhani hoja hapa sio kwamba posho ni ndogo au kubwa. Hoja ni je ni halali wabunge kulipwa posho ya kuingia ofisini kwao ambako ni bungeni na kulipwa posho kwa " kukaa" ofisini kwao? Ni sawa sawa na Meneja na Wakurugenzi wa Kampuni kwenda kwenye Management Meeting na kutaka walipwe posho wakati mikutano kama hiyo iko katika Hadidu za Rejea ( Terms of Service) za ajira yao. Nini kazi ya wabunge kama sio kukaa bungeni na kufanya tulichowatuma na kupokea ujira. Kwa nini Posho?
 
Namjua siku nyingi sana Dr Kitila Mkumbo, na nilikuwa namuweka kwenye kundi la watu makini lakini niliposoma kwa makini maelezo ya SOKOMOKO, na nikiangalia ule mchakato wa kuwapata wabunge wa viti maalum kweli Dr Kitila Mkumbo dhambi ya dhulma itakutafuna mpaka mwisho umekwenda kujaza Wachagga na wanawake wa kiongozi na wana ndungu, kina mama makini wote mmewatosa
 
Natilia shaka lengo lako. Kama ni mwanachama wa CDM tafadhali rejea taraibu za chama. Kama ni wa CCM haikuhusu na nadhani ingekua vyema ukajadiri taratibu za chama chenu hapa tuzilinganishe zinaweza kuwa bora. Ila sisi "wengine" tunaamini Dr. Mkumbo alifanya kazi kitaalamu.

Sokomarazote huwa natofautiana na wewe ila kwenye hili tuko pamoja mkuu
15. Joyce Mukya alijiunga na cdm june 2010 hata kusimama jukwaani kujieleza mpaka sasa ni utata wananchji wa arusha hamjui huyu ni mkazi wa tangibovu mbezi jiji dar arusha alikuwa na hawarayake EAComunity akaishi kama miezi mitatu akarudi dar

Kitila ulichemsha na kama lema anasema kuwa anaamini kwenye haki mbona hili hakuliongelea au kwa kuwa ndiye aliyemkuwadia kwa Mbowe?

Mkuu mimibaba Hata yeye anasisitiza watu wafanye kazi kitaalam au ndio yale ya fuata mafundisho yangu usifuate matendo yangu? hili la Joyce Mukya alitumia utaalam gani kama alivyotueleza mkuu carefree? Ifike wakati tujue mission and vision ya kila chama ifike mahali tusishabikie vyama tuangalie watu wenye utashi wa kukataa kila ovu kwa vitendo na anae walk on his/her words! ndio maana nina amini kupitia mgombea binafsi ambae anawajibika moja kwa moja kwa wapiga kura wake sio kupitia vyama. Maelekezo ya mchague huyu na yule awe viti maalum ni ubakaji wa demokrasia kwenye chama cha kidemokrasia tena na maendeleo! mbaya zaidi anaefanya hivyo ni mwaume what do you smell hapo? Tunaposisitiza maadili kwa wanafunzi wetu na sie tujiamgalie maadili yetu!
 
Maumivu ya kichwa huanza poole pole!

If symptom persist seek medical advise.
 
Back
Top Bottom