DODOMA:Mivutano Urais vs Uwaziri Mkuu

Kolimba Jr

Member
Nov 24, 2014
83
68
Kamati ya bunge PAC sasa imeingia doa baada ya baadhi ya wajumbe wake kutuhumiwa kupokea kitita kizito cha pesa kutoka kwa vigogo wa Urais, imefahamika. Kikao cha KOKAS ya CCM kinachoendelea baada ya kufanyika pia Jana usiku kimeendelea kubainisha mambo mengi yaliyojificha.

1.Lukuvi aambiwa na Hawa Ghasia atavalishwa gauni:
Waziri Hawa amemtuhumu Lukuvi kuita wabunge kadhaa na kufanya nao kikao ili wamsaaidie kumshambulia Pinda ili yeye apate nafasi ya uwaziri mkuu. Akiwapa ahadi ya kuwakumbuka

2.Wassira aumbuliwa
Waziri wa Uratibu Steven Wassira nae ameshambuliwa kudaiwa kuchochea njama za kuangusha serikali nae akipigania uwaziri mkuu

3.Vigogo wasaka Urais
Wabunge wamepaza sauti kuwa kama tatizo ni nia ya Urais, basi kila mmoja ana haki ya kutangaza nia. Mtu asihukumiwe kwa nia yake. Waliotajwa wawajibike lakini waziri mkuu Pinda hatajwi na ripoti yoyote. SENDEKA alisimama akisema kwa nguvu kuwa watauana lakini Pinda haondoki.

4.January Makamba amlaumu waziri mkuu
January Makamba anasema japo Pinda hahusiki lakini serikali imechelewa kuchukua hatua. Ndio mana tumefika hapa

5.Kibajaji-Pinda hahusiki
Mbunge wa Mtera Lusinde Amekaririwa akisema Pinda ndiye aliyeagiza uchunguzi ufanyike, asingeamua bila ya kufanya uchunguzi. Huwezi kukamua jipu kama halijaiva.

Kikao kimeendelea mchana huu huku kina Zitto, Filikunjombe na Luhaga Mpina wakituhumiwa kuhongwa na mgombea urais kutoka kaskazini na kusini ambao wanapambana kuona Pinda anaanguka.
 
Kolimba Jr kwa ID status yako kama hivi;
Join Date : 24th November 2014
Posts : 19
Rep Power : 304
Likes Received10
Likes Given0



Nashawishika kusema kuwa na wewe ni staili ya buku saba, umetumwa kuvuruga jamvi...
 
Last edited by a moderator:
kwanini tunatumia kuhisi na mategemeo zaidi bila kuangalia mfumo wa uongozi wa nchi ni wa kulindana kichama zaidi?
 
Acha ujinga kwahili Wassira yuko kimya sana na hawezi kujijasibisha na upuuzi kama huo. Hofu imewajaa kwanini.
 
Leo kila mtu atasema lake lakini ukweli utabaki pale pale, mwenyezi Mungu wasaidie waja wako hasa Kamati ya PAC, na awalinde wote wanaotoa maamuzi yawe ya sahihi bila kumuonea yoyote wala kumwaga damu Ameen.🙏
 
Back
Top Bottom