Dodoma: Dawa ya Wabunge wa CCM wakosoaji yapatikana

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Niko hapa Dodoma tangu mwanzoni mwa juma hili. Nashuhudia mtifuano usio na mfano wa Wabunge wakiuliza maswali, wakichangia hoja na kadhalika. Nawashuhudia Wabunge ndani na nje ya Bunge hapa Dodoma.

Kumejitokeza Wabunge wa CCM wanaojichora kama wakosoaji wa utendaji wa Serikali ya Rais John Pombe Magufuli. Wabunge hao wamejichora kwa kauli, michango na hoja zao. Wabunge hao wanahatarisha kupitishwa kwa Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari.

Dawa ya Wabunge hao imepatikana. Ndani ya CCM hakishindikani kitu. Maelekezo yametolewa kwa viongozi wa Wabunge wa CCM kuwasilisha majina na 'hoja-korofishi' za Wabunge hao ili wajadiliwe na 'kuonywa' kichama. Kuna mkutano maalum wa Wabunge wa chama (party caucus) utaitishwa kwa ajili yao.

Pamoja na hayo mambo ya kichama na udhibiti wake, naliona Bunge likirudi katika kuisimamia Serikali. Linarudi kwenye mstari!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 
Kuanzia sakata la Richmond ...ni wabunge wa CCM ndio waliokuwa mstari wa mbele kuikosoa serikali.

Sijui kiherehere cha wapinzani kinatokea wapi?
 
Mbunge gani wa CCM ameongelea mgao wa 10M? Mbunge gani wa CCM ameshawahi kuongelea ununuzi wa boat ya Bagamoyo? Mjadala wa Lugumi umeishia wapi? Mmetupatia Katiba mpya wabunge wa CCM?
Kuna kashfa yoyote iliyoibuliwa bungeni na kufanikiwa kuwaangusha vigogo wa serikali ambayo haikuongozwa na wabunge wa CCM?
 
Great thinkers asked this similar question when Major opposition party, Chadema under the chairmanship of Mbowe welcomed and cherish the accused father of grand corrupter...

The famous Richmond dady was born again under the name of Mabadiliko.

Mbowe used to deny that,the so called fisadi could never be the member of Chadema...OVER MY DEAD BODY ...

All over sudden it is the same Chairman who justified the Shift of story about fisadi....

It was the same Chairman who turn to be a ' stone face' against his general secretary Dr Slaa .

It is now the same chairman who is asking a childish question about 10 million Takrima.

HOW CREDIBLE IS MBOWE AND HIS FOLLOWERS??....GOD ALONE KNOWS.
 
Kuanzia sakata la Richmond ...ni wabunge wa CCM ndio waliokuwa mstari wa mbele kuikosoa serikali.

Sijui kiherehere cha wapinzani kinatokea wapi?

So, hutaki upinzani..? mbona mm CCM na nawasikiliza..? kwnn CCM wenzangu hampendi challenge au kujifunza KUSIKIA MSIYOYAPENDA..? Mnataka kuwa single minded tu, why..? Kwani hujui dunia ya leo wapinzani wako kihalali na ni dunia nzima ktk nchi za democrasia..!!

We CCM, lazima tujifunze kusikia tusiyoyapenda na kuyatafakari, sio yote ni ya uongo toka upinzani, na nikiri, wapinzani wana hoja nzuri sana tu kushinda wabunge wengi mno wa CCM.. hili liko wazi kabisa.
 
ccm inajitahidi kutengeneza mazezeta...
eti hata unapoona pombe useme ni chai..
hakuna dawa useme kuna dawa..
kimefeli useme kimefaulu..
duh !!
umuhimu wa elimu ndani ya ccm ni upi ?
ndio maana siku wanapojaribu kujenga hoja huchekesha umma !
 
So, hutaki upinzani..? mbona mm CCM na nawasikiliza..? kwnn CCM wenzangu hampendi challenge au kujifunza KUSIKIA MSIYOYAPENDA..? Mnataka kuwa single minded tu, why..? Kwani hujui dunia ya leo wapinzani wako kihalali na ni dunia nzima ktk nchi za democrasia..!!

We CCM, lazima tujifunze kusikia tusiyoyapenda na kuyatafakari, sio yote ni ya uongo toka upinzani, na nikiri, wapinzani wana hoja nzuri sana tu kushinda wabunge wengi mno wa CCM.. hili liko wazi kabisa.
Tofautisha upinzani na saccoss mkuu!
 
Sasa kumbe hamtuongozi wananch Bali mnajioongoza wenyewe yani MTU akitoa mkakati mzuri usio na unafiki anaonywa due hii Kali .
 
Back
Top Bottom