Dodoma - Chuo cha Mtakatifu John chafungwa

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John mkoani hapa, umekifunga chuo hicho na kutaka wanafunzi kuondoka chuoni hapo baada ya kutokea vurugu zinazohusiana na madai ya fedha za kujikimu kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu wa Juu (HESLB). Kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano wa Chuo hicho, Karimu Meshack, uongozi umeamua kufunga chuo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza hadi wale wa mwaka wa nne kwa wanafunzi wa Shahada ya Kwanza wakati wale wa Shahada ya Uzamili wataendelea kubaki chuoni.

Chuo hicho kimefungwa hadi Januari 2, mwakani. “Chuo kimetoa amri kwa wanafunzi wote kuondoka chuoni hadi leo (jana) saa 12 jioni na mwanafunzi yeyote hatakiwi kuonekana chuoni,” alisema Meshack. Alisema wanafunzi hao wamepewa masharti ikiwemo kulipa madeni yote wanayodaiwa na chuo na kutakiwa kuja na risiti siku ya kufungua chuo, pia wanafunzi watasaini hati za makubaliano kati ya mwanafunzi na chuo. Pia alisema kwa wanafunzi ambao wataonekana kuwa ndiyo chanzo cha vurugu hizo, hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao na watatangazwa baadaye baada ya kikao cha uongozi
wa chuo.

Kwa upande wake, Katibu wa Serikali ya Wanachuo, Isdory Msuva alisema sababu kubwa za kufungwa kwa chuo ni wanafunzi kuendelea kudai fedha ambazo waliambiwa wasubiri. Msuva alisema licha ya kumaliza kusaini vocha za malipo tangu jana asubuhi, walikuwa wakiimba nyimbo za kutaka kupewa fedha zao. Alisema fedha hizo tayari ziliingizwa Benki M kutoka Bodi ya Mikopo kwa ajili ya kufanya gawiwo lakini benki hiyo ilikuwa bado kutekeleza jambo hilo. “Tunaona lilikuwa tatizo la kibenki na si tatizo la chuo, lakini wanafunzi walikuwa wagumu kuelewa,” alisema Katibu wa Serikali ya Wanafunzi. Hata hivyo, Polisi kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa na magari matatu walipiga
kambi chuoni hapo tangu jana asubuhi ili kuimarisha usalama chuoni hapo.

Chanzo cha vurugu zilizopelekea kufungwa kwa chuo hicho ni baada ya kubandikwa notisi iliyowataka wanafunzi kusaini na kutakiwa kusubiri hadi fedha zitakapowasili chuoni hapo. Kwa mujibu wa notisi hiyo iliyotolewa Desemba 19, mwaka huu, chuo kilisema hakijapokea fedha za robo ya pili ya fedha za kujikimu zilizotolewa na Bodi, lakini Bodi ya Mikopo ilisema itajitahidi kuharakisha fedha hizo.

Habari Leo
 
Vijana wasifanye mchezo na vyuo vinavyomilikiwa na madhehebu ya dini. Masharti ya vyuo vya dini ni maadili mema, kufanya migomo ni kinyume na malengo ya malezi ya kumjenga mwanafuzi. Kinachotendeka katika vyoo vya serikali visiigwe na vyuo vya dini, kwani vyuo vya dini viko tayari kubaki na darala la wanafunzi watano waadilifu kuliko kundi lenye kuleta mtafaruku chuoni.
 
haya hadi watakatifu nao wanagoma ukiona hivyo mwisho umefika unajua tumezoea kusikia vyuo vya umma kama udom,udsm na leo st john hii inaonesha ni jinsi gani hii nchi inakwenda pabaya,ki ukweli awa vijana wanaishi katika mazingira magumu ya kifedha
 
Vijana wasifanye mchezo na vyuo vinavyomilikiwa na madhehebu ya dini. Masharti ya vyuo vya dini ni maadili mema, kufanya migomo ni kinyume na malengo ya malezi ya kumjenga mwanafuzi. Kinachotendeka katika vyoo vya serikali visiigwe na vyuo vya dini, kwani vyuo vya dini viko tayari kubaki na darala la wanafunzi watano waadilifu kuliko kundi lenye kuleta mtafaruku chuoni.


Maadili gani mbona hatuoni maadili yao kwenye taaluma wanazotoa kwa wanachuo wao zaidi ya uchachuaji wa shahada
 
Back
Top Bottom