Dkt. Tulia anaenda kuliua Bunge kama atachaguliwa kuwa Spika

econonist

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
15,948
22,014
Kwa maoni yangu kwa kauli ya jana ya Naibu Speaker Dr Tulia Ackson, ni kweli kama atachaguliwa kuwa speaker wa bunge bunge litakufa na kubaki kuwa kitengo cha ikulu.

Kwanza, anadai Rais ana nguvu Sana. Ina maana hajui kuwa bunge lipo pale kwaajili ya kuangalia na kumchunga Rais asitumie nguvu zake vibaya. Ndio maana katiba imeipa bunge nguvu ya kumuondoa Rais madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani naye.

Pili, anatoa ahadi mbele ya Rais na mawaziri yani serikali ya kwamba Bunge litaikosoa serikali kwa nidhamu. Swali Nani atapima na kujua huu ni ukosoaji wa nidhamu na huu sio ukosoaji wa nidhamu? Ukosoaji wa nidhamu kwa maana ni ukosoaji wa hofu au wenye uoga ndani yake. Mbona bunge huko nyuma limewahi kukosoa serikali hadi kupelekea waziri mkuu kujiuzulu? Je, huo ulikuwa Nini zaidi ya ukosoaji wenye nidhamu? Je, serikali ikifanya ufisadi wa kutisha bunge litaikosoa serikali kwa nidhamu au kistarabu?

Tatu, anadai sio lazima serikali ifuate ushauri wa bunge. Tatizo Ni kwamba Dr Tulia amekariri ya kwamba serikali ni Rais pekee. Amesahau serikali Ina vyombo vingi ndani yake. Hivi kwa mfano bunge likashauri Wizara au taasisi ya serikali Kama PCCB kuhusu mapungufu na jinsi ya kufanya ili iondoe mapungufu yake Ina maana kwa kauli ya Tulia hiyo Wizara au taasisi Ina hiyari ya kukataa au kukubali ushauri wa bunge. Kama hali ni hivyo bunge lina kazi gani au lina nguvu gani? Hata likitoa ushauri kwenye mikopo au bajeti serikali inaweza kusikiliza au kuacha.

Hivyo basi Ili bunge lirudishe nguvu yake iligopotea inahitaji speaker atakayejua nguvu na kazi za bunge kikatiba na atakayetambua bunge ni chombo kinachowapa a wananchi katika maamuzi na sio chombo au kitengo cha ikulu. Kama wananchi hawataki serikali ikope bunge lifikishe hayo maoni na sio vinginevyo.
 
Lini bunge lilikuwa kitengo cha wananchi?

Huyo ndugai mwenyewe alikuwa anaitumikia CCM ndo maana akaambiwa aandike barua apeleke kwa katibu mkuu wa ccm.
Kama spika wa bunge anatokea CCM unadhani atafanya tofauti na inavyotaka CCM?
 
Huenda tuendako mihimili yote mitatu ya Tanzania itaongozwa na kina mama na wanaume kuwa wasaidizi

Serikali - Mheshimiwa Raisi Samia S.H; Bunge Mheshimiwa Tulia A. na Mahakama .. Jaji .......
 
Mama ni mwanaharakati anataka asifiwe na wazungu kwa kutekeleza 50/50 hivyo Tulia atapewa naona.
 
Hilo bunge zaidi ya 90% wako huko bungeni kwa uchaguzi haramu ikiwemo huyo Tulia mwenyewe. Usitegemee mtu aliye bungeni kwa uchaguzi haramu awe na guts za kukosoa bila hofu. Hayo ndio madhara ya kuwa na bunge lililopo kwa amri ya rais na sio kura za wananchi.
 
Ni kweli ameonyesha atakuwa spika wa namna gani. Dawa ni wabunge kutomchagua. Spika anatakiwa kuwa msimamizi wa muhimili huru siyo representative wa serikali bungeni.
 
Bunge likishapoteza ubora wake tangu mzee Samuel Sita alipo liwacha mikononi mwa Makinda.
 
Lini bunge lilikuwa kitengo Cha wananchi?
Huyo ndugai mwenyewe alikuwa anaitumikia CCM ndo maana akaambiwa aandike barua apeleke kwa katibu mkuu wa ccm.
Kama spika wa bunge anatokea CCM unadhani atafanya tofauti na inavyotaka CCM?
Nakubaliana na wewe ndugu mzareeendo
 
Yeye mwenyewe aliletwa na Magu kugombea U-naibu Speaker unategemea nn mpaka hapo.
 
Back
Top Bottom