Dkt. Tulia anaenda kuliua Bunge kama atachaguliwa kuwa Spika

Matatizo ya hii nchi, yanaletwa na CCM lile sio bunge ni ukumbi wa kugawiana posho wana CCM
 
Tulia bado ajaiva kuwa speaker angalau ZUNGU kidogo anaweza vaa viatu
 
Nilichokiona kuna viongozi wanaangalia kesho yao,lakini hawana uchungu na selikari.Magu kilichomuharibia kuwatesa wapinza,lakini hii awamu tunayoenda nayo aibu,Rais Mwenyewe hana vision kabisa,siku fulani akifa,ndiyo tutaujua ukweli
 
Anajielewa. Mkiweza mchagueni spika wa CHADEMA ambaye anaamini;
  • -kuisimamia serikali ni kuitukana, kuidhalilisha na kuiamrisha!
  • -Ili spika uonekane huko huru basi ongoza kwa kupinga kila kitu cha serikali kama CHADEMA na wengine wanavyofanya
  • -Rais siyo mkuu wa nchi, bali ni kiongozi wa serikali kama ambavyo spika ni kiongozi wa bunge hivyo wako sawa kwa kila kitu. Nchi iwe na mafahali 3 wenye nguvu sawa! Hata elimu ndogo ya utawala hamuijui!
  • -Haiwezekani mihimili kufanya kazi kwa kuheshimiana navkutanguliza maslahi ya umma
 
Kwa maoni yangu kwa kauli ya Jana ya Naibu Speaker Dr Tulia Ackson, ni kweli kama atachaguliwa kuwa speaker wa bunge bunge litakufa na kubaki kuwa kitengo cha ikulu.

Kwanza, anadai Rais ana nguvu Sana. Ina maana hajui kuwa bunge lipo pale kwaajili ya kuangalia na kumchunga Rais asitumie nguvu zake vibaya. Ndio maana katiba imeipa bunge nguvu ya kumuondoa Rais madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani naye.

Pili, anatoa ahadi mbele ya Rais na mawaziri yani serikali ya kwamba Bunge litaikosoa serikali kwa nidhamu. Swali Nani atapima na kujua huu Ni ukosoaji wa nidhamu na huu sio ukosoaji wa nidhamu? Ukosoaji wa nidhamu kwa maana ni ukosoaji wa hofu au wenye uoga ndani yake. Mbona bunge huko nyuma limewahi kukosoa serikali hadi kupelekea waziri mkuu kujiuzulu? Je, huo ulikuwa Nini zaidi ya ukosoaji wenye nidhamu? Je, serikali ikifanya ufisadi wa kutisha bunge litaikosoa serikali kwa nidhamu au kistarabu?

Tatu, anadai sio lazima serikali ifuate ushauri wa bunge. Tatizo Ni kwamba Dr Tulia amekariri ya kwamba serikali ni Rais pekee. Amesahau serikali Ina vyombo vingi ndani yake. Hivi kwa mfano bunge likashauri Wizara au taasisi ya serikali Kama PCCB kuhusu mapungufu na jinsi ya kufanya ili iondoe mapungufu yake Ina maana kwa kauli ya Tulia hiyo Wizara au taasisi Ina hiyari ya kukataa au kukubali ushauri wa bunge. Kama hali ni hivyo bunge lina kazi gani au lina nguvu gani? Hata likitoa ushauri kwenye mikopo au bajeti serikali inaweza kusikiliza au kuacha.

Hivyo basi Ili bunge lirudishe nguvu yake iligopotea inahitaji speaker atakayejua nguvu na kazi za bunge kikatiba na atakayetambua bunge ni chombo kinachowapa a wananchi katika maamuzi na sio chombo au kitengo cha ikulu. Kama wananchi hawataki serikali ikope bunge lifikishe hayo maoni na sio vinginevyo.
Kale kadada kanapenda kujipendekeza sana. Eti hawa ndio wategemewe kuongoza nchi hii kweli!!!
 
Tanzania hakuna bunge, hilo mbona ni halmashauri kuu ya ccm. Hatuna bunge wala hatuna mahakama, vyote ni vitengo vya serikali ya ccm na inazitumia katika kufanikisha utawala wake uliopo bila ridhaa ya wananchi.
 
Back
Top Bottom