Dkt. Ruja, mwanamama aliyewatapeli watu pesa yenye ukubwa wa nusu ya bajeti ya Tanzania na kupotea kwenye uso wa Dunia

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,155
31,082
Miaka saba liyopita, Dr Ruja alikuwa akifanya kazi kama mshauri katika shirika moja la kimataifa linahusiana na mambo ya kifedha. Akiwa hapo, ndipo aliposikia habari za bitcoin, pesa mpya ya kimtandao ambayo ilikuwa imeanza kukua kwa kasi ya ajabu ikiwa huru bila kuhodhiwa na benki kuu. Bei ya bitcoin ilipoanza kupanda, Dr Ruja aligundua kuna fursa ya kutengeneza pesa. Lakini kwa upande wake aliamua kutowekeza kwenye bitcoin bali naye aliamua kutengeneza pesa yake iliyojulikana kama OneCoin. Kwa madai yake alidai kwamba pesa hiyo ilikuwa rahisi kuitumia, ina ulinzi wa kutosha kuliko BitCoin. Alidai ya wkamba haihitaji mtu awe mtaalam sana wa kompyuta ili aweze kununua OneCoin. Uachotakiwa ni kutuma pesa kwenye akaunti maalum ya benki kisha utapokea kiasi kinachoendana cha OneCoin kwenye akaunti yako ya mtandaoni. Alidai OneCoin imetengenezwa wka ajili ya kutumiwa na watu wote.

OneCoin ilianza kukua kwa kasi sana. Dr Ruja alionekana sehemu kadhaa duniani akiwahutubia watu kwenye makongamano huko London, Macau, Dubai na Singapore. Wawekezaji wakubwa walikuwa wakionyeshwa picha zake akiwa kwenye kurasa za mbele za majarida makubwa kama The Financial Times. Video yake akiwa anahutubia kongamano la kibiashara la wanauchumi ilisambazwa huko Facebook. Watu dunia nzima walikuwa wakituma ela kwenye akaunti ya benki aliyotoa na kufungua akaunti zao za OneCoin. Hata vijiji vidogo huko Uganda vilihimiza wakazi wake waungane kununue coins za OneCoin.

Matajiri kutoka Marekani walikuwa wakituma maelfu ya dola kununua OneCoin. Kufikia mwaka 2017 OneCoin ilikuwa imefika katika nchi 175 na inakadiriwa kuwa ilikuwa ishakusanya kiasi cha Euro billion 4 (Zaidi ya tilion 13 za kitanzania. Yani karibu nusu ya bajeti yetu yam waka 2020-2021). Kuna madai kuwa ilikuwa imekusanya Euro billion 12.7.

Kama ambavyo Dr Ruja alivyotabiri, bei ya OneCoin ilianza kupanda kwa kasi, kuto 43p mwanzoni mwa mwaka 2015 mpaka Euro 10 mwaka 2017. Alitabiri kuwa itafikia Euro 100 siyo muda mrefu na kupanda Zaidi. Aliwahidi wawekezaji wake kuwa siyo muda mrefu watakuwa na uwezo wa kuuza coins zao na hivyo kuweza kutengeneza faida kubwa sana.

Lakini kadri siku zilivyokwenda hakuna aliyeweza kuuza coins zake kila mara aliibuka na sababu ya kuzuia hilo. Mara tatizo la mfumo wa OneCoin mara uwepo wa tatizo wa kisheria ili mradi tu sababu. Watu wakaanza kuwa na mashaka. MWezi wa kumi mwaka 2017, Dr Ruja alikuwa amepanga kuhutubia wawekezaji wakubwa wa OneCoin huko Ulaya na mkutano huo ulikuwa unafanyika Lisbon. Katika mkutano huo ilikuwa awambie ni lini watakuwa tayari kuuza coins zao na kutoa pesa yao. Dr Ruja alikuwa mtu wa kujali muda na hakuwahi kuchelewa, lakini siku hiyo hakutokea jambo lilianza kuwatia wasiwasi wawekezaji. Majaribio ya kumpigia simu na kumtumia meseji hayakuzaa matunda. Watu wakaaanza kuwa na mashakalabda katekwa.

Dr Ruja hakutokea na hakuna ambaye aliwahi kumuona toka siku hiyo. Ukweli ni kwamba hakukuwa na pesa ya kimtandao bali ulikuwa ni utapeli wa kizamani ambao unajulikana kama pyramid scam. Bei ya OneCoin na thamani yake ilikuwa inaamuliwa tu kutokea ofisini kwake huko Sofia, Bulgaria. Hakukuwa na mfumo wowote wa OneCoin. Mwaka 2019, Marekani ilimfungulia mashitaka Dr Ruja ya utakatishaji wa pesa na utapeli. Pia kaka yake ambaye alichukua majukumu ya Dr Ruja alipopotea naye alikamatwa akiwa uwanja wa kimataifa wa Los Angeles. Alikubari baadhi ya mashitaka ili apunguziwe adhabu. Wawekezaji walikuwa wanadhani wameshikilia OneCoins zenye thamani ya mamilioni ya dola ila ukweli hawakuwa na kitu.

Nini kilimpata Dr Ruja?

Wengine wanahisi yupo kajichimbia sehemu anakula maisha.

Ila mimi ninafikiri kuwa utapeli huu hakuufanya peke yake, huenda kulikuwa na watu wakubwa nyuma yake na walimuua ili kupoteza ushaidi na ela wakaitafuna.
ruja.jpg
 
View attachment 1478736
Kwa urembo huu ilikuwa haki awalize.
 
dunia bila wajinga sio dunia
HIOOO IKOKILA SEHEMU
USISIKIEEE KABISAA AUMENIKUMBUSHA ILE MZIGOOO WAUPATU ULIOHIFADHIWA PALE BOT ACHAKABISA

NIKOWEKA LAKI NAZIONA LAK LADHA NKKFAFIKA MIL TATU....

WALIKUFA WENGISANA NA HUU MCHEZO..... SIKUNATAKA NKAWEKE MIL TATU NZIMA NKALETEWA TWODAYS EMAIL NATAKIWA KUSAFIRI ALL DOCS ZIWE SAWA.. DOH NKASEMA NIKIRUDI NTAKUA NA SOME DOLLERS NAWEKA MILS TANO.....

BOSS WANGU MMOJA ASHAWEKA MIL SABA ANASUBIRIA MIL KADHAA AKIRUDI
TUMEMALIZA SHULE DAH.. TUNATUA N\ONA NJE ANAPOKELEWA NA WANAWE WANALIA WAKAMTOA CHEMBA WAKAMNONGONEZA KITU.. GAFLA AKAJA BRIEFING AYUKOSAWA NAONA MAMA WAWATU ANATOAMACHOZI JAMAN KWA MLIOWEKA DESI MMESIKIA WAMELAMATWA NA HELA HAZIRUDI KAMWE NIMEWEKA MIL ZA WACHUNGAJI JAMAN NA ZANGU NTAONEKANAJE KANISAN KUMBE YALE MACHOZI NILIJUA ANALIA HELA ZAKE KAWAINGIXA CHAKA KUANZIA PAST MKUU NA VIONGOZI KADHAA MCHEZO ANAWAMBIAAJE.. SIJAJUA KAMA BOT WALIKUBALI KURUDISHA ZILE SADAKA JAMAN ZA WACHUNGAJI..DAH....
SHIKAMOOOOOOOOO DESIIIII
 
Watu tunapenda sana kukimbilia kila fursa bila tahadhari. Kwa mafno, watu waliojiunga na DECI watakumbuka walibyotapeliwa. Vile vile, PRIDE ilikuwa ya umma lakini wajanja wakaibadili na kuwa binafsi, wengi mtakumbuka namna waliokuwa nakopa PRIDE na kushindwa kurejesha mkopo walivyokuwa wananyang'anywa hadi samani za nyumbani kama vile vile sofa, meza, vitanda, nk. Ni majanga juu ya majanga!
 
Back
Top Bottom