“Dkt. Anna Peter Makakala kuendelea kuwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji ni kubariki uhujumu uchumi”

Apr 24, 2011
29
542
Jumapili, 12/2/2017 Rais wa Tanzania wakati huo Dkt. John Magufuli alisema sababu ya kuteua mwanamke katika nafasi ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, kuwa wanawake wengi ni waaminifu katika suala la fedha.

Moja kati ya maagizo makubwa wakati anateuliwa Dkt. Anna Peter Makakala lilikuwa ni kudhibiti utoaji hati za kusafiria (Passports) na katika suala la fedha akaagizwa akasimamie matumizi vizuri na kwa uaminifu.

Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2020/2021 inaeleza kwamba kuna mtandao wa maafisa 32 wa uhamiaji wameghushi hati za kusafiria feki na wakapiga Shs. 2.42 bilioni

Taarifa hiyo ya ukaguzi inafafanua kwamba wageni wa kigeni 21,208 walipewa stika za kughushi, Mtandao wa maafisa hao wakafuta taarifa (ushahidi) katika mfumo wa utoaji stika hizo. Hao Maofisa bado wapo kazini.

Ufisadi huu wa Shs. 2.42 bilioni umefanyika ndani ya siku 180) kkatika uwanja wa ndege wa KIA kuanzia 1/1/2019 hadi 30/6/2019 kwa mtandao wa maofisa hao wa uhamiaji kucheza na mfumo wa maombi ya viza (VAS)

Taarifa ya stika 21,208 za viza za wageni waliowasili nchini kupitia KIA zilifutwa katika kanzidata za VAS ambazo zilihusu wageni waliowasili nchini Tanzania lakini maofisa hao 32 wakawapa stika za kughushi kujipatia Shs. 2.4bn

CAG anapendekeza kwamba idara ya uhamiaji ichukue hatua stahiki za kisheri na kinidhamu kwa Maofisa wake 32 wa KIA waliohusika kusababisha hasara ya Shs. 2.4bn kwa Serikali. Binafsi sidhani kama wanapaswa kuishia hapo tu.

Agosti 2, 2019 Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa Ya Jinai (DCI) alibaini kuwepo stika za viza za kughushi katika uwanja wa KIA na JNIA na zinauzwa na Maofisa wa uhamiaji kama njugu katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA)

Ukaguzi ulibaini wageni 33,558 waliwasili Tanzania kupitia KIA ingawa taarifa zao ikiwa ni pamoja na ERV (fomu za kuingia nchini) na hakuna taarifa za uwekaji fedha benki. Hivyo CAG hakujua ni kiasi gani Serikali ilipaswa kupata.

Kwa mantiki hiyo, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji CGI Dkt. Anna Makakala anatakiwa kutoka hadharani atueleze, Shs. 2.42bn zilizotafunwa na Maofisa wake, amechukua hatua gani. Pia awajibike kwa ufisadi huu. Siyo vinginevyo.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, CGI Dkt. Anna Makakala ajitokeze hadharani mbele ya umma, atueleze pesa za umma, Shs. 2.42 bilioni zipo wapi na zimepotea vipi akiwa mkuu wa uhamiaji. Ni wazi hatoshi kuendelea kuwa ofisini.

Kamishina Jenerali wa Uhamiaji CGI Dkt. Anna Makakala ameshindwa kumudu majukumu yake ya kazi, hivyo aondolewe Ofisini na ikiwezekana, kwa utaratibu wa tuhuma za jinai achunguzwe kwa tuhuma za ‘organized crimes’ na huo mtandao.

Walipa kodi wa nchi hii tunapata maswali mengi sana ambayo majibu yake ni rahisi, Kama Kamishina Jenerali wa Uhamiaji anaweza kunyamaza kimya kwa ufisadi wa Shs. 2.42bn hadi CAG aseme kwa umma, kwanini bado yupo ofisini?

Sasa raia wa kawaida tu, Adv. Peter Madeleka anasimama kuongelea hilo la taarifa ya CAG, wanatishia kumuua na anakamatwa kinyamela, siku ya pili sasa hawasemi kama wapo naye na wanakanusha kwamba wao hawamshikilii..

Mambo ya ajabu sana yanafanyika katika ardhi yetu na lazima tuyakemee kwa sauti kubwa.. Muacheni Adv. Peter Madeleka aendelee na shughuli zake au mfikisheni mahakamani kama ana hatia siyo kukaa naye mafichoni.. Nchi yetu sote hii. Muacheni huru.

#MMM, Martin Maranja Masese
 
Hii ndio nchi inalinda wala rushwa kwa kutumia policeccm,yani mtu anasema anaushahidi wao wanamteka...makala ni police kwahiyo uwizi huo anauzoefu nao na macho kodo atamlinda kwa nguvu zote,msoga team wamerudi kumaliza kuiba pale alipoishia jpm kuiba
 
Hakuna wa kuchukuliwa hatua hapo.huyo wa kumuajibisha huyo makakala mwenyewe ni sehemu ya huo uozo.
Sasa ukimuwajibisha Anna akimuuliza muwajibishaji kuhusu wale wabunge 19 waliofurushwa chadema wanafanya nini bungeni atajibu nini? Akimuuliza kuhusu kura za kwenye mabegi atajibu nini? TATIZO LA NCHI HII SIO ANNA WALA UHAMIAHI. Tatizo ni ccm na sasa tufunge mwezi mtukufu huku tunawakumbuka tembo wetu maana jangili mkuu amerejea kwa kura za kishindo 1850( 100%)
 
Hii ndio nchi inalinda wala rushwa kwa kutumia policeccm,yani mtu anasema anaushahidi wao wanamteka...makala ni police kwahiyo uwizi huo anauzoefu nao na macho kodo atamlinda kwa nguvu zote,msoga team wamerudi kumaliza kuiba pale alipoishia jpm kuiba
huyu kateuliwa na magufuli na huo wizi unaotajwa pia umetokea wakati magufuli akiwa rais tuwache fitna tuwe wakweli.
 
Kwa viwango vya Upigaji ktk report ya CAG, 2B unaona kabisa hawa sio walafi...kuna watu wamegonga ma billioni ya kutosha mpaka haka ka 2B kanaonekana ni kapesa kiduchu...
 
Wakati wa uongozi wa Magufuli, inaonekana kila idara ilijaa wizi wa hali ya juu. Ina maana Magufuli hakujua? Au alijua lakini waliokuwa wanaiba, kwa namna namna fulani, walikuwa na baraka zake?

Hata kwenye uharamia wa Sabaya na Makonda, habari zilizopo ni kuwa Magufuli aliambiwa na Waziri Mkuu jinsi Sabaya na Makonda walivyokuwa wanawapora watu pesa kwa nguvu, lakini akanyamaza kimya, hata Waziri Mkuu asijue ni kwa nini!
 
Jumapili, 12/2/2017 Rais wa Tanzania wakati huo Dkt. John Magufuli alisema sababu ya kuteua mwanamke katika nafasi ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, kuwa wanawake wengi ni waaminifu katika suala la fedha.

Moja kati ya maagizo makubwa wakati anateuliwa Dkt. Anna Peter Makakala lilikuwa ni kudhibiti utoaji hati za kusafiria (Passports) na katika suala la fedha akaagizwa akasimamie matumizi vizuri na kwa uaminifu.

Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2020/2021 inaeleza kwamba kuna mtandao wa maafisa 32 wa uhamiaji wameghushi hati za kusafiria feki na wakapiga Shs. 2.42 bilioni

Taarifa hiyo ya ukaguzi inafafanua kwamba wageni wa kigeni 21,208 walipewa stika za kughushi, Mtandao wa maafisa hao wakafuta taarifa (ushahidi) katika mfumo wa utoaji stika hizo. Hao Maofisa bado wapo kazini.

Ufisadi huu wa Shs. 2.42 bilioni umefanyika ndani ya siku 180) kkatika uwanja wa ndege wa KIA kuanzia 1/1/2019 hadi 30/6/2019 kwa mtandao wa maofisa hao wa uhamiaji kucheza na mfumo wa maombi ya viza (VAS)

Taarifa ya stika 21,208 za viza za wageni waliowasili nchini kupitia KIA zilifutwa katika kanzidata za VAS ambazo zilihusu wageni waliowasili nchini Tanzania lakini maofisa hao 32 wakawapa stika za kughushi kujipatia Shs. 2.4bn

CAG anapendekeza kwamba idara ya uhamiaji ichukue hatua stahiki za kisheri na kinidhamu kwa Maofisa wake 32 wa KIA waliohusika kusababisha hasara ya Shs. 2.4bn kwa Serikali. Binafsi sidhani kama wanapaswa kuishia hapo tu.

Agosti 2, 2019 Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa Ya Jinai (DCI) alibaini kuwepo stika za viza za kughushi katika uwanja wa KIA na JNIA na zinauzwa na Maofisa wa uhamiaji kama njugu katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA)

Ukaguzi ulibaini wageni 33,558 waliwasili Tanzania kupitia KIA ingawa taarifa zao ikiwa ni pamoja na ERV (fomu za kuingia nchini) na hakuna taarifa za uwekaji fedha benki. Hivyo CAG hakujua ni kiasi gani Serikali ilipaswa kupata.

Kwa mantiki hiyo, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji CGI Dkt. Anna Makakala anatakiwa kutoka hadharani atueleze, Shs. 2.42bn zilizotafunwa na Maofisa wake, amechukua hatua gani. Pia awajibike kwa ufisadi huu. Siyo vinginevyo.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, CGI Dkt. Anna Makakala ajitokeze hadharani mbele ya umma, atueleze pesa za umma, Shs. 2.42 bilioni zipo wapi na zimepotea vipi akiwa mkuu wa uhamiaji. Ni wazi hatoshi kuendelea kuwa ofisini.

Kamishina Jenerali wa Uhamiaji CGI Dkt. Anna Makakala ameshindwa kumudu majukumu yake ya kazi, hivyo aondolewe Ofisini na ikiwezekana, kwa utaratibu wa tuhuma za jinai achunguzwe kwa tuhuma za ‘organized crimes’ na huo mtandao.

Walipa kodi wa nchi hii tunapata maswali mengi sana ambayo majibu yake ni rahisi, Kama Kamishina Jenerali wa Uhamiaji anaweza kunyamaza kimya kwa ufisadi wa Shs. 2.42bn hadi CAG aseme kwa umma, kwanini bado yupo ofisini?

Sasa raia wa kawaida tu, Adv. Peter Madeleka anasimama kuongelea hilo la taarifa ya CAG, wanatishia kumuua na anakamatwa kinyamela, siku ya pili sasa hawasemi kama wapo naye na wanakanusha kwamba wao hawamshikilii..

Mambo ya ajabu sana yanafanyika katika ardhi yetu na lazima tuyakemee kwa sauti kubwa.. Muacheni Adv. Peter Madeleka aendelee na shughuli zake au mfikisheni mahakamani kama ana hatia siyo kukaa naye mafichoni.. Nchi yetu sote hii. Muacheni huru.

#MMM, Martin Maranja Masese
Bora angekuwepo Mwendazake mtu anayechezea sharubu zake kiasi hiki asingeachwa angerumbuliwa na kunangwa hadharani
 
Wakati wa uongozi wa Magufuli, inaonekana kila idara ilijaa wizi wa hali ya juu. Ina maana Magufuli hakujua? Au alijua lakini waliokuwa wanaiba, kwa namna namna fulani, walikuwa na baraka zake?

Habari zilizopo ni kuwa Magufuli aliambiwa na Waziri Mkuu jinsi Sabaya na Makonda walivyokuwa wanawapora watu pesa kwa nguvu, lakini akanyamaza kimya, hata Waziri Mkuu asijue ni kwa nini!
Kwani Magufuli alikuwa haoni ile Range na Lexus za Bashite? Kwani hakusikia kuwa Bashite kamzawadia mkewe brand new BMW kwenye birthday? Kwani alikuwa hajui maujenzi ya apartment za kifahari Mwanza? Magufuli alikuwa mwoga sana wa upinzani tangu jimboni mwake,kwa hiyo mtu yeyote aliyekuwa anaweza kuteka,kutesa na kuuwa mpinzani alikuwa anapara credit kubwa sana kwa jiwe. Na Ni Mungu tu na kelele za umma zliepusha Bashite kupora ubunge Kigamboni Leo hii tungekuwa tunaongea mengine( Bashite angekuwa waziri kamili Wala sio naibu) NA WALA MAGUFULI ASINGETOKA MADARAKANI KAWA MSEVENI NA KAMA KAGAME. Huu ndo ukweli mchungu. Wote humu turejee uchaguzi wa serikali za mtaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020 hizo chaguzi mbili ndizo zilikuwa zinatoa dira ya muelekeo wa siasa za nchi. Ndo maana leo hii nchi inahangaika na vikosi kazi vya maridhiano na uponyaji wa maumivu. Na aliyeasisi biashara ya uchuuzi wa wapinzani kwa slogan ya kuunga juhudi ni Mnyeti na Bashite huku pia Bashite kapiga pesa mingi saaaanaaa,badae hii biashara ikarasimishwa pale lumumba chini ya kiroboto(pole pole). NARUDIA TENA NA KAMPENI YA MAGUFULI AENDELEE KUTAWALA ILI ETI AMALIZIE MIRADI YAKE WAS REAL MDA HUU NDO INGEKUWA IMESHIKA KASI. Asante Mungu kwa 17/3/2021
 
Mkubwa Martin nathamini mchango wako wa mawazo lakini Kwa hoja hizi ulizoandika hapa Naomba kutofautiana na Wewe kutokana na ukweli kwamba ulichokiandika hapa na ukweli ulioripotiwa kqenye vyombo vya habari ni tofauti kabisa.
Kwanza, Naomba nikueleze kwamba waliokamata visa feki nakutangaza adharani walikuwa uhamiaji kupitia taarifa Kwa vyombo vya habari tarehe 06/08/2019 rejea jamiiforum facebook akaunti na vyombo vingine vya habari kwa tarehe hiyo. Nimeandika hoja hii humu tufuatilie kuonyesha JPM alipopata hii habari alichukua hatua mara Moja akishirikiana na Makakala na Nadhani taarifa Zipo wapo mitandaoni ambapo Takukuru ilihusika lakini Kwa kukosekana ueledi na kwakuwa walitumia nguvu kuliko akili Jamhuri ilishindwa kesi baada yakubainika wahusiaka wa visa feki waliachiwa nakukukamatwa maafisa ambao Kwa ukweli kwenye Lile sakata awakuhusika.

Pili, Madeleka alikuwa na kesi ya kughushi vibali vya uhamiaji na alikamatwa yeye na mke wake. Hapa nataka ieleweke kwamba Madeleka na mke wake ambaye alikuwa afisa Uhamiaji wote ni Mawakili na Wana ofisi hapa Arusha; kilichomkost Madeleka ni yeye kumiliki kesi zote za Uhamiaji kama wakili ambapo Mke alikuwa anatetea upande wa Jamhuri akiwa mwendesha mashtaka wa Idara hiyo Kwa mkoa wa Arusha na Mme akiwa wakili wa utetezi. Hapa Naamini kulikuwa na conflict of interest na mara kadhaa Kati ya mwaka 2013 Hadi 2019 kesi hizi za Uhamiaji zililalamikiwa na Mawakili wengi Kwa zote ziliendeshwa kifamilia. Mawakili wengi walillalamikia kitendo hiki lakini wapi. Nadhani Martin unaweza kuverify taarifa hizi kupitia vyanzo vyako. Ugomvi wa Madeleka na system Hadi kupelekwa ndani ni yeye kuhudumia walioitwa mabeberu Kwa kuwasaidia wapate vibali kama wakili wa kampuni na Mzee alipoanza kufuatilia wizi wa wageni hapo kule Arusha wale wageni wote wakakimbia nchi huku nyaraka zao zikikutwa kwenye familia ya wakili mwenzetu Madeleka. Watu wengi walihojiwa Kuhusu sakata lake na hapa niseme Takukuru wanahisika kuifanya kazi hii.

Tatu, Kuhusu kuchepusha malipo KIA napingana na CAG report Kwa sababu serikali iliwakamata maafisa ikawafikisha mahakamani na TAKUKURU waliitisha mkutano na waandishi wa habari. Mimi nilikuwa kwenye jopo na watuhumiwa wale walikamatwa kipindi kimoja na Madeleka na baadaye wote walikwenda ndani Kwa uhujumu uchumi. Kilichobainika siyo wizi ni kwamba wageni wale elfu 22+ hawakulipa visa kwenye entry point Kwa sababu mfumo uliwaruhusu kulipa visa wakiwa kwenye mataifa Yao. CAG kama zilivyo taasisi nyingi za dola nadhani wanaelewa ukweli. Tulisimama imara na watuhumiwa wetu tukawakataza kubagain na DPP Kwa Sababu wote kwa pamoja hakuna aliyepatikana na ushahidi hata wa visa Moja. Takukuru walichunguza wakabaini Fedha zote zililipwa serikalini kupitia online services ambazo serikali yenyewe iliruhusu. Niwakumbushe pia kwamba uzinduzi wa Online visa kwenye mtandao unaonekana ulifanywa na Waziri Mkuu, hivyo wateja wetu walituhumiwa kwa makosa yasiyokuwepo. Serikali inaponyanyasa watu wake sisi watetezi wa hali tunapaswa kupiga kelele siyo kuungana na watu wachache kuwatesa wasio na hatia.

Nikuombe Tena Martin ufuatilie hukumu ya kesi ya visa ilishatoka ambapo maamuzi yaliyotolewa ni kuachiwa huru washtakiwa baada ya DPP kueleza mahakama Hana kusudio la kuendelea na kesi Ile. Leo CAG anazungumza hatua Gani zaidi ya hizo? Kwamba walioachiwa huru wakamatwe upya ?

Nimesema nasikitika na upotoshaji huu Kwa sababu madeleka knows each and everything na tulifight naye kwenye matatizo haya Leo yeye kama msomi alipaswa kueleza namna polisi na TAKUKURU walivyomuumiza Mmoja wa watuhumiwa aliyekuwa na Mtoto mchanga wakamtia ndani huku wakijua fika alikuwa na muda mfupi Toka ahamishiwe KIA, Madeleka alipaswa kueleza namna polisi na takukuru walivyokosa ueledi kwenye kesi ya KIA Kwa kumkamata mtumishi ambaye alihamishiwa KIA hata kazi ajaanza wakamuita muhujumi uchumi Mzee wa Watu akaenda ndani bila hata kuhojiwa. Alipaswa kueleza wazi kwamba ripoti ya CAG inapotoshwa kwamba hatua zichukuliwa wakati kesi imefunguliwa na kufutwa yeye akiwa anajua. Tukiruhusu Mawakili kama Madeleka waendelee kupotosha umma tutakuwa hakuna tunachowasaidia.

Mwisho nikueleze tu kwamba lengo kuu la Madeleka popote utakapomkuta ni kuona Dr. Makakala anaondolewa Uhamiaji. Siwezi kupingana naye lakini anapotumia nguvu nyingi anaweza kudhani anapambana na Makakala kumbe anawaumiza watumishi wale wale alioteseka naye gerezani yeye akabagain wenzake wakafutiwa mashtaka.

Tecknologia haikuwahi kudanganya; Martin fanya research disprove hoja zangu.
 
Back
Top Bottom