Martin Maranja Masese
Member
- Apr 24, 2011
- 29
- 544
Jumapili, 12/2/2017 Rais wa Tanzania wakati huo Dkt. John Magufuli alisema sababu ya kuteua mwanamke katika nafasi ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, kuwa wanawake wengi ni waaminifu katika suala la fedha.
Moja kati ya maagizo makubwa wakati anateuliwa Dkt. Anna Peter Makakala lilikuwa ni kudhibiti utoaji hati za kusafiria (Passports) na katika suala la fedha akaagizwa akasimamie matumizi vizuri na kwa uaminifu.
Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2020/2021 inaeleza kwamba kuna mtandao wa maafisa 32 wa uhamiaji wameghushi hati za kusafiria feki na wakapiga Shs. 2.42 bilioni
Taarifa hiyo ya ukaguzi inafafanua kwamba wageni wa kigeni 21,208 walipewa stika za kughushi, Mtandao wa maafisa hao wakafuta taarifa (ushahidi) katika mfumo wa utoaji stika hizo. Hao Maofisa bado wapo kazini.
Ufisadi huu wa Shs. 2.42 bilioni umefanyika ndani ya siku 180) kkatika uwanja wa ndege wa KIA kuanzia 1/1/2019 hadi 30/6/2019 kwa mtandao wa maofisa hao wa uhamiaji kucheza na mfumo wa maombi ya viza (VAS)
Taarifa ya stika 21,208 za viza za wageni waliowasili nchini kupitia KIA zilifutwa katika kanzidata za VAS ambazo zilihusu wageni waliowasili nchini Tanzania lakini maofisa hao 32 wakawapa stika za kughushi kujipatia Shs. 2.4bn
CAG anapendekeza kwamba idara ya uhamiaji ichukue hatua stahiki za kisheri na kinidhamu kwa Maofisa wake 32 wa KIA waliohusika kusababisha hasara ya Shs. 2.4bn kwa Serikali. Binafsi sidhani kama wanapaswa kuishia hapo tu.
Agosti 2, 2019 Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa Ya Jinai (DCI) alibaini kuwepo stika za viza za kughushi katika uwanja wa KIA na JNIA na zinauzwa na Maofisa wa uhamiaji kama njugu katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA)
Ukaguzi ulibaini wageni 33,558 waliwasili Tanzania kupitia KIA ingawa taarifa zao ikiwa ni pamoja na ERV (fomu za kuingia nchini) na hakuna taarifa za uwekaji fedha benki. Hivyo CAG hakujua ni kiasi gani Serikali ilipaswa kupata.
Kwa mantiki hiyo, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji CGI Dkt. Anna Makakala anatakiwa kutoka hadharani atueleze, Shs. 2.42bn zilizotafunwa na Maofisa wake, amechukua hatua gani. Pia awajibike kwa ufisadi huu. Siyo vinginevyo.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, CGI Dkt. Anna Makakala ajitokeze hadharani mbele ya umma, atueleze pesa za umma, Shs. 2.42 bilioni zipo wapi na zimepotea vipi akiwa mkuu wa uhamiaji. Ni wazi hatoshi kuendelea kuwa ofisini.
Kamishina Jenerali wa Uhamiaji CGI Dkt. Anna Makakala ameshindwa kumudu majukumu yake ya kazi, hivyo aondolewe Ofisini na ikiwezekana, kwa utaratibu wa tuhuma za jinai achunguzwe kwa tuhuma za ‘organized crimes’ na huo mtandao.
Walipa kodi wa nchi hii tunapata maswali mengi sana ambayo majibu yake ni rahisi, Kama Kamishina Jenerali wa Uhamiaji anaweza kunyamaza kimya kwa ufisadi wa Shs. 2.42bn hadi CAG aseme kwa umma, kwanini bado yupo ofisini?
Sasa raia wa kawaida tu, Adv. Peter Madeleka anasimama kuongelea hilo la taarifa ya CAG, wanatishia kumuua na anakamatwa kinyamela, siku ya pili sasa hawasemi kama wapo naye na wanakanusha kwamba wao hawamshikilii..
Mambo ya ajabu sana yanafanyika katika ardhi yetu na lazima tuyakemee kwa sauti kubwa.. Muacheni Adv. Peter Madeleka aendelee na shughuli zake au mfikisheni mahakamani kama ana hatia siyo kukaa naye mafichoni.. Nchi yetu sote hii. Muacheni huru.
#MMM, Martin Maranja Masese