jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 19,177
- 36,079
Mwanao wa kike akipata mimba utampeleka mfumo upi..?
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mambo ambayo lazima kama jamii yenye upekee wake tuyasimamie hata kwamba tunatofautiana kiitikadi.
Moja ya jambo hili ni mimba kwa wanafunzi. Siafiki mwanafunzi apate Ujauzito kurudi katika mfumo rasmi wa elimu kama wenzake ambao hawajapata.
Hapa tutahalalisha umama, baba na hata ushemeji katika shule/darasa na ile dhana ya uanafunzi kufa kifo cha kawaida.
Kila kitu kinautaratibu wake. Tutambue pia kuwa shule ni ni chombo ambacho jamii inawatengeneza wanajamii wa baadae katika kuiendeleza jamii husika kwa siku za usoni. Na kwamba, ni unapokuwa shuleni basi uzingatie ile miiko ambayo jamii imeona haipaswi kuvunja na watoto wake ndio maana wakapelekwa shule.
Sasa kama huyu aliyepelekwa shule ameona hawezi kufata misingi hiyo ya jamii ya nini kumuendeleza katika jambo ambalo hakulizingatia?
Shule zibaki kuwa shule na taratibu, sheria, utamaduni na majuzi zake zisimamiwe. Ikiwa ikatokea mwanafunzi akapata Ujauzito basi, apelekwe katika mfumo mbadala usio rasmi na ule aliokengeuka ili shule na malengo ya shule katika jamii yabaki kama ambavyo jamii inapenda iwe.
Sio kila atakalo mfadhili ni jambo jema ktk mfadhiliwa.
Sent using Jamii Forums mobile app