DC Mwegelo akabidhi Baiskeli 200 kwa Watoto wa Kike shule 10 Korogwe

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

MHE. JOKATE MWEGELO AKABIDHI BAISKELI 200 KWA WATOTO WA KIKE SHULE 10 KOROGWE

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo amekabidhi baiskeli 200 kwa Wanafunzi wa kike kwa Shule 10 za Sekondari Wilayani humo ambapo amesema zitawasaidia Vijana wa kike kufika Shuleni kwa wakati na kuondokana na utoro kwa kutokufika Shule mara kwa mara kutokana na umbali mrefu wanaotembea kutoka majumbani mwao hadi kufika Shuleni.

Akiongea wakati wa hafla maalum ya makabidhiano ya baiskeli hizo ambazo zimetolewa na Shirika la Uratibu na Ushirikano la Uturuki (TIKA) chini ya Ubalozi wa Uturuki Nchini Tanzania, DC Jokate amesema “Sisi tunawashukuru sana Mh. Balozi wa Uturuki kwa kuunga mkono juhudi za Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha mazingira ya elimu kwa Mtoto wa kike, kwakweli mmepanda mbegu ambayo inaishi kwa Watoto wetu na hii mmetoa hamasa kwao kuweza kusoma kwa bidii zaidi”

"Na ndio maana nimesisitiza hawa Watoto huko Shuleni wakazane na masomo watumie baiskeli hizi kwenda Shule na kurudi nyumbani kuwasaidia Wazazi wao na sio kuzitumia kwenye matumizi yasiyo sahihi”

Kwa upande wake Balozi wa Uturuki hapa Nchini Dr. Mehmet Gulluoglu amesema lengo la kukabidhi baiskeli hizo ni kuwasaidia Watoto kutokutembea umbali mrefu kufuata elimu na hivyo baiskeli hizo zitawasaidia kufika Shule kwa wakati na kufanya vizuri kwenye masomo yao”


FuiyE1xXoAEgOXL.jpg
FuiyE1xWwAEIqOT.jpg
Fud8SOPWAAA9SAv.jpg
 
Iwapo gharama ya kila baiskeli ni shilingi 120,000 mara idadi ya Baiskeli 200 ina fanya jumla ya shilingi 24,000,000. Yaani milioni 24.

Watanzania wangekuwa na roho ya kutoa, kiasi hicho kilikuwa kinaweza kukusanywa kupitia makundi rafiki ya WhatsApp kwa Wanafunzi waliowahi kusoma shule hiyo then wakanunua wao hizo Baiskeli na kutolewa kwa wadogo zao.

Misaada mingine inatudhalilisha na kutweza utu wetu Watanzania.
 
Back
Top Bottom