Dk Stephen Ulimboka Jembe na Nguzo ya MADAKTARI Nchini

Kwa waliopitia jeshini, kujificha ni moja ya mbinu za medani vitani. inakupa nafasi ya kujibu mashambulizi
 
Nilimwona jana kwenye taarifa ya habari ya ITV akitoa ufafanuzi kuhusu mgomo wao.
Jamaa alikuwa mtaratibu, makini, anatoa maelezo unayohitaji. Kikubwa cha tofauti, sikuona zile jazba ambazo vinara wengi wa migomo na maandamano huwa wanazo, including my Mbowe (Mb.),
kitu ambacho kilionesha kuwa huyu jamaa anajua anachokifanya, anafahamu mipaka yake, merits walizonazo na kadhalika.
Kwa jinsi jamaa anavyoonekana yuko makini, inaonekana hata mtoto wa mkulima na ujumbe wake walishindwa kumrubuni kama walivyofanya kwa Mgaya na TUCTA, ndio maana wakaja na blah blah kuwa siyo daktari, mara alishapokönywa leseni, ooh, alishaahidi kuwa hataongoza tena mgomo...
Sasa kama mtu sio dakitari anafanyani Muhimbili mpaka wa leo.
I love Dr. Stephen Ulimboka (MD)....
 
Kujitokeza hadharani maana yake nini? Si lazima iwe physically. Inatosha kama anaweza kuwasiliana na watu wake kama kiongozi. Kujificha kimwili si alama ya uoga au udhaifu, bali ni moja ya njia za mapambano. Kwa sababu kama akijitokeza na akakamatwa anaweza asiweze tena kama kamanda mkuu kuwasiliana na watu wake kwa vile watamnyima uhuru wa kufanya hivo. Kumbe ni sahihi kuwasiliana akiwa mafichoni.
Una akili sana wewe, unatisha! Nashangaa watu wengine sijui kwa nini hawalioni hili...
 
If anything happens to Dr, Ulimboka, PM Pinda will have to answer before his mother and father, all doctors in Tanzania, all Tanzanians and tomorrow before God the almighty!
 
Natetea ukweli na haki ilipo. Wewe unaona walichofanya hawa ni sawa kumwacha kwenye mataa Waziri Mkuu?

Amma kweli.

Wee FF sababu alishazito kuwa barua ya kutaka kukutana na waziri ilitumwa jana saa kumi na moja jioni na kwa sharti ikifika saa moja tiari awe ameshatuma majibuna hata hivyo barua aliijibu ila ilichelewa kufika ila ilifika, na mtoa mada hapa kuwa anajificha sio kweli mbona mlimani tv kulikua na mahojiano na madoctor na yeye alikuwepo pia mada ilikua jinsi mgomo ulivyokua na hatma yake pia wachangiaji wengi walipiga simu kusuport waendelee na mgomo na umma upo nyuma yao na still conclution ya madoctor ni kuwa mgomo unaendelea mpaka serikali itekeleze majukumu yanapaswa kutekeleza

Mfano:
kwenye mkataba ya ajira inasema watapewa 30% ikiwa ni posho au allowance ya nyumba mpaka dakika hii ni maandishi tuu awaipati na hii wanasema sio ombi ila kwenye mkataba wa ajira ipo hivyo kwanini awapewi? FF jibu kwanini na ni madai ya msingi na si ombwe jipya la kutaka posho.

Jingine ni mtu akiwa night shift analipwa elfu kumi tuu tokea mwaka 2004 je hiyo elfu kumi na kupanda kwa garama ya maisha itafanya nini wee FF? na mengine mengi kama mgebahatika kusikiliza mlimani tv ndio mgejua ukwelizaidi

Haya madai wanayo dai ni yale yapo kwenye mikataba na hayatekelezwi so, mkataba unaompa ni wa nini?

Kwa mara nyingine tena wewe FF, Rejao, ritz, raia mwema nk. nyie aidha ni UWT tena ni wale mlio kwenye panel ya mauaji na mnachangia kuwapotosha viongozi kwa propaganda za uongo sasa mlimdanya pinda jana je mmefaulu malengo yenu?

madaktari wanachokidai kipo kwenye mkataba wa ajira na sio nje ya mkataba wana JF uelewe ili kwanza.
 
we mngese nini?? ulikua na haja ya kuanzisha thread nyingine???

au ndio walewale mnaotumwa kuvictimise watu??
 
Inasikitisha sana na hizi kauli za hawa UWT eti mtu kajificha kweli unaweza kujificha hapa TZ? au ndio mkeshafeli hizo strategies zenu ndio mnakimbilia kashfa za kijinga aliyekuambia kuwa kajificha nani?
 
Mleta mada kapotosha, huu mkutano haukufanyika jana, wala juzi, huu ulifanyika kabla na Waziri Mkuu akaridhia kukutana nao Karimjee, lakini kwa kiburi hususan cha huyu mshawishiwa mmoja wakagoma kuonanan na Waziri Mkuu.

Suala hapa limebadilishwa, kwanza ilikuwa kurudishwa interns kwenye vituo vyao, limekubaliwa, kupatiwa nyumba limekubaliwa, kuongezwa malipo limekubaliwa, sasa hawa wana agenda zingine na si hayo madai yao, Kilichowafanya wakatae kuonana na Waziri Mkuu ni nini na wamgandishe Karimjee akiwangoja, hivi wanajianya wao ndio Munu na wenye kuwapa watu roho? Fnga tena kila kifo kinachosabishwa nao wahukumiwe kisheria. Kwani hawana faida yoote kwa wananchi wa Tanzania, wakumbuke kuwa wanasomeshwa kwa kodi zetu. Wasitulee kiburi chao.

Hawa wafanyiwe kama walivyofanyiwa wale wa UDSM, fukuza wote, wacha tupigane nao vikumbo mitaani. Serikali ilete madaktari kutoka kokote duniani kwa gharama zozote zile lakini hawa isiwarudishe kabisa.
 
Mleta mada kapotosha, huu mkutano haukufanyika jana, wala juzi, huu ulifanyika kabla na Waziri Mkuu akaridhia kukutana nao Karimjee, lakini kwa kiburi hususan cha huyu mshawishiwa mmoja wakagoma kuonanan na Waziri Mkuu.

Suala hapa limebadilishwa, kwanza ilikuwa kurudishwa interns kwenye vituo vyao, limekubaliwa, kupatiwa nyumba limekubaliwa, kuongezwa malipo limekubaliwa, sasa hawa wana agenda zingine na si hayo madai yao, Kilichowafanya wakatae kuonana na Waziri Mkuu ni nini na wamgandishe Karimjee akiwangoja, hivi wanajianya wao ndio Munu na wenye kuwapa watu roho? Fnga tena kila kifo kinachosabishwa nao wahukumiwe kisheria. Kwani hawana faida yoote kwa wananchi wa Tanzania, wakumbuke kuwa wanasomeshwa kwa kodi zetu. Wasitulee kiburi chao.

Hawa wafanyiwe kama walivyofanyiwa wale wa UDSM, fukuza wote, wacha tupigane nao vikumbo mitaani. Serikali ilete madaktari kutoka kokote duniani kwa gharama zozote zile lakini hawa isiwarudishe kabisa.

FF umezungumza upupu mwingi.
Ila nimenote kitu kimoja kulingana na uchangiaji wako,
ulishazungumzia nyumbani kwa wazazi wako, Kariakoo Lumumba St,
umeshawahi kumzungumzia mumeo, ambaye ni mwindaji,
lakini hujawahi kuzungumza kuhusu watoto wako wa kuwazaa,
is that what makes you angry, mpenzi?
 
Hakuna upande wowote unaofaidika na huu mgomo; si serikali si Madaktari wala sisi tunaochangia hapa. Sidhani ktk Nchi yenye demokrasia ndani ya 50 yrs ya uhuru ishindikane kupata muafaka, hata ifikie kupoteza uhai wa wenzetu. Kwa ambaye hajaathirika na huu mgomo ni raisi sana kuchochea na kusema uendelee na tuko nyuma yao.Hapa tunachezea uhai wa watu wasio na hatia. Mungu ashuke na afanye kazi yake.
 
Wewe jana ilikuwa siku ya kuabudu,na sio kuonana na manyang'au yasiomjua Mungu.

Acha unafiki wakutane naye wa nini ikiwa kama kila madai tyao yako kwa maandishi???? Huku kutafutana sababu tu. Think outside the box meeeeen.

Mara siku ya kuabudu (kwani Jumapili huwa hospitali zinafungwa)? Mara madai yao yapo kwenye maandishi: Hivi maana ya majadiliano ni nini? Kwa hiyo wao ni maandishi tu hawataki kukutana na upande wa pili uso kwa macho? Mara tunawasubiri wenzetu toka mikoani, looooooh nini ni nini sasa? Mwisho sasa wanaamua kujificha. Toka shujaaa pigania unachokiamini.

Kuna wakati Thomas Sankara aliambiwa kwamba Blaise Compaore ana mpango wa kukuua, akasema shujaa haogopi kuuawa. Hakukimbia wala kujificha.
 
Hii ni kweli kabisa wakiamua watawapukutisha wote,akija na Maralia unamdunga sindano ya omo yenye mchanganyiko na sumu,akafie mbele huko wanasiasa wao watakimbilia India

Sasa utakuwa umefanya nini? Adui yako ni mwanasiasa wewe unaenda kushambulia watu wengine wasio na hatia!
 
Tuone atakaa mafichoni mpaka lini? Ananchekesha!
wewe si ndiye unayewaunga mkono Boko haram wao wako mitaani au wamejichimbia mafichoni maduguri? Acheni ushabiki wa (...) Leo Ulimboka angefanya hivyo wakati Slaa ni Rais ungesema haya uliyoyasema?
 
Nchi inayumba yumba!kila kitu bei juu,hakuna huduma za hospitali!walimu nao wanakuja na mgomo wao kudai haki zao!uchaguzi ungekuwa mwaka huu,sijui ingekuwaje
 
Back
Top Bottom