Dk Stephen Ulimboka Jembe na Nguzo ya MADAKTARI Nchini

Sidhani kama amejificha,hao Channel 10 wamempataje na kuongea nae? Kama channel 10 wamempata serikali "yenye mkono mrefu" itashindwa? Hata hivo nayo ni mbinu ya mapambano tu! Unajificha unapanga mbinu zaidi za kukuwezesha kuendelea kupigana na hatimaye kushinda kuliko kusonga tu mbele ukakamatwa/uawa! Komaeni maDR!
 
Cha kushangaza ndio hicho, anaogopa nini kama kweli yupo kwenye haki?

Tukiwaambia hawa ni wachochezi, hamkubali.

Hivi wewe FF unafanyaje? katika dakika tatu unapost replies kwenye thread tofauti hata 6!

W#anakulipa ngapi? Au nawe umo kwenye hiyo 'gravy train' ambayo unailinda kwa nguvu zako zote na walalahoi potelea mbali?

Duh! wewe jasiri kweli kweli katika kuchinja!
 

Tangu lini serikali ya magamba inakuwa kwenye haki? wabunge posho juu sawa, madaktari mishahara juu hapana! sina muda wa kukutolea orodha ndefu ya ukiukwaji wa haki wa utawala wa magamba!


Msibadilishe yaliyopo, wamekataa kwenda kuonana na Pinda Karimjee, kwanini?
 
Na tukikukamata wewe kichwa yako halali yetu umetusababishia misiba na majonzi makubwa kwa ndugu zetu waliokufa kwa kukosa huduma kwasababu ya uroho wenu na ubinafsi!!
 
Ulimboka anakimbia kivuli chake kama wana Usalama wangemtaka wangemshughulikia mapema
 
Naunga mkono mgomo wa madaktari kwa 100% hadi pale watakapozikilizwa madai yao, kama ni ya msingi basi yatekelezwe kama sio ya msingi basi yatupiliwe mbali. Lakini hata hivyo naamini katika madai yao yote lazima yawepo japo kwa uchache ambayo ni genuine kwani sishawishiki kuamini kwamba hawa watalaam wanaweza kugoma tu bila kuwa na sababu yoyote ya msingi, kwani wote ni watu wazima, zadi ya miaka 18 lakini pia ni wasomi.
 
Ningefurahi sana Usalama wangemkamata Ulimboka na kumfungulia mashitaka ya kuua wagonjwa kwa makusudi
 
...Akiongea na Channel Ten,Mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari..Dr Ulimboka,ameongea kutoka mafichoni na kusema kuwa mgomo uko pale pale na utakuwa unashika kasi kwa mfumo tofauti tofauti..alipoulizwa kwanini hataki kujitokeza hadharani amesema amepata taarifa kuwa anatafutwa na usalama.Na amewaimiza madaktari kuendelea kugoma mpaka serikali itakapokuja kusikiliza madai yao.

source:Channel Ten.
Unamtania Mamba wakati upo mtoni. Huu ndio ujinga tunaousema kila siku. Ushauri wa bure kwa ulimboka na wajinga wenzake waliotusababishia vifo vya Watanzania wenzetu bila ya sababu za msingi, msipime maji kwa macho, mtaishia kunyea debe!
 
Naunga mkono mgomo wa madaktari kwa 100% hadi pale watakapozikilizwa madai yao, kama ni ya msingi basi yatekelezwe kama sio ya msingi basi yatupiliwe mbali. Lakini hata hivyo naamini katika madai yao yote lazima yawepo japo kwa uchache ambayo ni genuine kwani sishawishiki kuamini kwamba hawa watalaam wanaweza kugoma tu bila kuwa na sababu yoyote ya msingi, kwani wote ni watu wazima, zadi ya miaka 18 lakini pia ni wasomi.

bado siungi mkono mgomo wa madaktari dhidi ya wagonjwa
 
Unafikiri watanzania masikini tungejitolea kummuunga mkono angekuwa na haja ya kujificha?
Umasikini wetu unauhusiano gani na mgomo wa madakitari? Madakitari wanataka kuongezewa maslahi na kwa kuwa viongozi wetu hawapo tayari kupunguza maposho wanayojiliipa ni wazi kuwa wanachodai madakitari kinatakiwa kitoke kwa sisi haohao masikini. Mimi kwa hili nafikiri madakitari wanatakiwa waungwe mkono lakini hili lisihusishwe kabisa na suala la umasikini wa watanzania. kwani madakitari wakishinda kuishawishi serikali kuongoza posho au masilahi yao, hiyo inaweza kuwa ni furaha kwetu au kilio kwetu yote yanawezekana. itakuwa furahi ikiwa masilahi yao yatatokana na kupunguzwa kwa posho wanazojilipa vigogo kwa mambo yasiyo ya lazima na itakuwa ni huzuni ikiwa pesa hizo za kuboresha masilahi ya madaktari zitatakiwa zitoke kwa huyo mtanzania unayemwita masikini.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom