Dk. Slaa: Sigombei urais

Status
Not open for further replies.
Bungeni nako amekaa sana. Inavyoelekea hana mpango wa kumuandaa mrithi wake toka CHADEMA. Akikumbwa na lolote lile (Mwenyezi Mungu apishilie mbali) jimbo linarudi CCM.
 
Labda uwezo wake unaishia kwenye ubunge. Labda urais unaitaji uwe na kauzoefu kwenye uwaziri kwanza. Huyu atakuwa kabanwa na chama chake tu.
 
Jamani kwani wewe ulikuwa hujui siku zote hizi?mbona hajawahi kutamka popoter kwamba anataka kugombea Urais?
 
Ni maamuzi ya busara hayo Dr. Slaa big up ! maana urais hata iweje ccm wanashindwa na sasa wewe ungekosa uwakilishi. Cha muhimu sasa ni kujaza wapinzani through viti vya ubunge the baada ya hapo ndo urais. Na yule mgombea urais wa upinzani atakuwa ameshapatikana.
 
jamani si ikla mwalimu mzuri lazima awe mwalimu mkiuu!!.............. kama walimu7 wote wazuri watakuwa mabosi nani ataendelea kufundisha? na nafasi za mabosi zitatoka wapi nyingi iiasi cha kuwatosha wote walio na watakao kuwa wazuri???.............. tafakari..................

dr slaa kakomaa kisiasa.......................
 
What is the point yakugombea Urais wakati anajua kabisa JK anashinda.. It is equal to kugombea nothing. Opposition Tanzania inahitaji sana watu strong Bungeni, he is one of the less than a handful real MPs, ningesikitika sana angeenda gombea ujinga. I am not a supporter of CHADEMA, siridhiki na wigo wao, wanahitaji muda kujijenga wawe chama cha upinzani kiukweli in maybe 20 years we will see that. Lakini Slaa ameisaidia sana Tanzania kwa kuwaweka watawala on their toes, so we need him in the House. And hopefully the opposition can get more of this type of people, opposition iwe na ata viti 20% basi maana the current imbalance is wrong.
 
Nitarudia kusema kwamba Tanzania hakuna mtu ambaye ni mkweli na mwenye kujali maslahi ya nchi mbele ya chama ama yake binafsi..
Nilitegemea watu kama Dr.Slaa na Dr. Salim kusimama ktk mchaguzi huu lakini baada ya kusikia siasa nyingi zikipita nilijua kwamba hatuna watu isipokuwa kila mmoja wao anatazama kwanza maslahi yake,familia na ya chama..Hatuna kina Mandela na ajabu ni kwamba wanachukia wakiitwa Wapinzani maana kwao kila kitu kipo sawa tu, wana practice demokrasia ya vyamna vingi.

Someone has to step up kama kweli WAPO wanasiasa wanao-fahamu/pinga mwelekeo wa Taifa letu..kugombea Ubunge kwa mihula 3 au 4 hakuwezi badilisha dira ya taifa linalo angamia..
 
Nadhani Dr.Slaa hajawahi kutangaza kama atagombea.Pia sidhani kama mtu atasema tu wacha nigombea kwa kuwa watu wametoa maoni.Lazima apime na aone kama ni muafaka kwake kubeba jukumu hilo.Nadhani kama tuna hamu sana na mabadiliko basi tuyaanzie bungeni.Rais hatakua na nguvu ya kutuburuza kama opposition watakuwa na viti vingi bungeni

Hapo ndio itakuwa mwanzo wa kuingiza serikali iliyokaa kitaasisi.Hata kama Slaa atagombea urais akashinda huku CCM wakichukua viti vingi bungeni bado maslahi ya watanzania yatakuwa hatarani.
 
Nitarudia kusema kwamba Tanzania hakuna mtu ambaye ni mkweli na mwenye kujali maslahi ya nchi mbele ya chama ama yake binafsi..
Nilitegemea watu kama Dr.Slaa na Dr. Salim kusimama ktk mchaguzi huu lakini baada ya kusikia siasa nyingi zikipita nilijua kwamba hatuna watu isipokuwa kila mmoja wao anatazama kwanza maslahi yake,familia na ya chama..Hatuna kina Mandela na ajabu ni kwamba wanachukia wakiitwa Wapinzani maana kwao kila kitu kipo sawa tu, wana practice demokrasia ya vyamna vingi.

Someone has to step up kama kweli WAPO wanasiasa wanao-fahamu/pinga mwelekeo wa Taifa letu..kugombea Ubunge kwa mihula 3 au 4 hakuwezi badilisha dira ya taifa linalo angamia..

akigombea urais hapati kwa sasa hivi mkuu....bora awe mbunge tu
 
Labda kungekuwapo utaratibu kama wa Kenya kwamba mgombea urais anaruhusiwa kugombea pia ubunge ndani ya uchaguzi huo huo, ili ikitokea ameteleza kimoja apate kingine. Hii haitakitia hofu chama ya kupoteza kiti cha urais na ubunge kwa mgombea urais anayetokea bungeni.
 
Nitarudia kusema kwamba Tanzania hakuna mtu ambaye ni mkweli na mwenye kujali maslahi ya nchi mbele ya chama ama yake binafsi..
Nilitegemea watu kama Dr.Slaa na Dr. Salim kusimama ktk mchaguzi huu lakini baada ya kusikia siasa nyingi zikipita nilijua kwamba hatuna watu isipokuwa kila mmoja wao anatazama kwanza maslahi yake,familia na ya chama..Hatuna kina Mandela na ajabu ni kwamba wanachukia wakiitwa Wapinzani maana kwao kila kitu kipo sawa tu, wana practice demokrasia ya vyamna vingi.

Someone has to step up kama kweli WAPO wanasiasa wanao-fahamu/pinga mwelekeo wa Taifa letu..kugombea Ubunge kwa mihula 3 au 4 hakuwezi badilisha dira ya taifa linalo angamia..

Unafikiri kuwa Rais ndio kujali maslahi ya wananchi?au kuwa Mbunge ndio kutokujali hali za wananchi?
 
Unafikiri kuwa Rais ndio kujali maslahi ya wananchi?au kuwa Mbunge ndio kutokujali hali za wananchi?
Siku zote usiwe mwepesi kutafsiri maneno ya mtu ikiwa huelewi maana. Upumbavu ni pamoja nadhania mtu mwingine anafikiria nini ama alikuwa na maana gani.. kama hujui Uliza mkuu wangu sii dhambi wala haikufanyi wewe mjinga.
Huwezi kugombea Urais ikiwa hujali maslahi ya wananchi wako. hili sii swala la kufikiria hata kidogo ila kiongozi anaweza kuwahadaa wananchi kwamba anawajali kinyume cha imani yake..Sidhani kama Dr Slaa ni mtu wa aina hiyo na ndio sababu nilitegemea zaidi kugombea kjwake kuliko mtu mwingine yeyote.
Pili, Sikusema kuwa Ubunge ni kutojali hali ya wananchi isipokuwa niimani yangu kwamba mbunge hawezi badilisha kitu kwa kuzingatia hali halisi ya watu na mazingira ya uchaguzi huu. Tanzania ya leo inahitaji Mapinduzi na sii kugombea Ubunge ambao bado upo chini ya utawala wa katiba ya chama kimoja. Changes zinaanza kabla ya uchaguzi na kiti cha Urais ndicho kinalinda machungu yote.

Ikiwa mgombea yeyote anapinga muundo wa katiba iliyopo, lakini bado akagombea ubunge chini ya katiba ile ie anayoipinga kuwayanyasa wananchi, basi bila shaka Mgombea huyo kajiunga na utawala mbaya. Sidhani kama Mandela angekubali kujiunga na Uchaguzi mkuu wa South Afrika hata Ubunge chini ya Utawala wa Apartheid..Na kwa wale wote waliokubali kujiunga na kufanikiwa hutokea siku watakayo amua kumwondoa rais..Kenya ni mfano mdogo mzuri sana kwa awamu zote..Walijipanga kumwondoa Moi wakaweza kubadilisha katiba yao lakini majuzi tu kina Raila walipokubali ubunge wa majimbo na sii utawala wamejikuta ktk hali ngumu zaidi. wajaluo leo wapo ktk wakati mgumu kuliko wakati wowote na juhudi zao zimegota ukutani.
Sasa wewe nambie, huyo Dr. Slaa akirudi bungeni atawezesha kipi ikiwa CCM wataendelea kutawala. Hivi kweli unaamini kabisa kwamba CCM inaweza shindwa ktk uchaguzi ambao wao wenyewe ndio mahakimu? Unatumia kigezo kipi haswa..
Dr.Slaa bila shaka atashinda hili halina Ubishi lakini CCM nao wanabadilisha wagombea wake wengi sana kwa kutumia kura za maoni. wasiopendwa wataenguliwa mapema na kilichobakia ni mchele unaweza kuuzika! Kisha wanatumia wanawake zaidi kupata ushindi kwani wapiga kura wengi ni wanawake na unajua fika hii habari ya uuwiano ktk madaraka ni hadithi mpya. Tatizo la wanawake lipo ktk vyama vya upinzani, kama lilicyokuwa la udini mwaka 2005, hivyo tumepigwa tayari bao la kwanza..
Kwa njaa ya Mtanzania wagombea wengi wameisha anza kulisha sumu ya utajiri wao -Takrima. Na wenye uwezo mkubwa ni wagombea wa CCM..Matajiri wengi wako CCM na hakuna tajiri atakaye changia Chadema,Nccr wala CUF akaachwa na hasira za CCM..huu ndio ukweli na matajiri wote wanafahamu hilo, hivyo huo uwazi wa michango ni mtego mkubwa kwa wapinzani kwa hesabu Wabunge wengi CCM wapo kwa maslahi yao binafsi.. hili pia halina Ubishi.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom