Habarindiyohiyo
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 263
- 13
Dk. Slaa: Sitagombea urais
na Deogratius Temba
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilibrod Slaa, amesema hana mpango wa kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010.
Dk. Slaa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Karatu kwa mihula miwili mfululizo, alisema, jukumu alilonalo katika maisha yake ni kuwatumikia watu wa Karatu ambao wamemwamini na kumpa nafasi hiyo na si kugombea urais.
Akizungumza katika kituo cha Televisheni cha TBC1, katika kipindi cha Jambo Tanzania, Dk. Slaa alisema yeye ni mtumishi wa watu wa Karatu na hawezi kuwaacha kwenda kugombea urais.
Wananchi wangu waondoe wasiwasi, na wala wasijenge hisia kuwa nitasimama kuwania urais, wala sina wazo hilo, wala sijawahi kuota kuwa rais wa nchi hii, na sitakubali kuwasaliti wananchi wangu kwa kuacha kuwatumikia kama mbunge, alisema.
Akizungumzia kuhusu CHADEMA kusimamisha mgombe urais katika uchaguzi mkuu ujao, Dk. Slaa alisema lazima wamsimamishe mtu kwani chama hicho kinaaminiwa na kupendwa na wananchi.
Ni lazima CHADEMA tutamsimamisha mtu katika nafasi ya urais na kuendelea kupigania haki ya Watanzania mpaka mwisho, aliongeza Dk. Slaa.
Akizungumzia suala la kuungana kwa vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu ujao, Dk. Slaa alisema CHADEMA kitaungana na chama chochote chenye nia ya dhati ya kutaka kulikomboa taifa, na kilichojijengea sera yakinifu na imara zinazokubalika na wananchi.
Kuungana tutaungana, ila tutaungana na watu ambao ni serious (makini), wenye mipango, tutaelekezana tukiwa mezani kama ni nini tunataka kufanya, na kila mmoja aseme ana nini, lakini haya yatafanyika wakati muafaka ukifika, alisema.
Aliongeza kuwa, lengo la vyama vya upinzani, hasa CHADEMA, si kuitoa CCM madarakani tu, ni kuungana, maana kuna kitu cha msingi kinatakiwa kufanyika kwa umoja ili maisha ya Watanzania yabadilike na kufanyiwa mabadiliko ya kweli katika maisha ya watu.