Fredrick Sanga
JF-Expert Member
- Jan 27, 2011
- 3,153
- 697
Ni jambo la kawaida kabisa na endelevu, yaani kuwafunda vijana. hakuna jipya hapo. Watakaa sawa hatuhitaji msaada wa CCM.
Kivipi nawachochea? Najikosha kwa nani? Unaweza kufafanua kidogo ueleweke?
Mkumbo umekimbilia wapi? njoo ujibu hoja za watu hapa, vinginevyo tuamini kwamba wewe, Shibuda na Juliana lenu moja na ndiyo mnaoua CHADEMA. Ni katika mazingira gani unamweka Heche na Juliana katika kundi moja kwa haya yaliyotokea? acha kujificha na uje utuambie ni kwanini huyu Juliana wako anamshambulia Heche? Je katiba ya BAVICHA inampa mamlaka ya kuwa msemaji wa BAVICHA yeye Juliana?
Mkumbo nilikuwa nakuheshimu sana lkn sasa naanza kupata wasiwasi na ueledi wako ndani ya Chadema. Haiwezekani ukaweka kosa alilofanya Heche na Juliana kwenye kapu moja. Pia huwezi kukimbia hoja ya kuongelea kauli ya Shibuda kwamba HAKUNA CHAMA CHA UPINZANI KILICHOKOMAA NA KUWEZA KUKABIDHIWA DOLA, NA HAYO ANAYATAMKA KWENYE NEC YA CCM
Mkumbo naomba majibu otherwise nitaanza kuamini kwamba hata UDSM walipokunyima Udean majuzi kumbe walikuwa sahihi japo ulishatumika kama Head wa idara.
Yani unataka watu waache mambo ya msingi wamjadili Shibuda??
Kweli??
Who is shibuda katika politics za mageuzi??
He is nothing, he does not deserve the publicity he is even getting.
BAVICHA walichemka kutoa tamko, na huyo makamu nae kachemka. Wote ni vichwa maji tu.
The tamko wa unnecessary in all counts.
Yani unataka watu waache mambo ya msingi wamjadili Shibuda??
Kweli??
Who is shibuda katika politics za mageuzi??
He is nothing, he does not deserve the publicity he is even getting.
BAVICHA walichemka kutoa tamko, na huyo makamu nae kachemka. Wote ni vichwa maji tu.
The tamko wa unnecessary in all counts.
Kitila Mkumbo, mbona unaniacha hoi? Naomba ukumbuke ule usemi kuwa mdharau mwiba, mguu huota tende!Kivipi nawachochea? Najikosha kwa nani? Unaweza kufafanua kidogo ueleweke?
Gazeti la Rai Mwema | Jumatano, 24 Mei 2012
Malumbano baina ya Mwenyekiti wa BAVICHA na Makamu wake katika vyombo vya habari ni hatua ya kubalehe kisiasa, ambayo haipaswi kuwakatisha tamaa wapenzi wa mageuzi nchini. Bahati mbaya kubalehe huku kunaambatana na usumbufu na kero. Usumbufu na kero hizi zingekuwa za maana kama vijana hawa wangekuwa wanalumbana juu ya jambo la msingi la kifalsafa au kisera au kikanuni ndani ya chama na nchi. Bahati mbaya kwamba vijana hawa wanalumbana kwa jambo la kipuuzi. Ni upuuzi kulumbana juu ya kauli rejareja za Mbunge wa Maswa John Shibuda, mwanasiasa ambaye mbwembwe zake za kisiasa zinajulikana hata kabla hajahamia CHADEMA.
Kwamba Shibuda ametangaza kugombea urais ndani ya kikao cha CCM haiwezi kuwa tatizo kwa sababu kimsingi kufanya hivyo hakuvunji kanuni yeyote ndani ya CHADEMA kwa sababu hakuna kanuni yeyote inayoelekeza muda na mahali mwafaka pa kutangaza nia ya kugombea urais. Mwanachama anapaswa kuongozwa na busara zake tu juu ya muda na mahali pa kutangaza nia yake. Sasa kama mwanachama wa CHADEMA hana busara kiasi cha kutangaza nia ya kugombea urais ndani ya kikao cha mpinzani wake CCM, na kama busara za mwanachama huyo ni finyu kiasi cha kumuomba mwenyekiti wa CCM ndiye awe meneja wa kampeni zake, kwa nini iwe tatizo kwa BAVICHA au CHADEMA?
Hivyo, haikutarajiwa kwamba kuna mtu mwenye akili sawasawa ndani ya CHADEMA angemjibu Shibuda pale alipotamka, ndani ya kikao cha CCM, kwamba angegombea urais kupitia CHADEMA mwaka 2015. Kauli ya Shibuda haikustahili kupewa umakini wowote hasa kwa kitendo chake cha kusema kwamba Rais Kikwete ndiye angekuwa meneja wake wa Kampeni. Hili peke yake lilitosha kuonyesha kwamba kauli za Shibuda ni mwendelezo wa mbwembwe zake kisiasa zisizostahili kupewa uzito wowote ule. Hivyo, kwa Mwenyekiti wa BAVICHA kutoa tamko kali juu ya Shibuda ilikuwa sawa na mtu mwenye akili timamu kujaribu kumkimbiza kichaa aliyekimbia na nguo zake. Ni vizuri wanasiasa vijana wakaielewa kwa upana wake dhana ya uhuru wa maoni. Uhuru wa maoni ni pamoja na kukubali kusikia yale usiyoyapenda na kuyataka.
Katika kujitutumua kisiasa, Makamu wa BAVICHA naye anatoa tamko la kumkana bosi wake, tena hadharani na nje ya viwanja vya chama. Madai ya makamu huyu wa BAVICHA ni kwamba hakuna kikao kilichoidhinisha tamko la Mwenyekiti wa BAVICHA kusema hayo aliyoyasema. Haya, na yeye tunamuuliza kikao gani cha BAVICHA kiliidhinisha yeye kumpinga mwenyekiti wake hadharani mbele ya waandishi wa habari? Je, makamu wa BAVICHA aliona ugumu gani kwenda kumshtaki mwenyekiti wake kwenye vikao vya BAVICHA na/au CHADEMA?
Nafikiri vijana hawa wa BAVICHA wanahitaji kufundwa. Nawashauri viongozi wa CHADEMA kuchukua hatua muhimu za kuwafunda vijana wa BAVICHA ili ubalehe wao wa kisiasa upite bila madhara kwa chama. Kufundwa huko ni pamoja na kuwafundisha namna ya kufanya kazi na vyombo vya habari. Wanahitaji kuhariri matamko yao sawasawa, na kabla ya kuyatoa wapime athari za matamko yao kwa chama. Ukiona wewe ni kiongozi wa CHADEMA unatoa tamko na tamko hilo linapamba vichwa vya habari vya magazeti pinzani kwa chama chako kama vile Uhuru, ujue tamko lako limekiumiza chama.
Laiti viongozi wa BAVICHA wangekuwa makini wangejizuia kutoa matamko yao. Mwenyekiti wa BAVICHA angekuwa makini angetafakari maana ya kauli yake kabla hajaitoa, na angedundua kwamba tafsiri pana ya kauli yake ni kutaka kuzuia baadhi ya wanachama wa CHADEMA kugombea urais. Naye makamu wake angekuwa makini angetambua kwamba kumpinga mwenyekiti wake hadharani ni kutangaza mgogoro ndani ya chama, na ilikuwa ni kucheza mikononi mwa wapinzani wa CHADEMA. Viongozi hawa wanapaswa kutambua kwamba katika mawasiliano muhimu siyo unachosema, bali kile ambacho hadhira inasikia. Kwenye tamko la Mwenyekiti wa BAVICHA hadhira walisikia kwamba baadhi ya wanachama wa CHADEMA hawaruhusiwi kutangaza kugombea urais, na walichosikia hadhira ya makamu wake ni kwamba kuna mgogoro ndani ya CHADEMA! Je, huu ndio ujumbe ambao viongozi hawa walitarajia kuufikisha?
Msimamo wa CHADEMA dhidi ya kauli za Shibuda umekuwa ni kumdharau kwani, pamoja na kwamba zinasababisha usumbufu, kauli zake zimekuwa hazina madhara ya msingi kisiasa kwa chama. Hata hivyo kauli za Shibuda iliyoripotiwa katika moja ya magazeti ya Jumapili ni zaidi ya usumbufu. Kwamba viongozi wa CHADEMA wanamchukia Shibuda kwa sababu ni msukuma ni kukigombanisha chama na wapiga kura wa kanda ya ziwa. Huu sasa sio usumbufu tena bali ni uharibifu. Usumbufu unavumilika, lakini uharibifu hauwezi kuvumilika. Ni wazi kuwa Shibuda amepania kuiharibu CHADEMA. Kwa hivyo kuna haja ya kuangalia upya sera ya kumdharau Shibuda.
Tukumbuke kwamba mambo yote haya yanatokea kipindi ambacho Waziri mwandamizi katika serikali ya CCM ameapa kuona CHADEMA inasambaratika ndani ya mwaka mmoja. Vijana wa BAVICHA yawapasa kuwa makini, vinginevyo wataonekana wapo katika mkakati wa kuisambaratisha CHADEMA. Tumewaonya!
Dk Kitila Mkumbo ni Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Ndiyo maana nasisitiza kuwa huyu Juliana Shonza ana nguvu za kipekee ndani ya BAVICHA na ChademaMkumbo,
ulijitokeza mwanzoni ulivyogundua kwamba makala yako haijajibu hoja za msingi za Juliana Shonza (mwanafunzi wako), kwani makala yako ililenga kumsafisha msaliti Juliana na Shibuda na kutaka kuonyesha kwamba Heche naye amekivua nguo CHADEMA kama walivyofanya Juliana na Shibuda kitu ambacho hakuna mtu mwenye uelewa anayeweza kukubaliana na wewe katika hilo, kwani HECHE hakufanya kosa sawa na Juliana.
This is a missed opportunity! so sad. Tulitaraji CDM wasimame kidete na kusema, Shibuda enough is enough!, siyo kwa hoja ya kugombea urasi bali kwa hoja ya kuingiza ukabila katika chama kwa kauli yake ya 'naandamwa kwa usukuma'. Chama kinachojengewa tuhuma za namna hiyo na maadui mara ikitokea mbunge wake kuthibitisha ukabila kitatokea nini hapo.1. Vijana wa BAVICHA wanahitaji kufundwa baada ya kuharibu mambo? I expected this to be a standard procedure!
Nimeisoma taarifa ya Julianna. Its is clear kwamba ile taarifa siyo yake binafsi. Ile taarifa imeandikwa na kikundi cha watu ambao wamempa Julianna confidence ya kuita waandishi wa habari akijua kuwa "some big guys" in CDM are behind it.Kitila usikimbie mjadala njoo ufafanue. ...Kwamba tunatakiwa kuwatoa wapuuzaji wa chama kimoja (CCM) na kuwaweka wapuuzaji wa chama kingine (CHADEMA),tofauti kati ya CCM na CHADEMA ipo wapi sasa?Hawa wanasema "huu ni upepo tu, utapita", hawa wengine wanatuambia "puuzeni tu".
Ndio uongozi mbadala huu? Unaolea cancer katika chama na kutuambia tuipuuze tu?
Kitila Mkumbo, mbona unaniacha hoi? Naomba ukumbuke ule usemi kuwa mdharau mwiba, mguu huota tende!
Kwanza, Heche ni mwenyekiti na kikatiba ndiye msemaji mkuu wa BAVICHA tofauti kabisa na Juliana ambaye ni msaidizi tu, mamlaka ya kuwaita waandishi wa habari anayatoa wapi Juliana?
Pili, ikiwa ni kweli Shibuda, Mbunge wa Maswa kupitia Chadema ni mtu wa kupuuzwa tu na kudharauliwa, aliwezaje kuaminiwa hadi kupitishwa na Chadema kuwa mgombea Ubunge 2010?
Tatu, Shibuda ni mjumbe wa Umoja wa Taasisi za Afrika inayoshughulikia utawala bora kanda ya Afrika Mashariki, je tamko lake la kuponda Upinzani hapa Tanzania, kweli halina madhara kwa Chadema?
Nne, Baraza la Vijana wa Chadema litawezaje kukaa kimya kama moja wa Wabunge wake hata akiwa kichaa anadiriki kukidhalilisha hadharani na mbele ya mahasimu wao wakuu, Chama cha Mafisadi?
Tano, je operation vua gamba vaa gwanda litachukuliwaje na wananchi ambao wameanza kuamka na kuweka tumaini lao kwa Chadema kama Shibuda anaruhusiwa kukikejeli anavyopenda bila karipio?
Sita, Chadema inategemea nini mwaka 2015 kama mmoja wa wabunge wake unataka wanachi wamwone kama chizi, je wapiga kura watashawishiwa vipi kukipa uongozi chama kinacholea machizi?
Saba, ni hasara gani Chadema inapata kutokana na tamko lililotolewa na msemaji mkuu wa Bavicha na je, kwa mtu kama Wasira kuchangamkia hiyo hali Chadema haistuki kwamba labda upo moshi unafukuta?
Nane, Kitila Mkumbo, kwa nini wewe nawe umeamua kutoa tamko kama ni kweli Shibuda ni wa kupuuzwa na kwa nini kifanyike kikao rasmi cha BAVICHA kulitolea tamko kama anavyodai Juliana, who is she?
Mwisho, naamini hili jambo halikutaji kikao rasmi na alichofanya Heche ni sahihi kabisa kwani ni wajibu wa vijana kuhakikisha heshima ya chama inalindwa na kama Mwenyekiti hili liko ndani ya uwezo wake.
Huu uongozi wa kupuuza puuza mambo si ndio huu huu tunaukataa kwa CCM?
Si ndiyo habari za Kikwete kusema "huu upepo tu, utapita" alipoambiwa kubadili mawaziri?
Sasa kama viongozi wasomi wenyewe wa CHADEMA ndio hawa kina Kitila Mkumbo wanakuja hapa macho makavu kabisa, wanaandika habari ndeeefu, tupuuze mambo yanayoonyesha muelekeo wa chama waziwazi, mtu mmoja analeta cancer katika chama halafu anaachiwa, tunaambiwa "tumpuuze", wananchi tunatakiwa tupate picha gani hapa?
Kwamba tunatakiwa kuwatoa wapuuzaji wa chama kimoja (CCM) na kuwaweka wapuuzaji wa chama kingine (CHADEMA) ?
Kama habari zenyewe ndiyo hizi hizi za kupuuza mambo muhimu, tofauti kati ya CCM na CHADEMA ipo wapi sasa?
Hawa wanasema "huu ni upepo tu, utapita", hawa wengine wanatuambia "puuzeni tu".
Wote naona falsafa yao moja, kufunika vichwa chini ya mchanga kama mbuni anayefukuzwa ambaye hataki kukubali ukweli, anataka kuishi katika dunia ya kufikirika ambayo watu hawatatui matatizo yao, wanayapuuuza tu.
Ndio uongozi mbadala huu? Unaolea cancer katika chama na kutuambia tuipuuze tu?
The Kitila Mkumbo niliyepata kumfahamu miaka yote ndiye huyu huyu hapa kwenye superb logical thinking and sound arguement WITHOUT PREJUDICE the least.
Hebu kamtambue huyu rafiki yangu kuwa ni mtu wa ina gani kwa kupitia japo hicho kijipande hapo chini. Hakika Mkumbo kamaliza kila kitu kwa kuniibia mawazo yangu juu ya kiji-mzozo uchwara ndani ya BAVICHA - Vijana sasa elekezeni nguvu kwenye 'Vua Gamba' na ktu msiende huko anakowatafutia Mzee Shibuda - Mzee ambaye anazeeka vibaya baba yetu huyu:
... Kwamba Shibuda ametangaza kugombea urais ndani ya kikao cha CCM haiwezi kuwa tatizo kwa sababu kimsingi kufanya hivyo hakuvunji kanuni yeyote ndani ya CHADEMA kwa sababu hakuna kanuni yeyote inayoelekeza muda na mahali mwafaka pa kutangaza nia ya kugombea urais. Mwanachama anapaswa kuongozwa na busara zake tu juu ya muda na mahali pa kutangaza nia yake. Sasa kama mwanachama wa CHADEMA hana busara kiasi cha kutangaza nia ya kugombea urais ndani ya kikao cha mpinzani wake CCM, na kama busara za mwanachama huyo ni finyu kiasi cha kumuomba mwenyekiti wa CCM ndiye awe meneja wa kampeni zake, kwa nini iwe tatizo kwa BAVICHA au CHADEMA? ....