TANZIA DJ Ommy afariki dunia

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
19,643
33,439
Wakuu,

Inawezekana wengi mmeshapata taarifa ya kifo cha DJ Ommy lakini kwavile sijaona post hapa JF juu ya hili nimeona nigusie kutokana na umuhimu wake.

DJ Ommy ni moja ya madj wa mwanzo kabisa wa radio ambao walitikisa sana na kuleta mapinduzi hasa ya muziki wa dansi. Wanamuziki wa dansi hasa wa zamani wanajua jinsi alivyowapaisha enzi hizo.

Kipindi cha midundo motomoto pale radio one aliteka nchi kwa mixing zake za bolingo ambazo watu wengi nyakati hizo hawawezi kusahau.

R&B na hip hop namba moja alikuwa John Dilinga akichuana na Bonny Love lakini kwenye yenu pamoja na ukali wa Dj Charles wa Africa bambataa lakini DJ Ommy alikuwa kiboko na aliteka mitaa yote kwa kipindi chake hasa midundo motomoto pamoja na Dj show akiwa na Aboubakary Sadik.

Pumzika kwa amani Dj Ommy #mixingmaster

=====
FB_IMG_1610325983880.jpg

MMOJA wa Dj bora wa redio hapa nchini, Dj Ommy amefariki dunia juzi jioni.

Kwa mujibu wa mtangazaji wa redio One, Abdalla Mwaipaya ambaye amewahi kufanya kazi naye Dj Ommy ambaye ni miongoni mwa wazilishi wa Kwa fujo djs alifariki baada ya kuugua kwa muda.

Alisema Dj Ommy alikuwa na uwezo mkubwa wa kuchanganya muziki hasa wa dansi na alikuwa na kipaji cha ubunifu wa jingle za redio.

“Wakati yupo Radio One ndiye aliyebuni jingle zilizokuwa zinawataja watangazaji wote zikiimbwa na Papii Kocha na marehemu Mao Santiago,” aliandika.

“Kwa wale wanaozikumbuka ni ile inaimbwa wajifanya wanajuaaa kumbe waungua juaaa radio one kiboko yao. Dj Ommy amechukua ameweka waa Abubakari Sadiki shangilia ushindi unakuja.. nk,”.

Alongeza alijua kukaa kwenye kipindi chochote iwe Dj shoo au midundo motomoto kitambulisho chake kikubwa kilikuwa ni kicheko chake kilichoacha alama.

TAARIFA:
Ratiba ya kutoa heshima za mwisho kwa DJ OMMY

Saa Tisa alasiri Mwananyamala Hospitali

Saa kumi jioni mwili utaondoka kuelekea Same kwa mazishi
 
Daa! nammkumbuka vizuri sana DJ Ommy, alikuwa kwenye kipindi cha "dj show" saa 8 mchana mpaka saa 10 jioni, kama sikosei kuanzia jumanne hadi alhamisi, ijumaa ndio kulikuwa na "the heat" ya DJ JD. Alafu kila jumamosi kwenye mida ya jioni DJ Ommy alikuwa tena kwenye "midundo mototomoto".
 
Daa! nammkumbuka vizuri sana DJ Ommy, alikuwa kwenye kipindi cha "dj show" saa 8 mchana mpaka saa 10 jioni, kama sikosei kuanzia jumanne hadi alhamisi, ijumaa ndio kulikuwa na "the heat" ya DJ JD. Alafu kila jumamosi kwenye mida ya jioni DJ Ommy alikuwa tens kwenye "midundo mototomoto".
Yes, enzi hizo radio ziliwaka moto, Clouds yupo Bonny Love na Dj Charles huku Radio One yupo John Dilinga na Dj Ommy. Zilikuwa nyakati za pekee sana ....
 
Sikumbuki vizuri aliondoka radio one kwenye miaka gani lakini kwa miaka mingi nilikuwa najiuliza alienda wapi baada ya kutoka radio one? Yeye, DJ JD na DJ Fast Eddy ndio madj wa mwanzoni mwanzoni radio one. Kuna kipindi pia alikuwa ndani ya "kwafujo DJs" ya kina Abubakary Sadiki na Majay Majizo.
 
Yes, hao pamoja na Dj Rakim Ramadhan (rip) ndio waliochange djing atmosphere bongo
 
Wakuu,

Inawezekana wengi mmeshapata taarifa ya kifo cha DJ Ommy lakini kwavile sijaona post hapa JF juu ya hili nimeona nigusie kutokana na umuhimu wake.

DJ Ommy ni moja ya madj wa mwanzo kabisa wa radio ambao walitikisa sana na kuleta mapinduzi hasa ya muziki wa dansi. Wanamuziki wa dansi hasa wa zamani wanajua jinsi alivyowapaisha enzi hizo.

Kipindi cha midundo motomoto pale radio one aliteka nchi kwa mixing zake za bolingo ambazo watu wengi nyakati hizo hawawezi kusahau.

R&B na hip hop namba moja alikuwa John Dilinga akichuana na Bonny Love lakini kwenye yenu pamoja na ukali wa Dj Charles wa Africa bambataa lakini DJ Ommy alikuwa kiboko na aliteka mitaa yote kwa kipindi chake hasa midundo motomoto pamoja na Dj show akiwa na Aboubakary Sadik.

Pumzika kwa amani Dj Ommy #mixingmaster

Kuna sababu yeyote iliyokufanya usiweke picha yake?
 
Back
Top Bottom