benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Moja kati ya Ma-DJ ambao waliowahi kufanya vizuri katika muziki wa Bongo Flava hapa nchini akifanya kazi Clouds FM Radio, Steve Mdoe a.k.a "DJ Steve B" "DJ Skills" amefariki dunia jioni ya leo Julai 31, 2023 katika Hospitali ya Muhimbili Mloganzila alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa muda mrefu DJ Steve B alikuwa akiugua maradhi ya Figo.

Inna lillahi wa inna ilayhi rajiun.

UPDATES:
Zoezi la kutoa Heshima za mwisho zinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam
Jumamosi tarehe 05/08/2023.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku hiyohiyo ya Jumamosi tarehe 05/08/2023 kwenye Makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
DSC04090.jpeg

=============

Steven Mdoe maarufu kama DJ Steve B amefariki dunia leo katika Hospitalini ya Mloganzila jijini Dar es salaam huku chanzo kikitajwa kuwa ni kupanda kwa Shinikizo la Damu.

Amstrong Mdoe ambaye ni Kaka wa Marehemu amesema kuwa Steve B ambaye alikuwa akisumbuliwa na figo toka mwaka 2019 alipelekwa Hospitali na kuwekwa Chumba cha Uangalizi Maalumu (ICU) baada ya Kupata Shinikizo la Juu la Damu na baadaye Shinikizo hilo lilipanda zaidi na kumsababishia kupoteza fahamu kwa siku tatu kabla ya kufariki.

"Steve B alipoteza fahamu kwa siku 3 ambapo jioni ya leo saa 10 akafariki, alikuwa na tatizo la Figo kwa miaka minne tangu 2019 lakini Figo sio chanzo cha Kifo chake, taratibu za mazishi bado tunazungumza tupange utaratibu lakini tunapokea rambirambi kwa namba 0678689383"

"Steve hakuwa na Mke wala hajaacha Mke na wala Mtoto, hatuna taarifa za Mtoto wake"
 
Dj Steve B amefariki dunia, akiwa kwenye matibabu Muhimbili.

Dj Steve B ambaye ni Dj bora kabisa kuwahi kutokea hapa nchini Tanzania alikuwa na maradhi ya muda mrefu.
Tanzania itamkumbuka kwa album yake ya 'pamoja kwenye game' iliyokuwa na mikwaju mwanzo mwisho.

Moja ya Djs walioipambania sana bongofleva.

Kuelewa balaa lake pale bills na manyuki wenzie, you had to be there

Mungu Amlaze Pema Dj Skills
 
Back
Top Bottom