Diwani wa CHADEMA ashinda kesi ya uchaguzi Tabata

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
PATRICK Asenga Diwani wa Kata ya Tabata (CHADEMA) ameshinda kesi ya uchaguzi aliyofunguliwa na Sudi Kasim aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Kassim alifungua kesi hiyo akipinga matokeo ya kiti hicho katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana kwa madai kwamba haukuwa huru na haki.

Akitoa hukumu ya kesi hiyo jana katika Mahakama hiyo, Frank Moshi hakimu aliyekuwa akisikiliza shauri hilo amesema, anatupilia mbali kesi hiyo kwasababu mdai ameshindwa kuthibitisha malalamiko yake. Miongoni mwa vitu alivyoshindwa kuthibitisha ni pamoja na uwepo wa vurugu katika kituo cha majumuisho ya kuhesabia kura ambapo hata wakala wake ameshindwa kuthibitisha hilo katika ushahidi wake.

Kutokana na hali hiyo, hakimu alisema kwamba uchaguzi ulikuwa huru na haki na kwamba Asenga ni diwani halali wa kata ya Tabata na atalipwa gharama ya 30 milioni kama fidia ya kesi hiyo. Akizungumza nje ya mahakama, diwani Asenga amewashukuru wananchi wake kwa ushirikiano waliouonesha na kuahidi kuwa gharama za kesi atakazolipwa ataziingiza katika miradi ya maendeleo ya kata hiyo.

Amesema kuwa gharama hizo nakwamba atawasilisha madai ya fedha hizo mapema ili aweze kulipwa. “Nashukuru wananchi wangu kwani nipo pamoja nao,mahakama imetenda haki.Hii kesi ilinipotezea muda wa kuwatumikia ,lakini kwasasa nipo huru na nipo tayari kuchapa kazi “, amesema Katika kesi hiyo,wadaiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ilala.

Katika kesi hiyo, Kasim aliiomba mahakama hiyo itenguwe matokeo ya uchaguzi kutokana na dosari mbalimbali zilizojitokeza na kwamba imtangaze yeye kama mshindi.
 
Sera zenu na nani sijawahi kuwa shabiki wa vyama vya siasa nimetoa tu mtazamo wangu ila kwa kuwa mwenzangu uko kitwanga sawa
 
Kumbe CCM bado wanaendeleza makambalization policy ya kuwakatia rufani wapinzani wakishinda?
 
Sera zenu na nani sijawahi kuwa shabiki wa vyama vya siasa nimetoa tu mtazamo wangu ila kwa kuwa mwenzangu uko kitwanga sawa
Hapo upo Lumumba baada ya kuona huna hoja uneanza kusema huna chama tulua dawa ikuingie usiyempenda kaja.. mchezo huu hautaki hasira
 
Ingekuwa kesi ya ubunge ccm isingeachia, kesi kama hizo wanaacha ili wapumbazie kuna democracy
 
Back
Top Bottom