Dina Marios aacha rasmi kutangaza Leo tena

warumi

R I P
May 6, 2013
16,273
18,382
Yule mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm, Dina Marious leo ametangaza kuwa hataendelea kufanya kipindi hicho na badala yake anakuja na kipindi kipya cha TV.

Dina ambaye hajasikika kwenye kipindi hicho kwa miezi kadhaa baada ya kwenda likizo ya uzazi baada ya kujifungua mtoto wa kiume aitwaye Zion,
ametoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram. Hiki ndicho alichokiandika: "Ni miaka 8 sasa imetimia toka nilipokabidhiwa mtoto huyo. Nilimlea kwa
taabu sana siku za mwanzo zilikiwa ngumu wakati mwingine sikulala kuhakikisha anakuwa salama. Nyakati hizo nilionekana nisingekuwa mama bora wa
mtoto huyo lakini nilipigana kike na kuwa mtoto bora aliyependwa na kusifika nchi nzima".

Mtoto huyo anaitwa leo tena na Dina Marios. Leo tena ikawa leo tena na kuwa kipindi bora kinachopendwa tanzania na Dina Marios nikawa mtangazaji bora wa kike na wapili bora Tz nzima kwa kupendwa hii ni kwa mujimu wa research. Kupitia leo tena nimetengeneza mashabiki, marafiki, wapenzi na hata ndugu. Sasa leo tena imekuwa na sina budi kuiacha iendelee kulelewa na mtu mwingine.

Kama nilivyokabidhiwa leo tena kuilea nimepewa tena jukumu lingine kubwa la kulea mtoto mpya atakaeonekana kwenye luninga inamaana ntakuwa nikiuza sura luningani. Niliwapenda sana wasikilizaji wangu japo mlikuwa mkiniuliza narejea lini kwenye leo tena ukweli ni kwamba sirudi tena kwenye leo tena.

Naomba sala na dua zenu katika safari yangu mpya ambayo najua haitakuwa rahisi kama mlivyokuwa nami kwenye leo tena basi muwe nami katika hili. Wiki ijayo nitakuja rasmi kuwaaga kupitia leo tena ya Clouds FM. Nawapenda mno machozi kede kede yananimwagika
 
Hayaa wambea wenzetu wajeee usipokoment umetuogopaaa ukikoment we mbea mwenzetu tena umekubuhuuu yalaaaa yalaaaaaaaa

Wasipo comment humu wataenda wapi ?? Si wanajitoaga ufahamu wakat umbea wanaupenda sana.

Ivi ulikuwa unasikilizaga kipindi cha Leo ?? Dina na mwenzie geah walikuwa wambea aiseeh , nakumbuka hadi mikoan walikuwa wanasafiri kutafuta maubuyu , kipindi chao kilikuwa kizur sana
 
Nawajuaa wale balaaaaa kwa ubuyuuuuu alaaaaaaaa
 
Daah sasa sisi mashabiki wako wenye ving'amuzi vya Dstv si umeshatupoteza jamani Dina. Wakupe angalau basi hata taarifa ya habari.
 
Yule mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm, Dina Marious leo ametangaza kuwa hataendelea kufanya kipindi hicho na badala yake anakuja na kipindi kipya cha TV.

Dina ambaye hajasikika kwenye kipindi hicho kwa miezi kadhaa baada ya kwenda likizo ya uzazi baada ya kujifungua mtoto wa kiume aitwaye Zion,
ametoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram. Hiki ndicho alichokiandika: "Ni miaka 8 sasa imetimia toka nilipokabidhiwa mtoto huyo. Nilimlea kwa
taabu sana siku za mwanzo zilikiwa ngumu wakati mwingine sikulala kuhakikisha anakuwa salama. Nyakati hizo nilionekana nisingekuwa mama bora wa
mtoto huyo lakini nilipigana kike na kuwa mtoto bora aliyependwa na kusifika nchi nzima".

Mtoto huyo anaitwa leo tena na Dina Marios. Leo tena ikawa leo tena na kuwa kipindi bora kinachopendwa tanzania na Dina Marios nikawa mtangazaji bora wa kike na wapili bora Tz nzima kwa kupendwa hii ni kwa mujimu wa research. Kupitia leo tena nimetengeneza mashabiki, marafiki, wapenzi na hata ndugu. Sasa leo tena imekuwa na sina budi kuiacha iendelee kulelewa na mtu mwingine.

Kama nilivyokabidhiwa leo tena kuilea nimepewa tena jukumu lingine kubwa la kulea mtoto mpya atakaeonekana kwenye luninga inamaana ntakuwa nikiuza sura luningani. Niliwapenda sana wasikilizaji wangu japo mlikuwa mkiniuliza narejea lini kwenye leo tena ukweli ni kwamba sirudi tena kwenye leo tena.

Naomba sala na dua zenu katika safari yangu mpya ambayo najua haitakuwa rahisi kama mlivyokuwa nami kwenye leo tena basi muwe nami katika hili. Wiki ijayo nitakuja rasmi kuwaaga kupitia leo tena ya Clouds FM. Nawapenda mno machozi kede kede yananimwagika

Mmmh, jina la mtoto wake laitwaje, mbona sijaelewa, hivi Zayun kwa kiingereza inaandikwaje?
 
Sasa huku kwenye runinga hakuna kuropoka na hakuna mambo ya kupitiliza namtakia kila la kheri na Clouds Tv wajipange sana kwenye tv wana mwendo mwepesi sana ukilinganisha na umri wa clouds tv.

Wana takiwa wawe wabunifu sio kila kipindi kiwe cha burudani bali wajikite kwenye vipindi vya kijamii pia.

Lakini uzuri ana pakujifunzia.
 
Jamani mie nilikuwa namsubiria arudi nianze kusikiliza leo tena maana sasa hivi imepoozaaaa
 
Sasa huku kwenye runinga hakuna kuropoka na hakuna mambo ya kupitiliza namtakia kila la kheri na Clouds Tv wajipange sana kwenye tv wana mwendo mwepesi sana ukilinganisha na umri wa clouds tv.

Wana takiwa wawe wabunifu sio kila kipindi kiwe cha burudani bali wajikite kwenye vipindi vya kijamii pia.

Lakini uzuri ana pakujifunzia.

Clouds waache ku-copy vipindi kutoka EATV......Wawe wabunifu..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom