Diamond Platinumz vs Ali Kiba, nani mkali?

[Q UOTE=pinno;7751619]Robert kiyosaki huwa anasema baada ya kuuza nakala nyingi sana za kitabu chake "Rich dady ,poor dady" Watu wakamuuliza wewe inakuwaje unauza kuliko waandishi walobobea katika mambo ya personal finances, Maprofessa wa Harvard na Wataalam kutoka Wallstreet?? kwa nini???

akasema " Its because am a best selling author and not a Great author while those are Great Authors and not Best selling Authors".

This is true kwa Marlaw, Alikiba, na it was very true kwa King of Freestyle Albert Mangweha RIP. Ni watu wanaojua sana, ni kama hao maprofesa wa harvard, wanaoshindwa kuuza vitabu vyao kwa levo ya Kiyosaki kanjanja mmoja anaeandika juu ya nertwork marketing. Namfaham Marlaw since Iringa 2004 enzi hizo kwa 2d Thomas na Temmy G. tulikuwaga tunasema " Dah huyu jamaa akitoka, atakuwa juu sana" akatoka juu then akawa kawaida

Mtandao wenye bidhaa nzur kuliko zote unaweza kuwa zantel, lakin wenye wateja wengi na faida kubwa ukawa voda au tigo.
 
we ulikua ujui siye kila aliyezaliwa magomeni anaujua mji,,,wengine hata posta hawajawah fikaa!
 
i av a crush for diamond but am in love with ali kiba....though kimziki diamond mkaliiiiiiiiiiiiiiii......." now show me how u do it...ngoroooo .......ur my number one.......my darling, roho yangu mama" mwaaaaaah platnum " just thinking loud "
 
Usiseme kaubadilisha muziki WETU!muziki upi?me simkubali hata kidogo na asiombe ale msosi na mimi natafuta sumu ya panya af inauzwa sh mia tu...me nawaelewa akina hayati marijan,maneti,jery nashon dudumiz,mzee gurumo,hayati TX,nico zengekala,akina banzastone na watu dizain hiyo....huyo diamond hunishawishi kabisa labda wmbo wa mawazo tena napenda midundo ya wmbo tu na c kingine,mtazamo wangu tu.
 
hivi kumbe unaweza kuzaliwa na kukulia kariakoo na bado ukawa mshamba?

Inategemea ni kariakoo ipi..maana alikiba amekulia mchikichini bondeni kule ambako maji ya TBL yale machafu yanamwagikia yaani mtaa wa muheza mwisho kabisa kule alafu unaingia kwa chini.. Kiba kinachomsumbua ni ushamba na kutotaka kujifunza kitu ambacho ni tofauti na Diamond.
 
dah! Huyu jamaa namkubali kwenye song la "Mac muga" yaani alinituma sana, lkn naye katumika kivingine, mwambie huko ulikozamia hakuna mgeni, arudi atoe mac muga ii na ile karim, atauza sana. Hebu mwambieni. Pia kuna yule mwenzake aliyeimba "dunia tunapita" then kaimba na juliana, hata fb wala kwenye tv simuoni!
 
Hata kama sio shabiki wa diamond ila kuna kitu lazima uwe kinakuvutia kutoka kwake.Unaweza kujitahidi kumchukia labda kutokana na skendo zake za nje ya muziki wake ila ukirudi kwenye muziki wake nadhani anastahili kuwa pale alipo.
Kuanzia muonekane wake mpaka anavyoweza kuji-brand kimataifa na anavyojua kucheza na akili za mashabiki.

Wasanii wengi wa bongo flava wana tabia ya kurithika kwa mafanikio yao ila Diamond toka atoke na Kamwambie mwaka 2009 mpaka 2013 amezidi kwenda juu bila kuonyesha kusuasua wala kutetereka.
Angalia video ya number 1.Wimbo unaweza sema ni wa kawaida kabisa ukilinganisha na mbagala, kamwambie au nitarejea ila akili ya kwenda kufanya video cape town,south africa kumeifanya nyimbo iwe number 1 kama jina lake lilivyo.

Ushawahi kujiuliza Ali kiba yupo wapi pamoja na kuwa kila mtu anajua ni mkali kuliko diamond?Ali kiba toka atoe my everything mwisho wa mwaka jana amepotea hata video ajatoa.Tukaja kumuona kwenye kidela na Abdu kiba bila kurefusha maneno Ali anashindwa kuufanya mziki wake kama mashabiki wake wanavyotarajia labda pengine angekuwa anafukuzana na diamond ila matokeo yake vijana wake kama Rich mavoko na Dimpoz ndio wapo nyuma ya Diamond huku Ali akibaki msanii mkali ambae ameshindwa kuendelea kutuonyesha ukali wake sijui anawaza nini!

Ushawahi kujiuliza kama ule wimbo wa airtel hands across the world waliopiga wakina r.kelly,fall ipupa,2 face kama nafac ile angeipata diamond leo angekuwa wapi?
Diamond leo anatuletea remix ya number 1 f.t Davido kila mtu anaisubiri kwa hamu ila Ali alishindwa hata kutuletea remix ya Dushelele f.t Fally ipupa pamoja kukaa nae wiki nzima wakifanya wimbo pamoja.
Diamond ni mjanja anaejua biashara ya mziki ilivyo labda pengine ni management yake inayomsimamia.Diamond kaweza kuubadilia mziki wetu kwa kiasi chake leo ndio msanii anaelipwa pesa nyingi kwa show.

Nampenda ali kiba,naipenda sauti yake,anajua mziki kuliko Diamond ila Ali ameshindwa kubadilika na kukubali soko la mziki linataka nini.

Amka Ali huyu Diamond hakuwezi ila usipokuwa makini utajikuta nyuma ya rich,barnaba,dimpoz na ben pol maana mziki sio kuimba peke yake mziki ni biashara pia
Hapo kwenye msimbazi sikumwelewa kabisa huyo Ali kiba, katoka kufanya kolabo kali kama hiyo anatoa wimbo akijisifu alivyo kula mayai na kujam.pi.a watu ucku?
 
Usiseme kaubadilisha muziki WETU!muziki upi?me simkubali hata kidogo na asiombe ale msosi na mimi natafuta sumu ya panya af inauzwa sh mia tu...me nawaelewa akina hayati marijan,maneti,jery nashon dudumiz,mzee gurumo,hayati TX,nico zengekala,akina banzastone na watu dizain hiyo....huyo diamond hunishawishi kabisa labda wmbo wa mawazo tena napenda midundo ya wmbo tu na c kingine,mtazamo wangu tu.

nazungumzia mabadiliko kwenye malipo ya show mkuu....gurumo kaanza muziki toka diamomd ajazaliwa leo diamond kaja kumpa gari gurumo...kuna msanii yoyote alishawahi fanya hivyo hapa bongo?
 
Inategemea ni kariakoo ipi..maana alikiba amekulia mchikichini bondeni kule ambako maji ya TBL yale machafu yanamwagikia yaani mtaa wa muheza mwisho kabisa kule alafu unaingia kwa chini.. Kiba kinachomsumbua ni ushamba na kutotaka kujifunza kitu ambacho ni tofauti na Diamond.

kule mm ndio home na tumesoma shule moja primary mchikichini japo alinizidi madarasa kama matatu hivi...nadhani sio ushamba ila ujuaji mwingi sijui kwann aliamua kujitoa G.Record maana nayo ni sababu ya hivi
 
dah! Huyu jamaa namkubali kwenye song la "Mac muga" yaani alinituma sana, lkn naye katumika kivingine, mwambie huko ulikozamia hakuna mgeni, arudi atoe mac muga ii na ile karim, atauza sana. Hebu mwambieni. Pia kuna yule mwenzake aliyeimba "dunia tunapita" then kaimba na juliana, hata fb wala kwenye tv simuoni!

mwenzie kaenda kuuza unga south afrika
 
Mtu hata awe maarufu vipi, kwangu kama haja imba hata wimbo mmoja wa kuzungumzia uozo wa serikali na chama lake kwa kutuharibia nchi na kunyonya wananchi, huyo kwangu ni bure tu. Akili haiwezi kuishia kuimba mapenzi tu lazima kuta kuwa na tatizo la elimu kwa mtu huyo.

Nawapa salute akina Prof. J, Mr. II, Kala Jeremiah, E. Sanga na wapenda nchi kama hao kuliko wapenda magodolo, uroda na misifa ya kijinga.
Kwa uongo huyu! we unafikiri unaweza kuishi kwa amani kwa kusikiliza nyimbo za kununa,tafrani roho muda wote?most of the time unatakiwa uwe mindful not mindfull!Chillax!
 
huku hukiwa huna sababu ya kutompenda kama ipo basi sababu binafsi sio ya kimziki...ndio watanzania tulivyo
sio watanzania tu karibu kila mtu duniani kunakuwa kuna mtu humkubali hata iweje.Kama vile ambavyo sijawahi kuipenda Yanga,yaani Yanga hata ikicheza na timu ya Rwanda basi nitaishangilia timu hiyo ya kutoka Rwanda.
Nalog off
 
Robert kiyosaki huwa anasema baada ya kuuza nakala nyingi sana za kitabu chake "Rich dady ,poor dady" Watu wakamuuliza wewe inakuwaje unauza kuliko waandishi walobobea katika mambo ya personal finances, Maprofessa wa Harvard na Wataalam kutoka Wallstreet?? kwa nini???

akasema " Its because am a best selling author and not a Great author while those are Great Authors and not Best selling Authors".

This is true kwa Marlaw, Alikiba, na it was very true kwa King of Freestyle Albert Mangweha RIP. Ni watu wanaojua sana, ni kama hao maprofesa wa harvard, wanaoshindwa kuuza vitabu vyao kwa levo ya Kiyosaki kanjanja mmoja anaeandika juu ya nertwork marketing. Namfaham Marlaw since Iringa 2004 enzi hizo kwa 2d Thomas na Temmy G. tulikuwaga tunasema " Dah huyu jamaa akitoka, atakuwa juu sana" akatoka juu then akawa kawaida

Mtandao wenye bidhaa nzur kuliko zote unaweza kuwa zantel, lakin wenye wateja wengi na faida kubwa ukawa voda au tigo. "In business effective marketing of product is very important sometimes more than a product it self"

Kaka wewe ni mkali
 
Back
Top Bottom