Dhana ya USALITI ndani ya CHADEMA na Hatma ya Demokrasia ndani ya vyama vya Siasa

Huyu unayemsema diwani wa Kahama hata usimsemee kabisa.Hata leo hii ukimuuliza haogopi kukiri usaliti na anaona fahari kujaribu kukivuruga chama ili ccm iendelee kuwa madarakani.Kabla ya mkutano wa OPD Kahama alijaribu kupita kuwahadaa watu eti mkutano umeahirishwa hivyo watu wasijisumbue kwenda!Ila aibu ilimkuta kwani watu walifurika na wana machungu naye sana kwa kujaribu kudhoofisha chama ambacho ni tumaini pekee la wananchi

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
tunamaanisha ww mtoa mada kuwa na mwanaume mwingine nje huku ukiwa ndani ya ndoa.kama umenogewa vunja kwanza ndoa ili uweze kuwa na huyo mwingine!
 
Ukijarbu tu kuhoji yafuatayo utaitwa msaliti,
1. Mmiliki wa jengo lililopangishwa naCHADEMA Kinondoni kama ofisi za makao makuu na bei ya pango kwa mwezivimefanywa siri. Mara kadhaa swali hili limeibuliwa lakini hakuna jibulililoweza kutolewa na uongozi wa CHADEMA.

2. Wanachama walioomba fursa ya kushiriki tenda ya kununua magari ya chamawamenyimwa fursa hiyo na hatimaye tenda hiyo imetolewa kwa usiri mkubwa.

3. Swala la Katibu Mkuu wa chamakujikopesha mamilioni ya shilingi zilizochangwa na walalahoi kwa ajili yashughuli za chama. Ikumbukwe kuwa watu waliochangia M4C walifanya hivyo kwavile waliamini kuwa michango yao itakiwezesha chama kujiimarisha. Taarifa kuwapesa zimetumika kifisadi zimewavunja watu moyo.

4. Taarifa za Josephine Mushumbusi kulipwa mamilioni ya shilingi za chama kwakazi anayoiita ya kujitolea. Wadau walihoji kuwa na wao wangependa kujitoleakwenye shughuli za chama ili walipwe hayo mamilioni. Ilidhihirika kuwaJosephine alipata fursa hiyo kwa upendeleo.

5. Pesa za ruzuku zimekuwa zikiishia Makao Makuu. Watendaji wa chama mawilayaniwamekuwa wakifanya kazi bila nyenzo. Hii ilisababisha mpaka kukawa na mtafarukuhuko Mpanda kwa kukosa ofisi ya wilaya ambayo kimsingi ni jukumu la chama makaomakuu kuhakikisha chama kina ofisi za wilaya. Ikumbukwe pia kuwa matumizi hayamabaya ya fedha yalikuwa sababu ya mvutano wa kisiasa kati ya marehemu ChachaWangwe na kiongozi Mkuu wa Chama.

6. Kumekuwa na taarifa za matumizi mabaya ya pesa za Sabodo jambo ambalolimeelezewa kuwa sababu ya kumfanya Sabado kuahirisha ahadi yake ya kuijengeaCHADEMA ofisi za makao makuu na chuo cha siasa.

7. Katibu Mkuu wa CHADEMA ni miongoni mwa washutumiwa wa ufisadi wa mamilioniya pesa za mradi wa maji wa Karatu.

8. Viti Maalum vya ubunge vimetolewa kwa upendeleo ambapo akinamamawaliojitolea kukijenga chama wameachwa pembeni na nafasi hizo kupewa akinamamawalio karibu na viongozi wa juu wa chama. Lucy Mukya mzazi mwenzake na Mbowe,Rose Kamili mtalaka wa Dr. Slaa, dada yake Tindu Lissu, mtoto wa Ndensambulon.k

11. Hesabu za pesa zinazochangwa nawalalahoi kwa ajili ya M4C imekuwa ni jambo la siri kubwa ndani ya CHADEMA.

Tunamaanisha MHAINI(mtu ambaye alirenga kupindua dola usiulize majeshi na mahakama zetu ziko ufipa) lol
 
nice analysis mkuu
 
SIRI YA MADIWANI WA SHINYANGA NA CHADEMA YAFICHUKA,MBOWE ASEMA WASALITI WA CHADEMA HAWASAMEHEKI.

Katika hatua inayowashangaza Watanzania wengi kwa nini Chadema imewasamehe madiwani wa Shinyanga,tofauti na msimamo wa Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe alioutoa hivi karibuni kuwa wasaliti wa Chadema hawasameheki na huo ndio umekuwa msimamo wa chadema wa kutokuwasamehe wasaliti wote. Ikumbukwe kuwa madiwani hawa wa Shinyanga walikisaliti chama cha Chadema kwa kujiunga na Magamba wa CCM.

Madiwani wa Shinyanga waliamua kujiunga wenyewe na CCM na kuachana na Chadema ambao siku za usoni kimekuwa chama kinachoongozwa na fikra na maslahi ya Mwenyekiti Mbowe na Dr.SLAA.

Madiwani hao wa shinyanga walipojiunga na CCM wamekuwa wakipewa maisha bora na CCM.Pia madiwani hao wamekuwa wakikisaliti CHADEMA kwenye mikutano ya hadhara ya CCM hasa kipindi walipokabidhiwa kadi za CCM na NAPE MNAUYE na wakakichafua vibaya chama cha chadema mbele ya wananchi.

Lakini Madiwani hawa wa shinyanga walikwenda Kalenga na wakasaidia kukipatia ushindi CCM na Chadema ikashindwa vibaya huko Kalenga.Usaliti huu uliofanywa na madiwani wa chadema shinyanga hauvumiliki,kwani umekipotezea chama wanachama wengi na kufanya chadema kukosa kata za udiwani huko shinyanga ambapo ni hasara kubwa kwa uhai wa chama.

Bado tunakumbuka madiwani wa Arusha waliofukuzwa na Chadema kwa makosa ya usaliti wa kutafuta maridhiano na muafaka wa maslahi ya wana Arusha,madiwani hawa wa Arusha walikuwa wanatafuta hali ya amani kurejea jijini Arusha mara baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 kwani Arusha ilichafuka na wananchi kuishi maisha ya hofu kwa vitendo vya uvunjifu wa amani vilivyokuwa vinaendelea Arusha.

Madiwani watano wa Arusha wakakubali kuwa Wazalendo na kutafuta muafaka na viongozi wa CCM ili kurejesha hali ya amani jijini Arusha. Na muafaka huo ulizaa matunda ya amani kwani kiongozi wa maridhiano hayo alikuwa mkuu wa wilaya ya Arusha kipindi hicho Be.Raymond Mushi ambaye kwa sasa ni mkuu wa wilaya ya Ilala.

Kosa la madiwani wa Arusha ilikuwa ni kutafuta maridhiano ya kurejesha amani ya jiji la Arusha kwa maslahi mapana ya wana Arusha. Usaliti wao ulikuwa huo na hatimaye wakafukuzwa uanachama wa chadema eti wamekisaliti chama.Kwani Mbowe alieleza kwamba maridhiano lazima yapitie kwake na sio kwa viongozi wengine.

Hivyo Dr. Slaa alitoa tamko la chama kwa kuwafukuzu madiwani hao wa Arusha.Baadae madiwani hao wa Arusha wakaenda mahakamani na kufungua kesi dhidi ya Mbowe na Chadema.Ambapo kesi hiyo kimsingi walitakiwa kushitaki bodi ya wadhamini wa chama.

Madiwani wa Arusha walikuwa wazalendo wakafuata taratibu za kikatiba wakaandika barua ya kuomba msamaha kwa mamlaka iliyowafukuza uanachama.

Majibu wakapewa,yakisema kwanza wakakabidhiwa chini ya uangalizi wa Ndesamburo ambaye ni mwenyekiti chadema Kilimanjaro nao wakafanya hivyo.

Pia Dr. Slaa akasema wafute kesi mahakamani wakafuta kesi mahakamani. Mara baada ya madiwani wa Arusha kesi kama walivyoombwa na chadema na wao wakafuta kesi, Dr. Slaa kupitia kwa mwanasheria wa Chadema mkoa wa Arusha Bw.METHOD KIMOMONGOLO akishirikiana na katibu wa chadema mkoa wa Arusha Bw.AMAN GOLUGWA ambaye kwa sasa pia ni Katibu chadema kanda ya kaskazini waliwafungulia kesi madiwani hao wa Arusha,kesi ya kukazia hukumu ambapo mahakamani iliwaamuru walipe gharama za usumbufu wa kesi na wakalipa milioni kumi na tano na laki tano.

Lakini waliombwa na chadema wafute kesi baadae Dr. Slaa na wenzake wakawageuka madiwani na wakajipatia kiasi hicho cha pesa kutoka kwa madiwani hao. Dr. Slaa wakatengeneza kiasi hicho kikubwa cha pesa ambacho mpaka hivi sasa kwenye vitabu vya mahesabu vya chadema hazionekani.

Na wajumbe walipouliza waliambiwa wakae kimya wasitake kujua kila kitu ndani ya chama.Pesa hizo zilitafunwa na Dr. Slaa pamoja na Lema mbunge wa Arusha mjini.Madiwani hawa Wa Arusha wamekuwa wazalendo na wakaomba msamaha lakini hawakusamehewa hatima yake wakazungukwa na kuibiwa pesa hizo.

Leo mnawasamehe wasaliti wakubwa madiwani wa shinyanga,kwani chadema imetumia pesa nyingi kuwarudisha madiwani wa shinyanga na kutengeneza taarifa za uongo ionekane kuwa wamerubuniwa na kushawishiwa na watu. Mbowe amewapa madiwani wa Shinyanga milioni hamsini kila mmoja ili warudi chadema na kuwapa taarifa za uongo ili warudishe imani ya chadema kwa wananchi.

Chadema Makao makuu kwa sasa inaangaika kurejesha imani kwa watanzania kwa gharama kubwa. Ni vyema chadema mkaelekeza nguvu kwenye mikutano ya M4C.

CHADEMA NI MSINGI,PAMOJA DAIMA na oparesheni zingine badala ya kutengeneza na kupika taarifa za uongo kwa watanzania. MBOWE amesema wasaliti wote hawawezi kusamehewa,Ni ajabu wasaliti wa shinyanga wamesamehewa na madiwani wazalendo wa Arusha wakaachwa njia panda.

WATANZANIA HATUNA IMANI NA CHAMA CHA KIHAFIDHINA CHA CHADEMA.

TUNAHITAJI MBADALA WA VYAMA VYA WATU.
 
Hao madiwani ni experiment iliyofanikiwa sana kuwabaini wabaya wa democrasia wabaya wa CHADEMA... Sasa CDM iko salama sana inasonga mbele na Mamluki wote wanashughulikiwa kikamilifu mapema iwezekanavyo kabla ya uchaguzi Mkuu ...
 
Kwani madiwani wa shinyanga sio mamluki? Bado wana kadi za CCM.
 
walimu wa nchi hii ni mataahira na wachumia tumbo....kama mleta thread ni mwalimu kweli
 
Bahati nzuri ni kwamba walioenda ACT wote wametoka CHADEMA. Mnajuana waarabu wa pemba
Kwa sababu ACT hakuna mwenye akili wakutengeneza vijana, wametengenezwa wamekunywa maji ya bendera za kijani wafuasi wa jangiri la pembe za ndovu msomali anadictate terms
 
Back
Top Bottom